u mean
Viti Maalumu vya Wabunge Wanawake
[TABLE="align: right"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kulingana na Ibara Na. 66 na 78 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Vyama vya Siasa vitapendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina ya wanawake ambao Tume inaweza kuwatangaza kuwa Wabunge kama ikiridhika kwamba wana sifa zinazostahili.
Tume inatakiwa kutangaza majina ya wanawake kwa idadi isiyopungua asilimia 30 ya Wabunge wote kwa ajili ya viti maalumu kwa wanawake. Mgawanyo huo utazingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Bunge. Endapo mgombea ubunge amepita bila kupingwa, kura za mgombea Urais wa chama cha mbunge zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge huyo. Kama hakina mgombea Urais, asilimia 51 ya idadi ya wapiga kura walioandikishwa zitachukuliwa kuwa ndizo kura halali za mbunge wa chama husika. Hata hivyo, chama kinaweza kupata nafasi ya viti maalumu cha mbunge mwanamke endapo kimepata 5% ya kura zote halali za uchaguzi wa wabunge.
Ili kutekeleza hilo hapo juu, Vyama vya Siasa vina wajibu wa:
- Kupendekeza majina ya wanawake kwa idadi itakayopendekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulingana na Ibara ya 66(1b) na Ibara ya 78 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa mpangilio wa upendeleo (preference) na kuituma Tume siku 30 kabla ya Uchaguzi.
- Kuhakikisha kwamba wanaopendekezwa wanajaza Fomu za Uteuzi
Dokezo: Kujaza Fomu za Uteuzi
Wanawake watakaopendekezwa hawatakiwi kuweka dhamana ya shilingi Elfu Hamsini (50,000/=).
Viti Maalumu vya Madiwani Wanawake
Viti maalumu kwa upande wa madiwani, vinapatikana kutoka kwa kila chama kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya viti ambavyo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Madiwani katika Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya.
Viti hivyo ni theluthi moja ya jumla ya madiwani wa kuchaguliwa na wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi katika eneo husika.
Ili kutekeleza hayo:
- Vyama vipendekeze majina ya wanawake ambao watakuwa ni theluthi moja ya jumla ya madiwani wote wanaowakilisha kata na wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi. Orodha ya majina hayo ipelekwe siku 30 kabla ya siku ya upigaji kura.
- Vyama vya Siasa vihakikishe kwamba vinapendekeza wanawake wenye sifa za kuwa Madiwani
- Wanawake wa viti maalumu vya Madiwani wanaopendekezwa na vyama vya Siasa wanajaza Fomu za Uteuzi
- Wanawake hawatakiwi kuweka dhamana ya Shilingi Elfu tano (5,000/=).