Hizi coz huwa zinawekwa kwa vigezo vya ufaulu wa chini, yaani walau mtu awe na principal pass, lakini wanapoomba, wanafunzi wengi huwa na ufaulu wa juu zaidi hivyo kupelekea vyuo vikuu kupandisha madaraja (cutting point) ya kuchukua wanafunzi kwa ufaulu walionao.
Na hapo si mwishow Bali pia TCU hutoa kibali Cha namba ya juu ya wanafunzi wanaotakiwa kudahiliwa kwa kozi husika, piga hesabu labda MD UDOM wanahitajika wanafunzi 400, na walionaufaulu kuanzia Dv 1 ya tatu mpaka Div. 1 ya Saba ni 800 kwa awamu zote zaudahili, na hapo Bado Kuna wanafunzi wa Diploma yako wenye GPA labda za 4.3 na kuendelea wanahitaji nafasi pia, kwa sifa za nduguyo hawezi pata nafasi hiyo UDOM, asijepoteza muda tu mpaka anakaa sawa ashamiss vipindi vingi kwa kozi alochaguliwa.
Kama mnauwezo kifedha na mmedhamilia asome MD.
Vyuo vikishafungua achukue admission letter ya UDOM aende nayo kwenye vyuo binafsi vinavyotoa MD, ( Kairuki na vinginevyo) na aombe kuhamia chuoni hapo kw kozi ya MD, na matumaini atapata maana ada yake ni ndefu ni watu wachache sana wanaweza kulipa ivyo unakuta Ile idadi ya kudahili walopewa na TCU Bado haijafikia