Msaada: Jiko la gesi hutoa moshi mwingi kuchafua sufuria

Habari zenu wakuu. Nina jiko la gesi linatoa masinzi sana kwenye sufuria. Nikibandika sufuria nikaweka moto mkubwa kidodo, sufuria huwa nyeusi sana kwa masinzi. Naamini kuna tatizo mahali kwani mwanzo haikuwa hivi. Kama kuna mwenye suluhisho la hili tatizo naomba anipe msaada.

Barner yako itakuwa imechoka nadhani hayo masizi ni uchafu wa kutu au uchafu ulioziba kwenye vitundu vya kupitishia moto.
 
Habar wakuu nmenunua jiko la plate moja ila tatizo linatoa sana moshi kama napukia kuni vile tatxo ni nn??
 
Habar wakuu nmenunua jiko la plate moja ila tatizo linatoa sana moshi kama napukia kuni vile tatxo ni nn??

hata mimi tatizo ni hilo hilo, ngoja wataalam waje...

Jaribu kuangalia nozzles zake kama ni chafu au sio za liquid gas ni za dry gas. Pia angalai kama kile kichuma around nozzles kimekaa vizuri. Pia ni nani mtumiaji sana, kama ni msichana wa kazi ambao wengi intellectually ni wako chini sana yawezekana wanamchango kwenye hilo tatizo.
 
Unawasha moto mkali sana ndo maana.
Wengi wanaotumia majiko ya gesi wanadhani kuweka moto mkali mpaka mwisho wanadhani ndio kuivisha chakula haraka.
Wakati unawasha jiko hakikisha moto unaotoka ni ule wa blue. Ukishaweka level ya kuwaka sana ukatoka ule moto wa njano ujue lazima uchafue sufuria.
Kwa kifupi usiwashe moto mkali saaaanaaaa na wala usiwashe ukawa mdogo sana. Weka level ya kati.
Chakula kitaiva tu mkuu.
 
Niliwahi kuwa na tatizo kama hilo ila nilipobadilisha mtungi was gesi likaisha nafikiri ni aina ya gesi huenda imexpire kama nayo huwa inaexpire. Kwa vyovyote vile tatizo hilo linahusiana na gesi sio jiko.
 
Wakuu nimenunua leo gas ya Oryx mtungi mkubwa pamoja na jiko lenye plate mbili!! sasa cha ajabu linatoa moshi kama napikia kuni....nimejaribu kubalance moto nimeshindwa!!

Msaada wenu, natakiwa kufanya nini ili nipate luminous flame?
 
Mkuu hayo masikio yakoje? Nimeshindwa kuyatambua

Hayo hapo ingiza mkono kwa chini hapo pa kuwashia yazungushe taratibu mpaka upate moto wa blue moshi utaisha
 

Attachments

  • 1449670300492.jpg
    1449670300492.jpg
    53.3 KB · Views: 520
Wakuu nimenunua leo gas ya Oryx mtungi mkubwa pamoja na jiko lenye plate mbili!! sasa cha ajabu linatoa moshi kama napikia kuni....nimejaribu kubalance moto nimeshindwa!!

Msaada wenu, natakiwa kufanya nini ili nipate luminous flame?
Khaa!! Chief hiyo flame uliyonayo tayari ni luminous flame ndiyo maana inatoa moshi. Hii ndiyo sifa ya luminous flame. Nadhani unahitaji non luminous flame ili isiwe na moshi pia itoe joto kubwa. Ni rahisi kufanya hivyo kwa kuongeza kiasi cha gesi ya oksijeni katika flame. Na hii inafanyika kwa kufungua vidirisha vya hewa vilivyochini karibu na valvu za kufungulia hewa katika jiko lako. Fungua taratibu hadi usikie flame imeanza kutoa kelele. Hii ni sayansi niliyofundishwa darasa la sita :mvutaji:
 
Back
Top Bottom