Msaada - Gari yangu inakula sana mafuta

Msaada - Gari yangu inakula sana mafuta

Polisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
2,082
Reaction score
643
Yaani nadhani kati ya km nne au tano kwa lita moja. Wafundi wanasema nibadilishe nozzle niweke za tundu mbili maana zilizopo ni nne. Je itasaidia?
 
Mmh, wee sasa unataka kuharibu gari
Kama vipi vits au starlet inakuhusu
 
Mmh, wee sasa unataka kuharibu gari
Kama vipi vits au starlet inakuhusu

Hilo ni suluhisho la muda mrefu (longterm plan),mimi nataka suluhisho la muda mfupi (short term plan)
 
Anyway, siamini kama naweza badilisha koromeo la mtu miss wa urembo nikamwekea mbeba vyuma vizito eti ili ale chakula kidogo na ikafanikiwa, bora kama angekuwa naumwa unaokoa maisha, ila unabadili bure bure tu? Kuogopa gharama ya mafuta?

Warning: Mie sio dokta wala fundi gari, natumia Phd ya uraiani tu

Hilo ni suluhisho la muda mrefu (longterm plan),mimi nataka suluhisho la muda mfupi (short term plan)
 
Gari yako ni aina gani, capacity ya engine ni ipi?
 
Kuwa wider,gar aina gan,kabla ilikuaje,umeshawai fanyia overwhole?thn rud upate ushaur mkuu.
 
Ni gari aina gani!?? na ukubwa wa injini pia, kuna gari hicho kiwango cha mtoto..
 
Cheki plug kwa petrol na pump/nozzle kwa diesel, piaweka air cleaner mpya genuine....otherwise gari chakula chake kikuu mafuta....lazima ile ili itembee ... au fuata ushauri wa bujibuji...isilimishe....
 
Anyway, siamini kama naweza badilisha koromeo la mtu miss wa urembo nikamwekea mbeba vyuma vizito eti ili ale chakula kidogo na ikafanikiwa, bora kama angekuwa naumwa unaokoa maisha, ila unabadili bure bure tu? Kuogopa gharama ya mafuta?

Warning: Mie sio dokta wala fundi gari, natumia Phd ya uraiani tu

I like your comments hapa jamvini Kongosho. Thanks. Natumia mchina, ningelaiki hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Yaani nadhani kati ya km nne au tano kwa lita moja. Wafundi wanasema nibadilishe nozzle niweke za tundu mbili maana zilizopo ni nne. Je itasaidia?

Mkuu, toa information kamili ili upate msaada. Wataalam wapo.

1. Gari gani
2. Ya mwaka gani
3. Size ya Engine
4. Diesel, Petrol au Mafuta ya Korosho
5. Automatic of Manual Transimmission

Ukianzia hapo msaada utapatikana mkuu.
 
Shift to bajaj haiumizi kichwa,hakuna haja ya AC, foleni haikuhusu etc
 
fanya hivi ijaze full tanki alafu sukuma hadi nyumbani kwako, lipaki kwenye banda lake kama lipo , usiwashe engine hata siku1 ww washa taa tu na redio piga honi kila kitu alfu angalia kama litakula hayo mafuta
 
Yaani nadhani kati ya km nne au tano kwa lita moja. Wafundi wanasema nibadilishe nozzle niweke za tundu mbili maana zilizopo ni nne. Je itasaidia?

Hujasema ni gari gani usikute unatumia FORD EXPLORER cc 4500
 
Yaani nadhani kati ya km nne au tano kwa lita moja. Wafundi wanasema nibadilishe nozzle niweke za tundu mbili maana zilizopo ni nne. Je itasaidia?

Ni gari ya aina gani? Maana naona umekuja nusu!
 
Back
Top Bottom