Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Kichochoro

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,135
1,163
20220606_183417.jpg

Familia ya Abeid enzi za uhai wao

Habari wakuu ujumbe huu nimeupata kutuko group moja nikaona ni vyema kushare wa Watanzania wenzangu Ili tuchukue tahadhari Inauma Sana

Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,

Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.

Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.

"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia.

Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee.

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia.

"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde 0 wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake

Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi.

Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi ikae nje ya jiko, mpira wa Gesi ndiyo uingie jikoni hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.

UPDATE JUNI 06, 2022: Binti pekee aliyekuwa amebaki Afariki dunia.
 
wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate
Mimi pia mwaka Jana niliwasha jiko la gas hizi za plate ili nipashe
Mboga,nikaweka sufuria la Mboga nikaenda sebuleni ile nafika tu nasikia mayowe jikoni Moto umefika kwenye Gypsum

Kuweni makini na Gas wakuu,ile yangu iliripuka yenyewe tu bahati nzuri Moto haufika mbali
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom