Msaada kwa anayemjua vizuri Shetani

Msaada kwa anayemjua vizuri Shetani

Saa nane za usiku kunako kama dakika 2 au 3, usiku Tulivu kuna kunakuwa na kaupepo usiovuma..........ukiwa uchi wa Mnyama (mtupu) toka nje ya Nyumba yako pekee yako bila kusema chochote kasimame mbele ya uwanja wenu wa nyumba usawa na mlango(Hatua kati ya 3 hadi 5)..........haitachukua Dakika 5 nakuhakikishia utakiona kiumbe cha ajabu.........Tahadhali ukikiona kiumbe hicho ondoka taratibu bila ya kusema chochote ingia ndani, usipofanya hivyo huo utakuwa mwisho wa uhai wako..........
sasa nikifanya hivyo watu wakiniona hiyo saa nane na dakika 2 usiku nikiwa uchi wa mnyama si watasema naenda kuroga sasa halafu nitaonekana na wanga sasa kwa hali hiyo...

uone kitu cha ajabu halafu utulie una roho gani yaani hata kuhamaki hamna kweli...
 
Saa nane za usiku kunako kama dakika 2 au 3, usiku Tulivu kuna kunakuwa na kaupepo usiovuma..........ukiwa uchi wa Mnyama (mtupu) toka nje ya Nyumba yako pekee yako bila kusema chochote kasimame mbele ya uwanja wenu wa nyumba usawa na mlango(Hatua kati ya 3 hadi 5)..........haitachukua Dakika 5 nakuhakikishia utakiona kiumbe cha ajabu.........Tahadhali ukikiona kiumbe hicho ondoka taratibu bila ya kusema chochote ingia ndani, usipofanya hivyo huo utakuwa mwisho wa uhai wako..........

Kiranga fanya hii experiment ya MJINI CHAI halafu utuletee majibu maana hii ni moja ya njia za ku prove...
 
Last edited by a moderator:
Kiranga fanya hii experiment ya MJINI CHAI halafu utuletee majibu maana hii ni moja ya njia za ku prove...

Hahaha,

Experiment kuwa considered lazima iwe within the known limits of plausibility.

Besides, mimi kama mpingaji sishurutishwi kufanya experiments, natakiwa nielezwe experiments, methodologies na results.

Isitoshe kwangu nje kuna surveillance cameras 24/7.
 
Last edited by a moderator:
Natamani ningekuwa na uwezo wa kukueleza zaidi lakini sina uwezo huo.
Ijapokuwa umetaka kumjua shetani basi inshaallah utamjua....
 
habari wadau!
kwa muda wa takribani miaka 28 nimekuwa najifunza kuhusu Mungu huyu muumba wa vitu vyote. Na nimekuwa najifunza pia uwepo jba uwezo wa bwana Shetani.
Ili kumwelewa zaidi Mungu nadhani ni muhimu kumuelewa shetani pia. Yoyote mwenye taarifa zitakazonisaidia kumjua shetani anisaidie.

ukiwaangalia kwa umakini ccm wala huwezi kupata tabu kumjuwa shetani.
 
!
!
ungeweka kwa kiswahili ingependeza mno......kiingereza cha Biblia kigumu mno

Kaka ukiwa msomaji wa biblia sana utagundua biblia inakua ngumu kueleweka kwenye kiswahili kuliko kwenye kiingereza

Ezekiel
[h=3]Mlango 28[/h] 1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.
3 Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha;
4 kwa hekima yako na kwa fahamu zako umejipatia utajiri, nawe umepata dhahabu na fedha katika hazina zako;
5 kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako;
6 basi, kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu;
7 basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.
8 Watakushusha hata shimoni; nawe utakufa kifo chao waliouawa kati ya bahari.
9 Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni Mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.
10 Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,
12 Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.
 
