Mrithi wa REGIA ni Cecilia Paresso

Mrithi wa REGIA ni Cecilia Paresso

wakuu heshima kwenu sana.
taarifa za uhakika nilizozipata ni kwamba mrithi wa Rejia anatoka karatu anaitwa Cecilia Pareso.nampongeza sana mpambanaji mpya.

mwenye CV Yake aimwage hapa tafadhali.

Aliingia lini CDM? Mchango wake wa hali na mali ni upi? Mwaka 2010 aligombea Ubunge jimbo gani na kushindwa?
 
Hapa JF naona imekuwa kama soko la Kariakoo, maneno ni mengi wala hatusikilizani, tena kuna watu kwa makusudi kabisa wameamua kuweka watu kupindisha mada!!!!!!! Wengi wana post si zaidi ya 100 naona kabisa wako kazini, poleni saana JF ni watu makini mtachoka wenyewe!!!!!!!!!!
 
sheria za uchaguzi na uteuzi wa wabunge wa viti maalum unazifahamu? waombe wajf hapa watakupa nadhani utaridhika. Kwa kifupi tume ya uchaguzi ndiyo inapendekeza jina , linapelekwa ktk chama husika kupewa baraka.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubunge wa viti maalum, ndiye atakayemrithi marehemu Regia Mtema, aliyefariki dunia wiki iliyopita. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema hayo alipotakiwa na NIPASHE kutoa ufafanuzi kuhusu nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha marehemu Regia.
Habari zilizopatikana kutoka makao makuu ya Chadema, zinaeleza kuwa mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Nec, mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubunge wa viti maalum, ni Cecilia Daniel Pareso.
Cecilia ni Diwani wa Kata ya Qurus, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Habari nyingine zinaeleza kuwa awali, mwanamke aliyekuwa akishika nafasi ya 26 ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Leticia Mosore, ambaye baadaye alihamia chama cha NCCR-Mageuzi.
Dk. Slaa alisema utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti upo wazi kwa mujibu wa sheria na kwamba Chadema hawana mamlaka ya kuongeza wala kupunguza kitu chochote.
Alisema Chadema imeishamuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumuarifa rasmi kwamba kuna nafasi iliyo wazi, ambapo naye ataiandikia barua Nec kwa ajili ya kufanya uteuzi rasmi.
Dk. Slaa alisema kuwa kama kutakuwa na mabadiliko ya mtu aliyeshika nafasi hiyo ya 26, ikiwamo mtu huyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge kwa kuhama chama ama kuonekana na upungufu mwingine ambao unamnyima sifa, Chadema itaiandikia barua Nec ili achukuliwe mtu mwingine aliyeshika nafasi ya 27.
Alisema kama namba 26 na 27 wote hawatakuwa na sifa, Nec itachukua jina litakalofuata namba 28 ili kufanya uteuzi wa kiti hicho.
“Sisi kwa hili tulishalimaliza mwaka 2010 na tunachoweza kufanya kwa Nec ni kuisaidia itakapotaka maelezo yetu juu ya jina linalotakiwa kufanyiwa uteuzi,” alisema Dk. Slaa.
Alisema mwaka 2010 walifanya kazi kubwa na kupata majina 102 ambayo yote yana sifa za kuwa wabunge wa viti maalum na kwamba, Nec ndiyo yenye mamlaka yote ya mwisho na sio Chadema.
Chadema kina wabunge wa viti maalum 25 katika Bunge la 10.
SOURCE: NIPASHE
 
Wanazidi kutudhihirishia kuwa hiki chama ni cha watu wa KASKAZINI!!!

Bora umesema wewe Paresso, ningesema mimi wangesema ooh
Kanda ya ziwa tuna wivu!! Sasa hapo ni ubunge tu, ukawambia waunde
serikali, kwa maana ya Baraza la Mawaziri itakuwaje? Aibu! hadi mabeck 3
wataukwaa alimradi watoka kaskazini! AIBU!
 
Hapa napo kuna ujinga na ushabiki mwingi huyu cecilia aligombea na wanawake wote tanzania wa chadema kisha majina yote wa kwanza hadi wa mwisho yakapelekwa tume ya uchaguzi sasa tume wanafuata ile list na wala chama hakiulizwi wala kuhusika.kwanza kama kuna habari ya upendeleo au ukaskazini kati ya watu 25 vipi akose 2010?pili nani alijua kwamba kamanda regia angepata ajari na kufariki?tatu kama wanawake wa chadema walimchagua kwa kura ulitaka nani aondoe jina lake?nne mbona unaanza na ubaya je akiwa mwenye hoja kama regia utabadili msimamo?think big!
 
Sheria za kutafuta viti maalum zipo wazi ndani ya Chadema,sasa wewe unataka kuleta mada ya kijinga isiyokuwa na kichwa na miguu.
 
duh jamani wangependekeza kutoka jimbo la regia bila hivyo magamba yatatamba kwani aliyekuwa huko kutoka cdm ni ovyo
 
chademaaa! chademaaa, peoples power,
Tanzania ,tanzaniaaa! Peoples power
Twendee! Twendeeee! Peoples power*2
 
Mh...hongerakamanda;Lakini Dr,hivi wana CHADEMA Ifakara hawapo?
Ni vema kujiepusha na lawama toka kwa magamba kwa kuhakikisha si tu haki inatendeka,bali inaonekana kuwa imetendeka

Ulitaka atoke Ifakara?
Umeelewa taratibu za kuchagua wabunge wa viti maalum? Mh.R.Mtema (R.I.P) hakutoka jimboni.Haki inaonekana kutendeka pale utaratibu unapofuatwa badala ya kutafuta umaarufu na sympathy peke yake.Ingekuwa tunataka kufuata matamanio tu bila taratibu, basi hoja yako ya Ifakara ingekuwa na mashiko mkuu wangu.
 
