Ndiyo inawezekana kuvunja hiyo ndoa. Jambo la kufahamu ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa hakuna ndoa isiyoweza kuvunjika sabbu ndoa zote ni mikataba, iwe imefungwa kidini, kimila au kiserikali.
Ifahamike pia kuwa ndoa zote halali zinavunjwa kwa misingi ya sheria ya ndoa, iwe ni yakidini, kimila au kiserikali.
Kwa huyo rafiki yako anayo sababu ya msingi kabisa kati ya sababu zilizotajwa kwenye sheria ya ndoa. KUSHINDWA SHIRIKI TENDO LA NDOA
Sasa kitu gani afanye?
Kwa maelezo yako ni wazi ndoa yao bado changa sana (chini ya miezi 5) na kwa sharti la sheria ni kuwa ndoa itavunjwa ikiwa ina miaka miwili au zaidi, labda itokee sababu nyinginezo za lazima sana.
Kwa huyo rafiki yako, anatakiwa kwanza kupita bodi ya usuluhishi wa masuala ya ndoa, inaweza ikawa Baraza la Kata likikaa kama Baraza la usuluhishi wa ndoa au Baraz la usuluhishi wa ndoa katika kanisa lao ila hapo ni lazima hilo baraz la kanisa liwe limesajiliwa kwa ajili ya shuhuli hiyo. Sio baraza ilimradi baraza hapana.
Hapo watasuluhishwa watapewa na ushauri pia, ikigoma sasa atapatiwa cheti/shahada ya kushindwa kusuluhishwa.
Hapo atakwenda Mahakamani kwa ajili ya kufanya mchakato wa maombi ya talaka sasa, hapo anaweza kwenda Mahakama ya Mwanzo eneo alilopo, huko ataweka sababu hiyo ya KUSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA tangu ndoa ifungwe hadi wakati huo wa ombi la talaka.
Pia ataambatanisha nakala ya cheti cha ndoa, cheti/shahada ya kushindw kusuluhishwa pamoja na nyaraka zinginezo.
Hapo ataeleza pia kama kuna chumo/mali za pamoja hapa akumbuke kamwe hawezi kugawiwa mali alizomkuta nazo huyo mume wake has ukizingatia umri wa ndoa yao. Hatutegemei kuwepo na watoto hapo.
Basi watasikilizwa na Mahakama ikiridhika itatoa talaka.
Sasa baada ya kupatiwa talaka atatakiwa kwenda kwa msajili wa ndoa wilaya alimofungia ndoa na nakala ya maamuzi ya Mahakama yenye mhuri, pamoja.na cheti cha ndoa na nyaraka zinginezo, huko atakwenda kusajiliwa kama mtu asiye na ndoa.
Haya sasa arudi kwa mchepuko wake wakafanye jambo rasmi la kuoana.
Kila la kheri, japo hatupendi kuvunja ndoa zenu.