Msaada: Anayejua gharama za mashine za kupandia mahindi na mahali zinapopatika Dar es Salaam

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,170
11,572
Salamu,
Wapendwa nahitaji kujua mashine ya kupandia mahindi zinapopatikana na gaharama yake.

Nipo Dar es salamu muda huu. Nia na madhumuni yangu ni kuepuka hasara kubwa niliyoipata mawaka huu wa kilimo baada ya kupata mavuno duni sana, kutokana na mtindo wa kurusha mbegu huku nalifukuza trekta kwa nyuma likiwa linalima.

Kwa ekari kumi nilitumie kurusha zaidi ya nusu gunia na nikaambulia gunia 8 tu baada ya mavuno.

Nimeskia kuna mashine za kupandia, nimeshauriwa nikipata hiyo nitapata ahueni ya kupoteza mbegu nyingi lakini pia nitafaidika na upandaji wenye nafasi utakaochochea mazao yangu kukua na kukomaa vizuri na hatimae kupata mavuno yenye tija.

Asante sana kwa ushauri, maoni na msaada wako in advance.
 
kuna mashine niliiona arusha tfa imetengenezwa sido bei ilikua 850,000tshs mwezi wa 7 mwaka huu. Labda jaribu sido na veta huko uliko
 
Mashine hizo zipo za ukubwa tofauti. Zipo zile ndogo kabisa. Ambayo bei haizidi laki 2 na zipo kubwa ambazo bei inaanzia si chini ya milioni 6 na kuendelea
 
0692 43 02 63. Piga namba hizo, wapo Dar wanauza mashine ndogo za kupandia mazao
Asant sana ndugu nimewachek hawa jamaa, wamenisaidia sana wamenipa location walipo pale wazo hili tegeta, so, soon nitainyaka iyo mashine na hatimae nikatusue kwenye Kilimo mwaka ujao wa kilimo 2024.
Asant kwa mdau mwingine alie nielekeza chimbo lingine la vifaa vya kilimo ikiwa ni pamoja na ninachohitaji apo kigamboni asant kwa picha na ungwana.
Shukran nyute kilimo family.
 
Hakikisha kabla hujanunua hiyo mashine uwaelekeze namna ambavyo una andaa shamba lako kabla ya kupanda, ili wakushauri mashine ipi itakufaa. Hili ni la muhimu sana.
 
Salamu,
Wapendwa nahitaji kujua mashine ya kupandia mahindi zinapopatikana na gaharama yake.

Nipo Dar es salamu muda huu. Nia na madhumuni yangu ni kuepuka hasara kubwa niliyoipata mawaka huu wa kilimo baada ya kupata mavuno duni sana, kutokana na mtindo wa kurusha mbegu huku nalifukuza trekta kwa nyuma likiwa linalima.

Kwa ekari kumi nilitumie kurusha zaidi ya nusu gunia na nikaambulia gunia 8 tu baada ya mavuno.

Nimeskia kuna mashine za kupandia, nimeshauriwa nikipata hiyo nitapata ahueni ya kupoteza mbegu nyingi lakini pia nitafaidika na upandaji wenye nafasi utakaochochea mazao yangu kukua na kukomaa vizuri na hatimae kupata mavuno yenye tija.

Asante sana kwa ushauri, maoni na msaada wako in advance.
nichek Pm
 
mkuu pia unapaswa kufahamu kupata mavuno mengi sio tu aina ya upandaji, pia mbegu bora, kuweka mbolea, upigaji wa dawa n.k
 
Hakikisha kabla hujanunua hiyo mashine uwaelekeze namna ambavyo una andaa shamba lako kabla ya kupanda, ili wakushauri mashine ipi itakufaa. Hili ni la muhimu sana.
unachosema ni sahihi kabisa, kwa asilimia kubwa hizi mashine hasa za kichina tunazoziona mitandaoni hazifanyi kazi vzr kwny aina ya mashamba tunayoyaandaa sbb tunalima alafu hatulainishi udongo vzr tuna acha maudongo makubwa makubwa hivyo mashine ushindwa kufanyakzi vzr kadri ilivyokusudiwa
 
Mkuu Tlaatlaah kama hutojali unaweza kutupa mrejesho wa mashine,
Natamani kujua aina ya mashine ulionunua, bei ulionunulia, pia kama imefanya kazi vizuri shambani kwako.
Asante
 
Nakushauri nenda wizara/idara ya kilimo iliyo karibu na shambani kwako, kuna mashine aina nyingi za kisasa zinatolewa kwa mkopo nafuu pia kuna wataalam wa kutosha, ukabadiiishane nao mawazo.

Au wapigie namba hizi: +255 733 800 200
 
Back
Top Bottom