aseenga
Senior Member
- Jul 13, 2011
- 106
- 86
Kwa siku kadhaa zilizopita, tumemshuhudia mheshimiwa mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akichangia hoja bungeni. Hoja zake zimeibua hisia tofauti kati ya wengi kutokana na sababu mbalimbali.
Moja ya sababu hizo inaonekana ni mabadiliko ya ghafla ya mtazamo wake kiutendaji kabla na baada ya kuwa mbunge. Kama mkuu wa mkoa mstaafu, wengi wanadhani na wana haki ya kudhani kwamba alikuwa sehemu ya utekelezaji wa dhuluma mbalimbali walizofanyiwa watu waliokuwa katika himaya ya utawala wake. Hii ni kwa sababu yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Swali la kujiuliza kati ya maswali mengi ni, je mtazamo huu wa kwamba Gambo alikuwa sehemu ya udhalimu ni sahihi au sio sahihi? Maswali mengine muhimu ni, Je Gambo anapotoa hoja Bungeni, hoja zake zipuuzwe au zifanyiwe kazi? Je ni haki kumuandama Gambo kwa mchango wake kama mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Arusha mjini?
Ni wazi kwamba, kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, mwajiri wake mkuu alikuwa serikali/Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama mbunge, yeye ni mwakilishi na msemaji wa wananchi anaowawakilisha bungeni. Je aache kusema madhambi kwa sababu ataonekana kigeugeu? au aseme madhambi na uonevu uliotekelezwa na “Task force” ili aokoe jahazi la roho yake na wale ambao wameumizwa?
Nina imani kwamba Gambo ametafakari kwa kina hoja zake na ufunuo (revelations) wa yale ambayo yangepita kama ndwele. Lakini kuganga yajayo bila kufanyia kazi hoja zake, na kuandama nafsi yake bila ushahidi wa kutosha kwamba na yeye alikuwa mstari wa mbele kupora watu mali zao kwa sheria na kanuni kandamizi, itafanya watu wa Arusha na watanzania kwa ujumla tuendelee kushangaa kimetokea nini kwa Mrisho Gambo.
Kuungama au kutaja hadharani maovu ambayo mtu aliyafanya au alishiriki kuyafanya sio kitu kipya. Ipo mifano mingi tu hata katika vitabu vitakatifu. Mtakatifu Paulo awali aliitwa Sauli na alitesa watu wa Mungu. Baadaye, akapata wokovu na akawa Mtakatifu Paulo. Akaaza kuwa chombo chema na akaacha uovu wake.
Mtakatifu Augustino wa Hippo ni mfano mwingine. Baada ya kuishi maisha yasiyompendeza Mungu, alitubu hadharani akaandika kitabu cha The Confessions of Saint Augustine na akaongoka.
Ni imani yangu kwamba, Gambo hatoi hoja zake ili kuchochea taharuki kwa watu, wala hatoi hoja zake ili kukwepa maswali na uchunguzi kama ule wa viongozi wengine ambao unaendelea, bali ana nia ya dhati ya kuchangia katika kurekebisha hali ya haki na usawa katika jamii.
Ni wazi kwamba pale msalabani, mwizi aliyetubu kwa Yesu alipata msamaha na akaonja pepo haraka sana akilinganishwa na mwizi ambaye aliendelea kumtukana Yesu badala ya kuomba msamaha kwa makosa yake.
Hali kadhalika, mwana mpotevu aliporudi kwa baba yake na kutubu, alisamehewa haraka sana kuliko mwana mkubwa ambaye alijiona ana haki na hivyo hakupenda hata ndugu yake arudi nyumbani. Mwana huyo aliangalia mabaya ya kaka yake tu.
Kwa kusema hivi, sio kwamba namtuhumu Gambo kwa ubaya wowote, bali nampongeza kwa ushujaa anaouonesha licha ya changamoto ambazo atazipata kutoka kwa wengi ambao watamuona msaliti, mnafiki au kigeugeu. Nadhani sio haki kumtazama yeye kama sehemu ya uovu, bali kumtazama katika nafasi mbili za uongozi (ubunge na ukuu wa mkoa) ambazo kwa bahati mbaya zinafungamana sana.
Hoja na ujasiri wa Gambo pia ni dalili kwamba hata wale ambao walikuwa watiifu bila kutumia hulka zao na utashi wao binafsi, kuna wakati wanaangaziwa na mwanga wa ukweli na wanarudi kwenye mstari. Nionavyo mimi, mbunge Gambo ni wa kumpongeza, ni wa kumpa sikio letu ili atusaidie kujua mengi ambayo yeye kama mla kiapo cha utii kwa Rais, ameona awe muwazi na aweze kuliponya taifa.
Jambo la muhimu katika haya yote, ni kwamba Gambo ana kinga za kibunge na hivyo hatuwezi kumuadhibu nje ya Bunge kwa sababu anayotamka yana kinga za kibunge. Labda Bunge lenyewe liamue kinyume chake kwa mfano kumfukuza Bungeni ili akitoka nje ya Bunge serikali imshughulikie.
Je, kuna mbunge mwenye nia ya kusikiliza hoja za Gambo au wabunge wengi wanakimbilia kutoa taarifa na kuomba mwongozo ili Gambo ashindwe kuendelea kuongelea mambo ambayo yeye mwenyewe anayaita ‘ya maana’?
Je, kugonga meza bungeni wakati mbunge anatoa hoja, iwe hoja chanya au hasi, ni ishara kwamba Bunge litatoa maamuzi na mwelekeo kuhusu hoja, au ni sehemu ya ushereheshaji kama ambavyo tumeshuhudia katika mabunge mengine? Binafsi, napendekeza meza za Bungeni ziwe za chuma ili tupunguze milio ya wagonga meza, au ziwe za kioo, ili kuwe na tahadhari kati ya ushangiliaji hoja na uchangiaji hoja.!