Mrembo aliyepotea

Mrembo aliyepotea

32.

“..Eeeh Mungu baba.., nitazame hapa nilipo weza kunilinda Baba, nitolee hali yote ya hofu, Baba tazama haya ndio maisha yangu na nikishindwa hapa sintokuwa na kitu kingine Baba, Mungu Baba nioneshe njia, niponye kichwa changu ambacho kimeanza kunisumbua, tazama Baba bado natetemeka, sitaki kushindwa, sitakiiii..??, nakuomba nioneshe njia, Ameeen..!!!”
Alice alisali sala fupi chooni kisha alipomaliza aliizima simu yake nakurudi nyuma ya jukwaa.
“..Mbona umechelewa sana Alice..”
“..Nilizidiwa mwalimu.., nilibanwa na haja..”
Alice alidanganya huku akimtolea macho mwalimu wak e alionesha kuchukizwa kidogo na tabia ya Alice kuchelewa kurudi chooni wakati mashindano yameanza.
“..Haya mavazi yako ya jioni yapo tayari..?? kwani muda si mrefu itakuwa zamu yako kupanda jukwaani..”
“..Ndio yapo tayari mwalimu..”
“..Haya yavae haraka si unajua namba yako ya pembeni hiyo ni namba sita na sasa hivi ameenda Rosemary mwenye namba tano. Jitahidi uvae haraka upande jukwaani Alice…??”
Mwalimu wa alice alikuwa bega kwa bega kumuwaisha Alice afanye haraka. Haraka haraka Alice alivua na kubadilisha zile nguo ambazo zilikuwa zimebuniwa na mbunifu chipukizi hapa Tanzania, Abduel Urassa. Alice alikuwa tayari kwenye Vazi hilo la jioni la rangi ya kijani lililopambwa kwa manyoya ya mng’aro yenye kuwaka waka mithili ya taa za rangi nyingi. Tabasamu alilolionesha mbele ya umati wa watu alipopita Alice lilihamsha hisia za makelele kila mmoja kujikuta akipiga shangwe kwa furaha. Lile vazi lilikuwa limemkaa Alice vilivyo kwani lilimbana nakumonesha umbo lake halisi ikiwa ni pamoja na umbo la namba nane. Majaji walibaki bize kwa kumpa maksi kupitia karatasi zao.
“..Mpeni ushindi tu huyooo, wengine wanajikongoja..??”
Aliropoka mmoja wa kina Dada ambaye alikuwa akihudhuria hali iliyochochoe zaidi kelele zilizoambatana na vigelele huku Alice akigeuza na kupishana na mrembo mwingine. Muda wakuonesha mavazi yote muhimu ulikuwa umeshakatika, onesho lilihudhuliwa na watu takribani hamsini na mgeni rasmi alikuwapo mheshimiwa Joseph Kazindaki mkuu wa manispaa ya Ilala. Na sasa mheshimiwa Joseph Kazindaki akawa kwenye meza kuu akifuatilia kwa makini Majaji wanachozungumza. Homa na presha za hapa na pale zilikuwa zimeshawatawala washiriki wote wa Miss Chang’ombe. Wote walikuwa wamepanga mstari sasa kujua nani atatangazwa mshindi wa kwanza na nani atakuwa wa pili na hata wa tatu. Alice muda wote alikuwa kimya huku akijiamini kwa asilimia zote mshindi ni yeye wala hakuwa na mpinzani licha ya kuwa aliambiwa atapitishwa moja kwa moja kuwa mshindi. Alijitahidi kuliangalia jukwa a lote japo kumshuhudia Baba yake wa kufikia John lakini alishindwa kumuona zaidi ya kumshuhudia Janet mke wa John. Jaji mmojawapo alisimama na kuanza kumtaja mshindi wa tatu na wa pili ambapo Alice hakuwepo kati ya hao, hali iliyowakosha mashabiki kufura kwa furaha ukumbi wote. Na sasa yule Jaji akamkabidhi bahasha ya mshindi wa kwanza mhesimiwa Joseph Kazindaki kumtangaza mshindi wa shindano la Miss chang’ombe kwa usiku huu.
 
33.

“..kabla ya yote ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuweza kualikwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano haya ya kumtafuta mrembo wa Chang’ombe ambaye ataenda kugombea kuiwakilisha Tanzania. Ni matumaini yangu waote walikuwa wazuri na walivaa mavazi mazuri ambayo kila mmoja yalimvutia. Siku zote kwenye mashindano kuna kushinda a kushindwa na asiyekubali kushindwa si mshindani kabisa.. Labda nisiwapotezee muda sana kwa kuwa kila mmoja ana hamu ya kujua nani atakuwa mrembo mpya wa mwaka huu atakayeiwakilisha vilivyo katika kinyanganyiro cha Miss Tanzania na Dunia kwa ujumla..”
Warembo wote ambao hawakutajwa wakawa kimya ikiwa ni pamoja na Alice. Wote walikuwa wakimuangalia mgeni rasmi kwa jicho la hofu huku wengi wao sura zao zikipambwa na tabasamu pana la kujua kuwa watakuwa washindi. Mapigo ya moyo ya Alice sasa yakawa yanaenda mbio baada ya yule mgeni rasmi kuchelewesha kutaja matokeo. Maongezi mengi aliokuwa nayo mgeni rasmi yalimfanya Alice azidi kutetemeka..
“..Na mshindi wetu usiku wa leo ni…, Mshindi wetu ni.., Nasema hiiivii mnanisikia wote”
“..Ndioooooooooo…!!!”
Ukumbi wote ukajibu kwa mbwembwe na miruzi
“…Mshindi wetu wa usiku wa leo ni ni niii…. AISHA SULEIMAN…”

