Msaada: Jinsi ya kuvunja ndoa ya kikristo

Msaada: Jinsi ya kuvunja ndoa ya kikristo

Ndiyo inawezekana kuvunja hiyo ndoa. Jambo la kufahamu ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa hakuna ndoa isiyoweza kuvunjika sabbu ndoa zote ni mikataba, iwe imefungwa kidini, kimila au kiserikali.

Ifahamike pia kuwa ndoa zote halali zinavunjwa kwa misingi ya sheria ya ndoa, iwe ni yakidini, kimila au kiserikali.

Kwa huyo rafiki yako anayo sababu ya msingi kabisa kati ya sababu zilizotajwa kwenye sheria ya ndoa. KUSHINDWA SHIRIKI TENDO LA NDOA

Sasa kitu gani afanye?
Kwa maelezo yako ni wazi ndoa yao bado changa sana (chini ya miezi 5) na kwa sharti la sheria ni kuwa ndoa itavunjwa ikiwa ina miaka miwili au zaidi, labda itokee sababu nyinginezo za lazima sana.

Kwa huyo rafiki yako, anatakiwa kwanza kupita bodi ya usuluhishi wa masuala ya ndoa, inaweza ikawa Baraza la Kata likikaa kama Baraza la usuluhishi wa ndoa au Baraz la usuluhishi wa ndoa katika kanisa lao ila hapo ni lazima hilo baraz la kanisa liwe limesajiliwa kwa ajili ya shuhuli hiyo. Sio baraza ilimradi baraza hapana.

Hapo watasuluhishwa watapewa na ushauri pia, ikigoma sasa atapatiwa cheti/shahada ya kushindwa kusuluhishwa.

Hapo atakwenda Mahakamani kwa ajili ya kufanya mchakato wa maombi ya talaka sasa, hapo anaweza kwenda Mahakama ya Mwanzo eneo alilopo, huko ataweka sababu hiyo ya KUSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA tangu ndoa ifungwe hadi wakati huo wa ombi la talaka.

Pia ataambatanisha nakala ya cheti cha ndoa, cheti/shahada ya kushindw kusuluhishwa pamoja na nyaraka zinginezo.

Hapo ataeleza pia kama kuna chumo/mali za pamoja hapa akumbuke kamwe hawezi kugawiwa mali alizomkuta nazo huyo mume wake has ukizingatia umri wa ndoa yao. Hatutegemei kuwepo na watoto hapo.

Basi watasikilizwa na Mahakama ikiridhika itatoa talaka.

Sasa baada ya kupatiwa talaka atatakiwa kwenda kwa msajili wa ndoa wilaya alimofungia ndoa na nakala ya maamuzi ya Mahakama yenye mhuri, pamoja.na cheti cha ndoa na nyaraka zinginezo, huko atakwenda kusajiliwa kama mtu asiye na ndoa.

Haya sasa arudi kwa mchepuko wake wakafanye jambo rasmi la kuoana.

Kila la kheri, japo hatupendi kuvunja ndoa zenu.
Asante ndugu kwa ushauri
 
Ikigundulika mwanzoni Kuna shida ikaachwa bila kufunga ni Batili ila mapungufu Makubwa Kama hayo ya kuivunja ndio yanaitwa Batilifu .

Hiyo Ni kupeleka taarifa tu.

Ndio maana Makanisa mengine Kuna chumba na kitanda cha kukamilisha ndoa yenyewe kwa tendo.
Hapo Ndoa bado haikukamilishwa.
Ndio maana wanaoangalia maswala ya kiroho vizuri siyo vizuri kwenda ukumbini au Magest ya ajabu ya uzinzi kukamilisha hii kazi takatifu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Inaonesha huyo muolewaji mwenyewe ni mcharuko sana yaani miezi miwili tu baada ya kutoka kwa bwanaake tayari ana mchumba wa kumuoa.
 
Habari ndugu zangu, naishi Kigoma, nina lafiki yangu wa kike alifunga ndoa na mwanaume mmoja hivi toka wameona mwanaume hajawahi kushiriki tendo la ndoa na hana uwezo kabisa.

