Msaada, Email Hijacked! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada, Email Hijacked!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Hume, Dec 4, 2008.

 1. H

  Hume JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Bosi wangu mmoja hivi majuzi alipokea email ikimwambia kuwa kutokana na marekebisho anuai yanayofanywa kwenye account za yahoo katika kuboresha huduma, wanamtaka atoe password yake ili asije akapoteza data za kwenye account yake.

  Bila kufikiria sana akatuma passord hiyo, walichokifanya hao jamaa ni kubadiri password na information zote za account ambazo zingemsaidia kuretreive account yake, kisha wakaanza kutuma email kwa contacts zake AKISEMA ALISAFIRI KWENDA NIJERIA, ILA MIZIGO YAKE YOTE KAISAHAU KWENYE TAXI HIVYO ANAOMBA ATUMIWE HELA USD 2500 ILI AKATE TIKETI YA KURUDI NYUMBANI, AKIAHIDI KUZIRUDISHA MARA ARUDIPO.

  Tatizo kubwa zaidi ni kuwa bosi wangu huyu ambaye ni profesa ana taarifa zake muhimu mno kwenye account hiyo, alijaribu hata kupiga simu kwa yahoo wenyewe ili wamsaidie kurecover document zake ila alikuwa bado kuwapata, hivyo hadi sasa bado anazihangaikia.

  Kwa yeyote anayeweza kusaidia, au mwenye wazo la namna ya kumsaidia huyu NAOMBA MNISAIDIE JAMANI!!!!
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Dec 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Watu wa kwanza kukusaidia katika hilo ni yahoo wenyewe hakuna mwingine mwenye mamlaka ya kutoa huduma hiyo ni kuvunja sheria
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hume

  umejaribu option ya forgot your password? Kama unakumbuka secret question na answer, na huku ukiomba Mungu kuwa hao hijackers hawajaibadilisha, labda unaweza fanikiwa. Vinginevyo ndio hivyo tena, hangaika na yahoo wenyewe.
   
 4. H

  Hume JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Washabadilisha information zote, alijaribu ikaoneka information zote, kama birthday, secret question vyote vishabadirishwa.


  Yuko radhi hata kuwalipa yahoo kwa huduma hiyo lakini ndohivyo mawasiliano bado hayajakaa sawa!

  Nilijaribu kuwasiliana na hao hackers kiupole hata hawarespond!
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ndio basi tena hiyo, there is no way to get back in, yahoo will not help you. Best thing to do is create another account and e-mail all your friends to let them know what happened so they don't start sending money to Nigeria.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Iliwahi kunitokea na mimi pia.
  Siku hiyo hiyo usiku nikapigiwa na mtu wangu toka Marekani simu akitaka uhakika kama ni kweli nimekwama Nigeria, na aliponipata akaniambia stori nzima. Asubuhi nilikuta wamebadilisha password kweli kwa hiyo ikaniwia vigumu kuingia. Na walikuwa wamemtumia barua hiyo kila mtu kwenye address book yangu ( About 70 )
  Kesho yake asubuhi Nikaenda kwenye option ya forgotten password, nikaletewa swali nijibu jibu lile la siri ambalo kwa kweli sio rahisi wao kulibadilisha, maana hakuna anayeweza kulijua ila mimi. Wao wanachoweza kufanya ni kubadilisha password kwa njia za kawaida tu. Lakini lile swali huwa halibadilishwi kwa namna yoyote ile.
  Nilipolijibu nikaruhusiwa kubadilisha password yangu na nikarudi kwenye account yangu tena.
  Hivyo kama bado anakumbuka jibu la swali la siri njia ni hiyo tu, la sivyo kama alifanya bila ku mean na hakumbuki, hapo ameshaliwa, si rahisi kuingia tena. Atakuwa ameumia. Na aangalie wasije kuwatapeli watu wake.
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Jibu lile linabadilishika, wewe ulibahatika tu, labda alikua learner huyo mwizi kwa kawaida kitu cha kwanza wanachofanya ni kubadilisha hizo information ili usiweze kubadili password.
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama washabadilisha kila kitu wasusie tu email, tatizo kama kuna data muhimu humo ndani na hakuna sehemu nyingine za kuzipata.

