Mrembo aliyepotea

65.
“OOhh..!!, Onesmo na Sheray. ….”
Yule mlinzi akawakaribisha kwa lugha ya Kinyarwanda. Wakaongoza pamoja mpaka lango la kuingilia sebuleni na walivyofika tu getini Alice na Mama yake wakashangaa kufunguliwa na kijana mtanashati. Mwenye asili halisi ya kinyarwanda.
“Welcome to my world ”
“Murakoze databuja..!! (Asante bosi)”
Sheray na Onesmo wakaitikia kwa lugha ya kikwao yakinyarwanda. Mtoto wa rais, Aloyce ndiye aliokuwa amewafungulia lango la kuingilia sebuleni. Alikuwa ameshawaandaa wahudumu takribani ishirini. Kila mmoja akiwa ameshikilia kitu chake kuna waliokuwa wakiranda randa sebuleni huku wakizunguka na Aloyce mikononi mwao wakiwa na sahani zilizobeba pombe kali sambamba na glasi. Wengine wakiwa jikoni kwa kuandaa maakuli na baadhi wakimfuata Alice na Mama yake wakiwapepea japokuwa jumba la Aloyce lilizungukwa na viyoyozi vyenye kutoa harufu nzuri na ya kuvutia.
“Welcome miss Tanzania..!!”
Aloyce akaongea kwa tabasamu huku akimtolea macho Alice. Alice kwa uoga akajikuta anashika mapigo yake ya moyo huku akihoji kwa kutokujiamini.
“unaongea na mimi..??”
“Yes, its you mrembo angu. Mrembo nambari moja Tanzania. Na nionavyo you deserve to be the first one and ever in Africa and the whole world. Aboslute honesty wewe ni miss world wangu.. naitwa nani..?”
“Alice Majaliwa.”
Alice akajikuta anatoa tabasamu pana huku macho yake akiyalekeza kwa mama yake wa kufikia,Janet. Zile ndoto za kuishi maisha mazuri zikamteka Alice kwa haraka sana. Akajihisi kusisimka mwili wake mara kwa mara akiyatolea macho mazingira ya sebule. Moja kwa moja akajikuta moyo wake ukiafiki kuwa na Aloyce maishani mwake.
“How about Journey, Sheray..?? Mekuwaje huko..? firstly …..”
Aloyce akawageukia Onesmo na Sheray akawahoji juu ya safari yao.”
“ikuwa mzuri sana. Tumesafiri hakuna shida njjani. Shortly it was good…”
Sheray akamjibu Aloyce kwa ufupii na kiufasaha huku nayeye akichanganya kumjibu kwa lugha ya kiingereza.
“na huyu ni nani..? from Tanzania too..?”
“ni mama wa Alice. Inaitwa Janet. Ni muzuri tu na haina mineno. Tumeichukuwa iwe karibu na itoto yake Alice. Ifarijike..”
Aloyce akafurahi sana. Siku hiyo ikawa kama sherehe kubwa sana kwake. Akatamani sana baba yake angekuwepo lakini ikashindikana kutokana na safari za kikazi za baba yake Aloyce. Wakasherekea peke yao na wahudumu wake. Furaha ikatawala jumba lote. Onesmo na Sheray wakajiona wao ndio wanafuraha mara mbili jumba zima kuliko hata bosi wao Aloyce. Kwanza wakajiona wanafuraha ya kufanikisha zoezi zima la kumpata mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania na pili kitita cha mapesa walichohaidiwa na Aloyce. Wakasherekea kwa muda wa masaa matatu mfululizo huku kila mmoja akibadilishana mawazo kwa kuongea stori mbili tatu na mwenzake. Siri kubwa ya watu wanne juu ya yaliotokea huko Tanzania ikabaki moyoni mwao. Siri ya Alice kuua na pili siri ya Alice kupokwa ushindi na kuhairishwa kwa mashindano. Baada ya kushereke kwa masaa kadhaa, Aloyce akaelekea chumbani kwake na punde akarejea na sanduku dogo mkononi mwake. Akawaita Onesmo na Sheray wakaelekea mpaka nje wakajificha katika kona.
“Hii ni kwa ajili yenu.. nice job ……”
Akawakabidhi lile sanduku. Sanduku ambalo lilijazwa kwa pesa nyingi sana. Ikiwa ni kama sehemu ya makubaliano baada ya Aloyce kufikishiwa kitu ambacho alikitamani maishani mwake. Ndoto ya siku nyingi sana kwake. Akwakabidhi wakatokomea zao kisha Aloyce akarejea peke yake sebuleni. Kabla hajakaa chini akawa kama amekumbuka kitu akatoka tena nje kabisa kuwaita Onesmo na Sheray.
“Mesema hakuna tatizo huko mtokako..? hakuna sumbufu yeyote..??”
“Yes boss..!!”
 
66.
Aloyce akaonesha tabasamu la furaha, akawakumbatia kila mmoja kisha akarejea tena sebuleni alipokuwa ameawaacha Alice na mama yake.
“Mama, Alice jiskie iko nyumbani. Sisi ni watu mema sana. Pana mabaya hapa. Mimi ndio toto ya Rais.. hapa nchini.”
Aloyce akaongea kwa kujiuma uma huku akimtazama muda wote Alice. Akavutiwa kwa jinsi alivyoumbika. Alivyopendeza kwa gauni lake refu na la heshima. Macho yake yalivyopambwa kwa kope ndefu za bandia. Akachanganyikiwa sana kutokana na kuona Alice alivyo tofauti na mabinti wa kinyarwanda ambao huwa hawatindi nyusi zao wala kubandika kope.
“Mama na Alice. Samahani ikuje inifuate kwa nyuma mimi.”
Alice na mama yake wakatii amri kutoka kwa Aloyce. Wakainuka nakumfuata Aloyce kwa nyuma. Wakaingia chumba cha kwanza.
“Mama hii ini spesho kwako. From now onwards. There is choo, bafu na kila kitu nayotaka katika hii chumba. Taka pika mwenyewe humu humu chumbani juu yako..”
Aloyce akamwelekeza Janet kila kona ya kile chumba. Kilikuwa chumba kikubwa sana kilichokamilika kwa kila kitu. Janet akaona kama nyumba mbili kwa vitu vilivyokuwa ndani yake lakini jibu lillikuwa pale pale kuwa kile ni chumba kama vyumba vingine. Baada ya kumuelekeza, Aloyce akamshika mkono Alice nakutoka naye kwenye kile chumba alichiokabidhiwa Janet.
“Kuanzia sasa wewe ni kama muke yangu. We are moving straight to our room and not my room..”
Kozi fupi fupi za kiingereza ambazo alikuwa ameshasomea Alice kabla hajashiriki kabisa mashindano ya urembo Chang’ombe na Tanzania kabisa ikamfanya aambulie maneno machache kutoka kwa Aloyce huku akiendelea kuongozana naye. Alice hakujua kuongea kiingereza kiufasaha lakini kutamka baadhi ya maneno wala haikumpa shida. Wakaongozana pamoja mpaka wakafika chumba cha Aloyce. Kufunguliwa tu mlango kukamfanya Alice ajione yu mbinguni. Akaona kama ni ndoto anayoiota. Akajitahidi kuiweka kwenye fikra za ukweli. Akazidi kuchanganyikiwa kwa jinsi chumba kilivyokuwa kimenadiwa kwa nakshi nakshi za kuvutia. Umaridadi wa kitanda kilichounganika na kabati la vipodozi lilimchanganya sana Alice.
“Hii nakununulia leo hii ipo hapo, ni yako..” utachagua the most suitable kwa kutumia wewe muke yangu. Penda sana wewe..”
“I love you too”
Ule uzalendo aliokuwa nao Alice ukamshinda. Akajikuta akitawaliwa na furaha ya ajabu. Furaha ambayo hakuwahi kuipata maishani mwake. Machozi ya furaha yakaanza kuchukua nafasi katika paji lake la uso, yakaanza kumlenga lenga. Akaamini hakuna duniani kama Mungu kwani ndiye kiongozi wa maisha yake. Akamshika mkono Aloyce.
“Najua ni Mungu tu ndiye kaniunganisha na wewe Aloyce. Sina budi kumshukuru kwa kunionesha wewe Aloyce. Nasema I love you honey..”
Aloyce akajihisi kusisimka kwa maneno matamu yaliokuwa yakitokea mdomoni mwa Alice. Uzalendo na yeye ukamshinda akajihisi maneno yale matamu yanapenya katika ngome za masikio yake huku yakiendelea kutoka mdomoni mwa Alice. Akajikuta ule mkono alioshikana na Aliceukimponyoka moja kwa moja nakukimbilia kiunoni mwa Alice. Alice naye akatoa mikono yake nakuhamishia mpaka mabegani mwa Aloyce. Hisia za ajabu zilizochanganyikana na furaha kati yao zikatawala. Wakajikuta kila mmoja kuwa na hisia kali kwa mwenzake. Alice hakuwahi kukumbatiwa na mwanaume maishani mwake zaidi ya baba yake wakufikia,John tena mara chache sana. Na hakuna mwanaume mwingine yeyote aliyejua joto la Alice akikumbatiwa maishani mwake. Joto hilo sasa akawa amemkabidhi rasmi John. Akalifurahia sana kupokea joto la Aloyce. Akatoa uso wa tabasamu taratibu huku akiendelea kumtizama aloyce. Aloyce naye akashindwa kabisa kuuacha moyo wake uvumilie. Moyo ukashinda uwezo na nguvu. Akauachia moyo umpeleke unavyotaka. Akajikuta anautoa mdomo wake na kuushikanisha na wa Alice. Wakaanza kupeana ndimi na Alice. Wakafurahia mioyoni mwao kila mmoja. Aloyce akazidi kupeana ndimi na Alice huku moyo wake ukimlazimisha kutamani kuvua gauni la Alice. Alice naye akalegea sana. Akawa tayari kuvuliwa gauni lake na Aloyce. Akasogezwa na kulala mpaka kwenye likitanda kubwa la Aloyce. Kwa pupa aliokuwa nayo na msukumo wa moyo wa Aloyce akajikuta akivua vishikizo vya shati lake nakulitupa kisha akaanza kuvua zipu ya suruali yake taratibu. Kitendo cha Aloyce kuvua zipu ya suruali yake kikaingia moja kwa moja katika fikra za Alice. Alice akaogopa sana. Mwili wake ukawa kama umemwagiwa maji ya baridi ghafla. Akajikuta ule msisimko aliokuwa nao unapotea baada ya kufananisha lile tukio la Aloyce kuvua zipu ya suruali yake. Akakumbuka kile kitendo cha baba yake kuvua zipu ya suruali na kumbaka mpaka kutolewa bikra yake.
“Noo..!!, Noo Aloyce. Noo usiendelee kuvua pliiz..??”
 
67.

“Kuki Alice..? Kuki..? Urakizi iringiro Alice..?? (Kwanini Alice..? Kwanini..? unajua nakuamini sana Alice) Pliiz nakuomba furaha yangu isipotee kwako coz its my first time kufanya hivi na mwanamke..”
Aloyce akajikuta akichanganya lugha tatu yakinyarwanda, kiingereza na Kiswahili kwa wakati mmoja. Mwili wake ulikuwa tayari kumkabidhi Alice.
“Aloyce..?? I trust you. But pliiz nashindwa kufanya kwa sasa. Am not ready nielewe pliiz, I promise you. Lets do it later. Pliiz nakupenda..”.

*********

Taarifa juu ya mapolisi kuhusika katika njama za kula rushwa na kuwaachia watuhumiwa wawii katika kesi ya mauaji iliokuwa ikiwakabili Alice na mama yake wa kufkia Janet ikawa imeshaingia baadhi masikioni mwa watu. Vyombo vyote vya habari hususani magazeti ya udaku Tanzania yakaripoti habari huku mengi yao yakiongezea mbwembwe na uongo ndani yake.
“Nchi yetu imejaa rushwa sana kila kona, ona sasa upuuzi waliofanya hata siku tatu hazijaisha..?”
Alihoji msoma magazeti mmojawapo ambaye alikuwa akitazama vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali ya siku hiyo.
“Rushwa..??, rushwa…?? rushwa kila pembe..?. Lini haki itakaa usawa wake?? Inabidi hawa polisi wawajibishwe..??”
“Kwanini nchi yetu tu..? kama hujasikia hao hao polisi wameachiwa, basi utasikia mara ohh watafunguliwa kesi mahakamani, wala rushwa wakubwa..!!”
Wakaendelea kujibizana sana kuhusiana na habari ile ya kutoroshwa kwa Alice na Janet. Haikujulikana haswa walipotokomea zaidi ya madai ya kutoroshwa kupamba vichwa vya habari vya magazeti yote.
John Mapunda, mratibu mmoja wapo wa mashindano mwenye nyadhifa kubwa na pia ndiye mume wa Janet mbaye alitoroshwa na mtoto wake wa kufikia ,Alice, akawa ameshatoka Mwanza alipokuwa amekwenda kwa ajili ya mazishi ya mshiriki mmojawapo wa mashindano haya ya mrembo wa Tanzania, Jamila Said. Aliporudi Dar es salaam zoezi la kwanza kwake lilikuwa nikufualtilia juu ya watuhumiwa waliokuwa wamewekwa ndani yaani mkewe,janet na mtoto wake wa kufikia,Alice. Pia kuthibitisha kauli za magazeti na baadhi ya maneno ya watu kuhusiana na polisi kula rushwa na kuwatorosha Janet na Alice.
Moja kwa moja akaongoza mpaka kituo cha polisi ambapo mara ya mwisho aliwaachia majukumu polisi ya kuwaweka hatiani mkewe Janet na mtoto wake wa kufikia Alice.
“Enhee vipi wanaendeleaje hao watuhumiwa humo ndani..?”
John akauliza kwa kujiamini uku akiwa ameweka mikono yake mifukoni mwa suti yake.
“Bosi kuna matatizo yamejitokeza yakichangia na uzembe mdogo wa kikazi..”
“Bado Sijawaelewa na vigumu kuelewa mnachoongea. Kwanza wako wapi hao watuhumia nataka niwaone..??”
“Ndio maana bosi tunakuambia kuwa ni uzembe umefanyika. Usiku ule ule tukiwa tumemfunga pingu yule binti kabla hatujalifikia gari tukashangaa majambazi yametuvamia. Tukaanza kulushiana risasi. Kwa bahati mbaya yakafanikiwa kumchukua yule binti. Tukaanza kuyafukuza. Tumewafuatilia mpaka barabara iendayo Morogoro bila mafanikio yeyote. Basi tukarudi kituoni napo kufika tunakuta mmoja wetu tuliomuacha kazimia huku na yule mama naye hayupo..”
 
68.

“Bado hamjaniingia akilini hata kidogo?? Naona hamjanifahanmu vizuri mimi ni nani..? Mnajua tukio la kifo hiki limeteka maelfu ya watanzania..? sasa leo mnakuja kuniambia kirahisi rahisi tu eti ooh uzembe, uzembe pumbavu..”