*****************

Ukumbi wote ulinyamaza kwa muda wa dakika mbili nzima. Kila mrembo aliyekuwa akishiriki alibaki kutoa macho na mdomo kuuachia wazi kwa mshangao. Hakuna hata mmoja aliyeamini matokeo yaliotajwa na mheshimiwa Joseph Kazindaki. Alice alijihisi kulegea mwili mzima na hata alijihisi tayari mkojo umepenya katika chupi yake ya ndani. Majaji walibaki kutazamana peke yao huku wakichekelea kutolewa jibu la mshindi.
“..Mbona mmenuna sasa..?”
Mheshimiwa Kazindaki alibaki akiwaambia tena wageni wote waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mtanange huo wa kumtafuta mrembo atakayeiwakilisha Chang’ombe katika mashindano mengine ya Miss Tanzania ya mwaka huu. Baada ya kumtaja AISHA SULEIMAN kama mshindi kila mmoja wa washiriki alibaki kumtolea mwenzake macho kwa kumshangaa mheshimiwa Kazindaki kutaja jina la mshindi ambaye hata hawamjui na hakukuwa na mshiriki katika shindano hilo mwenye jina la AISHA SULEIMAN. Kila mmoja alionekana kumnong’oneza mwenzake kuwa mheshimiwa kachemka. Baadhi ya wafuatiliaji wakawa wameshaligundua hilo tatizo na sasa kilichofuata ni kuanziasha zomea zomea ndani ya ukumbi.
“..Hapana jamani..!!, Hapana hatuendi hivyo..?? Unajua wengi naona mkiguna tu nakushindwa kunielewa, Ni kwamba hakuna mshiriki anayeitwa AISHA SULEIMAN kati ya washiriki wote unaowaona hapa zaidi ya ishirini, Na mimi nimefanya kusudi niwajue mtakuwa na muamko gani..”
Baada ya maneno hayo ukumbi wote ukarudia katika hali ya makofi na vigelegele huku wale warembo walioshiriki, kurudisha hali yao ya kawaida na kuendelea kusisimka zaidi kumsubiria mshindi atatangazwa nani. Sasa Alice akajihisi amepuliziwa feni ghafla katika mwili wake wotr, Lile paji lake la uso ambalo lilishaanza kuvimba sasa likawa laini huku likifanya mashavu kubonyea sambamba na tabasamu zito lenye hamu kubwa ya kumjua mshindi. Akili yote ikawa ni kumtizama Mama yake wa kufikia ,Janet eneo ambalo alikuwa ameketi lakini hakuwepo tena hivyo moja kwa moja Alice akajua huenda alichukizwa na matokeo ya uongo yaliotajwa na mheshimiwa Kazindaki.
“..Na sasa namtaja mshindi mwenyewe ambaye ndiye atakayetuwakilishia hapa Chang’ombe katika mashindano ya kumtamfuta mrembo wa Tanzania. Namleta kwenuuuu ALICE MAJALIWA..”
Hakuna aliyeacha kupiga kelele. Alice alikuwa na haki zote za kushinda kutokana na sifa zote alizokuwa nazo. Washiriki wenzake waliokuwa wamesalia waliafiki matokeo bila ya kipingamizi chochote. Alice alivyotajwa tu alijikuta mwili wote unamsisimka Alichukuwa mikono yake na kuufumba mdomo kwa furaha aliyoukuwa nao. Na sasa moja kwa moja jicho lake likahama kutoka kwa mgeni rasmi aliyemtangaza mpaka katika mlango wa kutokea ambapo jicho lake lilikutana moja kwa moja na Mama yake wakufukia ,Janet akirudi kushuhudia mshindi kwa mara ya pili. Alice alipita kwa mikogo huku akiinyanyua mikono yake kuwapa ishara ya asante kwa washiriki wenzake na wageni wote waliokuwa wamehudhuria. Sasa akawa analetewa taji na aliyekuwa mrembo wa chang’ombe mwaka jana YASINTA HAULE. Alivalishwa kichwani mwake sambamba nakutupiwa maua madogomadogo yenye kumelemeta kisha akapewa kipaza sauti aongee chochote.
“..Kwanza kabisa kabla ya kuongea chochote nakuomba Mama yangu usogee karibu hapa mbele..”
 
34.
Alice alikuwa na hamu maneno yote ayasikie Mama yake wakufikia Janet ambaye alikuwa amekata tamaa mara ya kwanza alipotangazwa mshindi ni AISHA ASULEIMAN. Janet alisogea kwa ukaribu huku akiyaweka masikio yake sawa tayari kwa kumsikiliza Alice.
“..Napenda kutoa shukrani zangu kwa washiriki wenzangu wote tuliokuwa pamoja kuanzia kambini mpaka hapa kwenye mashindano. Pia nitakuwa mchoyo wa fadhila endapo sitamshukuru mwalimu wangu kwa kuweza kunifundisha mambo mengi sana. Yeye ndiye chachu kubwa sana ya ushindi huu nasema asante sana mwalimu wangu. Shukrani zangu pia ziwaendee waandaaji wote na majaji ambao mmefanya kazi kubwa sana ya kuweza kupambanua mpaka mkanipata mimi Alice kama mshindi. Mwisho wa yote asanteni sana kwa wote mliohuduria na kunipa faraja kila nilipokuwa napita hapa jukwaani najua maisha ni safari na mpaka nilipofika hapa ni kwa juhudi za mwenyezi Mungu tu..”
Alice alishukuru wote kisha akajikuta akishindwa kuendelea na kumwaga mchozi. Si machozi ya furaha peke yake bali alikuwa akilia kwa kumpoteza Dada yake Angel kipindi cha nyuma ambaye yeye ndiye alimfanya mpaka amjue John na hata kufika hapa. Pia alilia sana alipokumbuka maisha yake aliyotoka nayo ya kukaanga samaki na kuwauza na kilichomuumiza sana ni kitendo cha Baba yake kumpiga sana Mama yake na kutoroka hivyo akabaki katika mateso makali ya kubakwa kila kukicha na mzee wake mpaka alipotoroka kwao na kutokomea kusikojulikana. Waandishi wa habari walikuwa sambamba na Alice kwa kumpiga picha mbali mbali za kupamba magazeti yao kesho yake. Zawadi kubwa ya nyumba ikiwa na kila kitu ndani yake ambayo ilitolewa na wadhamini wakuu wa shindano hili sasa wakawa wanamkabidhi Alice funguo wa nyumba hiyo sambamba na hundi ya shilingi milioni mbili. Alice hakuamini macho yake, alitamani sana haya maisha kwani alikuwa akiyaota ila leo hii yamemtokea kweli. Alice akiwa bado kwenye dimbwi la mawazo ya ghafla huku akipokea zile zawadi, Jaji mkuu alichukuwa kipaza sauti na kumpa maswali Alice.
“..Unachagua Kiingereza ama Kiswahili..??”
“..Kiswahili.!!”
“..Sasa ningependa kumuuliza kidogo mshiriki wetu wa mwaka huu AlICE MAJALIWA. Wewe ndiye tuliokuteuwa kama mshindi wa kwanza na pia ndiye utakayeenda kuiwakilisha Chang’ombe katika masindanio haya ya mrembo wa Tanzania embu tuambie unatuahidi yapi..?”
“..Kwanza kabisa nitajitahidi kupigania ushindi huu nilioupta hapa leo huko niendapo. Nitahakikisha nafanya yale yote yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuibuka mshindi wa kuiwakilisha Tanzania katika mashindanio ya mrembo wa dunia..”
Kile kipaza sauti alichukuwa Jaji wa pili yake naye akatoa swali lake.
“..Unachagua Kiingereza Kiswahili?”
“..Kiswahili..”
“..Swali la kwanza, Utaepukana vipi na skendo ambazo zinawakumba warembo wetu wa hapa Tanzania. La pili kwakuwa warembo wote wanaopita huwa wanajishughulisha na shughuli za kijamii, sasa wewe ukiwa kama mrembo atakayeikwalisha Chang’ombe yetu umepanga vipi kuisaidia jamii yako inayokuzunguka..?”
“.. Labda kwa kuanza na swali lako la kwanza ni kwamba, Nitahakikisha najiepusha na skendo hizi kwa kuwatumia mawakili na hata waratibu wa mashindano haya ya urembo pale linapotokea swala la mimi kuchafuliwa na vyombo vya habari. La pili nitaandaa mipango kabambe kwa ajili ya kusaidia jamii haswa kwa wazee ambao hawajiwezi, mayatima na vijana walioathirika kwa madawa ya kulevya na umalaya..”
Alice alijibu kwa kujiamini hali iliowafanya ukumbi wote uendelee kulipuka kwa shangwe. Baada ya maswali hayo alikaa pamoja na mshindi wa pili pembeni yake na kulia kwake akawepo mshindi wa tatu wote wakipigwa picha na waandishi wa magazeti mbali mbali hapa nchini. Baada ya picha hizo sasa Mama wa kufikia, Janet akawa ameshafika karibu na Alice na kilichofuata walikumbatiana kwa hisia zote.
 
