Haimaanishi kitu kusema bila ya ushaidi zaidi ya kuonyesha upungufu wa kufikiria kwenye fikra yako dhaifu.
Jifunze kutafiti kabla ya kupayuka. Ndio maana nilikwambia sina muda na longalonga kwasabau wewe umejaa longa kichwani mwako ambazo hazina ushaidi.
Umeshindwa hata kutetea IMANI yako ya kuto amini na umebakia na bayana za kitamthilia. Huo ndio UTAFITI wa kwenu Tanzania. Kupayuka na kubwabwaja tu bila ya Ushaidi halafu unasikia rahaa mwenyewe. Lakini umaskini wa kuelewa unacho dai ndio umejaza akili na fikra zako. Hapo nakupa ongera.
Jibu swali langu la mwanzo kwa ushaidi na sio kutumia "KAMA". Sina muda na "KAMA" zilizo jaa udhaifu na zisizo na uhakikisho zaidi ya bayana za kitamthilia. Pole sama mfuasi wa Imani ambayo imekushinda kuitetea.
Wewe mtu umeshindwa hata kunitajia mungu wako ni mungu gani kwa woga wa huyo mungu wako kubomolewa!
Taja jina la mungu wako na tabia zake hapa tumbomoe.
Otherwise umeshindwa mjadala.
Huwezi kuniambia nitoe ushahidi wa kutowapo kwa mungu kabla ya kuthibitisha kwamba.mungu.yupo kwa ushahidi.
Kwa sababu ishahidi ni tabia ya vitu vilivyopo, si tabia ya vitu visivyopo.
Leo hii nikitunga kitu tu, kitu ambacho hakipo, kama kikombe cha dhahabu kinachoelea juu ya mloma Kilimanjaro, nikakwambia kikombe hiki kipo, na kama unabisha toa ushahidi kwamba hakipo. Hutaweza kunipa ushahidi kwamba hakipo, sio kwa.sababu kipo, bali kwa sababu hakipo.
Utaanzia wapi kunipa ushahidi kwamba kikombe hakipo kama hakipo?
On the other hand, kama kikombe kipo, kutoa ushahidi kwamba kipo ni rahisi tu. Watu watakiona, watakipiga picha, satellite zitakiona, television crews zitakiona et cetera et cetera.
Kwa hiyo, kazi ya uthibitisho ipo kwa.wale wanaosema mungu yupo.
Wanaobisha hawana kazi ya kuthibitisha.
Kwa sababu, visivyopo havithibitiki.