*****************

Baada ya mashindano yale ya kwanza ya kumtafuta mrembo wa Tanzania kumalizika kwa kukatishwa pale ukumbini huku Alice akipokwa ushindi yaliwaumiza sana wazazi halisi wa Alice, Juliana na Majaliwa. Majaliwa alipoteza fahamu papo hapo siku ya mashindano. Juliana alikuwa hajitambui alishindwa amsaidie nani kati yao kutokana na Jukwaani Alice alidondoka na pembeni yake mumewe naye alidondoka na kupoteza fahamu. Alibaki akimpepea mumewe,Majaliwa huku akishuhudia mapolisi wakimfunga Alice pingu wakimburuta akiwa amezimia. Juliana alipandwa sana na hasira kali pale ukumbini. Alipiga sana makelele lakini kutokana na wahudhuriaji wa pale kutoa makelele mengi zaidi yao juu ya mfarakano wa mashindano hayo kuahirishwa Juliana alijikuta sauti yake ikimezwa na wingi wa sauti za watu wengu mule ukumbini. Alilia sana huku akiendelea kumpepea mumewe Majaliwa japo azinduke ashuhudie mwanae akiwa chini ya ulinzi bila mafanikio yeyote. Watu wote walitawanyika ukumbini nakumuacha akiwa anampepea mumewe, Majaliwa.
Juliana hakuwa na uwezo wowote wa kifedha wa kumuwaisha mumewe hospitali. Alijitahidi sana kutoa macho mule ukumbini huku na kule huenda akamwona yule msamalia mwema aliowasaidia kuingia ndani ya ukumbi,john. Illimchukuwa zaidi ya nusu saa bila kuambulia chochote. Ukumbi mpaka ukabaki mtupu huku akiwa yeye na mumewe. Alimbeba begani mumewe akajikokota naye mpaka nje. Magari nayo yalikuwa yamepungua sana. Alianza zoezi la kugonga dirisha la gari moja baada ya jingine. Kuna ambao bado walikuwa hawajaondoka na wengine hawakuwepo kabisa ndani ya magari yao lakini Juliana hilo hakulitambua zaidi ya kutembea kila gari na kubisha hodi kupitia kwenye vioo vya madirisha ya gari zao. Hatimaye akafanikikwa kufunguliwa kioo na gari mojawapo.
“mnataka nini usiku huu..?? hapa hakuna msaada samahani..”
“hapana shida yetu ni..”
Kabla Juliana hajajieleza alishangaa yule mtu kufunga kioo cha gari kisha akiliwasha gari lake na kusonga. Alibaki akilia sana, mumewe bado alikuwa amening’inia begani mwake huku kazimia. Alijihisi kukata tamaa ya kupatiwa huduma. Alijigeuza vizuri huku akili yake akielekeza kurudi kwake kwa miguu akiwa amembeba kwa begani mumewe. Aliamini atazinduka tu akiwa njiani. Akiwa bado anajikokota njiani mara ghafla gari ikataka kuwagonga.Ikapiga honi kwa sauti ya juu sana mithili ya matarumbeta yakipulizwa kipindi cha harusi.
“Vipi tena usiku huu..?? kulikoni mbona hivyo jamani tuantiana gundu usiku huu..??, basi mjitahidi mtembee pembeni ya barabara..”
“Samahani sana baba, tunahitaji msaada wako, hali ndio kama unavyoiuina kwa mume wangu. Amepoteza fahamu..”
“Pole sana..”
Yule kijana ambaye alitaka kuwagonga akalipaki gai lake pembeni vizuri kisha akawarudia.
“Vipi ilikuwaje mpaka akapoteza fahamu..”
“Baba ni hadithi ndefu sana. Nahitaji kwanza huruma yako. Nakuomba tumpeleke hospitali baba..”
Yule kijana akaonekana mwenye huruma japokuwa alionekana kipesa hana matatizo kutokana na mavazi aliokua amevalia ya kung’aa na mwili wake ukizungukwa na cheni za dhahabu na za ming’aro ya silva na hata gari lake lilionekana la kisasa zaidi na lenye thamani. Walisaidiana na Juliana kumbeba Majaliwa huku kila mmoja akimweka begani wakisonga taratibu mpaka kwenye gari na kumpakia kwenye gari na zoezi zima la kumpeleka majaliwa hospitali likaanzia hapo.
Hali ya majaiwa haikuwa ya kawaida kwa mgonjwa wowote. Walipokuwa njiani kabla hawajamfikisha hospitali majaliwa alionesha kubadilika sana mwili. Ile kansa ya ngozi aliokuwa nayo ilimfanya ngozi kubadilika kwa kipindi kifupi kabla hajafikishwa hospitali. Alizinduka na kuanza kufurukuta mwenyewe kabla hawajafika hospitali. Juliana akaonesha kutoa tabasamu kwa mumewe kurudiwa na fahamu. Wakaingia hopsitali ya taifa ya muhimbili. Walipokelewa na manesi waliokuwepo zamu nusiku ule. Moja kwa moja wakamkimbiza wodini huku nyuma Juliana pamoja na yule msamaria mwema wakaambiwa wasubiri nje.
 
69.
“Umesema mgonjwa alikuwa akisumbuliwa na nini..?”
Yule ijana msamaria mwema akamhoji Juliana kwa sauti ya chini na ya utaratibu huku akitaka kujua yaliomsibu Majaliwa mpaka kuwa vile.
“Kama niilivyokuambia hapo awali. Mume wangu anamatatizo makubwa sana. Ni pombe, pombe za asili ndio chanzo..??”
Juliana akainama chini kwa masikitiko makubwa. Machozi ya uchungu yakaanza kuchukuwa sura mpya katia paji lake la uso. Huzuni ikamwingia yule kijana.
“Pole sana, pole. Ikawaje sasa..??”
“Tulikuwa na mtoto wetu anaitwa Alice. Tulimpenda sana lakini mume wangu ndio chanzo cha kuvuruga yote haya. Alibadilika ghafla nakuwa mlevi hali iliyomfanya kurudi usiku sana akiwa amelewa na kunipiga sana. Niliumia na kuvumilia kwa kipindi kirefu sana. Lakini ukawa ndio mchezo wake kila akirudi amelewa mimi ndio nikawa suluhisho lake kwa kunipiga mangumi na hata kwa kutumia fimbo. Nakumbuka siku moja usiku alikuja na kuni kubwa akaingia mpaka ndani nakuanza kunipiga nayo uku nikiwa usingizi ni nimelelala na mwanangu. Alinipiga sana haswa maeneo ya usoni. Maumivu yakanizidia ikanibidi nitafute njia nitoroke na kukimbilia kusikojulikana. Niliumia sana kumuacha mwanangu angali alikuwa ndio kwanza binti wa miaka kumi na nne. Kiasi cha hela kidogo ambacho nilikuwa nimekifunga katika kanga yangu kikanisaidia kuweza kusafiri mpaka kijijini kondoa kwa wazazi wangu. Nilikaa zaidi ya miaka minne bila kuwa na mawasiliano yeyote huku nikiamini endapo nitarudi nitauliwa kwani sikuwa na wazazi, wazazi wangu wote walishafariki nikiwa mdogo sana.
“Pole sana, dahh pole..!!”
“Asante.Ni mwanangu pekee ndio aliyenichochea kurudi vivyo hivyo kwangu. Nilijikaza sana na kurudi kwangu kwa mara ya pili huku nikihofia kuuliwa na mume wangu. Hali nilioikuta ikawa ni tofauti. Mwanangu alikuwa haishi tena na baba yake kwani na yeye alishatoroka baada ya kuona sionekani na sijulikani nilipo kwani hakuwa hata akijua nilipokimbilia. Nilimkuta mume wangu akiwa ndani kitandani hajiwezi tumbo limekuwa kubwa sana kutokana kuishi kwa kunywa pombe kali kwa muda mrefu bila ya kula chakula. Alikuwa ana siku tano hajapata chakula chochote, yupo hoi..”
Juliana akiwa bado anamsimulia yule msamaria mwema mara dokta naye akatokea. Akawafuata mpaka eneo walipoketi Juliana na yule kijana.
“nani muhusika wa mgonjwa yule mzee alioletwa..”
“sisi hapa..!!”
Alijibu yule kijana kwa kujiamini baada ya kumuona Juliana akisita sita kujibu.
“ Ni kwamba tumejaribu kumcheki vizuri kwamba tumegundua mgonjwa alikuwa na tatizo la kansa ya ngozi ambayo imemsumbua kwa muda mrefu. Pia inaonekana kapata mshtuko mkubwa hali iliyompelekea kupooza kwa mwili wake upande mmoja. Hapa namaanisha upande mmoja kutoka kichwani mpaka miguuni. Uwezo wa kuongea hatakuwa nao kwa kipindi kirefu mpaka pale hali hiyo itakapokuwa inaanza kubadilika..”
“Kwahiyo dokta inamaana mume wangu ndio hawezi kuja kupona kabisa..?”
“ Sio kila mgonjwa wa kupooza hawezi kupona maishani mwake hapana. Mazoezi madogo madogo ya viungo atakayokuwa akipatiwa kwenye viungo vyake mbali mbali vya mwili yatamfanya mgonjwa wenu kuanza kupata unafuu na pengine kumpelekea kupona kabisa..”
Kabla dokta hajamalizia kuwaelezea, nesi mmoja akatoka wodini haraka nakumkimbilia dokta.
“Dokta..?? dokta yule mgonjwa aliyeletwa kazidiwa sana anafurukuta twende ukamtibie..”
“Haya, jamani samahanini nakuja sasa hivi..?”
Yule dokta alikimbia mpaka wodini. Ilimchukuwa dakika kumi tu akawa amesharudi na makaratasi mpaka walipokuwa wameketi Juliana na yule kijana.
“Samahani nakuomba wewe kijana mara moja..”
akamuita yule kijana msamaria mwema huku wakimuacha Juliana kwenye hali ya mshangao..
“Nimekuita wewe kama mwanaume mwenzangu na mtu mwenye uwezo wa kujikaza kiume. Nilivyorudi mara ya pili mule ndani yule mgonjwa wenu nimemkuta anakata roho. Nimejitaidi sana kufanya kadri ya uwezo wangu lakini nimeshindwa kuokoa maisha yake. Mwenyezi mungu kamchukuwa. Poleni sana hivyo tunaupeleka mwili wake mochwari muda si mrefu.. Mwambie mama kwa utaratibu usije ukasababisha maafa mengine.. take care..!!”.
Yule daktari akamaliza kumnong’oneza kitu yule kijana. Baada ya hapo akasogea taratibu karibu na eneo alipokuwa ameketi Juliana uku akimwacha daktari kurudi wodini.
“Vipi tena dokta kakwambiaje jamani maana nafikiria sana jinsi ya kumtibia huo ugonjwa wa kupooza ili hali sina hata pesa..”
Kabla yule kijana hajasema chochote wakashangaa baiskeli lya kubebea machela ikipita mbele yao. Yule kijana hakuwa na jinsi tena ya kueleza zaidi ya kushangaa. Juliana na yeye macho yake yalikuwa sambamba na kile kibaiskeli kilichokuwa kikikokotwa na manesi watatu kwa haraka haraka. Juliana akiwa bado amezubaa anakitolea macho mara kwa mbali akaliona shati la mumewe likining’inia kwenye kile kibaiskeli. Pumzi zikaanza kumuishia. Mishipa ya mwilini mwake ikaanza kumsimama. Mapigo ya moyo yakabadiklisha uelekeo.. akajihisi kutetemeka huku macho yakimtoka vilivyo..
“Mume waaanngu uu mee niii aa chaaaa mmmwwenyeewwww..!!!!!!!!!!!!!”

Aloyce alikosa kabisa amani usiku kucha. Ile hali ya kufanya mapenzi ikamrudia tena kwa mara ya pili. Ikawa imeshamtawala kwa kipindi kirefu toka Alice alopogoma kufanya naye mapenzi. Akawa ameshavumilia sana na amechoka, akashindwa kabisa kuuzuia moyo wake ambao ulikuwa hauko tayari kumuona Alice akipata usingizi.
“Alice..??, Alice?? Amuka basi..??”
Alice ambaye alikuwa amepitiwa na usingizi. Akashtuka na kujigeuza vizuri, uchovu ukiendelea kuutawala mwili wake.
“Jamani Aloyce nimechoka sana na safari naomba unielewe pliiz..??”
“Najua mwili wakangu iko na mihisia tangu nalala hapa just wake up mupenzi.. I need you..??”
Alice akainuka kitandani na kuketi. Alikuwa amevaa taulo tu kutokana na kutokuwa na nguo ya kulalia. Aloyce akaonesha sana sura ya upole na huruma. Akatamani hata amrukie Alice kwa nguvu lakini moyo wake ukamvuta hivyo akabaki kuwa na sura ya kusubiri jibu. Jibu ambalo Alice atalitoa kwa mdomo wake mwenyewe, jibu ambalo litakuwa muafaka wa kile anachokitaka. Akili na hisia za Alice hazikuwa kabisa katika kufanya mapenzi lakini ikambidi akubali ili tu moyo wa Aloyce uridhike na vile vile apate kulala kwa amani.
“Aloyce..?? nakupenda na nahitaji sana unitunzie penzi langu. Sijawahi kamwe kufanya mapenzi na hii ni mara yangu ya kwanza kwako. Nakukabidhi rasmi mwili wangu kwako uufanye utakavyo...”
Maneno matamu kutok kwa Alice yakawa yamegonga vilivyo ngome ya masikio ya Aloyce. Akajiona anaelekea kuridhika na alichokuwa akikitaka tangu ameingia chumbani kwake na Alice. Hakutaka kuchelewesha muda. Akalivuta lile taulo ambalo Alice alikuwa amelivaa, taulo ambalo ndani yake hata hakukuwa na nguo ya ndani kutokana na Alice kuifua alipokuwa amekwenda kuoga na hakuwa na nguo ya kubadilisha. Alice akaanza kujihisi hisia zikimtawala taratibu katika mwili wake. Ile hali ya kutokufanya mapenzi siku nyingi akailaani sana, akajuta hata ni kwanini hakuwahi kufanya mapenzi baada ya kubakwa na baba yake. Aloyce akaanza kuupapasa vilivyo mwili wa Alice kuanzia katika nywele zake mpaka mpajani. Zile ndoto zakez a muda mrefu kumpata na kuishi na mrembo nambari moja Tanzania akawa anajivunia. Alijivunia akajiona ni yeye pekee ndiye anayepata raha kuliko raia yeyote wa nchini Rwanda. Akazidisha utundu hali iliomfanya Alice ajihisi kama yupo angani. Utundu mwingine hata alikuwa haujui zaidi ya kuubuni papo kwa hapo ili mradi ampagawishe Alice. Alice akachanganyikiwa kweli kwa mapenzi aliokuwa akipewa na Aloyce.
 
70.
“Baby, katika maisha yangu sijawahi kupata raha ninayopata..?”
“True..? (Kweli..?)”
“Yes baby. Napenda tuendelee tena hata ukitaka mpaka asubuhi. Tuendelee tu baby kwani mwenzio nasikia uhhh..!! uhhh…!! Uhhh..!! uhhh..!!! malizia baby mwenzio nah..”
Alice akamkumbatia Aloyce kwa mara ya pili. Akamkumbatia kwa nguvu zake zote uku akitoa makucha yake nakuanza kumparaza kuanzia mgongoni mwake. Utamu ukamnogea sambamba na mwili wake kumsisimka, akachomoa meno yake na kuhamishia mpaka shingoni mwa Aloyce. Kwa utamu wa mapenzi aliokuwa nao Alice akajikuta amemuweka Aloyce alama ya mapenzi. Ikawachukuwa saa mbili nzima wakiwa kitandani uku kila mmoja akijiona yupo katika bahari ya mapenzi. Bahari ambayo ina kila kitu, mtumbwi, maboya na fimbo zake. Walipomaliza kufanya mapenzi wakapeana pongezi kila mmoja kwa kupeana ndimi zao sambamba na mate.
“Mupenzi sasa tunaweza pumzika..”
“Sawa baby wangu utakavyo..yaani usiku huu sintoweza kuusahau maishani mwangu kwani umenifanya kuwa mwanamke kweli aliyekamilika. Nakupenda sana Aloyce..”
“Hata mie penda sana kuanzia sasa na kuendelea nahitaji nikuoneshe kwa tendo..”