35.
“..Hongera mwanangu umenipa faraja kubwa sana moyoni mwangu, naamini unaweza na utazidi kuweza mwanangu..!!, ashukuliwe mwenyezi Mungu..”
“..Asante sana Mama yangu mungu yu pamoja nami kila mahali..!! Baba yupo wapi..?”
“..Amesafiri kwenda Mwanza kusimamia mashindano kama haya..”
“..Sawa Mama..!!”
Alice aliongea kwa uchungu huku wakiachiana na Janet. Na sasa ikawa zamu ya Alice kuwaaga baadhi ya washiriki wenzake mbali mbali aliokuwa nao katika mashindano. Aliwaaga majaji, mgeni rasmi na baadhi ya wahudhuliaji waliojitokeza kuangalia mashindano hayo. Alipiga picha na kila mmoja aliyekuwa akihitaji. Tabasamu lake aliliendeleza mpaka wanatoka na gari ambayo ilikuwa imetayarishwa kwa ajili ya kumpeleka mrembo na wazazi wake mpaka kwenye hotel maalum kwa siku mbili ndipo arudi kwao. Usiku huo Alice hakupata kabisa usingizi, Mawazo yake yalikuwa mengi sana. Kila alichokiwaza alikuwa akikikataa. Aliwaza hata hiyo nyumba atakayokabidhiwa akaishi huko lakini wazo lilimfukita kwani Baba yake wakufikia John asingekubali kamwe. Aliwaza kuanzisha mtaji kwa hizo millioni mbili lakini nalo wazo likabaki pale pale katika kulifuta kwani aliamini mtaji hautadumu hata hivyo alijiwekea mashaka ya kutokukubaliwa kufungua chochote zaidi ya kutunziwa pesa zake na wazazi wake hao wa kufikia. Hotel kubwa ya Kilimanjaro Kempinski ndipo alipokuwa amehifadhiwa Alice na Mama yake wa kufikia, Janet. Alice alilaala chumba kimoja na Janet. Usiku kutwa Alice alikuwa sebuleni akiranda randa huku amemuacha Janet chumbani . Hakuweza kupata kabisa usingizi. Nguo za mara ya mwisho alizokuwa amezivaa hakutaka kabisa kuzivua kwani aliamini ndizo zilizochangia kumpa ushindi kwaa usiku ule. Alisogelea mpaka kwenye kioo nakujigeuza huku na kule huku akijiangalia vizui kwa furaha ya hali ya juu. Mpaka inafika saa nane za usiku Alice alikuwa kapitiwa na usingizi sebuleni tena chini kwenye sakafu ya maru maru pale hotelini huku Mama yake wa kufikia akiwa chumbani amelala peke yake. Taa za hotelini zile za kuning’inia zilizokuwa zimedaniwa vizuri kwa urembo urembo sasa zikawa zinatoa mwanga hafifu pale sebuleni, Kuna kipindi mwanga uliongezeka nguvu na kipindi ulipungua. Alice hakuwa anajielewa kabisa, Alikuwa kama mtu aliyekunywa pombe nyingi akalewa. Hata ule mwanga wa zile taa hakuweza kuushudia zaidi ya kupitiwa na usingizi mzito sana. Na sasa ule mwanga ulikuwa umezidi kasi mpaka mwisho na kupasuka pasuka na kudondoka mpaka chini katika lile eneo alilokuwapo Alice. Nyaya ambazo zilikuwa zimeshikana na lile taa kubwa sasa zikawa zimetapakaa baada ya kudondoka mpaka chini. Kutokana na hali ya uchovu wa siku nzima na pilika pilika za mashinano zilizomfanya Alice alale fofofo sasa akawa anajipindua bila ya kuelewa chochote mpaka akajikuta amekumbatia zile nyaya ambazo zilikuwa na shoti ya umeme..
“..Mama nakufaaaaaaa..?? Mama niokeoeeee..??, mamaaa..?”
Alice alipiga sana kelele mule hotelini hali iliyomfanya Mama yake wakufikia Janet atoke mule chumbani na kumfuata hadi sebuleni alipokuwepo Alice. Hakuweza kumuona alipo Alice kutokana na lile taa kuungua na kuanguka hivyo sebule yote ikapamba kwa giza pana.
“..Alice mwanangu, Alice uko wapi mwanangu..?”

