beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema Tanzania ina 'Double Standard' ambapo kuna baadhi ya maeneo maamuzi yanafanyika haraka, yapo ambayo maamuzi yanafanyika kwa kuangalia maslahi mapana ya Nchi na mengine maamuzi yanachelewa
Vilevile akiwa Bungeni leo wakati wa majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge huyo amesema licha ya dhamira ya Urasimishaji kuwa nzuri, zoezi hilo ni 'kichefuchefu'. Ameeleza, mambo hayo hayatoi sura nzuri kwa Serikali na suala la urasimishaji litapunguza umaarufu alionao Waziri William Lukuvi kwa Wananchi licha ya kwamba anafanya kazi kwa weledi na watendaji wake wanaendana na kasi yake