BAADA YA MWAKA MMOJA

Maisha ya Aloyce na Alice yakawa mazuri sana. Mama yake wa kufikia,Janet akawa bega kwa bega na wao. Raisi wa Rwanda, Kagwa Rwisereka ambaye ndiye baba yake na Aloyce akawa anajua mahusiano kati ya mtoto wake Aloyce na Alice. Katika maisha ya Alice hakuwahi hata kushikana mkono na rais yeyote lakini sasa kwake yakawa kama mazoea kila baada ya wiki yeye na Aloyce ni lazima waingie ikulu kumsalimia rais Kagwa Rwisereka. Chuo cha Loyce Trainging Collage sasa kikawa chini ya Alice. Alice akakabidhiwa kusimamia miradi mingi mbali mbali. Mingi kati ya hiyo alimpa mama yake amsaidie kusimamia. Watu wote maarufu nchini Rwanda wakawa wanamtambua Alice kama mchumba wa Aloyce. Kamwe hakupenda majigambo wala kumnyanyasa mtu yeyote kwa pesa alizokuwa nazo. Mipango mikubwa ikawa ni kutaka kuanza vikao vya harusi kati ya Alice na Aloyce. Taarifa za kutaka kuoana zikasambaa zaidi karibia Rwanda yote wakawa wanalitambua hilo. Baba yake aloyce, Kagwa Rwisereka akawa ameshajitolea kusimamia na kuendesha harusi yote kuanzia ukumbi, chakula, usafiri na vinywaji na hata kuwaalika marais wenzake. Aloyce akafurahia sana. Mipango ya harusi na vikao vikaanza taratibu. Janet akawa kama msemaji mkuu badala ya Alice. Alimdanganya mambo mengi sana Aloyce. Kwa mujibu wa Janet, Aloyce akawa anajua kuwa Alice hana baba, alishafariki hivyo anaishi na mama tu na ndiye Janet.
Miezi mitatu kabla ya Ndoa yao mara Alice akaanza kujiona tofauti. Amani ikaanza kumpotea kutokana na ndoto ambazo zilikuwa zikimuandama mfululizo. Ndoto mbaya juu ya maisha yake. Ndoto kubwa iliomsumbua ni juu ya mauaji alioyafanya kipindi cha nyuma akiwa anashiriki mashindano ya mrembo wa Tanzania. Mauaji ya mashiriki mwenzake Jamila Said. Mashindano yaliompelekea Alice kuua kabla siku yenyewe ya mashindano ili apate kushida taji la membo wa Tanzania. Duku duku likamjaa sana moyoni, ila alipokuwa akitembea Alice akawa anahisi anaongozana na Jamila. Hata usiku akilala na mchumba wake Aloyce bado alikuwa akijihisi Jamila yupo pembeni yake uku akimuongelesha. Ndoto zikamzidia na kumnyanyasa hali iliomfanya akose kabisa raha ya usingizi. Kichwa chake Chote kikatawaliwa na jina la Jamila. Akajitahidi japo kulala lakini kwa bahati mbaya akashtuka usingizini na kutaja jina la Jamila. Akatoka usiku huo huo nakuelekea mpaka chumbani kwa mama yake napo alipofika tu mlangoni akahisi ametokewa na mzimu wa Jamila. Alice akadondoka chini nakuanza kutapatapa. Kile kifafa chake cha muda mrefu kikachukua nafasi yake. Akaanza kutapatapa uku mdomoni akitoa mapovu na kujinyonga nyonga mithili ya nyoka wa kwenye maji. Usiku huo huo Aloyce akashtuka kutoka usingizini nakujikuta yupo peke yake kitandani.
“Alice muke yangu..??, Alice..??”
Akaita sana uku akitoka nakuelekea kumtafuta bafuni bila mafanikio. Akaenda mpaka sebuleni napo hakumuona ndipo akasikia sauti ya Alice ikiguna chumbani mwa Janet. Kwa ujasiri aliokuwa nao Aloyce akajikuta ameufungua mlango bila hata ya kupiga hodi. Macho yake yakakutana uso kwa uso na mchumba wake, Alice akitapatapa uku akiupiga ukuta kwa mateke na mdomoni akitoa povu jingi.
“Tubebe hii mama, nini natokea..? ebu tuipeleke hospitali..”
“Twende tumuwaishe mwanangu..”
Aloyce na Janet wakambeba Alice. Alice akawa na nguvu zaidi kushinda wao kwa kujitupa. Ikabidi waite askari wa getini wakaja wakasaidiana kumbeba nakumpakiza kwenye gari na safari ya kuelekea hospitali ikaanza. Haikuwa mbali sana kwani kwa mwendo wa dakika tano wakawa wameshafika. Wakamshusha nakusaidiwa na manesi kumpakiza kwenye machela lakini Alice akawa tayari ameshapoteza fahamu na lile povu liliokuwa likimtoka mdomoni likabadilika nakuwa damu damu nzito na nyeusi. Wakamkabidhi daktari na kisha wao kutoka nje wakisubiria alice atibiwe.
“I cant..!!, Nataka kuelewa muke yangu inakuwaje..?”
“Aloyce mwanangu, ni story ndefu lakini naomba nieleweke. Nakuomba tena unisikilize ili tujue namna ya kumsaidia..”
“Go on, …endelea Janet..??”
“Mwanangu Alice toka nimemzaa ana matatizo ya kifafa na huwa anapoteza fahamu anapopata hali ya kushtuka. Hatakiwi kupigiwa makelel sana na hata kupewa habari za kushtua moyo wake. Na hata hivyo nilijua kashapona kutokana na daktari aliyemtibiwa mara ya mwisho kuniambia kuwa amepona hataangauka tena..”
Mama wa kufuikia na Alice,Janet. Akajikaza na kutoa maneno ya uongo ili kuweza kumchochoea Aloyce aelewe na kutuliza hasira ambazo zilikuwa zimempanda.
“Na mbona hamukuniambia..? kuki..? kuki Janet..?(kwanini)”
Aloyce alilia sana. Akarudi mpaka wodini alipokuwa amelala Alice hajitambui kwa kuwekewa mirija ya kutolea hewa(oxygen). Daktari alikua ameshatoka hivyo ni manesi pekee ndio walikuwa wamemzunguka Alice. Walipomwona Aloyce wakampisha.
“Alice, Alice nakupenda sana muke angu.. you’re the only one in my life(wewe ni wa pekee maishani mwangu).. sipendi ikakupoteza mupenzi angu..”
Aloyce akalia sana mithili ya mtoto mdogo akinyang’anywa kitu chake cha kuchezea. Akajiona ni mtu wa kukata tamaa kwa matatizo aliokuwa nayo Alice. Aliithamini sana bahati aliokuwa nayo ya kuishi na mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania. Akajiona kamwe hawezi kumpata msichana kama Alice. Kwa upole na ukarimu aliokuwa nao, ucheshi na hata alipendwa na kila mtu hata baba yake.

*********

Taarifa juu ya kuanguka kwa ugonjwa wa kifafa ghafla kwa Alice na kisha kuwahishwa hospitali ya Theodore Hospital pembeni kidogo ya mji wa Butare nchini Rwanda zikawa zimeshamfikia rais wa Rwanda Kagwa Rwisereka, baba wa Aloyce. Alizipokea kwa masikitiko makubwa sana na alikuwa na roho ya chafu. Akaona endapo Aloyce atafunga ndoa na Alice basi itakuwa aibu kubwa sana haswa kwa yeye alivyokuwa na madaraka makubwa ya kuiongoza nchi ya Rwanda. Akaona ugonjwa wa kifafa aliokuwa nao Alice utakuwa doa kubwa sana katika familia yao. Akalifikiria sana swala la mtoto wake kunyanyasika na mapenzi tena kwa binti ambaye si wa nchini mwao. Mawazo yake yakachanganua sana juu ya swala hilo. Kamwe halikumuingia akilini. Halmashauri ya kichwa chake haikuafikiana na hilo swala. Alichomaua kukifanya alipiga simu moja ka moja kwa aloyce.
“..Akana Aloyce.. (Mwanangu Aloyce)“
“Yego data ( Naam baba)”
“Nakuomba ikuje ikulu mara moja..??”
Aloyce akaonekana kuitii amri ya baba yake. Akamuangalia sana Alice kwa mara ya pili. Alice alikuwa bado hajarudiwa na fahamu hivyo Aloyce akamshika eneo la usoni na kumbusu. Safari ya kutokea hospitali mpaka ikulu alipokuwa baba yake hapakuwa mbali sana. Ikamchukua Aloyce kama nusu saa akawa ameshafika.
“Aloyce..?”.
“yes baba”
“nasikia hiyo msichana naumwa fafa..? ipo dalili ya yeye pona..?”

“dady, just a long story..(hadithi ndefu baba)”
John akamuhadithia kama alivyokuwa ameambiwa na Janet. Kagwa Rwisereka akasikiliza kwa makini maneno aliokuwa akiambiwa na mwanaye Aloyce juu ya Alice.
“Manangu ipo penda sana mie.. wewe ni pekee..Koya (achana naye) itatutia aibu kubwa sana na gonja yake hiyo..”
“Baba nooo, sipo tayari kumuacha alice, nampenda sana dady, yeye ndie mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania na sintokuja kupata kama yeye dady..?”
“Hiyo gonjwa ya fafa huwa haina tiba. Haiponi hiyo and her life itakuwa vivyo hivyo.. itakusumbua sana na mwishoe itakufia believe me manangu.. just leave, iache ikwende kwao Tanzania tapata ingine..”
Maneno yale yalimkosesha sana Aloyce nguvu. Akayafikiria sana mambo ambayo aliyapanga yeye na Alice. Ahadi walizokuwa wamewekeana ndani ya mwaka mmoja. Harusi kubwa na ya kifahari ambayo baba yake Aloyce Kagwa Rwisereka ndiye alikuwa ametoa ahadi ya kuigharamia leo hii ndio huyo hataki tena mwanamke aoe msichana mwenye kifafa. Aloyce aliumia sana. Akabaki nji panda bila ya kuelewa afanyaje. Kamwe hakuwahi kumbishia baba yake. Akatoka mule ikulu uku akiwa ametii amri ya baba yake japokuwa alikuwa na hasira sana. Akaingia ndani ya gari na kuliwasha kwa hasira sana akielekea hospitali alipokuwa amewaacha Alice na mama yake.
“Sina jinsi acha iende kuwafukuza yote. Mungu kubwa sana ipo Nampata ingine soon. My dad itabaki kuwa dady na nitazidi kumheshimu na sitaki kamwe nimuuzi.. Alice nitaipenda ‘ariko’(lakini) wacha irudi tu kwao, no way out..”
Aloyce akajikuta akizungumza mwenyewe njiani akiendesha gari. Haikumchukuwa mwendo wa nusu saa kama ilivyokuwa mara ya mwisho. Kwa sasa ikamchukua dakika kumi na tatu tu kuingia hospitali ya Theodore. Akamkuta Alice ameshastuka anaangaza macho huku na kule uku bado kawekewa mirija ya kupumulia. Janet alikuwa pembeni yake. Aloyce akawaangalia kwa uchungu na hasira uku machozi yakimtoka kila akifikiria amri aliopewa na baba yake.
“Janet, Alice iko penda sana nyinyi, penda sana. ‘Ariko’(lakini) kuanzia sasa na…”

Janet akabaki mdomo wazi akimtolea macho Aloyce vivyo hivyo na Alice.
“Hata sisi tunakupenda sana kwani vipi mbona umekuja uko na hali hiyo kuna nini tena Aloyce..??”
“Pana kitu. Mimi penda sana nyinyi na Alice penda na wewe..”
Aloyce akajikuta anarudia rudia maneno. Akili yake yote ikawa imezungukwa na amri ya baba yake. Amri ya yeye kuachana na mpenzi wake anayempenda sana kutoka moyoni. Mpenzi ambaye alipata shida mpaka kuhakikisha anakuwa mikononi mwake kutoka Tanzania mpaka Rwanda. Kila akiuangalia uzuri wa Alice na akijenga picha kichwani kwake kuwa ndiye mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania roho yake ilikuwa ikimuuma sana.
“Janet..??, Janet embu ikuje mara moja hapa pembeni..??”
Aloye akamvuta Janet kwa pembeni kumnong’oneza kitu.
“Najua kuwa Alice iko umwa sana, sana na gonjwa ake ni fafa, is it..?”
“Kweli kabisa Aloyce..”
“My dad iko chukia sana hiyo gonjwa na Alice..? na ndio iliniita baada kusikia kuwa Alice gonjwa sana kwa hiyo fafa. na mimi siko tiyari kukosana na dady yangu wala kuacha hii Alice potee..”
“Aloyce..? ugonjwa wa kifafa ni kama ugonjwa mwingine tu. Unaweza kupona taratibu na kuhusu baba yako wewe mwambie kuwa Alice atapona tu asiwe na wasi wasi..”
Aloyce akakaa kimya zaidi ya dakika tatu nzima uku akiinamisha kichwa chake chini.
“Anyway..!! itamwambia pana shaka..”
Aloye hakuwa na jibu lolote zaidi ya kujiuma uma nakumfariji Janet ili tu aridhike. Akili yake bado ilikuwa imevurugwa. Akajikuta akibaki peke yake nyuma uku janet akirudi kitandani alipokuwa amelala Alice.


BAADA YA WIKI


Hali ya Alice ikakaa sawa. Kule kudondoka mara kwa mara kukapungua, japo Aloyce bado aliweka duku duku moyoni mwake. Hakuwa tayari kumuona Alice akirudi kwao Tanzania nakumuacha mpweke kisa maamuzi ya baba yake. Hali ile Ikamfanya awaambie ukweli wote juu ya siri hiyo kubwa kutoka kwa baba yake ambaye alionesha kubadilika na kuyapinga mahusiano yao kutokana na ugonjwa huo wa kifafa. Siku Alice alipoambiwa wazi na Aloyce juu ya kutokupendwa na baba yake Aloyce alidondoka tena kifafa lakini kwa safari hii hawakumpeleka hospitali

itaendelea
BURE SERIES/USER]
 
71.

kutokana na tiba yake kuwa nayo. Dawa ya kumpulizia akiishiwa pumzi ilikuwa haibandiuki mifukoni mwa Aloyce ama Janet.
Alice akawa kama mfungwa aliekosa gereza. Mfungwa kwa kutokuwa na bahati maishani. Mawazo mengi yalikuwa yakimtawala mara kwa mara. Akajikuta akijutia sana kitendo cha yeye kumuua Jamila. Akaona kitendo hicho huenda kimezua mikosi zaidi katika maisha yake ambaye yamekuwa yakibadilika kila mara.
“Mama ipo siku yatakwsha tu mama yangu..”
Alice akaongea kwa sauti ya taratibu uku akitaka kutoa machozi. Uso wake ulishabujikwa na limbi la majonzi. Mama yake wa kufikia, Janet akamsogelea Alice mpaka pembeni nakumbusu.
“Mwanangu siku zote ni kumuomba mungu sana kila penye matatizo hata pasipo matatizo. Kuna neema huenda inakaribia mwanangu na hivi ni vizuizi tu. Tafadhari tusikate tamaa. Nakuapia kuwa Aloyce ameniahakikishia kuwa bado anakupenda na amini usiamini hivi karibuni utafunga naye ndoa kubwa sana haijalishi wapi lakini Aloyce ndiye atakuwa mume wako wa ndoa..”
“Kweli mama..??”
“Amini hivyo mwanangu, Aloyce bado anakupenda na yale ni maneno ya baba yake tu wala yasikuumize kichwa mwanangu..”
Janet akawa akimfariji sana Alice. Alice akaanza kujihisi tofauti kutokana na yale maneno aliokuwa akipewa na mama yake. Yakamwingia kabisa mpaka kwenye moyo wake. Moyo ukakubaliana nayo. Ukatabasamu na kucheka kwa taratibu.

*********

Makubaliano kati ya Aloyce na Janet pamoja na Alice juu ya kuhama kwenye nyumba yakawa yameshafika. Aloyce aliamua kuwatufutia jumba kubwa jingine lenye thamani kubwa kama ile nyumba yake. Akawahifadhi Janet na Alice kwa siri kubwa sana huku akiwahaidi kuwahudumia kwa kila kitu watakachokitaka.. Ile miradi yote ambayo Alice alikuwa akisimamia na hata mingine alikuwa akisaidiana na mama yake kusimamia sasa ikarudiswhwa mikononi mwa Aloyce. Yote kuitokana na baba yake Aloyce asielewe chochote. Ule umaarufu aliokuwa nao Alice toka kipindi anasimamia mali za Aloyce ukaanza kufutika taratibu. Baadhi ya vyombo vya habari uku vingine vikiripoti kuvunjika kwa mahusiano kati ya Alice na Aloyce chanzo baba yao. Wananchi wa Rwanda walipokea jambo hili kwa mitazamo tofauti kuna waliokuwa wakiwaponda nakusema siku zote watu maarufu huwa hawadumu na hata wengine wakifurahia sana sana wasichana ambao walianza ukaribu na Aloyce kwa kutaka wachukuliwe wao na kuolewa. Kitendo cha Aloyce kumuacha Alice kikamfurahisha sana rais Kagwa. Akaonesha kumpenda na kumthamini mtoto wake,Aloyce kwa kutii amri yake ya kumuacha Alice na kumrudisha kwao Tanzania.Aloyce akafanyiwa sherehe kubwa sana na baba yake. Sherehe ambayo ilifanyika kifamilia nakuhudhuliwa na watu maalumu.
“Manangu penda wewe, ile siyo sichana taka oa wewe, sichana gani na fafa..??, fafa..? no noo sipendi manangu sipendi kabisa upate shida tika ndoa ako..”
“oke dady nimekuelewa..”
Aloyce akajibu kwa sauti ya upole. Hakutaka kabisa kupoteza muda katika sherehe hiyo ambayo ilikuwa ni ya muda mfupi. Akili yake kubwa ikawa ni kumuwaza kipenzi chake cha roho Alice. Akawa hana amani kabisa. Akatoka sherehe ikiwa inaendelea moja kwa moja mpaka kwenye makazi mapya waliokuwa wakiishi Janet na Alice.
“Mama Alice. Nataka harusi etu ifanyike mara moja. Dady mumy wala rafiki sitaki hata moja jua mimi nafunga ndoa na nani na wapi.? Nataka tufunge harusi inchi ingine na siyo hapa Rwanda..”
“Mwanangu hilo jambo kubwa na naamini itakuwa hatua kubwa kwa kumuonesha furaha mwanangu mpendwa Alice. Eti mwanangiu Alice..?”
“Mama nashindwa kabisa hata furaha hii niiweke wapi.? Mama nimeamini kweli Aloyce ananipenda na hata wewe pia. Sikuamini kama mpaka sasa tungebaki hapa Rwanda. Aloyce..”
“Ndio muke angu nasemaje..??”
Alice akainuka na kumsogelea Aloyce kisha akausogeza mdomo wake mpaka usoni mwa Aloyce na kumbusu..”
“Hakuna kama wewe duniani. Wewe ni mwanaume wa ukweli unayejua nini maana ya mapenzi. Nakuahidi kukutendea mema maishani mwangu na hata zile ahadi za kukuzaliwa watoto niko tayari kuzitimiza hata sasa hiv..”
Kabla Alice hajamalizia kuongea, akajihisi mapigo ya moyo kama yanaenda kasi mwilini mwake. Mwili ukaanza kupoteza nguvu taratibu. Akajihisi kama amemeza kitu cha uchachu na anataka kukitoa mdomoni. Haraka haraka akakimbia mpaka jikoni, kabla hajafika jikoni akasimama ghafla baada ya kuzidiwa kwa nguvu za mdomo. Kitu kizito kikaanza kumsukuma kutoka tumboni mwake kuelekea kwenye kinywa chake. Mdomo wake ukawa umeshakula kiapo na kusaliti hivyo kubaki wazi kuachia kitu kinachotoka tumboni mwake. Alice akatapika mfululizo. Haikuwa tapika ya kawaida.
“Muke yangu vipi tena..?”
 