Mlango ulivunjwa na wahusika wa hotel baada ya kuhisi kuna tatizo limetokea katika chumba ambacho alilala Alice na Janet. Ule mshindo wa lile taa kubwa lililokuwa limedondoka mpaka chini na kutawanyika nyaya zake ambazo zilimsababishia Alice shoti katika mwili wake hali iliyompelekea kupoteza fahamu kabisa. Wale wahudumu walifanikiwa kuuvunja mlango, Walimchukuwa Alice na Mama yake ambapo wote walikuwa wamezimia na kuwapa huduma ya kwanza kwa kuwasha kiyoyozi kwa spidi kubwa. Ndani ya dakika kumi nzima Alice alikuwa hajaweza kupata fahamu yeyote zaidi ya Mama yake wa kufikia Janet kushtuka.
“..Kafanyaje tena mwanagu..??, Hapa ni wapi..? si nawauliza nyie..??”
“..Tulia kwanza Mama..!!, Hapa mpo hotelini.., Unaona pale..??”
Janet alioneshwa lile taa lilivyoanguka. Alijiziba mdomo kwa mshangao huku akimtolea macho Alice.
“..Niambieni na mwanangu kapona..??, Mwanangu Aice mzima..??, nawauliza nyie Alice mzima..??”
 
36.
“ ..Mama si unaona bado anapigwa na hicho hapo kiyoyozi huku tukimsaidia kwa kumpepea, Hata na wewe ulikuwa umepoteza fahamu hivyo tumekupepea umepata fahamu. Msubiri atazinduka tu wala usijali..”
Janet alitulizwa pembeni huku akiendelea kupepewa na wale wahudumu wa ile hoteli. Muda wote Janet alikuwa akitetemeka kuanzia midomo mpaka miguu na mikono yote. Alisali taratibu na kwa haraka haraka kumuomba mwenyezi Mungu aweze kufungua njia japo Alice azinduke. Aliona aibu kama hii ataipeleka wapi? Na hata John akijua kuwa Alice amezimia ama amekufa atakuwa mgeni wa nani? Dakika takribani ishirini za kumpepea Alice kwa kutumia kiyoyozi zilizokuwa zikimefikia tamati. Hakukuwa na dalili yeyote ya Alice kuzinduka zaidi ya kuanza kutoka Damu nyingi puani. Kila mmoja alianza kutetemeka kwa hali ambayo ilimtokea Alice ya kutokwa na damu nyingi puani. Baadhi yao walianza kuondoka ili kuepusha lawama huku baadhi yao wakijishuku kwa kuzima kiyoyozi ambacho walihisi huenda kimechangia kusababisha damu nyingi kumvuja kupitia puani. Muda wote Janet alikuwa amezidi kuchanganyikiwa asijue afanye nini kumnusuru Alice zaidi ya kuendelea kumuombea kwa Mungu kupitia sala fupi fupi.
“..Huyu tumpelekeni hospitali haraka anaweza kuwa ametufia hapa hatujui kwani hata na mapigo yake ya moyo si unayaona hayadundi kabisa..?”
Aliongea mmoja wa wahudumu wa ile hoteli huku akimnong’oneza mwenzake kwa sauti ya chini chini ambayo Janet hakujua chochote. Walimfuta Alice zile damu ambazo zilikuwa zinaendelea kumtoka puani kisha wakambeba nakuongozana na Janet mpaka nje kabisa ambapo huwa kuna gari ya msaada wa dharula kwa ajili ya wageni wa hoteli hii ya Kilimanjaro Kempinski. Hospitali ya Regency ambayo ipo pale Upanga ndio lilikuwa jibu sahihi kwa hoteli hii ya kempinsiki kutokana na wateja wao wote na hata wafanyakazi kuwa wakitibiwa hapo. Alice alifikishwa kwa haraka zote kisha akapokelewa kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa na kufikishwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi. Mama wa kufikia wa Alice, Janet alionekana kuzidi kuchanganyikiwa kwa kitendo kilichotokea, Alihisi kama ni ndoto tu iliyotokea. Alianza hata kulaani kitendo cha kupelekwa hapo hotelini na kamati ya warembo ambao ilipendekeza mshindi alale hapo hotelini na famiilia yake..
“..Kwanini nilikubali kirahisi vile..??, Ona sasa nitamweleza nini John wangu kuhusu yaliotukuta. Hapana sitamwambia..??”
Janet alichanganyikiwa kwa muda nakujihisi anajiuliza maswali mwenyewe na kujijibu. Eneo la hospitali ya regency aliliona dogo kwa muda kwani alipiga hatua kila kona huku aijiongelesha mwenyewe na kujijibu mithili ya mtu aliyechanganyikiwa. Ilichukuwa lisaa zima kwa Daktari kumtibu Alice na sasa yule Daktari mkuu akawa anatoka kwenye chumba ambacho alikuwa akimtibu Alice huku akiwafuata wahudumu walliokuwa wamemleta Alice pale hospitali.
“..Nani mhusika wa huyu binti..??”
“..Ni yule pale Mama..!!, We Mama..??, Mama..?”
Janet alirudi mbio mpaka eneo ambalo alikuwepo yule Daktari na wahudu mu wa hoteli.
“..Ndio Dokta mimi hapa..??, Vipi mwanangu kapona..??, Nauliza kapona..??”
“..Ndio maana nimekutafuta nikupe maendeleo yake..!!, Haya tuongozane wote ofisini ,twende..??”
Janet aliongozana na yule Daktari mpaka ofisini kwake. Akili yote ya Janet haikuwa sawa kwa kila hatua aliyokuwa akiipiga kuelekea ofisini kwa Daktari.., Alijihiisi mapigo yake ya moyo yanakwenda mbio hivyo anastahili kupumzika. Lakini aliweza kujikizua mpaka wakafika ofisini kisha akaketi na kumsikiliza Daktari yule alitemtibu Alice.
“..Mgonjwa ni mwanako kabisa..??”
“..Ndio Dokta..”
“..Kuna tatizo lolote ambalo liliwahi kumpata hapo awali..??”
“..Ndio nakumbuka mara ya mwisho alipoteza pumzi kabisa tukamuwaisha hospitali ambapo aliwekewa mirija ya kupumulia...”
Janet alijitahidi kujibu kwa kubahatisha kwani alishawahi kusimuliwa na John hapo awali kuwa Alice aliishiwaga pumzi na hivyo wakajua amekufa mpaka wakamuwaisha hosptali ndipo akapona. Sasa hilo jibu alilikariri na kumjibu yule Daktari kama vile alikuwepo..
“..Ok..!!, Nimejalirbu kumpima kila kitu kwa haraka na kwa vyombo vyetu vya kisasa zaidi..”
“..Ndio Dokta..!!”
“..Ebu niambie tena..??, Anafanya kazi gani huyu binti yako..??”
“..Hapana hafayikazi ila janajishughulisha na maswala ya urembo na hivi jana alikuwa akigombea mashindano ya urembo kanda ya Chang’ombe na akaibuka kuwa mshindi hivyo akapewa zawadi sambamba na kupewa ofa ya kulala hoteli ya Kilimanjaro ambapo alipata tatizo la kudondokewa na zile kubwa za sebuleni na kumpelekea kupata shoti kupitia zile nyaya za lile taa..”
“..Anhaa!!, Ok nimejaribu kuangalia hapa na nimegundua kwanza kabisa mwanao anatatizo la kuishiwa na pumzi. Tatizo hili huwa linajijenga sana haswa ukiwa na mbanano wa mawazo na kufikiri huku ukihema kwa haraka zaidi na pia ukichanganya na hasira kali huku unahema kwa nguvu mara kwa mara huchangia kupungua ama kukosa pumzi kabisa. Pili inaonekana alivuta hewa chafu aina ya Carbon YG 18RR8YD ambayo huwa inakaa katika taa nyingi za kichina ndani yake, Hivyo baada ya taa hiyo kupasuka ilitoa hewa hiyo chafu nakuingia mpaka mwilini mwake kupitia puani. Na hivyo kumsababishia kitu kinachoitwa (Heart Attack) ninaposemea (Heart attack) namaanisha shambulio la moyo. Tatizo kama hilo mara nyingi humsababishia mgonjwa kuwa na ugojwa wa kuanguka mara kwa mara pindi mapigo ya moyo yanapoenda kasi..”
 
37.
“..Inamaana mwanagu tayari ana kifafa, Mwanangu huyu Alice..??”
“..Tuliza jazba Mama nimalizie kukueleza najua wewe ni kama mzazi mwenzangu na tatizo kama hili halimaanishi kuwa mgonjwa kafa au atakufa la hasha! Ni kwamba linaweza kutibika haraka iwezekananvyo kama litafanyiwa upembuzi yakinifu..”
Janet aliangua kilio pale ofisini kwa Dokta, Hakutaka tena kumsikia yule Daktari, Alitamani akamchukuwe mtoto wake Alice warudi nyumbani. Alitamani hata Alice aachane na maswala ya kuwa mrembo wa Tanzania tena. Kilio kilimzidia mpaka ikambidi Dokta awaite wahudumu wamtoe nje. Napo nje alizidisha kelele zaidi lakini baadaye mwenyewe akapoza sauti nakuanza kulia kwa sauti ya chini chini.
“..Nirudisheni kwa Dokta..??”
Janet aliwaamrisha wale Manesi na baadhi ya wahudumu wa hoteli aliokuja nao waliokuwa wamemtoa Janet nje kwa kupiga makelel kupita kiasi. Walimchukuwa na kumrudisha tena ndani kwa Dokta.
“..Anhaa..!!, Katulia sasa..??”
“..Ndio Dokta..!!!”
“..Sasa Mama yangu ni kwamba kama nilivyokueleza hapo mwanzo juu ya mwanao. Kinachotakiwa ni uangalizi wa hali ya juu. Siku zote mtu mwenye matatizo haya ya kifafa huwa tunashauri kama ni mdogo basi aisiwekwe mbali na wazazi ama msimamizi wa karibu. Na kwa huyu mwanao kwa mzunguko tu na jinsi nilivyompima huenda akawa anasumbuliwa na tatizo hilo kwa mwezi mara moja ama hata mbili kulingana na mzunguko wa mwezi na pia hasira, mawazo yakumtawala kichwa na hata mshtuko wowote hatakiwi kuwa navyo kwani vitamfanya awe anadondoka ovyo.”
“..Sawa Dokta nimekuelewa..!!”
Janet alibaki amechanganyikiwa kwa jinsi alivyoambiwa na yule Daktari. Mawazo yake mengi yalikuwa juu ya mumewe, John ni kwa jinsi gani atamueleza na pia Alice mwenyewe ataanzaje kumwambia matatizo ambayo anayo. Ushawishi mkubwa ambao ulitanda katika halmashauri yake ya kichwa ni juu ya kumshawishi Alice aachane na kugombea mashindano ya mrembo wa Tanzania. Sasa Janet akaongozana na Daktari moja kwa moja mpaka chumba alichokuwa Alice amelazwa. Alimkuta Alice akiwa bado amewekewa oksijeni ya kuweza kumsaidia kupumua vizuri sambamba na kumpa hewa ya ziada.
“..Alice mwanangu..??, Alice..”
Janet alinyanyua mkono wake nakuanza kumshika maeneo ya shingoni mpaka usoni. Mirija mirefu na kitu kama kibakuli kilichokuwa kimemfunika pua na mdomo ndicho kilichomfanya Alice aonekane tofauti na lushindwa kuongea kabisa. Tabasamu alilokuwa nalo na gauni lile lile lililomfanya kuwa mshindi wa shindano la mrembo wa Chang’ombe ndilo lilikuwa likileta hisia tofauti kwa Janet na kumfanya kutoa machozi. Alice hakuweza kuongea zaidi ya kutoa macho tu. Macho yaliokuwa yamerembwa kwa kope za bandia nakuwa kama mdori sasa yakawa yakimuangalia Mama yake wa kufikia, Janet.