Hapa ndipo CDM walipokosea....ingebidi mrithi wake atoke angalau Morogoro. Hawajawatendea kabisa haki wale vijana wote waliotumia nguvu zao siku ya msiba wa Regia kule Ifakara.

Rejao huwa nakuona una busara sana pamoja na ushabiki wako wa vyama, lakini hapa umeniangusha sana.Ubunge huu haugaiwi kama pipi.Kuna mchakato na taratibu zake.Ingekuwa hamna taratibu, basi matamanio yako ya kuwapa kifuta machozi wana Ifakara yangefikiwa mara moja kwa vile hakuna asiyekuwa na hisia kali linapokuja suala la marehemu Regia.
 
Aisee kweli wewe mama porojo.nami nakubatiza jina lingine kuanzía leo utaitwa mama chaumbea.
Hiyo list ilipatikanaje? Hapa si ndipo pale ilipotumika model ya dr. na kutupilia mbali matokea ya uchaguzi?
 
Nafasi hii kapewa naye Dr aingize wake baada ya mkewe.

Kwani Mh Ndesamburo amepewa nafasi ya Mtoto na Mkwe.
Mh mgombea urais wa Znz kupitia Chadema ametoa mtoto wa Dada yake.
Tindu lisu ametoa dada yake.
Padre Slaa ametoa mke na labda huyu mrithi wa Regia.

Mh Alfi -- hajapewa
Mh Zitto -- hajapewa.

Je kunani hapo? Dini au shares hazikutosha kwa Zitto na Alfi kupewa nafasi nao waweke wao?

ndio maaana tunasema viti maalum ni unafiki mtupu na upendeleo na ikhsani na fitna kubwa kwa jamii. mfikirie kuviondoa.
Mkuu ZZK alipewa ila akaamua kutoa nafasi kwa mtani wake toka huko Mara!
 
Magamba wana tabu kweli. Chief secretary mpya sio wa kaskazini? Mbona hamkulalamikia uteuzi wake?
Now mnampigia debe Deputy UN Gen. secretary eti kwa kuwa ni mwanamke apewe uraisi. Mmesahau kuwa na ni wa Kaskazini? Jamani Tuanze kufikiria kwa ubongo ili tusiupe usemi wa masaburi nguvu hapa jamvini.
 
Magamba wana tabu kweli. Chief secretary mpya sio wa kaskazini? Mbona hamkulalamikia uteuzi wake?
Now mnampigia debe Deputy UN Gen. secretary eti kwa kuwa ni mwanamke apewe uraisi. Mmesahau kuwa na ni wa Kaskazini? Jamani Tuanze kufikiria kwa ubongo ili tusiupe usemi wa masaburi nguvu hapa jamvini.
 
Ulitaka atoke Ifakara?
Umeelewa taratibu za kuchagua wabunge wa viti maalum? Mh.R.Mtema (R.I.P) hakutoka jimboni.Haki inaonekana kutendeka pale utaratibu unapofuatwa badala ya kutafuta umaarufu na sympathy peke yake.Ingekuwa tunataka kufuata matamanio tu bila taratibu, basi hoja yako ya Ifakara ingekuwa na mashiko mkuu wangu.

Thanks mkuu;ni kweli sikuwa nikielewa vizuri taratibu za kuchagua wabunge wa viti maalumu;ila baada ya kupitia hii thread,imenisukuma kutafuta na kuelewa!
Thanks!!!!
 
Msione CDM imefikia hapa,kuna wanachama na baadhi ya maeneo hapa nchini wamepigana vita kubwa wkt wengine wakiwa pembeni wakijinasbu kama wafuasi watiifu wa CCM. Sasa mambo yamekuwa mazuri mnaanza kutaka kuvuna ambacho hamkupanda.
 
umetaja watano tu,angali hapa sasa,
mambo ya nje Benard membe
Uwekezaji-maria Nagu
Biashara-Cyril chmi
Mifugo-David Mathayo
Nishati na Madini-wilium Ngeleja
Utalii-Ezekiel
Maji-Markson mwandosya
michezo-Emmanuel ..............................................................nk nk nk.mnaulizana dini na ukabila mnataka kutambika?

Mkuu tunaongelea Wizara Muhimu siyo Wizara zote. Ukishajaza watu wako kwenye Wizara Muhimu tano za Nchi inatosha. Zilizobaki zitakuwa zinaitikia ndiyo Mzee! Kampige Dk Slaa, Ndiyo Mzee! Fungia MwanaHalisi! Ndiyo Mzee! Chagua Muislamu, Ndiyo Mzee! Iba kura Igunga, Ndiyo Mzee! Nk.

 
Back
Top Bottom