72.
Aloyce akahoji baada ya kumuona Alice kusimama nakuendelea kutapika. Macho ya Janet moja kwa moja yakahamia mpaka kwenye shingo ya Alice. Akagundua kitu, akatabasamu baada ya kuona kitu kwenye shingo ya Alice kikidunda haraka haraka.
“Hongera sana mwanangu. Sasa umeingia katika usichana..?”
Alice akabaki amekodoa macho asielewe chochote. Aloyce naye akabaki njia panda kwa kuendelea kumuangalia Alice.
“Mama hongera ya nini tena..?”
“Mwanangu nakupa hongera kwa kuweza kutimiza ndoto zenu. Na hiyo tapika ni dalili tosha ya mimba. Ona shingoni mwako mapigo ya moyo yanavyokwenda mbio.? Tayari mwanangu una mimba amini hivyo..”
Si Alice wala Aloyce ambaye hakutaka kabisa kuamini maneno ya Janet. Aloyce akamuwahi Alice nakumkumbatia hivyo hivyo bila kujali wingi wa yale matapishi chini na hata baadhi ya kwenye nguo ya Alice.
“Muke yangu, cant belive, cant., twaweza kwenda sipitali..?”
“ndio mume wangu..”
Dakika kumi zikwatosha kabisa kufika hpspitali kupima na kuchukuwa majibu. Mimba ya mwezi na nusu ilikuwa imeanza kulijaza tumbo la Alice. Aloyce akajivunia sana kujiita baba karibuni. Maisha ya furaha yakatawala kwa kipindi. Mipango ya kufanyika kwa ndoa kati ya aloyce na Alice kimya kimya ikaanza kufanyika.
.
***************

Siku zilikuwa zinazidi kusonga. Zile ahadi za wapenzi kati tya Alice na Aloyce juu ya kufunga ndoa ya siri siri bila wazazi wa Aloyce kujua sasa zikawa zikikaribia kufika ukingoni. Wiki moja kabla ya mipango yao ya ndoa kufanyika kila mmoja alionesha kuchanganyikiwa na shughuli hiyo. Kwa upande wa Aloyce aliamua kusafiri mpaka Lagos, Nigeria kwenda kuandaa mazingira ya kufungia ndoa ikiwa ni pamoja na kumuandaa mchungaji wa kuwafungisha ndoa. Nyumbani akabaki Alice na mama yake wa kufikia, Janet.
“Mwanangu Alice, embu tazama muda umekarbia kuisha na hapa tutapata aibu kubwa sana mwanangu kama tutarudishwa Tanzania. Ndio unaelekea kuolewa hivi karibuni na si unakumbka kuwa rais mwenyee wa nchi hii hakutaki uolewe na mtoto wake..?”
“Ndio mama lakini si kama tulivyopanga ndoa yenyewe itakuwa ya siri kubwa. Na naamini kwa hilo mama yangu tumeanza kukaa hapa kwa siri bila kutujua kama bado tupo Rwanda ni siri kubwa. Wewe unazani itakuwa rahisi kujua hiyo siku ya ndoa..?”
“sikatai kuishi kwa siri mpaka sasa hivi tunaishi hivyo. Ila ninachotaka mwanangu tufanye kitu kimoja. Na mimi niko tayari kukusaidia kuwa bega kwa bega na wewe mpaka mwisho..”
“kitu gani hii mama..?”
“Mwanangu tusiwe kama wajinga na mapunguani. Hivi si unajua dhiki tulizoziacha huko Tanzania..?”
“Bado unaniweka njia panda mama yangu embu niambie nini hicho..?”
“Mwanangu nataka tuandae mipango kabambe mimi na wewe. Mipango ambayo hata Aloyce hawezi kujua chochote kama sisi ndio tumehusika..?”
“enhee, mipango gani tena hiyo mama..??”
“Mwanangu Alice. Nataka tufanye juu chini tuweze kumuua Rais wa Rwanda ,Kagwa yaani huyu baba yake na Aloyce. Tumuue kwa mikono yetu..”
“Mama hapana mimi siko tayari kufanya hivyo, hapana..? niue tena kwa mara ya pili..?? hapana..??”
“Kama hutaki jua gereza linakuita Tanzania, wewe unafikiri kuna ndoa ya siri hata siku moja kwa mtoto wa rais ambaye anajulikana nchi nzima. Hapo si lazima baba yake ajue na akijua..? unafikiri hana uwezo wakutuua ama kuturudisha Tanzania. Na si unajua tulichokifanya Tanzania nakuja huku..?? Haya ukiachana na hayo kama tutafanikiwa kumuua basi kaa ukijua mali zote zitakuwa kwetu. Yaani Aloyce lazima awe mrithi wa baba yake hivyo atakuwa rais na wewe ndio utakuwa ‘first lady’ haya niambie hiyo furaha na amani ya ndoa itakavyokuwa..? hata aje rais watanzania hatuwezi kufungwa tena..?”
Yale maneno yakamjaa Alice. Moyo wa Alice ukayapokea nakuyaweka akilini kwa muda mrefu. Akapingana sana na moyo wake lakini moyo ukamzidi nguvu nakuamini maneno yote yalioukua yakitoka kwa mama yake wa kufikia,Janet.
“Sawa mama nimekubali..”

“Hapo mwanangu umenifurahisha sana, sana tu na cha kufanya inatubidi mikakati hi tuianze mapema kabla hata Aloyce hajarudi kutoka Nigeria..”
“Mama..? ila mbona kama moyo wangu unasita kufanya hivyo..? kwanini mama tusimuue lakini tuishi kwa siri siri hivi hivi..?”
“Alice sasa nadhani hapa kama tunabishana enhee? Kwanini unakuwa sio mwelewa mwanangu..? mimi bado nakupenda tena sana tu na kwa kukuhakikishia hilo niko tayari nife mimi ili wewe uishi vizuri na Aloyce”
“Hapana mama usiseme hivyo..?”
“Alice tambua kwamba nafanya yote haya kwa sababu nakupenda na najua matatizo ambayo yamekuandama. Wewe unafikiri mimi napenda turudishwe wote Tanzania tena tukaukumiwe..? Cha kufanya naona niachie mimi nitatumia kila njia kuhakikisha namuua rais ikibidi namimi nitajiua”
“Mama..? mama? Hivi ni wewe leo unaoongea haya au..?”
“Mwanangu Alice nimechoka na maisha haya. Kama unavyoniona naumia sana katika hii dunia wewe angalia ni nani atanioa wakati sina hata uwezo wa kupata ujauzito. Mme wangu John alikuwa akinisaliti kwa sababu hiyo hiyo. Umri wangu sasa hivi umekwenda sana na bado naishi na wewe na sihitaji hata kuwa na mwanaume maishani mwangu na ndio maana nimeamua nife nikapumzike kwa amani..!!”
Yale maneno yakamuingia sana Alice mpaka kwenye halmashauri ya ubongo wake. Akajihisi huenda yeye ndio chanzo cha kuchangia matatizo yote. Kuishi kwao kwa siri ndiko kukamuumiza sana Alice.

BAADA YA WIKI MOJA


‘NAFURAHI KUKUALIKA KATIKA HARUSI YANGU NITAKAYOIFANYA LAGOS NCHINI NIGERIA MIMI NA MTOTO WAKO ALOYCE. HAKIKA KWA MUNGU HAKUNA LISHINDIKANALO. ALOYCE HAWEZI KUKUALIKA BALI NI MIMI PEKEE’ ALICE MAJALIWA. ‘
Ujumbe mkali ulikuwa umeshaandaliwa kwa kuandikwa vizuri na Janet bila hata ya kumshirikisha Alice. Malengo yake makubwa yalikuwa nikuona rais Kagwa akihudhuria harusi hiyo na papo hapo ndipo atakufa naye. Kiasi cha dola za kimarekani elfu arobaini kilimtosha kabisa Janet kufanya kile alichokusudia kufanya. Siku mbili kabla hawajasafiri kwenda Lagos, Nigeria asubuhi na mapema alikuwapo maeneo ya ikulu anapoishi rais Kagwa wa Rwanda. Akamtafuta mlinzi mmoja wapo wa zamu kisha akamuita kwa siri siri nakumnong’oneza kitu.
“Nipo hapa kwa shida moja tu..”
“iko bado elewa mama..? shida migani..?”
Alijibu mlinzi kwa sauti ya chini chini. Alikuwa akimfahamu fika Janet toka kipindi kile akiongozana na Aloyce pamoja na mtoto wake wa kufikia,Alice kumsalimia rais Kagwa.
“Chukua kwanza hizi pesa halafu ndio nikwambie”
Kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa umemtawala mlinzi. Akutaka hata kujifikiria mara mbili zaidi ya kugeuka huku na kule kuangalia kama kuna mtu yeyote anamuona kisha akapokea.
“Haya tell me..”
“Hiyo pesa ni kama zawadi yangu kwako endapo utanifanyia kitu kimoja tu mzee wangu.. Si unajua nipo hapa kimakosa na hatutakiwi hata kufika hapa..?”
 
73.
“Ndio ipo jua na bosi kama natokea hapa sa hizi iko timua mimi pana tena pata job kwake..”
“Ni kwamba chukuwa karatasi hii. Ikifika keshokutwa mchana mpe rais kikaratasi hiki akisome na usimwambie kimetoka kwangu bali mwambie kimetoka kwa Alice, sawa..?”
Yule mlinzi akakipokea kama kilivyo kisha akakidumbukiza katika mfuko wake wa suruali. Akafurahia sana kiasi cha hela ambacho alikuwa akikipata kila baada ya mwisho wa mwezi sasa kakipata ndani ya dakika chache.
“Hapana wasi wasi tafika hiyo keshokutwa chana..?”
Janet akamkabidhi nakutoka katika eneo hilo akiwa na furaha ya hali ya juu. Furaha ya yeye kufanikisha kile alichokuwa akikitaka. Akarudi mpaka kwake alipokuwa akiishi na Alice kisiri siri.
“Alice mwanangu zoezi la kwanza nimeshalimaliza hapa bado zoezi moja tu..”
“Mama zoezi gani tena..?”
Alice akiwa bado njia panda punde Janet akapigiwa simu.
“Haloo mama..”
“Ndio mwanangu Aloyce embu tuambie baba mbona umekaa kimya tena tangu jana hatujapata mawasiliano na wewe?”
“Ni kwamba bado tunaendelea na mipango ya harusi na kwa kusema kweli hapa tulipofikia ni pazuri . Mpaka sasa wageni takribani ya kumi kutoka sehemu tofauti tofauti tena kwa siri kubwa wameshapata mualiko na wengine bado naendelea kuwaalika na tunachosubiri ni harusi tu mama yangu..”
“Kweli baba..? haya embu ongea na Alice”
“Haloo”
“muke aku tarajiwa. Alice?”
“Abee mme wangu niambie unaendeleaje.?
“Almost kila kitu inaenda sawa. Iko nunulia gauni muzuri sana kwa harusi. Keshokutwa iko tuma ndege kuja kuchukua nyinyi uko”
“Saa ngapi”
“iko kuja keshokutwa asubuhi sana ipo uko”
“Sawa nakupenda sana Aloyce”
“I love you too my princess”
Alice akajihisi mwili kumtekenya kwa furaha. Tabasamu pana akalitoa huku akiikata ile simu na kuibusu.

************

Urafii wa karibu aliokuwa amejiwekea Aloyce Kagwa kwa baadhi ya wahusika wa masuala ya urembo na marafiki wa karibu kutoka nchi mbali mbali ni kati ya vitu vilivyokua vikimpandisha chati jijini Butare,Rwanda. Aloyce alikuwa na idadi kubwa sana ya waandaaji kutokana na kusaidiana na waandaaji wao kuwainua wanafunzi wanaotoka katoka chuo chake cha urembo na utalii cha Loyce Training Collage. Siku moja kabla ya harusi yake kufika Aloyce alichukuwa simu yake ya kiganjani pamoja na kitabu chake cha kumbu kumbu nakuanza kuwaalika marafiki ambao aliwaona wana umuhimu kuhudhuria sherehe ya harusi yake. Akaanzia Botswana akamualika raifiki yake mkubwa na muandaaji wa mashindano ya urembo Edgar Zokhilima. Alipomaliza akampigia tena muandaaji wa Lilongwe,Malawi Thumbiko Msiska. Ikamchukuwa zaidi ya lisaa kuwapigia nakuwapa taarifa za ghafla. Jeuri ya pesa aliokuwa nayo Aloyce ikamfanya akodi ndege binafsi ikawachukue wale wote ambao amewalika kesho yake. Akalipia gharama zote za hoteli mpaka siku ya kuondoka kwa wageni waalikwa.

*******

Miaka kenda ikawa imeshapita tangu John apotelewe na Alice na mke wake, Janet. Uzembe wa mapolisi kwa kula rushwa na kuwaachia Alice na Janet kulimuumiza sana John. Akajitahidi kuifuatilia kesi. Kesi ikamchukuwa muda mrefu bila mafanikio yeyote. Ikambidi akubaliane na ukweli juu ya kutoroshwa kwa Alice na Janet. Hakuwa akijua ukweli walipotokomea zaidi ya kuweka katika kumbu kumbu zake kuwa Alice na Janet hawapo tena Tanzania. Maisha yake yakawa ya shida sana kutokana na mazoea ambayo alijijengea ya kupikiwa chakula na mkewe,Janet. Alijutia sana kitendo cha kumnyima ushindi Alice. Akajikuta hata kwanini aliamua kutembea na marehemu Jamila. Akawa ameshazoea sasa maisha ya kuishi peke yake huku akila kiapo na moyo wake kuwa kamwe hatokuja kutembea na mwanamke wa aina yeyote maishani mwake labda Mungu awakutanishe tena na mkewe, Janet.
Thumbiko Msiska raia kutoka Lilongwe, Malawi alipopata tu habari ya kupokea mualiko wa kuhudhuria harusi Lagos, Nigeria ya mtoto wa rais Aloyce. Thumbiko alikuwa akisoma na Aloyce kipindi cha nyuma nchini Malawi kabla hajaamishiwa kuelekea Napoli, Itali. Kitendo cha Aloyce kumuoa mtanzania kikamgusa sana Thumbiko. Akachanganya akili yake kwa haraka zaidi. Akamkumbuka sana rafiki yake wa zamani sana ambaye walishasoma wote katika chuo cha ST. ETTIENNE UNIVERSITY lakini alikuwa akiishi Tanzania.
“John!! John?? yeah nimekumbuka alikuwa akiitwa John Mapunda”
Kwa haraka haraka Thumbiko akachukuwa kitabu chake kidogo cha kuhifadhia kumbukumbu nakumtafuta John. Akafanikiwa kupata namba ya simu ya Johh Mapunda. Akaipiga hapo hapo bila kupoteza muda.
“Helow John my friend..?”.
“Halo, naongea na nani mwenzangu??”
“Oohh, John wajua siku zote sauti inaweza kupotea lakini mutu yenyewe kamwe haiwezi potea. Unaongea na Thumbiko hapa”
“Thumbiko?, mbikoooo!! wa wapi?”
“Ca’mon John thumbiko from Malawi”
“Ohhh, Thumbiko Msiska?”
 