  Mimi kila siku napiga kelele Ikulu yetu pamoja na polisi wakubwa wote kutumia hizi free web based emails, watu wengine wanaona ni kitu kidogo.

  Tatizo hata Yahoo itakuwa si rahisi kuverify chochote hata kama wakitaka, na kwa vile hii ni service ya bure (well, tunauza attention yetu kwenye ads) sidhani kama wana muda wa kusikiliza issues kama hizi, especially kutoka Africa.

  Kilichobaki Prof. atoe mawasiliano kwa ndugu jamaa na marafiki wote kuwa kaibiwa email na wakipata email kutoka ile address ya zamani wasizitambue.

  Kila mtu na nyanja yake, yaani Professor mzima wamemchezea kama mshamba fulani hivi.
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu muulizaji wa swali nazidi kukusisitizia wafuate yahoo wao ndio wasaidizi wao wa kwanza na wamwisho kisheria hakuna mtu wowote wala kampuni inayotakiwa kuingilia makubaliano yako na yahoo unapotumia huduma yao mwingine akiingia na kukufungulia maana yake anavunja sheria na pengine anaweza kuwekwa kundi moja na wahalifu wengine wote wa masuala ya mtandao
   
 10. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Duh Prof anaingizwa mjini kilaini hivyo
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hume,
  Kama alivyosisitiza Shy, unahitajika kuripoti yahoo mapema iwezekanavyo. Kwa njia ya simu sio rahisi sana kupata msaada.

  Naamini wanayo mikakati ya kukabiliana na tatizo la email hijacking. Napendekeza uanzie hapa,
  Yahoo! Customer Care
  That statement is not entirely correct. For security reasons, you can't easily just change everything on someone's email account. Prof. alipofanya registration ya hiyo account alihitajika kuweka "alternate email address". Ili hijackers waweze kuibadilisha hiyo, lazima wajue password ya kuingia kwenye hiyo "alternate email address". Maana katika process ya kuibadili, a verification link will be sent to it.

  Kuna uwezekano ukatumiwa password mpya kwenye hiyo "alternate email address". Yahoo system automated process can easily do this without human intervention, so calling them by phone may not be necessary.
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  To reset your yahoo password,
  (NOTE: The new password will be send to your "alternate email address"
  Kama anaikumbuka na anaweza ku-login, hii itamsaidia)

  We'll help you sign in to Yahoo!
   
 13. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sure, but it is not that easy for hijackers to do that.
  To change the secret question and or answer, they'll need to verify the answer to the current Secret Question.  .
   
 14. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Mkuu, siku ya kufa nyani miti yote huteleza...
   
 15. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa sababu yeye prof alishawatumia password then wale jamaa wana full control ya account yake, watabadirisha kila kitu kama wapendavyo, ni sawa na wewe unapotaka kubadiri info kwenye account yako.
  Kuhusu Alt email hiyo inafanya kazi pale tu ukisahau account password yake, kama jamaa wamebadirisha info ya account hiyo alter email haisaidii kitu chochote.
  Pia yahoo kukusaidia itakuwa ngumu kwani hawatajua nani ni mkweli Je ni wewe au wale waliyo na account yakko....
  Nimeisha wahi kuwaomba hotmail kuretrieve password yangu wakakataa wakanambia wata-block ila ni sign up account mpya....
   
 16. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 17. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 18. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijui kama unafahamu kinachofanyika unapotaka request thru forgot password? Kwa kifupi system ita-display swali au maswali yale ulilyojaza ulipokuwa una-sign up hiyo account, then system inalinganisha na majibu ya maswali yaliyopo(currently) kwenye account hiyo, yakifanana inatuma reset kwenye alter address uliyo-supply wakati ule....

  Issue yenyewe ni kwamba jamaa wameingia kwenye account ya prof na kufanya changes kwenye account na majibu ya maswali if possible kwani wana full-access. kwa hiyo password reset haita work!!!
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  No you don't, if you have the password you can change whatever you want.
   
 20. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mwanjelwa and Kang, you should prove me wrong then. Fanyeni hilo zoezi, na ikidhihirika kuna mahali nimetoa information isiyo sahihi, nitaisahihisha kwa faida ya members wengine. It is not a good thing to do some guess work, isn't that so?
   
Loading...