Hapo tatizo ni fuel to air ratio na sio uchafu wa gesi au nini sijui! Chungulia chini ya jiko lako utakuta vijibati vya kuziba au kuachia hewa inayo ingia kwenye vijitundu vinavyo ingiza hewa kabla ya mchanganyiko wa hewa na gesi haujaingia kwenye bunners, cha kufanya pale washa jiko lako, alafu adjust vijibati hivyo slowly huku ukiangalia rangi ya flame/moto kwenye burner endelea ku-adjust mpaka moto uonekane totally blue, ukiona moto umechanganyika wa bluu na majano basi endelea kurekebisha.
Adjustment/vibati hivyo vipo chini za duct ya chuma inayoingiza gesi kwenye burner kila bunner ina adjustment moja - kazi ya vibati hivyo ni kurekebisha hewa inayo changanyika na gesi kabla haijafika kwenye bunner, hewa ikingia ndogo rangi ya flame inakuwa yellowish kama ya kibatali na kutoa moshi mweusi/masizi - hewa ikingia ya kutosha basi rangi ya flame inakuwa blue (i.e complete combustion) ukifanikiwa ku-adjust vijibati hivyo hutaona tena masizi. Goodluck.