74.
“Yap, jina yangu hiyo. Niambiye za masiku friend. Niko na habari njema nataka niku postiye?”
“Tell me Thumbiko, niambie tu hakuna shida kwani ni muda mrefu kidogo hatujaonana? Toka kipindi kilee tukisoma wote huko Malawi.”
“Ndio, na kwani si bado unajishugulisha na ile masuala ya urembo tuliosomea?”
“siwezi kuacha bwana kwani ndio yanayoniweka mjini, haya niambie habari gani tena mpya unataka kuniambia rafiki?”
“Wajua niko bado closed sana na rafiki yetu moja hivi tulishasoma naye hapo nyuma pale ST. ETTIENE.”
“NAni tena huyo”
“Aloyce kagwa yule mtoto aliokuwa na miakili sana lakini ilikuwa ikipenda sana misifa”
“Yeah, nimeshamkumbuka kwani yupo wapi sasa hivi??”
“Jana kanipigia simu kuwa nihudhurie harusi yake na anafunga na msichana kutoka Tanzania tena ameniambia kuwa ni mrembo balaa. Hivyo fanya juu chini bwana tukahuhurie kwani anaifanyia Lagos, Nigeria na atatuma ndege ije kunichukua hapa Malawi kesho.”
“Ratiba zangu zinaniruhusu na kwa sasa nipo katika likizo ya miezi miwil. Kwahiyo mimi nije mpaka hapo Malawi?”
“Ndio jitahidi anza safari hata sasa hivi ili kesho asubuhi uwe umeshafika hapa Lilongwe tukaondoka wote. Kwanza itakuwa na furaha ya kuonana na wee tena pili hata Aloyce tutakuwa tumemfanyia maajabu sana kutokea kwa pamoja kutokana na siku mingi hatujaonana naye”
Thumbiko na John wakawa wameshawekeana ahadi ya kukutana Lilongwe, Malawi kesho yake kwa kusubiri ndege ambayo itatumwa na Aloyce. Ndege ambayo itawapeleka moja kwa moja mpaka Lagos, Nigeria ambapo harusi kubwa itafanyika.

********

Saa sita ya mchana, jula lilikuwa kali sana. Joto lilizidi kulitikisa jiji la Butare. Kila mmoja alitamani japo kuvaa nguo nyepesi kutokana na joto lililokithiri. Alice na mama yake wa kufikia, Janet walikuwa tayari uwanja wa ndege kisiri siri. Ndege aina ya Concord 064 ikawa ipo tayari kuwachukuwa. Wakafuata maelekezo yale yale waliopewa na Aloyce. Melekezo ya wao kupanda ndege na kufikishwa mpaka Lagos, Nigeria. Muda wote mpaka wanapanda ndege Alice alikuwa mwenye furaha sana, furaha ya yeye kwenda kuolewa na mtu aliyempenda maishani mwake. Akawa ni mtu wa kuvuta taswira nzima ya harusi yao itakavyokuwa. Akazidi kujenga picha ukumbi utakavyokuwa umerembwa, akajiangalia vizuri mwili wake. Akaangila sana eneo la mikono yake. Furaha yake yote ikawepo katika kuangalia kidole kimoja cha mkononi. Kidole ambacho yeye atavalishwa pete kwa mara ya kwanza na Aloyce. Kidole ambacho kitamfanya aape mbele ya mchungaji kwa kumvalisha Aloyce pete. Akajikuta akicheka mwenyewe nakuuchukua mkono wake akaubusu nakuuweka kifuani.
Yale mapinduzi ambayo Janet alikuwa akiyafikiria sasa yakawa yanaenda ukingoni. Mpaka wanapanda ndege akili ya Janet ilikuwa bado ipo katika mfuko aliokuwa ameushika. Mfuko mdogo wa kaki ambao hata Alice hakujua kuna kitu gani kwa jinsi ulivyokuwa umefungashwa. Njia pekee ambayo ilimfanya mpaka Janet akatafute kambi za jeshi za nchini Rwanda kisiri siri nakununua mabomu mawili ikawa imefanikiwa. Ule mfuko wa kaki ndio ukawa na kazi ya kubebelea mabomu yale. Janet akaona hakuna tena umuhimu duniani. Ni bora akifika huko ajiuena rais ili mradi Alice apate maisha mema na mchumba wake Aloyce. Akili ya Janet kubwa ilikuwa ni jinsi atakavyoiona tu sura ya rais Kagwa, iwe kanisani ama ukumbini ndipo ataenda kumkumbatia na kulipuka naye hivyo kutawafanya wote na rais kupoteza maisha.
Ikawachukuwa masaa saba kufika Jiji la Lagos,nchini Nigeria. Hapakuwa mbali sana kutokea Rwanda. Watu maalumu ambao walitumwa na Aloyce kwa zoezi zima la kuwachukua Alice na Janet kisha kuwapeleka mpaka hotel maalum likawa likifanyika. SONDOLEE HOTEL ya kifahari ndipo walipokuwa wamefikia Janet na Alice. Hawakuwa na mizigo mingi zaidi ya kibegi kidogo tu ambacho Alice alikuwa amekibebelea toka wametoka Rwanda. Kibegi ambacho kilikuwa na nguo chache sana za kubadilisha.

ASUBUHI

Hali ya hewa katika Jiji la Lagos, Nigeria ilikuwa ya ubaridi kidogo. Janet na Alice waliamka salama. Hawakupata bahati ya kuonana na Aloyce zaidi ya kuwasiliana naye toka wamefika Nigeria. Aloyce akawa ameshawatuma watu wake wampelekee Alice nguo za kwenye harusi sambamba na gari maalum la kuwachukua yeye na mama yake. Milton na Onyise ni kati ya raia wa Nigeria waliokuwa wamepewa majukumu mazito ya kuhakiskiha Alice na Janet wanapatiwa huduma zote kuanzia saluni, mpaka wanaingia kanisani vivyo hivyo mpaka kanisani.
 
75.
Milton na ONyise wakawa ndani SONDOLEE HOTEL uso ka uso na Janet na Alice. Wakasubiri wakijiandaa. Alice akawa ni mtu wa kwanza kuingia bafuni kuoga. Ikambidi janet amsubiri mpaka atoke na ndani ya dakika kumi Alice akatoka nakuingia Janet. Alipomaliza kuoga wote wakapewa zile nguo moja kwa moja kutoka kwa Onyise na Milton. Gauni zuri la harusi likampendeza sana Alice. Akajihisi kama anaenda kushindana tena katika mashindano ya urembo kwa nchi ya Nigeria. Mawazo ya ghafla yakateka kichwa chake nakujiona kana kwamba yupo katika kuingia mashindano ya mrembo wa dunia. Akajikuta akiifariji roho yake kwa muda mfupi. Baada ya muda Janet naye akawa ameshamaliza kuoga na kuvaa kabisa.
“We are okey..”
Janet akawaambia Milton na Onyise. Wakatoka mpaka nje tayari kwa kuingia kwenye gari.
“OOH my God, a moment please..!”
Janet akawa kama amesahau kitu wakati wanaingia tu kwenye gari. Akashuka haraka nakukimbia mpaka ndani ya hoteli. Mawazo yake yakawa sahihi kwani alikuwa amesahau kile kifuko kilichokua na mabomu. Akayachukuwa moja kwa moja nakufunga na kamba kisha akayapitisha kwenye kiuno chake mithili ya shanga zile za kiunoni. Akajirudishia nguo zake vizuri na zoezi zima la kurudi kwenye gari likaanza.
*********************************

*******

OMMOSE BEAUTY PARLOUR saluni mpya kabisa na ya kisasa iliyokuwa na kila hadhi ya kuitwa saluni. Wasanii wote wa kike maarufu nchini Nigeria walikuwa wakipenda sana kutumia saluni hiii ambayo ilikuwa ikimilikiwa na tajiri mdogo kutoka ukoo wa Baisee, Juniour Obange. Mandhari ya saluni hiyo yalikuwa yakuridhisha kutokana na kuwepo kwa eneo kubwa sana la kupaki magari sambamba na miti ya maua iliokuwa imezungushiwa kila baada ya hatua tatu nne. Walinzi wawili wawili waliokuwa wameketi kila baada ya uzio wa maua walifanya kupendezesha sana saluni hii. Muda wa saa sita za mchana Milton na Onyise wakawa tayari wameshaingia katika eneo la saluni ya Ommose huku wakiwa na watu waliokuwa wameagiziwa na Aloyce. Watu ambao mmoja wapo angetakiwa kuolewa na Aloyce. Ambao ni maalum na ndio waliofanya Milton na Onyise kujipatia fedha za bure kutoka kwa Aloyce kwa ajili ya kuwafuata kuwa peleka saluni na kisha kuwapeleka mpaka kanisa la St. Gasper liilopo mji mkongwe wa Abuja, Nigeria.

Muda wa masaa mawili yalitosha sana kwa Alice kupambwa na kuwa bibi harusi kamili. Bibi harusi wa kimataifa. Ule uzuri aliokuwa nao kipindi cha nyuma wakati anashiriki mashindano ya urembo wa Tanzania sasa ukawa umemrudia upya. Alice akang’aa sana mara mbili zaidi.

“Mwanangu umependeza sana, sasa uko tayari kwa kuolewa na hata Aloyce akikuona lazima ashtuke sana na kufurahi na moyo wake”

“Kweli mama?”

“Kweli mwanangu embu jiangalie hapo kwenye kioo halafu jiangalie juu mpaka chini?”

Alice akafanya kama alivyokuwa akiambiwa na mama yake. Akajiangalia kila pande huku akionesha tabasamu. Akajihisi ana amani na moyo wake. Amani ya yeye kupendeza.

“Take it??”

Milton akatoa ua kubwa katika mfuko wake nakumkabidhi Alice alibebelee. Lilikuwa ni ua kubwa la urembo. Ua spesho kwa mabibi harusi pindi wanapokuwa kanisani hata ukumbini.

“Ohh thanks”

“Ok sasa tunaweza kwenda mwanangu Alice”

“Mama, wewe huseti? Mimi najua nawewe unatengeneza hizo nywele?”

“Hapana mwanangu nahisi mpaka namimi nianze kuandaliwa tutachelewa hata hiyo harusi na sipendi itokee hivyo”

Janet akajitahidi kutumia uongo mfupi ili Alice asielewe chochote. Akaona haina umuhimu tena kwake wakujiandaa kutengeneza nywele zake kwani alipokuwa akielekea ni kujitoa muhanga kwa kujilipua. Alichokifanya akachukua kitana kikubwa pale saluni nakujichana nywele zake kawaida tu kisha akamalizia kwa kuzibana na kibanio kidogo. Kamwe hakutaka asaidiwe na mtu yeyote wala kuketi katika kiti kwani aliona kufanya hivyo huenda ingetokea bahati mbaya yale mabomu yakalipuka mule saluni.

“Twaweza kwenda sasa”

Janet akamwambia Alice kisha akawaoneshea ishara Milton na Onyise wakaelekewa katika gari na safari ya kuelekea kanisa la mtakatifu Gasper ikaanza. Kadri walipokuwa wakitembea na gari ndipo na hisia za Alice zikawa zinazidi kumkumbusha vitu mbali mmbali ambavyo vilikuwa kama ndoto kwao. Kwanza ndoto ya kuolewa maishani mwake. Pili jinsi atakavyopokelewa kwa shangwe ukumbini. Umbali wa kilomita mbili kutokea kitongoji cha Baisee mpaka Jiji la Abuja ukawa umeshakamilika. Kanisa kubwa la mtakatifu Gasper lililokuwa lina uwezo wa kuingiza mpaka waumiini zaidi ya elfu moja sasa likawa limetawaliwa na waumini chini ya thelethini. Kikundi cha matarumbeta ndicho kiliongeza idadi kubwa ya wahudhuriaji. Kitendo cha Alice kuingia ukumbini pembeni yake mama yake wa kufikia,Janet akiwa amemshikilia mkono kiliamsha hisia miongoni mwa wahudhuriaji ukumbini. Aloyce tayari alikuwa upande wa mbele kabisa ya kanisa akimsubiria mchumba wake Alice. Macho ya Alice yakaanza kuangaza huku na kule kumuangalia Aloyce. Hayakuchukuwa muda yakagongana uso kwa uso na Aloyce. Mwili wa Alice ukasisimka. Hakutaka kabisa kuamini kama zile ndoto zake leo hii zinakamilika. Matarumbeta yakazidi kuhamsha hisia ndani yake. Nyimbo mbali mbali za sherehe kwa lugha ya kinaijeria zikaliteka kanisa. Si Alice wala Aloyce na hata Janet waliokuwa wakizifahamu nyimbo hizo nzuri zenye lafudhi ya kuvutia kwa lugha ya kinaijeria.
 
76.

Alice akawa akisindikizwa na matarumbeta kuelekea mbele ya kanisa alipokuwa Aloyce. Aloyce naye akasimama huku akimsubiri mchumba wake Alice afike karibu ili wafungishwe ndoa. Ndoa ambayo ilikuwa ndoto katika vichwa vyao tangu zamani sasa ikawa ni kweli. Machozi ya furaha yakaanza kutirirrika katika paji la uso la Alice. Alice hakuweza kuyafuta kutokana na ua kubwa aliokuwa amelishika mikononi mwake. Pembeni yake alikuwepo mama yake wa kufikia,Janet akilishika gauni lake lisimdondoke. Wakasogea taratibu mpaka wakafika eneo la mbele kabisa ya kanisa. Sasa wakawa wameshamkaribia Aloyce. Furaha ikalipuka ndani ya kanisa mara mbili ya pale ilivyokuwepo. Furaha ya Aloyce kutaka kumkumbatia mchumba wake Alice ikasisimua sana mwili wake. Akaitoa mikono yake miwili nakuielekeza upande alipokuwa anatokea Alice. Alice akalitupa lile ua pembeni nakumkumbatia Aloyce kwa nguvu na kwa hisia kali. Hisia za yeye kugusana na mwili wa mchumba wake kwa mara nyingine. Yale machozi yaliokuwa yakiendlea kumtirirrika sasa yakaongeza kasi zaidi. Yakaanza kuteleza mpaka katika gauni lake. Macho yake yakazidi kuwa meupe zaidi kwa furaha aliokuwa nayo Alice. Aloyce naye akajihisi mwili wake kama umemwagiwa maji ya barafu ghafla. Moyo wake ukawa umezungukwa kwa wingi wa ubaridi ambao ulichochea hisia zake kifuani mwake. Alipomaliza kumkumbatia Alice akachukuwa mikono yake nakutaka kumkumbatia na Janet.
.
“Noo!!!, nooo!! Aloyce, nooo???”

**********

Thumbiko Msiska muda wote alikuwa stendi ya mabasi ya Lilongwe akimsubiri kwa hamu sana John na usiku hiyo hakuweza kupata hata tone la usingizi. Furaha yake kubwa ilikuwa ni kukutana na rafiki yake John waliosoma wote chuo cha ST Ettiene, Malawi. Ilimchukuwa John masaa zaidi ya kumi mpaka kufika hapo Lilongwe,Malawi. Sasa John na Thumbiko wakawa wameshakutana pamoja. Kila mmoja akawa na furaha ya kuonana na mwenzake. Wakatafuta hoteli pale pale stendi ya mabasi Lilongwe wakalala. Usiku wote wakawa ni kupiga soga tu nakukumbushiana mambo ya zamani pini wakisoma. Asubuhi na mapema Thumbiko na John wakaelekea uwanja wa ndege. Malengo yao makubwa yakawa ni kusubiri ndege ambayo walikuwa wamehaidiwa na Aloyce kutumwa. Ndege ambayo itawatoa na kuwapeleka mpaka Lagos,Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria sherehe kubwa ya kifahari ya harusi kati ya Aloyce na binti mrembo kutokea Tanzania.

“Kwani msichana mwenyewe anayeolewa, humjui hata jina Thumbiko??”

“Hapana jua. Wajua yeye alini tell kuwa anatokeya Tanzania na ni mrembo balaa but kwa jina hakuniambiya wala sikumuuliza”

Wakabaki wote wasindikizaji tu huko wanapoelekea. Siri kubwa ikabaki mioyoni mwao. Siri iliyojificha. Si John wala Thumbiko aliyetambua siri ya harusi wanapoenda kuwa itakuwa ya Aloyce na nani zaidi ya kujua kuwa Aloyce anaoa binti mrembo kutoka Tanzania. Wakawa bado wapo uwanja wa ndege wa Lilongwe,Malawi wakizubaa wenyewe. Thumbiko akawa anahangaika kufanya mawasiliano na Aloyce kwa kutumia simu yake ya mkononi japo kujua kama hiyo ndege imeshatumwa ama haijatumwa. Mawasiliano kwake yakawa hafifu. Aloyce hakuwa akipatikana kwenye simu kwa muda huo. Thumbiko akahangaika sana kuirudia ile namba ambayo ilipigiwa mara ya mwisho na Aloyce kisha kupewa mualiko bado jibu likabaki kuwa pale pale kuwa hapatikani. Mara wakashangaa ndege aina ya Concord 096 ikiwa na bendera ya Nigeria mkiani mwake ikitua huku ikiwa imepakiza watu wawili na rubani.

“Are you Thumbiko (wewe ni Thumbiko?)”

“Yes it’s me. (ndio mimi)”

“We are from Nigeria and we have come to take you? (Tumetokea Nigeria na tupo hapa kwa ajili ya kuwachukuwa)”

“I’ts okey but am with my friend?(Sawa lakini nipo na rafiki yangu?)”

“Let’s go certainly all (hapana shaka twendeni wote tu)”

Thumbiko na John wakaingia ndani ya ndege. Safari ya kutokea uwanja wa ndege wa Lilongwe,Malawi kwenda Lagos,Nigeria ikaanza. Hapakuwa na umbali sana kwani iliwachukuwa mwendo wa masaa tisa kuwa hewani mpaka Nigeria

“The wedding was held in Abuja afternoon. And now we take to Darlington Hall.(harusi ilishafanyika Abuja mchana na tupo hapa kuwapeleka ukumbi wa Darlington)”

“Even in hall no problem if we joined our friends at the wedding ceremony.(hata huko ukumbini haina shida kama tutaungana na rafiki yetu katika sherehe ya harusi.)

Wakashushwa uwanja wa ndege Lagos nakupakizwa kwenye taksi kisha mmojawapo akawasindikiza moja kwa moja mpaka ukumbi wa Darlington. Mandhari ya ukumbi wa Darlington kwa jinsi ulivyokuwa umepambwa ukawavutia sana Thumbiko na John. Kamera ndogo ambayo John aliibeba kutokea Tanzania sasa ikawa imeshapata kazi. Akaanza kupiga picha hapa na pale.wakaingia ndani ya ukumbi ambapo shangwe na vigelegele vilizidi kutanda. Kila meza ilikuwa imejazwa vinywaji mbali mbali huku ikizungukwa na watu wawi wawili tu. Thumbiko na John wakaingia mpaka ndani. Wakapatia siti ya nyuma nyuma kwakuwa walikuwa wamechelewa kidogo kufika ukumbini. Hawakuweza kumuona Aloyce na msichana aliyefunga naye ndoa kutokana na wao kukaa mbali sana. Kadi ya pongezi kwa wahudhuriaji ambayo ilikuwa mezani ndiyo ilimchanganya sana John. Akaiangalia mara mbili mbili bila kupata jibu. Hakutaka kabisa kuamini jina la Alice Majaliwa ndiye huyo anayemjua zaidi ya kusubiri kama atapata bahati ya kumuona huyo bibi harusi. Amani ikampotea kabisa John. Akawa hatulii kabisa ukumbini. Akaichukuwa tena kamera yake japo kuwavuta kwa karibu kwa kutumia ile kamera yake napo haikusaidia chochote. Kamera ikashindwa kabisa kuvuta mandhari halisi. Picha ya mwanga hafifu haikusaidia kumgundua bibi harusi aliyekuwepo ameketi mbele pale na Aloyce. Wakabaki wakizungumza wenyewe wakijipa moyo lazima wataonana na Aloyce na pia watapata tu bahati ya kumuona huyo mrembo anayejisifu Aloyce kuwa ni mzuri. Wakiwa bado katika maongezi Thumbiko na John mara wakashangaa kumuona mzee mnene mrefu aliyevalia suti nyeusi akiingia ndani ya ukumbi pembeni akiwa na mwanamke huku nyuma akiongozana na rundo la mapolisi waliovalia sare za mapolisi wa Nigeria. Mikononi mwao walikuwa wameshika silaha kali. Thumbiko na John wakabaki midomo wazi wakiendelea kutoa macho. Ukumbi wote ukawa kimya ghafla kuwatazama mara wakashangaa kumuona mwanamke akipita mbele yao. Akiwa katika hali ya kujiamini yule mwanamke akazidisha mwendo kasi huku akiwa katika kukutana nao uso kwa uso na yule mzee. Kabla hajakaribia kuwafikia wakashuhudia yule mwanamke akivua gauni lake nakubakiwa mtupu kama alivyozaliwa huku kiunoni mwake akiwa amezungushia vitu viwili vikubwa mithili ya hirizi. Kabla hawajawafikia tu..

*********
 
77.

Taarifa juu ya Aloyce Kagwa kufunga ndoa na Alice Majaliwa Lagos nchini Nigeria zikamfikia moja kwa moja baba yake na Aloyce, Kagwa Kwisereka ambaye ni rais wa nchi ya Rwanda. Kikaratasi kidogo ambacho alipatiwa na mlinzi wake ndicho kiliahamsha hisia tofauti kwa rais Kagwa. Akajihisi presha inataka kumtawala. Majasho yakamtoka sambamba na macho huku asiamini kile kikaratasi. Kile kikaratasi alichopewa na mlizi akampatia mkewe moja kwa moja asome na yeye ajionee.

“Alice yupi mume angu?”

“Yule tuliofukuza, ile nakaa Tanzania”

“So, leo ndio nafunga ndoa?”

“Yes”

Rais kagwa akachanganyikiwa zaidi. Akachukuwa simu yake ya mkononi nakumpigia mtoto wake Aloyce. Simu ya Aloyce haikuwa ikipatikana. Akajaribu zaidi ya mara tano lakini jibu nalo likabaki pale pale kuwa hapatikani.

“Tukwende kake?”

Rais Kagwa akamuamrisha mkewe, akamchukuwa bodigadi wake nakupanda gari binafsi mpaka nyumba alipokuwa akiishi Aloyce. Wakajaribu kumuuliza mlinzi lakini hakukuwa na jibu lolote la kuridhisha.

“Hiviii..!!!, najua mimi muzuri?? Takufunga wewe?? Taenda ozea gerezani sasa hivi. Ebu nambie manangu iko wapi? Where is Aloyce?”

Hasira kali zikampanda rais Kagwa. Akamshika mlinzi wa Aloyce shingoni. Akajitahidi kumbana aseme ukweli Aloyce alipo lakini mwisho kabisa yule mlinzi akatoa siri.

“Baba pana jua kabisa. Belive me. But kuna siku nasikia aki talk kuwa iko funga ndoa nchini Nigeria”

Ikabidi baba yake Aloyce akubaliane na maneno ya yule mlinzi kuwa ni kweli mtoto wake anafunga ndoa nchini Nigeria. Akamuachia nakumchukuwa mkewe na bodigadi mpaka uwanja wa ndege. Ndege kubwa ambayo rais Kagwa huitumia kwenye safari za kikazi sasa ikawa kwa kazi moja tu ya dharula. Dharula ya yeye kuelekea Lagos, Nigeria tena kwa haraka sana. Haikuwachukuwa muda wakawa wameshafika Lagos, Nigeria. Akapokelewa kama rasi kwa heshima japo palikuwa usiku kidogo na giza lilishatanda. Moja kwa moja akapelekwa kupumzika hotel ya Victoria Island. Akawapa kazi mapolisi wote wa Lagos kuhakikisha ndani ya nusu saa awe amepata jibu la kufungwa ndoa kwa mtoto wake Aloyce na binti kutoka Tanzania jina la Alice. Aliwaamuru mapolisi pia kufuatilia nakujua kumbi gani unatumika kwa harusi hiyo.

Zaidi ya nusu saa bado rais Kagwa alikuwepo na mkewe pamoja na bodigadi wake kwenye hotel maalum ya Victoria Island. Hotel ambayo viongozi wakubwa wanchi hufikia. Akawasilishiwa majibu kuwa wamefanikiwa kujua Aloyce alipofunga ndoa mpaka jina la ukumbi wa Darlingtion kusherekea harusi hiyo.

“Now we bring the hall” (tupeleke sasa hivi ukumbini?) safari ya kutokea hotel ya Victoria Island ya rais Kagwa na mkewe pamoja na bodigadi wakisaidiwa na mapolisi ikaanza. Ndani ya dakika kumi wakawa wameshawasili ndani ya ukumbi wa Darlington Jijini Lagos. Ukumbi ambao Aloyce alikuwa akifanya sherehe ya harusi yake na Alice Majaliwa. Rais Kagwa akashuka kwenye gari na mkewe pembeni huku upande wa nyuma akiwa na bodigadi wake pamoja na mapolisi zaidi ya kumi huku kila mmoja akiwa na silaha. Kitendo cha wao kuingia ndani ya ukumbi kikafanya ukumbi wote unyamaze ghafla. Kila mmoja akayaelekezea macho yake kwenye lango la kuingilia ndani. Woga ukatawala ukumbi wote. Rais Kagwa na wafuasi wake wakawa bado wanaelekea mbele ya ukumbi alipoketi Aloyce na Alice. Kabla hawajafika mbele wakashangaa mwanamke akitokea upande wa mbele yao kwa haraka haraka akiwafuata kwa kujiamini. Alipokaribia tu eneo alipokuwepo rais Kagwa yule mwanamke akavua nguo zake zote kisha akataka kumkumbatia rais kagwa lakini rais Kagwa akamsukuma yule mwanamke mpaka akadondoka chini kabisa nakuanza kutapatapa.

“Hey, arresting this woman?” (mkamateni huyu mwanamke?)

Rais kagwa Kwisereka akawaamrisha mapolisi aliokuwa nao wamkamate yule mwanamke. Uchafu aliokuwa nao mwilini mwake mithili ya staa aliyejipaka tope vitani ukamfanya rais Kagwa ashtuke zaidi na kutokuelewa yule mwanamke ametoka wapi katika ile sherehe usiku ule. Bodigadi ambaye alikuwa bega kwa bega na Rais Kagwa toka wametoka wote Rwanda huku wakisaidiana na mapolisi kutoka Nigeria, wakafanikiwa kumuweka hatiani yulemwanamke.

Kwa muda wote huo, Thumbiko na John bado walikuwa wameduwaa wakitoa macho wakifuatilia tukio zima la yule mzee alivyoingia ukumbini akiwa na mapolisi mpaka kuvamiwa na mwanamke aliyeonekana kama ni kichaa. John akabaki bado ameishikilia ile kadi. Kadi ambayo ilikuwa ni ya shukrani kwa wageni waalikwa. Akainuka lile eneo aliokuwa amekaa. Akamchukua Thumbiko wake nakuongozana naye wakifuata taratibu nyuma nyuma ule msururu wa mapolisi na yule mzee mpaka eneo la mbele kabisa walipokuwa wamekaa bibi na bwana harusi.

“Where is my Aloyce? Why are you deceived me?” (Aloyce wangu yupo wapi? Kwanini mnanidanganya?)

Rais Kagwa akawageukia mapolisi aliokuwa nao nakuanza kuwagombeza. Akawagombeza kwa kudaganywa kuwa Aloyce anafanya sherehe ya harusi hapo ukumbini.

“Papaa!! here are two venues we forgot to tell you. First floor is the number one venue called Darlington 1 and upstairs there is another venue number two called Darlington 2. And there also is celebrated as these encounters often (Mzee!! hapa kuna kumbi mbili tulisahahu kukwambia. Hapa chini huu ukumbi namba moja unaitwa Darlington 1 na juu kabisa kuna ukumbi mwingine namba mbili nao unaitwa Darlington 2. Na huko nako huwa kunafanyika sherehe kama hizi mara kwa mara.”
.
Wale mapolisi wakajiteteaa kwa Rais Kagwa. Rais na mkewe wakawaelewa.

“Let’s go, Let’s go upstairs?” (Twendeni, Twendeni juu)

Si Thumbiko wala John wote wakabaki wameduwaa. Wakaangaliana mara mbili mbili huku wakimwangalia bwana na bibi harusi pale mbele. Hakuwa Aloyce kama walivyodhania. John hakutaka kuamini kabisa. Akapingana na halmashauri ya kichwa chake. Akaitoa ile kadi aliokuwa ameishika nakuangalia vyema kwa mara ya pili jina la kwenye kadi. Akaanza kujicheka mwenyewe. Marue rue pindi alipokuwa akiingia ukumbini na Thumbiko yalimfanya asiweze kugundua kiurahisi ile kadi. Jina la Alongise Mengaliwa akawa amelifananisha kabisa na la Alice Majaliwa. John akamalizia kwa kujicheka kwa mara ya pili huku akiichana ile kadi.
 
78.
“Thumbiko kumbe wasingekuja hawa polisi tungeumbuka hapa?” “Ni mukweli kabisa John. Kumbe hili limukumbi lina sehemu kubwa mbili? Dah!! Ndio maana watu ilikuwa mingi sana wakati Aloyce alini tell itakuwa michache tu”

“Yeah, halafu inavyoonesha huyu atakuwa baba yake na Aloyce?” “Sijui huenda ikawa ni mukweli John?”

John na Thumbiko wakagongeana mikono huku wakijicheka wenyewe kwa ujinga wao wa kutokujua kama kuna kumbi mbili. Wakafuata nyuma ya ule msururu wa mapolisi wakiongozwa na rais Kagwa. Hapakuwa na umbali sana kutokea ghorofa ya chini. Ikawachukuwa dakika kama tatu kwa kutumia lifti. Wakakutana na sherehe nyingine kubwa sana na ya kifahari kwa muonekano wa juu juu. Ilikuwa ni sherehe ya harusi iliokuwa na idadi ya watu chini ya ishirini. Macho ya Thumbiko na John yakaanza kusambaa kwa udadisi wa kutaka kujua. Thumbiko akawa mtu wa kwanza kumuona Aloyce mbele kabisa ya ukumbi.

“John? Aloyce ile kule meiona, hihi, hiiii, Mependeza!!”

John akahangaika sana na yeye kutoa macho bila kumuona vizuri. Akiwa bado katika hali ya mshangao katika eneo la mbele yake akimtafuta huyo Aloyce, mara jicho lake likakutana uso kwa uso na mkewe Janet. Janet akawa anatembea kwa madoido na kwa haraka haraka akiwafuata kwa kujiamini. Alipofika karibu yao akamkumbatia yule mzee mwenye suti aliokuwa ameongozana na mapolisi. Yule mzee akaonesha kuwa mkali lakini Janet akawa amemkumbatia kwa kumng’ang’ania kwa nguvu. Akiwa bado amemng’ang’ania akashangaa kitu kimemdondoka Janet kutoka kwenye gauni lake. John akaendelea kutoa macho kwa kuangaza kile kitu kilichoanguka. Akaangalia vizuri nakugundua kuwa ni bomu. Bomu lile la kuvutwa kamba na kulipuka. Kitendo cha John kuendelea kulishangaa lile bomu chini uso wake ukawa umeshaonekanika mbele ya macho ya Janet. Wakawa wameshaonana uso kwa uso.

“ Lazima tufe wote sasa hivi John?”

******

Muda wote ndani ya ukumbi wa Darlington namba mbili Alice na Aloyce walikuwa ni watu wenye furaha sana. Harusi ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mc kwa sauti ya taratibu huku ikionesha uchache wa wahudhuriaji. Ilikuwa kivutio kikubwa sana kwa Alice na Aloyce kwa jinsi walivyokuwa wameng’aa. Janet alikuwa pembeni yao muda wote huku akishikilia kitambaa cha jasho nakumfuta Alice kila baada ya muda usoni mwake.

