ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,107
- 49,808
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15, 2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kufanyika kwa marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220 kwa kuongeza Ushuru wa Barabara na Mafuta kwa kiasi cha shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya Petroli na Dizeli.
“Aidha, inapendekezwa pia kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 4A cha Sheria ya Ushuru wa Barabara SURA, 220 kwa kuongeza kipengele ‘c’ kitakachoelekeza fedha zitakazokusanywa kutokana na ongezeko hili la ushuru wa barabara na mafuta la shilingi 100 kwa mafuta ya petroli na dizeli zitumike kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati iIi kupata vyanzo vya uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hatua hii inatarajia kuongeza Mapato ya Serikali kwa kiasi cha.."
-----
Nawakumbusha tuu kwamba Jerry Silaa alipendekeza tozo ya mafuta kwa Dar na bila shaka ndio hii hapa japo haijaelezwa kiundani ila hii itawahusi watu wa Dar.
Swali, kuna tozo ya mafuta ya Tsh. 100 ilianzishwa mwaka juzi, je, nini tofauti yake na hii?
My Take
Chonde chonde Serikali hii tozo mpya ya 100 ilipwe Dar Ili kuleta msawazo wa bei za mafuta na Mikoani.
Kama ikiwa ni kwa ajili ya Nchi nzima Wabunge kataeni.

Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam. Jerry Silaa amesema amesema...
www.jamiiforums.com