Msaada kwa anayemjua vizuri Shetani

Msaada kwa anayemjua vizuri Shetani

Kama hakifikiriki kwa upeo wa kibinadamu unajuaje kwamba mungu yupo?


Nakusoma tu hapa kila siku.
Sikia
Mungu ni roho na anaabudiwa katika roho.

Na ww mpaka unakufa hutakaa u proove km Mungu yupo kwasbb haya ni mambo ya rohoni sio ya mwilini.
So hutakaa uelewe.

Shetani pia ni roho pia na anafanya kazi zake hivyo hivyo so hutakaa uelewe wala u proove uwepo wake kwa jinsi ya mwili.

Haya mambo yanatambulika kwa watu wa rohoni sio mwilini km ww unavyotaka.

Ipo cku utajua Mungu yupo u jus wait
 
Nakusoma tu hapa kila siku.
Sikia
Mungu ni roho na anaabudiwa katika roho.

Na ww mpaka unakufa hutakaa u proove km Mungu yupo kwasbb haya ni mambo ya rohoni sio ya mwilini.
So hutakaa uelewe.

Shetani pia ni roho pia na anafanya kazi zake hivyo hivyo so hutakaa uelewe wala u proove uwepo wake kwa jinsi ya mwili.

Haya mambo yanatambulika kwa watu wa rohoni sio mwilini km ww unavyotaka.

Ipo cku utajua Mungu yupo u jus wait

Roho no nini? Unajuaje kwamba ipo na si stories tu?
 
habari wadau!
kwa muda wa takribani miaka 28 nimekuwa najifunza kuhusu Mungu huyu muumba wa vitu vyote. Na nimekuwa najifunza pia uwepo jba uwezo wa bwana Shetani.
Ili kumwelewa zaidi Mungu nadhani ni muhimu kumuelewa shetani pia. Yoyote mwenye taarifa zitakazonisaidia kumjua shetani anisaidie.
Shetani ni yeyote liechagua au anaefanya mambo ambayo mwisho wake ni mototoni it means shetani wa kijini shetani wa kibinaadamu ..ok kuna mkubwa wao ambae anaitwa ibilis
Speaking of ibilisi (Shetani) ni kiumbe jamii ya kijini ameumbwa kwa moto kama majini wengine ila tofauti na majini wengine ni kwamba shetani anaelimu kubwa sana (aliopewa na mungu)..anamugopa mungu vibaya mno na ni kiumbe pekee wa kwanza kukataa peponi na kukubali motoni..
Kunacontradiction ya kwamba huyu shetani ni malaika ...hi si kweli kwa sababu malaika ni( built order follower ) hafanyi ila aliloamrishwa na aliemuumba (wanamabawa lakini sio kama Yale ya kuku) na (sio wanawake wala mwanaume)
So shetani ni jinni na binaadamu
The following are characteristic of iblis(shetani)
1.anaelimu kubwa sana aliofunzwa na mungu kupitia malaika
2.yuko tayari kuumia kuingia Moroni
3.anamuogopa mungu vibaya sana
4.MTU akikufuru sana na kumtukana mungu yeye hukimbia kwa kuogopa dharuba itakayofika kwa huyo MTU
 
habari wadau!
kwa muda wa takribani miaka 28 nimekuwa najifunza kuhusu Mungu huyu muumba wa vitu vyote. Na nimekuwa najifunza pia uwepo jba uwezo wa bwana Shetani.
Ili kumwelewa zaidi Mungu nadhani ni muhimu kumuelewa shetani pia. Yoyote mwenye taarifa zitakazonisaidia kumjua shetani anisaidie.
Maoni ya Biblia

Shetani Ni Nani? Ni Kiumbe Halisi?


WASOMI fulani wa kisasa wanasema kwamba Shetani si kiumbe halisi. Wanadai kwamba alibuniwa tu katika mawazo ya wanadamu. Ubishi wa aina hiyo umekuwapo kwa muda mrefu. “Ujanja wa hali ya juu wa Ibilisi,” akaandika Charles-Pierre Baudelaire, mshairi wa karne ya 19, “ni kutushawishi tuamini kwamba yeye hayuko.”

Je, Shetani ni kiumbe halisi? Ikiwa ndivyo, alitoka wapi? Je, yeye ndiye nguvu isiyoonekana inayosababisha matatizo ambayo wanadamu wanakabili? Unaweza kuepukaje kuathiriwa na uvutano wake?