******

Alice alipata nafuu nakuweza kurudi tena nyumbani. Zile damu ambazo zilimvuja usiku kutwa sasa zikawa zimeshakatika kabisa kutokana na matibabu ya pale hospitali. Alipewa madawa mengi sana kwa ajili ya kujilinda na afya yake sambamba na kichupa ambacho huwa kinatumika kujipulizia mdomoni pindi hewa inapokuwa imeisha ama inataka kukatika. Walikodishiwa teksi haraka haraka sambamba na kupitia vitu vyao pale hotelini na hii yote ni kukwepa waandishi wa habari na hata waandaaji wenyewe kutokujua kinachoendelea ama kilichotokea usiku. Mawazo ya Janet na wenye hotel yalikuwa sahihi kwani waliambizana kutokuzieneza habari hizi popote huku wenye hotel wakiogopa kufunguliwa kesi endapo itabainika taa lile kubwa lilimdondokea mrembo hivyo ni kosa lao la kutokuwa makini na vifaa vyao. Kiasi kidogo cha pesa ambacho alipewa Janet kwa ajili ya kuendelea kumuuguza Alice kama ataendelea kuumwa toka kwa wahusika wa Kilimanjaro kempinsik ilikuwa ni siri kubwa sana kwa Janet.
“..Kwa heri mgonjwa..!!, Nakutakia uugue salama..!!”
“..Asante..!!”
“..Tuko pamoja nawewe katika maombezi, Utapona tu mdogo wetu..!!”
Yule mhusika mkuu wa hotel ya Kilimanjaro alimuaga Alice. Alice alijibu kihuzuni huku akili yake yote akiirudisha jana yake alipotangazwa kuwa mshindi wa kuiwakilisha kanda ya Chang’ombe katika mashindano ya Miss Tanzania. Aljiangalia mara mbili mbili lile vazi ambalo bado lilikuwa mwilini mwake huku akielekea ndani na Mama yake wakufikia, Janet.
“..Mama..? Jana uliniona vizuri jukwaani wakati napita na vazi langu hili..??”
 
38.
“..Ndio mwanangu.., Mhh ulipendeza kweli..!! Ujue mwanangu una vigezo vyote na ndio maana ushindi ulikuwa kwako. Halafu nikwambie kitu mwanangu..?”
“..Ndio.., Niambie tu Mama yangu..?”
“..Siri ya ushindi wako ni kujiamini, Yaani umejieleza mpaka nikasisimka hiyo jana..!!”
Janet alijitahidi kumpoteza Alice mawazo kwa kukumbushia matukio ya mashindano ya jana yake usiku ambapo yalimpelekea Alice kuibuka na ushindi katika kanda ya Chang’ombe. Alice alijihisi kusisimka mwili wote kwa maneno aliyokuwa akiyapata toka kwa Janet. Alitamani tukio kama lile la kushinda liwepo kote anapopita kuanzia mashindano ya miss Tanzania hadi yale makubwa ya mrembo wa dunia. Janet alikuwa na dukuduku kubwa ambalo bado lilijijenga katika halmashauri ya kichwa chake. Halikuwa dukuduku la hasira bali lilikuwa ni dukuduku la kumwambia ukweli Alice juu ya ugonjwa ulioibuka kwake. Machozi ya huruma aliokuwa akiyatoa dhahiri yalimfanya Alice ajihisi kuwa Mama yake huyo yupo tofauti na alivyomzoea.
“..Mama vipi tena..?? Mbona machozi yanakutoka Mama yangu..??”
“..Hapana mwanangu, Haya ni machozi ya furaha.., Hujajua tu jana ulinigusa sana katika maisha yangu.. mwanangu kweli sasa umepiga hatua na kama kweli ulisema malengo yako ni kutusaidia sisi wakina mama na vijana wenzako hapo mwanangu Mungu atakuzidishia..”
Janet alijitahidi kumbadilishia Alice maada. Alice alionesha tabasamu pana kisha akamsogelea na kumkumbatia Janet kwa hisia huku na yeye machozi yakimlenga lenga.
“..Mama..?”
“..Abee manangu..”
“Mungu ndiye anajua vyote.. mpaka kufika hapa unajuwa wazi safari yangu ilivyokuwa. Nimefikiria sana juu ya zawadi ya nyumba ambayo nimepewa. Lakini kabla hata hamjaamua chochote ninyi kama wazazi wangu, Mimi nimeamua tuipangishe tu na pesa hizo zitasaidia kuniendesha mimi na nyie kwa ujumla na pesa nilizokabidhiwa kama zawadi mojawapo nitakupa milioni moja kama shukrani yangu kwa wewe mama. Najua nitapata zawadi nyingi zaidi nikishinda taji kubwa la miss Tanzania, napo nakuhaidi mama yangu kukupazawadi nyinginenzuri zaidi nitakazopewa..”
Alice aliongea kwa hisia hali ambayo ilizidi kuyachochea machozi ya Janet kumdondoka zaidi bila ya kuyafuta. Janet alijihisi atakuwa mkosaji mkubwa endapo atatunza siri hii ya ugonjwa wa kifafa ambayo imempata Alice. Kitu kikubwa kilichokuwa kikimsukuma asiweze kumwambia ni katika hali alionayo sasa. Na alijihisi endapo atamwambia basi inaweza kumsababishia mshtuko na kifafa kikamuanza tena. Alighairi hata swala la kumzuia Alice kushiriki mashindano hayo.
“..Eeeh Mwanyezi Mungu..!!, Weza kumlinda na kumuongoza mwanangu Alice afanikishe ndoto zake za kuwa mmoja wapo kati ya wanaoiwakilisha nchi hii.. Baba mfanye Alice awe mshindi katika mashindano makubwa yajayo..Ameni..”
Janet alijisalia kimoyo moyo huku akiendelea kumkumbatia Alice kwa hisia kali. Na baada ya kumuachia alichukuwa kitambaa chake nakujifuta yale machozi kisha akaenda jikoni tayari kutengeneza chakula.
Baada ya wiki mbili kupita, Alice alikuwa tayari ameshakabidhiwa zawadi yake ya nyumba maeneo ya kurasini. Jumba kubwa liliokuwa na vyumba vinne pamoja na chumba kimoja chaa kujitegemea chenye choo na bafu ndani yake. Nje kulikuwa na uzio mkubwa na sehemu kubwa ya kuhifadhi hadi magari hadi matano. Alice Hakuifanyia chochote zaidi ya kukabidhi funguo kwa mama yake wakufikia, Janet. Furaha kwake iliongezeka mara mbili. Mpaka siku hiyo ya kukabidhiwa kwake zawadi, John hakuwa akipatikana kwenye simu japokuwa walilitambua kuwa anakazi nzito ya kusimamia warembo katika jiji la mwanza. Janet aliaamini Mwanza ni jiji kubwa hivyo watakuwa na kazi ngumu sana kufanya mchujo mpaka kumpata mshindi. Hawakutaka kabisa kumsumbua John baada ya kujaribu kumpigia simu nakumuona hapatikani. Furaha waliokuwa nayo yakukabidhiwa nyumba Alice kama sehemu mojawapo ya zawadi ya mshindi wa kanda ya Chang’ombe katika mashindano ya u miss, waliituza moyoni mpaka siku ambayo John arudi ndipo waanzishe tena kufurahia.