Wameishi miezi 3, hali hiyo imefanya binti arudi kwao. Kwa sasa anamiezi 2 na amepata mchumba mwingine, je, anawezaje kuvunja ndoa?

Naomba ushauri wapendwa.
Daaah,miez mitatu tu?? Amsubiri kwanza amsaidie kutatua tatizo siyo kumuongezea tstizo,wanaume wengine ni suala la saikolojia tu,sidhan hata kama amewahi kwnda naye hospitali
 
Ndoa haivunjiki mnatengana tu ila wewe huruhusiwi kuoa na mwenzio haruhusiwi kuolewa hadi mmoja wenu afe
Ndoa ni kitendo cha mume kumuingilia kimwili mchumba wake
Ndiyo maana huitwa tendo la ndoa kama tendo Hilo halijafanyika na halitaweza kufanyika basi makubaliano hayo kanisani yata tanguka
 
Ndoa ni mkataba wa watu wawili, wewe wa tatu ndio nuksi yenyewe.

Huyo mwanamke nae hatari, kaachana na mtu mieizi mitatu iliopita, hafu miwili iliopita ameshapata mtu wa kumuoa?

Inaelekea alikua nae tokea zamani.
 
Shida mwanaume hataki kuja kila tunapo ongea nae wala kanisan
Wewe una uhakika jamaa kuwa jamaa hajawahi kushiriki naye tendon la ndoa,kama ndivyo ilikuwaje mpaka akaoane naye.kuna issue hapo huyo rafiki yako anavificha.
Nakushauri achana na mambo ya ndoa za watu
 
Habari ndugu zangu, naishi Kigoma, nina lafiki yangu wa kike alifunga ndoa na mwanaume mmoja hivi toka wameona mwanaume hajawahi kushiriki tendo la ndoa na hana uwezo kabisa.

Wameishi miezi 3, hali hiyo imefanya binti arudi kwao. Kwa sasa anamiezi 2 na amepata mchumba mwingine, je, anawezaje kuvunja ndoa?

Naomba ushauri wapendwa.
Tutaamini vipi kama huyo jamaa haisimami.
Mpe namba angu nimfanyie mtestisho nihakikishe, maan wanawake siku hizi shida sana.
 
Aisee hii kali inamaana kabla ya kuoana hawaku-test mitambo kwanza yaan aliingia kichwa kichwa ?
✍️
Ndio maana nasema huyu mtoa mada anaingilia mambo asiyo yafahamu.Hadi Huyo binti kwenda kuolewa na jamaa kwamba alipakiziwa
 
Miezi mitatu iliyopita amefunga ndoa.
Amepata mchumba ndani ya miezi miwili tu ya kuwa kwao.
Mke yupo speed sana huyo.
 
....yachumbani yakimwagika hadharani ujue ni haya, haya wanashika nini washkaji washika mabaya, jogoo hajawika alfajiri, washayaanika kariakoo, hawakai maneno yamewakalia koo.....
Mpaka moshi unavuka juu ndani pamotooo
 
Hiyo ndoa kuivunja ni rahisi sana

Ndoa bila tendo la ndoa ni ndoa batili.

Kama hataki mzunguko mrefu Asiende kanisani.

Aende baraza la kata. Watawasikiliza wote wawili kisha watapewa cheti cha kata. Ambacho watapeleka mahakamani na kuivunja hiyo ndoa kisheria. Ndani ya mwezi mmoja tu kila kitu kinakamilika

Kanisani watawazungusha zungusha sana
Ikivunjwa kiserikali kanisa litaendelee kuitambua na hivyo hataweza kuolewa tena kanisani.

Amandla..
 
Habari ndugu zangu, naishi Kigoma, nina lafiki yangu wa kike alifunga ndoa na mwanaume mmoja hivi toka wameona mwanaume hajawahi kushiriki tendo la ndoa na hana uwezo kabisa.

Wameishi miezi 3, hali hiyo imefanya binti arudi kwao. Kwa sasa anamiezi 2 na amepata mchumba mwingine, je, anawezaje kuvunja ndoa?

Naomba ushauri wapendwa.
Ndio haivunjwi....wakati wanaoana huyo binti hakumkagua⁉️⁉️
 
Back
Top Bottom