Msaada jamani nikila chakula nasikia njaa baada ya muda mfupi

sindesunde

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
358
346
Wajuzi nisiwachoshe nina tatizo limejitokeza toka mwezi wa 12 kwa siku naweza kula chakula ata mara 5-6 na bado ndani ya muda mfupi njaa inarudia! hili tatizo nahisi linataka kuniyumbisha kiuchumi maana maisha yenyewe ya kubaingaza sasa pesa inakatikia katika milo isio na idadi.

Naomba ushauri nifanye nini kuepukana na hii hali na kuna tiba ya kunisaidia
 
Wajuzi nisiwachoshe nina tatizo limejitokeza toka mwezi wa 12 kwa siku naweza kula chakula ata mara 5-6 na bado ndani ya muda mfupi njaa inarudia!hili tatizo naisi linataka kuniyumbisha kiuchumi maana maisha yenyewe ya kubaingaza sasa pesa inakatikia ktk milo isio na idadi.Naombe ushauri nifanye nini kuepukana na hii hali na kuna tiba ya kunisaidi
Huwa unakula chakula gani mkuu?

Kula ugali wa dona na njugu wiki mojamfululizo,
Kuanzia asubuhi unapiga nusu kilo,
Mchana nusu kilo,
Na usiku nusu kilo.

Lazima uwe vizuri ndani ya wiki tu!!

!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafta kitu kinaitwa "albendazol"

Hakikisha alfajiri kabla hujapiga mswaki unamumunya vidonge viwili. Ukishatumia dose 1 urudi kuleta feedback baada ya siku 3.
Dah! itabidi leo ninunue kesho mapema nianze doz maana
 
Kazi unazofanya kwa siku pia zinaweza changia ulaji huo,pia kacheck minyoo.
 
Mara ya mwisho kunywa dawa ya minyoo ni lini?
Wajuzi nisiwachoshe nina tatizo limejitokeza toka mwezi wa 12 kwa siku naweza kula chakula ata mara 5-6 na bado ndani ya muda mfupi njaa inarudia! hili tatizo nahisi linataka kuniyumbisha kiuchumi maana maisha yenyewe ya kubaingaza sasa pesa inakatikia katika milo isio na idadi.

Naomba ushauri nifanye nini kuepukana na hii hali na kuna tiba ya kunisaidia

Jr
 
Mkuu nakula sana si unajua life letu la MERU huku ugali napiga wa kutosha na dagaa wa nyumba ya mungu/au kutika babati ila nikikuambia mpaka hapa nishakula mara 3 kwa leo uoni ni balaa hilo chalii angu
Uko yente dingii. Mimi tokea jana sijagusa kitu nipo nawaza niende kwanani angalau wanipe hata nguna nile.
 
Wajuzi nisiwachoshe nina tatizo limejitokeza toka mwezi wa 12 kwa siku naweza kula chakula ata mara 5-6 na bado ndani ya muda mfupi njaa inarudia! hili tatizo nahisi linataka kuniyumbisha kiuchumi maana maisha yenyewe ya kubaingaza sasa pesa inakatikia katika milo isio na idadi.

Naomba ushauri nifanye nini kuepukana na hii hali na kuna tiba ya kunisaidia
Pole sana.
Uzito wako ni kilo ngapi? Urefu wako?
Umepungua sana uzito siku za karibuni?
Una umri wa miaka mingapi?
Unafanya shughuli gani?
Unakunywa sana maji? (Kusikia kiu mara kwa mara)
Unapata hali ya kukojoa mara kwa mara?, (hasa wakati wa usiku?)
 
Unaweza kuwa na minyoo au km una dalili hizo nyingine huenda n Sukari haipo balanced heb fika hospitali haraka kama ni sukari ni mbaya ukichelewa madhara huwa zaidi ya hapo
 
Pole sana.
Uzito wako ni kilo ngapi? Urefu wako?
Umepungua sana uzito siku za karibuni?
Una umri wa miaka mingapi?
Unafanya shughuli gani?
Unakunywa sana maji? (Kusikia kiu mara kwa mara)
Unapata hali ya kukojoa mara kwa mara?, (hasa wakati wa usiku?)
Uzito-68
Umri-38
Shughuli-muda mwingi nakua kibaruani ila cha kukaa ktk kiti kwa muda mwingi
Maji-mpaka sasa nashapiga lita 4 na ushee nasikia kiu kilawakati ikimbatana na njaa kali
Kukojoa-usiku sio sana mara 2 azidi hapo mkuu
 
Nenda kwa daktari haraka, wakati mwingine huwa tunachukulia vitu poa kumbe Kuna Tatizo. Dalili zingine ni zipi? Mwili unachoka Sana? Una kunywa maji mengi? Choo unapata vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nitafanyia kazi ushauri wenu maana mpaka sasa nishapiga msosi mara 3 maji nikimaliiza hii chupa inakua lita 6 sasa achiliambali ugonjwa lkn napata hasara inafikia wakati inabidi msosi uwe ktk hotpot ili ktkt ya usiku wa manane nipige ndio nitoboe asubuhi vizuri!
 
Back
Top Bottom