“Alice mwanangu unaonaje siku ya leo?”

“Yaan mama hata nashindwa hata kuielezea. Haielezeki mama. Ni nzuri sana na sintokuja kuisahau maishani mwangu”

Janet alikuwa akiongea na mama yake wa kufikia, Janet muda wote huo. Harusi haikuwa na wasimamizi wa pembeni, ilikuwa ya aina yake. Ulipofika muda wa shampeni, Aloyce akakabidhiwa kuifungua. Akasimama na kuelekea mbele. Suti ya bei ya gharama aliokuwa ameivalia iliwachanganya sana watu waliohudhuria. Haikuwa suti ya bei rahisi kwani matilio yake yalikuwa ya kumeremeta sana na aghali sana. Kwa mbwembwe alizokuwa nazo Aloyce akashikilia ile chupa ya shampeni kwa kujidai nakuanza kuitikisa taratibu juu chini. Akafanya kwa muda kama wa dakika tatu kisha akafungua kikaratasi cha kung’aa katika ile chupa ya shampeni. Lile povu la kwenye Shampeni likatoka kasi ya ajabu na kufanya ukumbi uanze kutamba kwa vigele gele. Aloyce akakabidhiwa kipaza sauti na mc aseme chochote.

“Alice ikujae hapa karibu nikupe”

Aloyce akamgeukia mchumba wake Alice na kumuita. Kwa mwendo wa maringo Alice akachukua glasi mbili nakusogea mpaka alipokuwepo Aloyce na ile shampeni. Aloyce akammiminia na nyingine akajimiminia kwenye glasi yake. Akaishika ile glasi iliokuwa na shampeni kisha akanyanyua mkono wake mmoja nakumshika begani Alice huku ule mkono wake uliobaki akiutumia kumnywesha Alice ile shampeni. Wakawa wananyweshana. Ukumbi ukaendelea kulipuka kwa shangwe. Mshika chochote (mc) akaamuru dj afungulie nyimbo ya kilugha. Nyimbo ya kimila yenye lugha ya ki Nigeria. Akafanya hivyo.

“Aloyce kamwe sintokuja kukuacha mpenzi?”

“Hata mimi iko fanya vivo”

Wakawekeana ahadi huku wakisakata rumba kwa kucheza ile nyimbo iliokuwa ikiimbwa kwa lugha ya ki Nigeria. Hawakujua maana halisi ya ile nyimbo lakini wakawa wakifuata mdundo taratibu wakiicheza. Walipomaliza kucheza mc akaamuru iwekwe na nyimbo ya taratibu. Ikapigwa nyimbo laini kutoka marekani. Bluzi ya mwanamuziki Celine Dion. Nyimbo ya ‘power of love’ ikamkosha sana Aloyce na Alice. Wakajikuta wakifuata maneno taratibu wakiimba kwa pamoja ule mziki. Aloyce akazidi kumkumbatia Alice kwa hisia zote huku wakiicheza ile nyimbo taratibu wakizunguka. Alice hakuwa na uvumilivu, machozi ya furaha yalikuwa karibu na paji la uso wake yakimtoka muda wote kila hatua walioukuwa wakicheza. Kichwa chake kilichanganyikiwa kwa kuzidi kuifikiia siku nakuona kama bado ni ndoto. Wakatumia zaidi ya dakika tano nzima kuucheza muziki. Mc akawaamuru waongoze moja kwa moja kwenda kupakuwa vyakula.

“We will begin to get food for Mr. Aloyce and Mrs. Alice, the next landing seated and began to follow one line.” (wataanza kupakua chakula bwana na bibi harusi kisha wote mtafuata nakuanza kupakuwa kwa kufuata mstari mmoja)

Wote wakatii maneno ya mc. Aloyce akampakulia chakula cha kutosha Alice naye Alice akampakulia Aloyce. Kamwe Alice hakujua vyakula vingi vilivyokuwa vimeandaliwa. Vilichanganyika navykula vya asili vya Nigeria. Vingi Alice alijipakulia tu ili mradi aijaze sahani kwani hakupenda kamwe aonekane mshamba mbele ya harusi ya kifahari.

“Aloyce? Mama yangu yuko wapi?”
 
79.

“Hapana jua, lakini si tuliiacha hapa?”

“Ndio sasa atakuwa ameelekea wapi?”

Alice akashtuka baada ya kurudi kuketi kwenye eneo la mbele kabisa ambalo walikuwa wameketi awali na mama yake wa kufikia,Janet. Janet hakujulikana alipotoweka. Alice akaweka mezani ile sahani iliokuwa na chakula. Akili yake yote ikambadilika nakuhamisha mawazo kwa Janet. Hamu ile ya kula ikaanza kumpotea kabisa.

“Alice, don’t worry, inaweza kuwa imetoka mara moja itarudi tu”

“No Aloyce. Hapana kabisa wacha nimtafute”

Aloyce akajaribu japo kumpooza Alice kwa maneno lakini Alice hakuwa akielewa kitu. Akili yake moja kwa moja ikamrudisha zamani. Ikamkumbusha huenda ameenda kufanya lile tukio ambalo Janet alilizamilia,tukio la Janet kujitoa mhanga. Alice akatoka moja kwa moja mpaka kwa mc. Ukumbi wote ukaonekana kumshangaa Alice. Aloyce akabaki macho akimtolea macho Alice.

“Please, Allow me to give me the microphone immediately.” (Samahani Naomba unipe hicho kipaza sauti mara moja?

Alice akamuomba mc kipaza sauti. Mc akamkabidhi Alice kile kipaza sauti.

“Dear special guests. Thank you for attending my wedding and my husband Aloyce there. I came with my mother and now it does not seem on the venue. wherever you hear my voice come to me.” (Ndugu wageni waalikwa. Asanteni kwa kuhudhuria harusi yangu na mume wangu Aloyce pale. Nimekuja na mama yangu na sasa simuoni hapa ukumbini. Popote ulipo na kama unanisikia njoo mama.)

Alice akamaliza kisha akamrudishia kipaza sauti mc. Akarudi eneo la mbele alipokuwa ameketi na mumewe Aloyce awali.

“Pana kuwa na wasiwasi muke yangu? mama itakuwepo tu na itaonekana”

Aloyce bado akawa ni mtu wa kumfariji Alice. Siri kubwa iliombatana na duku duku ilikuwa bado ikiendelea kumtawala Alice. Siri ya Janet kujitoa mhanga. Kamwe Alice hakutaka Aloyce ajue chochote kuhusiana na hilo. Akakaa kimya. Akachukua glasi yake ile ya shampeni nakuanza kuinywa.

“Basi tule mupenzi angu, tule tu?”

“Aloyce mume wangu. Yaani akili yangu haijakaa sawa. Mpaka nione japo sura ya mama yangu ndio nitaridhika”

Alice akagoma kabisa kula. Aloyce akajitahidi kuzidi kumbembeleza bila mafanikio yeyote. Aloyce akiwa katika hali ya kumbembeleza mkewe Alice mara akashangaa Janet kutokea mlango wa chooni.

“mama yako ile pale nakuja sasa?”

Aloyce akawa mtu wa kwanza kumnyooshea Alice upande aliokuwa akitokea Janet. Tabasamu pana lililoambatana na kicheko cha furaha kikamtoka Alice. Moyo wake ukaonekana kutulia kabisa. Mwili ukaanza kumsisimka ghafla. Akajihisi kama mtu mwenye furaha ya ajabu na iliopitiliza. Furaha yakuanza maisha mapya na pia furaha ya kuiona sura ya mama yake wa kufikia, Janet. Furaha ikahamia moja kwa moja kwa mc baada ya kuona Janet ameonekana. Akamuamuru dj aweke nyimbo nzuri ya kuchezeka ya ki Nigeria. Mc akausimamisha ukumbi kwa mara nyingine, ukumbi ukalipuka upya kwa shangwe huku baadhi yao wakipiga vigele gele na makofi mfululizo. Wakiwa katika hali ya furaha mara ukumbi ukanyamaza haraka. Mc akawa mtu wa kwanza kukimbia ukumbini akikitupa kipaza sauti. Mzee mrefu na mnene aliyekuwa amevalia suti huku pembeni yake akiwa na mwanamke na nyuma kabisa akiwa na rundo la mapolisi waliovalia sare za mapolisi wa Nigeria alikuwa akiingia ukumbini.

“Alice?? Dady huyo, my dady na mumy hao ipo kuja hapa?”

Alice akajihisi jasho linamtiririka mwili wote mithili ya maji yanayofuata mkondo. Akaanza kukata tamaa taratibu. Tumbo lake likaanza kuunguruma kuonesha ishara ya uwoga. Sura ya Rais Kagwa ikawa imemuingia haswa katika halmshauri ya kichwa chake. Akaanza kuhema haraka haraka. Damu zikaanza kumtoka taratibu kupitia pua zake. Macho yakamlegea sambamaba na kuhema kwa haraka haraka huku akianza kujikunja kunja, zile dalili zake za kifafa zikaanza kuchukuwa nafasi yake.
.
“Alice? Alice?? Aliceeeeeee?”

Aloyce akamuwahi kumbeba kabla Alice hajaanguka chini na kuanza kutapatapa. Fahamu zikawa zimempotea Alice kabisa. Aloyce akajisachi mifukoni lakini kwa bahati mbaya hakuwa na ile dawa ya kumpulizia Alice mdomoni pindi anapoishiwa pumzi. Alice akawa ameshapoteza fahamu hajitambui.
 
80.
Aloyce akaonekana kuchanganyikiwa ghafla. Kuchanganyiikiwa kwa kuwashuhudia wazazi wake wakiingia ndani ya ukumbi na pia kuchanganyikiwa kwa mkewe Alice kuanguka kwa kifafa na kupoteza fahamu. Rais Kagwa akawa anakaribia eneo lile alipo mtoto wake Aloyce na mkewe. Kabla hawajafikiwa wakashangaa Janet akitoka mbio nakuwafuata. Alipofika karibu bodigadi akamuwahi kumzuia lakini Janet akawa ameshawakumbatia wote wawili. Polisi wakahangaika sana kumtoa lakini Janet akawa amezidi kung’ang’ania suti ya rais Kagwa huku mkono mmoja akivutwa na bodigadi wa rais Kagwa. Nguvu zikamlegea Janet kwa kiasi kikubwa. Yale mabomu yaliokuwa kiunoni mwake hayakuweza kufanya kazi kwa haraka. Janet akaonekana kama kukata tamaa. Akapigwa sana na virungu vya mapolisi wa Nigeria huku baadhi wakimtishia kumfyatua na bunduki. Akajitahidi kuvumilia maumivu huku akiyatoa macho yake kuangaza huku na kule uso kwa uso yakakutana na mume wake wa zamani,John Mapunda. John naye akataka kuingilia kati amuokoe Janet. Ikambidi Janet aachie ule mkono aliokuwa amemvuta bodigadi wa rais Kagwa kisha akachomoa bomu moja kiunoni mwake nakulipigiza chini kwenye sakafu. Moshi mkubwa ukaanza kutoka katika lile bomu aliokuwa amelipigiza chini. Halikuwa bomu la kulipuka bali lilikuwa ni bomu la machozi. Akili ya Janet ikawa kwenye bomu lililobakia. Asilimia zote alijipa uhakika huenda walimpa mabomu mawili tofauti. Wale mapolisi na watu wa karibu wote waliomsogelea wakaanza kutoa machozi huku wakiwa hawaoni kabisa mbele kutokana na lile bomu. Janet akauchukuwa mkono wake nakuupeleka mpaka kiunoni kwake kulitafuta lile bomu jingine bila mafanikio..

********

Macho yote yalikuwa yakiendelea kumuwasha Janet. Ile mikono ambayo bado alikuwa ameing’ang’ania kwa bodigadi na rais sasa ikawa imeishiwa nguvu kabisa. Akazidi kukata tamaa huku akiendelea kulipapasa lile bomu lililobaki kwa upande wa pili. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu hatimaye akafanikiwa kulipata. Lilikuwa limeshazunguka mpaka kufika maeneo ya mgongoni mwake. Akajitahidi kutumia hisia zake nakulichomoa mpaka karibu na mdomo wake. Akiwa bado macho yake hayaoni. Hayaoni kutokana na lile bomu la kwanza la machozi kuliachia ikabidi atumie hisia. Hisia za kulipeleka lile bomu mpaka maeneo ya karibu na mdomo wake.

“Eeeh Mungu baba, weza kumponya na kumlinda mwanangu Alice, na hii ndio safari nilioamua mimi”

Janet akasali kimoyo moyo nakulivuta kamba fupi lile bomu. Bomu likafanikiwa kulipuka papo hapo. Si John wala si Thumbiko,mke na rais kagwa, bodigadi wala mapolisi wote wakawa nyang’anyang’a kwa kuathirika na lile bomu.

********

Aloyce bado alionesha kuchanganyikiwa kwa kile alichokuwa akikishuhudia kamwe hakutaka kuamini kama baba yak e rais Kagwa kaingia ukumbini hapo. Majasho mengi yakaanza kumtiririka huku akiwa amemshikilia Alice. Akiwa bado katika hali ya mshangao, Aloyce akashangaa Janet ametoka mbio na kwenda kuwahi ule msururu uliokuwa ukiwafuata ukiongozwa na rais Kagwa. Mapigo ya moyo ya Aloyce yakatulia kwa kuona Janet ana akili sana. Akili ya kwenda kuzuia msafara ili baba yake asijue chochote ama kumpata yeye na Alice.

“Sante sana Janet, penda sana wee”

Aloyce akampa pongezi la sauti ya chini chini Janet ambayae alikuwa umbali kidogo na eneo la tukio akiwakumbatia wazazi wa Aloyce. Alichokifanya akamchukuwa Alice wake nakumbeba begani mwake.

“Bye mummy na dady hapa hamumpati Alice yangu tena”

Akatoa maneno ya kejeli japokuwa eneo lilikuwa mbali kidogo kwani hawakuweza kumsikia. Walikuwa wakitapatapa kwa kujikuna maeneo ya machoni mwao kwa muwasho wa lile bomu la machozi ambalo hata Aloyce hakujua kinachoendelea pale. Hatua kumi zilimtosha kabisa Aloyce kuondoka katika lile tukio akiwa amembeba Alice begani na akiingia ndani ya lifti. Akili yake yote ikawa ni kumkimbiza Alice katika chumba maalum ambacho alikuwa amekiandaa kwa ajili ya kupumzika naye pindi akimaliza sherehe yake ya harusi. Akawa amefika chumba alichokabidhiwa namba 33 akafungua kwa kutumia kadi maalum mpaka ndani na kumlaza Alice kitandani. Akamkagua Alice mara mbili mbili huku kichwa chake akikiinamisha katika kifua cha Alice kama atahisi mapigo ya moyo yakipiga. Jibu lake likawa sahihi. Alice alikuwa akipumua lakini kwa shida sana kwani hata mapigo ya moyo yakawa yanaenda tofauti. Yakawa yanaenda kwa taratibu sana. Aloyce akaanza kutafuta dawa ile ya Alice pindi akiishiwa pumzi katika suruali zake alizokuwa amekuja nazo amezihifadhi katika brifkesi yake spesho. Ikamchukua zaidi ya dakika mbili nzima akifungua bifkesi yake nakusambaratisha nguo zake zote na vitu vyake vya muhimu kama vile pesa na vito vya dhahabu vya mikononi na shingoni akitafuta kichupa cha plastiki ambacho ndio huwa kuna dawa ya kumsaidia Alice kupumua vizuri. Hatimaye baada ya kuhangaika kwa muda mfupi akafanikiwa kuipata katika koti lake la suti ambao lilikuwepo ndani ya brifkesi yake .

“OOhh thanks God, santé sana”

Akaanza kumpulizia Alice mdomoni. Akawa akibonyeza kwa nguvu sana ili itoke hewa ya kutosha. Akiwa bado katika hali ya kumpa hewa Alice kwa kutumia kile kichupa cha plastiki mara mlio wa mlipuko katikka jingo lote alipokuwepo ukamshtua sana Aloyce. Hakujua mlipuko umetokea wapi lakini kwa mtikisiko ule mithili ya tetemeko la ardhi akaamini wazi mlipuko kama ule azima utakuwa umetokea maeneo ya jingo hilo hilo. Haukuwa mlipuko wa kawaida, jengo zima likabaki likiendelea kutetemeka mithili ya radi ikipiga mawingu. Aloyce akamwacha Alice mara moja nakukimbia mpaka chini kwa lengo la kumchukua Janet ili ajue Alice yuko wapi na pia kumnsuru katika mlipuko huo. Akashuka kwa kutumia lifti ile ile aliokuwa amepanda mwanzoni pindi alipombeba Alice.