Ufunuo
[h=1]Ufunuo 12[/h] 1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
 
[h=1]Ufunuo 13[/h] 1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
 
kama unazijua amri kumi za M 'Mungu na unazifuata inamaanisha wewe ni mfuasi wa M'Mungu, usipozifuata unakuwa mfuasi wa Mpinzani wa Mungu (shetani). Shetani ni mpinzani wa Mungu, Roho ya Uovu, na Mpinga Amri zote za Mungu na wafuasi wake ni wote wanaovunja amri za Mungu.
 
shetan ni mpinzan wa mungu kivip? kwan na yy c ameumbwa na uyo mungu au? kitu kilichokuumba kweli unaweza ukawa nacho sawa na kua mpinzani wake?
 
shetan ni mpinzan wa mungu kivip? kwan na yy c ameumbwa na uyo mungu au? kitu kilichokuumba kweli unaweza ukawa nacho sawa na kua mpinzani wake?

Katika mafundisho ya vitabu vitakatifu hakuna maelezo kuhusu lini na kwa namna gani Mungu aliwaumba malaika ambao inavosemekana shetan alikuwa ni mmoja wa hao malaika. Kwa akili yangu ya kibinaadamu kama kuna pande mbili zinatofautiana katika matakwa fulani basi tunasema zina upinzani, pia vitabu vinaeleza kuwa shetan ana nguvu ambazo hazipimiki ndo maana anauwezo wa kuwa na ushawishi kama Mungu. Kama una imani kuwa Mungu yupo basi ukubali tu upande wa pili kuna shetani .
 
shetan ni mpinzan wa mungu kivip? kwan na yy c ameumbwa na uyo mungu au? kitu kilichokuumba kweli unaweza ukawa nacho sawa na kua mpinzani wake?

mfano rahisi binadamu anaweza kutengeneza robot likawa na akili na ushawishi zaid kuliko binadam wa kawaida.
 
habari wadau!
kwa muda wa takribani miaka 28 nimekuwa najifunza kuhusu Mungu huyu muumba wa vitu vyote. Na nimekuwa najifunza pia uwepo jba uwezo wa bwana Shetani.
Ili kumwelewa zaidi Mungu nadhani ni muhimu kumuelewa shetani pia. Yoyote mwenye taarifa zitakazonisaidia kumjua shetani anisaidie.

Niko naye hapa mkuu! Anauliza akusaidie nini?
 
Katika mafundisho ya vitabu vitakatifu hakuna maelezo kuhusu lini na kwa namna gani Mungu aliwaumba malaika ambao inavosemekana shetan alikuwa ni mmoja wa hao malaika. Kwa akili yangu ya kibinaadamu kama kuna pande mbili zinatofautiana katika matakwa fulani basi tunasema zina upinzani, pia vitabu vinaeleza kuwa shetan ana nguvu ambazo hazipimiki ndo maana anauwezo wa kuwa na ushawishi kama Mungu. Kama una imani kuwa Mungu yupo basi ukubali tu upande wa pili kuna shetani .

Thibitisha kwamba mungu yupo.

Vinginevyo kubali unaongelea hadithi za kufikirika zaidi.
 
Thibitisha kwamba mungu yupo.

Vinginevyo kubali unaongelea hadithi za kufikirika zaidi.

tarehe 13-7-1917 , watoto watatu;Lucia, Francisco na Jacinta walitokewa na Mama maria, aliwaonyesha maono ya kuzimu jinsi kulivo! Na kuwasisitizia Mungu anataka kuokoa roho za wengi ziokolewe kwa njia ya sala. Hapo inaonyesha Mungu yupo na Shetani yupo.
 
Kwanza hujathibitisha kwamba walitokewa na Maria au walikuwa na njaa tu wakapata hallucination.
 
Katika mafundisho ya vitabu vitakatifu hakuna maelezo kuhusu lini na kwa namna gani Mungu aliwaumba malaika ambao inavosemekana shetan alikuwa ni mmoja wa hao malaika. Kwa akili yangu ya kibinaadamu kama kuna pande mbili zinatofautiana katika matakwa fulani basi tunasema zina upinzani, pia vitabu vinaeleza kuwa shetan ana nguvu ambazo hazipimiki ndo maana anauwezo wa kuwa na ushawishi kama Mungu. Kama una imani kuwa Mungu yupo basi ukubali tu upande wa pili kuna shetani .

kwa uelewa wangu mdogo nimesoma tu sehemu shetani alikuwa malaika mkuu baada ya kuasi mungu akamtupa duniani hakumnyan'ganya zile nguvu alizonazo na wala hakumuangamiza kwanini?
 
Back
Top Bottom