Biblia Inasema Nini?

Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8;2 Timotheo 2:26) Pia inasimulia mazungumzo kati ya Shetani na Mungu na pia kati yake na Yesu.—Ayubu 1:7-12;Mathayo 4:1-11.

Kiumbe huyo mwovu alitoka wapi? Muda mrefu kabla ya mwanadamu kuumbwa, Mungu alimuumba Mwana wake “mzaliwa wa kwanza,” ambaye alikuja kuitwa Yesu. (Wakolosai 1:15) Baada ya muda, ‘wana wengine wa Mungu,’ wanaoitwa malaika, wakaumbwa. (Ayubu 38:4-7) Wote walikuwa wakamilifu na waadilifu. Hata hivyo, mmoja kati ya malaika hao akaja kuwa Shetani.

Malaika huyo hakuitwa Shetani alipoumbwa. Jina hilo ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu.

Kiumbe huyo wa roho akaanza kukuza hisia za kiburi na za kushindana na Mungu. Alitaka wengine wamwabudu yeye. Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu alipokuwa hapa duniani, Shetani alimtaka Yesu ‘amfanyie tendo la ibada.’—Mathayo 4:9.

Shetani “hakusimama imara katika kweli.” (Yohana 8:44) Alidai kwamba Mungu alikuwa mwongo, ilhali kwa kweli, yeye ndiye alikuwa mwongo. Alimwambia Hawa kwamba angekuwa kama Mungu, lakini ni yeye hasa aliyetaka kuwa kama Mungu. Na kupitia mbinu zake za ujanja, alitosheleza tamaa yake yenye ubinafsi. Alimfanya Hawa amwone kuwa mkuu kuliko Mungu. Kwa kumtii Shetani, Hawa alimkubali kuwa mungu wake.—Mwanzo 3:1-7.

Kwa kuchochea uasi, malaika huyo ambaye awali alikuwa mwenye kuaminika akawa Shetani, yaani, mpinzani na adui ya Mungu na wanadamu. Neno “Ibilisi,” linalomaanisha “Mchongezi,” likawa pia jina la malaika huyo mwovu. Malaika huyo ambaye aliongoza katika kutenda dhambi mwishowe aliwachochea malaika wengine wakose kumtii Mungu na wamwasi kama yeye. (Mwanzo 6:1, 2; 1 Petro 3:19, 20) Kwa kufanya hivyo malaika hao waliwaongezea wanadamu shida. Kwa sababu ya kuiga njia za Shetani zenye ubinafsi, “dunia ikajaa jeuri.”—Mwanzo 6:11;Mathayo 12:24.

Uvutano wa Shetani Una Nguvu Kadiri Gani?

Mhalifu anaweza kupangusa alama za vidole ili asiache kitu chochote ambacho kitamtambulisha. Hata hivyo, polisi wanapofika, wanatambua kwamba iwapo uhalifu umetendwa, lazima kuwe na mhalifu. Shetani, “muuaji” wa zamani hujaribu kuficha kitu chochote ambacho kitamtambulisha. (Yohana 8:44;Waebrania 2:14) Alipozungumza na Hawa, Shetani alijificha kwa kutumia nyoka. Bado anajaribu kujificha leo. “Amezipofusha akili za wasioamini” ili watu wasitambue uvutano wake wenye nguvu umeenea kadiri gani.—2 Wakorintho 4:4.

Hata hivyo, Yesu alimfichua Shetani kuwa mhalifu mkuu anayeongoza ulimwengu huu wenye ufisadi tunamoishi. Alimwita “mtawala wa ulimwengu huu.” (Yohana 12:31; 16:11) “Ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu,” akaandika mtume Yohana. (1 Yohana 5:19) Shetani hutumia “tamaa ya mwili na tamaa ya macho na mtu kujionyesha mali yake maishani” ili ‘aipotoshe dunia nzima inayokaliwa.’ (1 Yohana 2:16; Ufunuo 12:9) Yeye ndiye yule ambaye wanadamu kwa ujumla humtii.

Kama ilivyokuwa kwa Hawa, wale wanaomtii Shetani, humfanya kuwa mungu wao. Hivyo, Shetani ndiye “mungu wa mfumo huu wa mambo.” (2 Wakorintho 4:4) Matokeo ya utawala wake yanatia ndani unafiki na uwongo; vita, mnyanyaso na uharibifu; uhalifu, pupa na ufisadi.

Jinsi Unavyoweza Kuepuka Uvutano Wake

Biblia inaonya hivi: “Tunzeni akili zenu, iweni wenye kulinda.” Kwa nini? Kwa sababu “adui yenu, Ibilisi, anatembea huku na huku kama simba anayenguruma, akitafuta kummeza mtu.” (1 Petro 5:8) Ingawa andiko hilo linatoa mwito wa ushindani, inatia moyo kujua kwamba wale tu ambao hawatunzi akili zao, yaani, wale ambao hawaendelei kukesha, ndio ‘watakaoshindwa akili na Shetani.’—2 Wakorintho 2:11.

Ni muhimu kwamba tukubali ukweli kuwa Shetani yuko na tumruhusu Mungu ‘atufanye kuwa imara’ na ‘kutufanya tuwe wenye nguvu.’ Katika njia hiyo ‘tunaweza kuchukua msimamo kumpinga Shetani’ na kusimama upande wa Mungu.—1 Petro 5:9, 10.

JE, UMEJIULIZA HIVI?

▪ Shetani alitoka wapi?Ayubu 38:4-7; Yohana 8:44.

▪ Shetani huathiri ulimwengu kadiri gani?Yohana 12:31; 1 Yohana 5:19; Ufunuo 12:9.

▪ Tunaweza kufanya nini ili kujilinda kutokana na mbinu za uovu za Shetani?1 Petro 5:8-10.
 
 
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote apende sana kuabudiwa?

Huyu mungu hana vitu vikubwa zaidi vya kufanya kuliko kupoteza attention yake kufuatilia jinsi anavyoabudiwa na binadamu?

Huyu mungu ana inferiority complex gani mpaka awe addictive na kuabudiwa hivi?

Mimi ninavyojua kupenda kuabudiwa ni tabia ya binadamu madikteta na megalomaniacs kama kina Idi Amin na Joseph Stalin, kwa nini mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote apende kuabudiwa?

Kuabudiiwa na binadamu kutamuongezea nini mungu huyu ambaye kila kitu ni mali yake?

Huyu mungu muweza yote kwa nini yuko needy sana na ana weakness ya kupenda kuabudiwa kiasi cha kushurutisha watu wamswalie mara tano kwa siku?

Halafu hujajibu swali langu, kama mungu anapanga kila kitu, ina maana hata shetani kuwepo kwake kulipangwa na mungu.

Shetani anaweza kulaumiwa kwa kuishi kama alivyopanga mungu?
me nadhani kuna kitu pengine unakijua zaidi kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwake (MUNGU) kwa namna unavyowabana wenzako maswali.

lakini pia tukienda mbali zaidi ni kweli Mungu ni muweza wa yote.

kila kinachotendeka hapa dunia yaani kule kukubali shetani aje kutusumbua au kutaka yeye kuabudiwa ilihali ni muweza wa yote,yaani ni alipenda tu iwe hivyo lakn haimaanishi kushindwa kumfanya binadamu aliyemuumba mwenyewe kuishi kwa amani bila mtego wa dhambi ndiyo siyo muweza wa yote.

ni quote ujumbe wako huu haswa kujibu tu pale ulipoulizwa kuhusiana na uweza wa yote
 
me nadhani kuna kitu pengine unakijua zaidi kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwake (MUNGU) kwa namna unavyowabana wenzako maswali.

lakini pia tukienda mbali zaidi ni kweli Mungu ni muweza wa yote.

kila kinachotendeka hapa dunia yaani kule kukubali shetani aje kutusumbua au kutaka yeye kuabudiwa ilihali ni muweza wa yote,yaani ni alipenda tu iwe hivyo lakn haimaanishi kushindwa kumfanya binadamu aliyemuumba mwenyewe kuishi kwa amani bila mtego wa dhambi ndiyo siyo muweza wa yote.

ni quote ujumbe wako huu haswa kujibu tu pale ulipoulizwa kuhusiana na uweza wa yote
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo kweli, na si hadithi za watu tu?
 
Ukitaka utajiri wa chapchap ni mda mwafaka wa kumjua shetani A up to Z
 
Back
Top Bottom