Makelele yakawa yameuteka ukumbi wote wa Darlington 2. Hayakuwa makelele ya sherehe ya harusi ya Aloyce kama ilivyokuwa mwanzo bali yalikuwa ni makelele ya vilio vya watu, woga wa lile tukio la bomu. Ukubwa wa Lile lango la kutokea ukaonekana kuwa mdogo kama mlango wa chooni. Wageni waalikwa wa harusi ile ya Aloyce wakawa wanakanyagana kwa hofu ya kuondoka mule ukumbini kwa kudhani huenda mabomu mengine yakalipuka zaidi. Aloyce akawa kama kmtu aliyepigwa na bumbuwazi. Bumbuwazi kwa kustaajabu lile tukio. Hakuelewa aanzie wapi na amalizie wapi kutokana na ukumbi wote kuwa na kelele na eneo moja tu likiwaka moto mkali. Macho yake yakawa bado na kama ukungu wa kutotambua mbele zaidi ya kuendelea kuona mbanano katika lango la kutokea.

“Dadyyyyyy?” (Baaaabaaa?)

Uwezo wa macho ya Aloyce ukaweza kutambua moja kwa moja mpaka eneo alipokuwa baba yake mara ya mwisho wakivutana na Janet. Rais Kagwa alikuwa chini na kilchomfanya Aloye kumgundua ni ile suti aliokuja nayo. Kwa mwendo mkali Aloyce akawa ameshamsogelea na kumfikia karibu. akaanza kumshika baba yake eneo la kichwani.

“Dady, dady wake up my dady!” (baba, baba amka baba!)

Machozi ya uchungu yakawa yameshauteka uso wa Aloyce. Akajikuta analia kwa uchungu akimlilia baba yake ambaye alikuwa ameshaathirika na lile bomu upande mmoja mzima alikuwa yu mauhututi hajiwezi hata kuinuka, kutembea wala kuongea.

“Excuse me Who are you?” (samahani wewe ni nani?)

“Then do not ask stupid like that, I'm his son and he is my father, you fools”. (usiniulize ujinga kama huo, mie mtoto wake na huyu ni baba yangu wapumbavu nyie?)

Aloyce akazidi kuwa mkali hata alipoulizwa na baadhi ya mapolisi waliokuja kuwaokoa wenzao. Akaendelea kulia huku akiangaza hapa na pale.

“I'm sorry but we need to take Mr. President We raise an urgent hospital prepared a body for his wife is in the car.” (samahani lakini, tunahitaji kumchukua mheshimiwa rais tumpeleke haraka sana hospitali kwani tayari mwili wa mke wake upo ndani ya gari)
 
81.

“Where is? My mother has survived?,. has survived.?” (yupo wapi? amenusurika mama yangu?, .amenusurika.?)

Yale mawazo yaliomleta Aloyce kuja kumchukuwa Janet yakawa yamebadilika kwa ghafla baada ya kushuduia baba yake akiwa hajitambui. Akachomoka kwa mwendo wa kasi nakutoka mpaka nje kabisa ya hoteli ya Darlington 1. Macho yake kwanza kabisa yakaangaza mpaka kwenye gari la msaada la kubebea wagonjwa. Alipofika hakutaka kuambiwa chochote zaidi ya kukuta miili mingi imefunikwa ndani ya lile gari. Aloyce akaanza kuifungua mmoja mmoja.

“Jesus! Janet umekufa, umekufa Janet? Nani kakuua? Alice nitamwambiaje mimi?”

Wimbi a machozi likaanza tena kujirundika kwa mara ya pili katika uso wa Aloyce. Lipsi za midomo yake zikaanza kumtetemeka sambamba na kwikwi ya hasira. Mishipa ya pembeni ya uso wake ikaanza kuchukuwa nafasi. Akajikaza kiume kwa kubusu kichwa cha Janet aliokuwa amebaki kichwa tu huku akiwa hana kiwili wili. Akafungua maiti nyingine.

“Who is this?” (Huyu ni nani?)

Aloyce akatahamaki kwa kuwahoji wale mapolis wa ki Nigeria ambao walikuwa wakizipakiwa maiti zote na ndio waliokuwa katika tukio zima toka wanamsindikiza rais kagwa kutokea hotel alipotokea mpka kuingia ukumbini.

“She is the wife of the president Kagwa” (Huyo ni mke wa rais Kagwa)

Akaropoka mmoja wa polisi hali iliomfanya Aloyce kuishiwa na nguvu baada ya kusikia kuwa ni mke wa rais. Akajihisi kizunguzungu kikimchukua. Akaifunua miili yote kuhakikisha kwa mara ya pili. Miili yote ya Janet na mke wa rais Kagwa ilikuwa imenusurika eneo la kichwani tu hivyo kufanya kujulikana ki urahisi japo walikuwa wameshapoteza maisha. Eneo la la chini lilikuwa nyang’a nyang’a kwa kuathiriwa na bomu. Aloyce akajikuta akishindwa hata kutoa neno zaidi. Miguu ikamlegea sambamba na kupoteza fahamu.

*********

Usingizi mkali ambao ulikuwa umempitia Alice kutokana na kupoteza fahamu ukawa umefika ukingoni. Akajikuta ameamka yupo chumbani peke yake. Hakuwa nakumbukumbu yeyote kwa kilichotokea. Akatamani sana japo kujua muda ni saa ngapi kwa kipindi kile lakini hakuambulia chochote zaidi ya kulisogelea dirisha nakufungua pazia. Mwanga ulioashiria jua kali ukamfanya kujua muda tu japo saa hakujua ni saa ngapi imetimia.

“Mama yangu yupo wapi? Na Aloyce wangu?”

Akalazimisha kuzirudisha fahamu lakini hakufanikiwa. Kitendo cha kujikuta mwenyewe hotelini chumbani kikawa kimemzidishia sana woga. Akawahi mpaka mlango wa bafuni nakufungua mlango.
.
“Aloyce? Aloyce mume wangu?”

Hakuambulia kitu zaidi ya sauti aliokuwa akiitoaa kumrudia mwenyewe. Akanyong’onyea nakurudi mpaka eneo la kitandani huku machozi yakianza kumtiririka. Akiwa bado katika hali ya woga Macho yake yakaanza kupepesa kuangalia hapa na pale na kwa sasa yakawa yamegota katika brifkesi ya Aloyce ambayo ilikuwa chini yake. Brifkesi ambayo Aloyce alikuwa akiipenda sana kutumia kusafiria pindi alipokuwa Rwanda. Alice akaisogelea nakuanza kuikagua. Mawazo yakauteka sana moyo wake. Akili yake ikazidi kufikiria mambo mengi, tabasamu la furaha likamtawala alipoliona boksi la kung’aa likiwa na mkufu wa dhahabu ndani yake. Kwa hisia kali akalichukuwa na kulibusu nakuirudishia alipoikuta. Pembeni yake kukawa na begi zuri aliokuwa amenunuliwa na Aloyce. Begi la kuwekea vitu vidogo vidogo vya urembo.

“Nakupenda sana Aloyce”

Alice akajikuta akiongea peke yake. Njaa kali ikaanza kumzidia katika tumbo lake. Hakuelewa aanzie wapi na amalizie wapi. Akatamani sana japo Aloyce atokee amueleze njaa aliokuwa nayo. Njaa ya yeye kutokupata kitu tumboni mwake toka usiku wa harusi aliposhindwa kula chakula. Akiwa bado amezubaa akiranda randa peke yake chumbani mara akajihisi amekanyaga kitu chini. Akautoa mguu wake haraka haraka kwa woga. Akainama mpaka chini nakuangalia alichokuwa amekikanyaga.

“OOOh my God!!”

Kichupa cha plastiki ambacho huwa kinamsaidia kurudisha pumzi wakati akiishiwa kikawa mikononi mwake. Akakifikiria sana imekuwaje kipo pale chini lakini bado fahamu zikashindwa kumrudia vizuri. Akikishikilia kwa nguvu akijiinamia ukutani.

“Why me?, why always me?, Mungu nioneshe njia? Aloyce wangu yupo wapi sasa?? Naumia mie ahhggrrr”

Uchungu ukawa umeshamzidia Alice. Haukuwa uchungu wa kulia peke yake la hasha ulikuwa ni uchungu wa tumbo lake, tumbo ambalo lilikuwa limebeba mimba changa ya Aloyce. Hasira zikawa zimemjaa sana Alice akalifuata lile brifkesi nakuchomoa kile kiboksi kilichokuwa na mkufu kisha akachukua kitita cha pesa ambacho kilikuwepo pale nakuziweka katika kibegi chake alichokuwa amenunuliwa na Aloyce nakuondoka mule ndani.

Viatu virefu alivyokuwa amevivalia Alice havikumpa shida kutokana na kuzoea mambo ya urembo licha ya kuwahi kushiriki mashindano makubwa Tanzania. Mashindano ya kumtafuta mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania mpaka kufikia hatua ya kuwa mshindi halali japokuwa alipokwa ushindi wake. Akatoka mule ndani ya ile hoteli. Hakuwa mshamba tena kwani hata lifti alikuwa akizifahamu kuzitumia. Ndani ya muda mchache akawa yupo eneo la ukumbi wa chini kabisa ‘Darlington 1’

“Where are you going?“(Unakwenda wapi?)

“'M’ going to restaurant” (Naelekea mgahawani)

“Ok, if you leave do not forget to hand over the keys to our office here when you come back, you know the restaurant?.” (Sawa, kama utatoka usisahau kukabidhi ufunguo wetu hapa ofisini mpaka utakapokuwa umerudi tena, unapajua mgahawani?)
 
82.

“No, Show me please” ( Hapana, tafadhari nielekeze)

“Passed through it there, Go straight you will see it before you hit the restaurant.” (Pita njia hiyo hapo, nyooka moja kwa moja utaona kibao cha mgahawa mbele yako.

“Thanks”

Alice alikuwa akiongea na mhudumu wa mapokezi ambaye alimuona akiwa katika hali ya kutoka. Akamjibu kwa kujiamini nakuomba maelekezo ya kuelekea katika mgahawa nakuelekezwa. Ikamchukuwa dakika mbili kufikia eneo la mgahawa wa hotel ya darlington. Akatafuta siti akakaa.

“Waiter, waiter”

Alice akaita mhudumu, akaja lile eneo alipokuwa amekaa.

“where is menu?” (Kitabu cha kuchagua chakula kipo wapi?)

“Sorry today we are not providing a service and not here in the restaurant area. It’s all venues, DARLINGTON 1 and 2” (Samahani leo hapa hatuna huduma na siyo hapa katika mgahawa ni eneo lote na kumbi zote za darlington 1 na 2”

“For what reason? Means even food to eat for my money?, where to eat now.?” (Kwa sababu gani? Inamaana hata chakula nisile kwa pesa yangu?, nile wapi sasa?)

Alice akaanza kuwa mkali kwa kutokuelewana na mhudumu wa pale hotelini.

“There is a problems which occurred yesterday on the porch, problems which culminated in the president injury situation badly. And since morning here policemen are from the entry, and from the outside you will see massive police fence prevents anyone from entering inside and out, I think you have taking in this room? If it is not exempt from the inside until give information to the police.” (Jana yalitokea matatizo hapa ukumbini hali iliyopelekea rais kujereuliwa vibaya. Na tangu asubuhi hapa mapolisi wanatoka na kuingia, na ukitoka hapo nje utaona uzio mkubwa wa mapolisi wakizuia mtu yeyote kuingia ndani wala kutoka nje, nadhani wewe uechukua room humu ndani? Kama ni wa ndani hamtakiwi kutoka mpaka mpewe taarifa na polisi)

“Why are you confused me now? Tell me what has happened since yesterday because I had sleep so much?” (Mbona unanichanganya sasa? Embu niambie kwani jana kumetokea nini maana mie niliwahi kulala sana?”

“Yesterday there were two wedding venues to Darkington 1 and 2 and the president of Rwanda he would come to his son in Darlington 2.” (Jana kulikuwa na harusi mbili kumbi ya darkington 1 na 2 na rais wa Rwanda alikuwa akija kwa mtoto wake.)

“what happened?” (enhee ikawaje?)

Alice akawa anamdadisi yule mhudumu kujua atasemaje.

“There was a women with bombing” (kumbe kulikuwa na mmama alikuwa na mabomu”

“died?” (akafa?)

Alice akadakia kujua mama yake wa kufikia hatma yake.

“Yes and blow up with bombs died with the wife of the president, but the president is having great care” (Ndio akajilipua na mabomu akafa pamoja na mke wa rais lakini rais yupo chini ya uangalizi wa madaktari)

Alice akajihisi kuishiwa na nguvu akijihisi pumzi kumkata tena. Mikono yake akaiwahi katika pua zake ambazo zilikuwa zikitaka kuruhusu kutoka damu. Akautoa mkono wake haraka haraka akuwahi mpaka katika pochi yake nakutoa kichupa cha kujipulizia kurudisha pumzi. Akajipuliza kwa haraka haraka akihema juu juu.

“oohhhh uuhfff thanks God asante sana”

Pumzi zikawa zimemrejea Alice. Hakutaka tena kusimuliwa kwani akili yake yote ikawa imeshajua kuwa amempoteza mama yake wa kufikia, Janet. Mama ambaye alimpenda sana mpaka kuja naye huku alimchukulia kama ni mama yake wa kumzaa. Akatoka haraka haraka mpaka eneo la lifti karibu na mapokezi.

“"Heeeeeyy sorry come here?" (heeeeeyy samahani njoo hapa?)

Aliita yule dada wa mapokezi na safari hii alimwita Alice kwa sauti ya ukali kidogo. Alice akasita kuendelea na safari ya kurudi chumbani akamfuata kwa hasira kali.

“"what sayest?" (unasemaje?)
 
83.

“Sorry I forgot to tell you that today there is no service at restaurant. " (Samahani nilisahau kukwambia kuwa leo huduma hakuna hapo restaurant)

“"Well I understand" (Sawa nimekulewa)

Alice akamjibu kimkato nakuendelea na safari.

“I still have not finished, I need to ask you, I'm sorry but since when policemen are out and I have been tasked to look at all the events yesterday on our security camera. I was follow up the first wedding at Darlington 2. (Bado sijamaliza, nahitaji kukuuliza, samahani lakini kwani mapolisi wapo hapo nje na nimepewa kazi ya kuangalia matukio yote ya jana hapa kwenye kamera zetu za ulinzi. Na nilikuwa nafutilia harusi katika ukumbi wa Darlington 2.)

Yule dada wa mapokezi akamsogezea Alice komputa aangalie vizuri. Lilikuwa ni tukio la yeye kunyweshana shampeni na Aloyce na baada ya hapo likamuonesha Alice akichukuwa kipaza sauti na kumtafuta mama yake. Baada ya hapo tena likamuonesha rais Kagwa akiingia na Janet akimuwahi kuwakumbatia na punde akaona moto mkali ukilipuka kuashiria bomu. Wakiwa bado wanashangaa mara mapolisi wawili wa ki Nigeria wakatokea.

“Can you record all the events yesterday at the wedding?” (Umeweza kurekodi matukio yote ya jana katika harusi?)

“"Yes!!, right here I end recording" (Ndio hivi hapa namalizia kurekodi)

Wale mapolisi wakaendelea kuongea na yule dada wa mapokezi. Muda wote mwili wa Alice ulikuwa katika hali ya kutetemeka. Akajihisi kojo likitaka kumotoka katika gauni lake la harusi.

“It wasn’t me?” (sio mimi?)

Alice akakana mbele ya yule dada. Akaanza kurudi nyuma nyuma akikataa na aliipozikaribia ngazi tu akaanza kupandisha kwa kukimbia lile eneo akielekea juu bila kutumia lifti. Akiwa ameshafika ghorofa ya kwanza huku wale mapolisi akiwaangalia kwa chini, kizunguzungu kikaanza kumtawala. Akajihisi kama mtu mwenye presha ya ghafla tena ile ya kushuka. Tumbo lake likawa limeshachoshwa kwa kile kiumbe kilichokuwa ndani yake. Kiumbe ambacho baba yake ni Aloyce.Akakiona kimemzidia uzito japo mimba ilikuwa ni changa sana. Akajihisi kama kile kiumbe kinataka kumtoka huku asielewe afanyaje.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom