teac kapex
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 470
- 136
Kwa kweli simu nilizoamini ni nzuri ni pamoja na Samsung lakini kwangu imekuwa tofauti, mwanzoni simu ilikuwa vizuri lakini sasa hivi natamani kurudi kwenye tecno na infinix, maana nikiwa safarini nawaona wenzangu wakivinjari kwenye mitandao ya kijamii mwanzo mwisho wa safari lakini hili la kwangu limekuwa kimeo halikamati namaanisha netwok hakuna, na siwezi kupiga simu nikiwa safarini, linapoteza mara kwa mara mtandao ingawa ukiangalia pale juu unaona bar zipo zimejaa, lakini kumbe ni emergency calls tu. Hivyo naomba kujua kama kuna mahali pa kurekebisha ili lirudi kama zamani au ndo limekwisha kazi? Natanguliza shukrani