***********
.
Jiji la mwanza lilikuwa limelipukwa kwa sherehe mbali mbali. Usiku wa kuanzia saa mbili karibu kumbi zote zilikuwa zipo katika sherehe zao mbali mbali. Kuna waliokuwa wanafurahia kwa watoto wao kupata kipaimara kanisani, baadhi yao wakisherekea kubatiza watoto wao. Wapo waliokuwa wakisherekea kicheni pati na hata harusi. Baa nyingi zilikosa wateja kutokana na watu kukimbilia kwenye sherehe hizo ambapo zilikuwepo bia na vyakula vya bure.
 
39.
Katika ukumbi maarufu wa Gold first ambao upo Kinyapa road, Nyamagana ulikuwa umesheheni warembo mbali mbali ambao walikuwa wakishiriki mashindano ya kumtafuta mlimbwende ambaye ataiwakilisha vyema jiji hili la Mwanza katika kinyang’anyiro kingine cha kumtafuta mrembo wa Tanzania mwaka huu. Takribani ya washiriki ishirini walikuwa wamepanga mstari huku majaji zaidi ya watano wakiwa sambamba na mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Nyamagana jiji la mwanza (Mheshimiwa Ezekiel Wenje). Kati ya majaji hao waliokuwa wameketi mbele huku wamevalia suti nyeusi, alikuwepo John Mapunda. Taarifa juu ya jana yake Alice kushinda taji ndio ilimfurahisha haswa na kumfanya kila muda awe na furaha. Sasa kichwa chake kikawa pamoja na kufikiri ushindani ambao atakutana nao Alice katika mashindano makubwa yafuatayo. Ni Jamila Said peke yake aliokuwepo katika halmashauri ya kichwa cha John mara zote. Jamila alikuwa mzuri sana na alikuwa na kila sifa ya kuwa mshindi katika jiji hili la Mwanza, lakini kwa hilo halikumsababishia yeye kushinda taji hilo la Mwanza mbele ya washiriki wenzake zaidi ya kumi na tisa, Mpaka pale alipolala na John katika hotel ya Savoy siku mbili kabla ya mashindano haya. Muda wote Alipokuwa Jamila akipita, John alikuwa akimpa maksi japo kwa kutetemeka. John alijitahidi kutoa pesa kwa majaji wenzake ili tu Jamila aweze kupita na kumtimizia malengo ya siku nyingi ambayo yalikuwa yakimpa tabu licha ya kusuluhishwa yakaisha.
“..Hapa kinachoangaliwa ni mtoto tu..!, Ndipo nitaridhika na maisha, Ndio mtoto..!!”
John alijikuta akiongea mwenyewe kimoyo moyo huku akichukuwa karatasi yake na kumpitisha Jamila. Baada ya warembo wote kumaliza kupita pale mbele, John aliwaweka majaji wenzake chini kisha wakalipitisha jina la mshindi na kumkabidhi mgeni rasmi. Kamwe John hakulifikiria swala la Alice, alijua fika atamwaga tu Jamila kwa kumpa ushindi wa pili wa mashindano makubwa na pia malengo yake yatakuwa yameshatimia ya kumpa mimba. Punde mgeni rasmi mheshimiwa Ezekiel Wenje akapanda na kisha kumtangaza mshindi wa shindano la kumtafuta mrembo wa jiji la mwanza. Alimtaja yule yule aliyopitishwa na John pamoja na majaji wenzake,Jamila Said. Wapo baadhi waliguna lakini wengi wao waliafiki juu ya ushindi huo. Moyo wa John sasa ukawa umesharidhika huku ukitambua fika sasa malengo yake yatatimia juu ya kumpata mtoto kupitia mrembo huyo Jamila Said. John alitamani kesho yake ifike ili alale naye tena kwa mara ya mwisho na kisha arudi Dar es salaam kupanga mikakati mingine.
Baada ya siku moja kumpata mrembo atakayeliwakilisha jiji la Mwanza Jamila Said. Sasa ikawa ni zamu ya John kwa ahadi walizokuwa wamepeana. John alifurahi kuwa na Jamila kwa mara ya pili. Na kwa usiku ule alifanikiwa kupata Hotel ya Savoy ambayo ilijificha sana, kisha wakaagiza chumba na kulala na Jamila.
“..Baby umenifurahisha sana jana..!!”
“..Ok.., kwangu mie wala usiwe na shaka Jamila, Na kama utashika mimba tu kabla hatujaingia kwenye fainali ya kumtafuta mrembo wa Tanzania nakuhaidi moja kwa moja wewe utakuwa wa kwanza na nitahakikisha siri ya wewe kuwa na mimba yangu yote inafichwa mpaka unajifungua nakuendelea kuhudumia kwa kila kitu..”
“..Kwani umeoa John..??”
“..Kuoa..??, Hapana.., Ila nilishawahi kuishi na mwanamke lakini kama bahati Mungu akanionesha, Hakuwa na uwezo wa kushika mimba hivyo nikamrudisha kwao na kwa sasa naishi na mtoto wa Dada yangu tu, tena ni kabinti kadogo sana na nakasomesha kapo kidato cha pili..”
John alizidisha kumdanganya Jamila. Jamila hakujua lolote hivyo ilimbidi kukubaliana na yote kutokana na wazazi wake kumwachia laana kwa kukataa kuendelea na masomo huku akitanga tanga na wanaume sambamba na kujihusisha na kuigiza filamu za kibongo japo hazikumpa umaarufu sana katika jiji la mwanza. John aliyafurahia mapenzi usiku mzima huku akiamini malengo yake lazima yatimie ya kuitwa Baba, haijalishi mtoto atampata wa kiume ama wa kike.
 
40.

Muda wa wiki mbili za kuwasili warembo wote watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia sasa ukawa umeshafika. Warembo zaidi ya thelathini kutokea mikoa mbali mbali ya hapa Tanzania wakawa tayari wameshaanza kuwasili katika hoteli maarufu kwa kudhamini mashindano haya ya ‘Giraffe Green View. Ni mikoa michache tu ndio ilikuwa bado wawakilishi wao wako njian na wengine wakiendelea kuwasili, na kati ya mikoa hiyo ni pamoja na Dodoma., Morogoro na Jiji la Mwanza. Kwa upande wa jiji la Mwanza tayari wale warembo wawili waliopatikana walikuwa ndani ya ndege kuelekea Dare s salaam huku wakiongozwa na John pamoja na baadhi ya waandaaji. Ndani ya ndege John bado aliendelea kuwa karibu sana na mrembo aliyeshinda taji katika Jiji la Mwanza, Jamila Said. Japo baadhi ya waandaaji walioongozana naye walikuwa wakijua fika kuwa John alitembea na Jamila kutokana na kuwapa pesa kidogo kisha wakampitisha kuwa mshindi.


********


Taarifa juu ya John kuwepo njiani na ndege pamoja na baadhi ya washindi watakaoiwakilisha Mwanza sasa ikawa imeshamfikia mke wa John, Janet. Taarifa hiyo alimpa moja kwa moja mwanawe, Alice. Alice alijihisi pungufu ndani ya moyo wake endapo ataripoti kambini bila ya kumpokea Baba yake wa kufikia, John. Alichokifanya ni kuchukuwa baadhi ya nguo zake muhimu zitakazomsaidia huko kambini kisha wakachukuwa taksi na kwenda mpaka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere. Mapigo ya moyo ya Janet hayakuwa sawa na hii yote ni kutokana na vitu viwili vilivyokuwa vikiisumbua halmashauri yake ya ubongo. Kwanza ni presha juu ya kumuona John na kumpa taarifa za ushindi wa Alice walivyoupokea. Pili ni kuhusiana na ugonjwa uliomkuta Alice. Aliwaza sana ni jinsi gani atamuanza kumwambia John.
“..AAhh…!!!! Liwalo na liwe..??”
Janet aljikuta akiropoka mwenyewe punde baada ya kushuka katika taksi hali iliyomfanya Alice ausikie ule mguno kutoka kwa Janet.
”..Mama vipi tena mbona unaonekana haupo sawa..?”
“..Hapana mwanangu mbona nipo sawa tu..!!”
“..Mama., Nakujua Mama yangu hata ukiwa na hasira.. unaonekana umechukia kitu, au mimi nimekukera.. kama nimekukosea kwa chochote nisamehe Mama yangu..?”
“..Mwanangu Alice..? Hujajua tu ni kwa kiasi gani nakufikiria hadi nakasirika..?”
“..Unanifikiria kwa kitu gani tena Mama mbona unanitisha,,,??”
“..Mwanangu..??, ujue unaniacha katika majonzi mazito. Ndio unaelekea huko kambini, ujue nimekuzoea sana mwanangu kuwa karibu na wewe, ona sasa unaniacha mwenyewe unaenda huko kambini. Ndio maana naumia sana..!!”
Janet alijitahidi kumdanganya Alice huku akimwangalia kwa jicho la uongo. Alice alijihisi kusisimka karibu mwili wote hali iliyomfanya kumkumbatia Mama yake huyo kisha wakaelekea kumsubiri John. Ndani ya lisaa moja tayari ndege ya shirika la Tanzania ambayo inafanya ruti zake kutokea Mwanza mpaka Dar es salaam ndani ilikuwa imeshawasili katika Jiji la Dar es salaam. Shauku kubwa kutoka kwa Alice na Mama yake wa kufikia Janet sasa ikawa kama imezidishwa. Kila mmoja alikuwa akitoa macho kuangaza huku na kule huku wakipishana na baadhi ya abiria wakitoka.
 
41.
“..Mama..??? Baba yule kuleee..!!!, umemuana..??”
“..AAnhaa..!!, Ndio mwenyewe na kishatuona..”
Alice pekee alikuwa mtu wa kwanza kumtambua Baba yake wa kufikia, John. John alionekana kuongozana na warembo wawili huku wakiwa wamebebewa mabegi yao na wasaidizi katika uwanja wa ndege. Sasa akawa naye kashawaona Alice na mkewe. Mwanzoni alionesha kama kushtuka lakini alijikaza na kusogea taratibu mpaka pale walipo Alice na Janet. Alianza kwa kumkumbatia Alice kisha akamfuatia mke wake.
“.. Nafurahi kuwaona mpo salama.. sasa..?”
John alionekana kuwa na haraka sana.
“..Inanibidi niende mpaka kambini na hawa wahusika nikawakabidhi na baada ya hapo niingie ofisini nikaripoti ndio nirudi kwangu.. vipi na wewe Alice mimi najua upo kambini..??”
“..Hapana Dady..!!, nilikuwa nataka kwanza kuja kukupokea kisha ndio nikaripoti kambini. Nakupenda sana Dady yangu..”
Alice alishindwa kujizuia hisia zake nakujikuta anamkumbatia tena kwa mara ya pili Baba yake wa kufikia, John. Kile kitendo cha kumkumbatia moja kwa moja kikawa kimeshapita katika mboni ya macho ya Jamila ambaye muda wote alikuwa na wenzake kwa umbali kidogo wakimsubiri John. Hasira kali zilizochanganyikana na wivu wa ghafla vikaanza kumtawala Jamila. Ni wazi alijua huenda john ni Malaya hivyo wale ni wasichana wake tu. Jamila alijikuta akiubetua mdomo wake ovyo huku sura yake akiikunja vilivyo mithili ya yule muimbaji mkongwe wa taarabu kutoka Zanzibar, Bibi Kidude. Dakika takribani kumi nzima zikakatika kwa John kusimama na Janet pamoja na Alice. John alifarijika sana kusikia Alice amekabidhiwa nyumba kama sehemu mojawapo ya ushindi wake. Alichokifanya alichukuwa begi lake na kisha kumkabidhi mkewe, Janet.
“..Sasa mke wangu hili begi tangulia nalo nyumbani. Halafu wewe Alice sisi tunaelekea wote kambini na wale kulee..??’
“..Sawa Baba..!!”
“..Haya tuongozane kuna gari spesho limekuja kutuchukuwa tena nadhani litakuwa lile kule twende..”
John aliongozana na Alice huku wakimwacha Janet akirudi mwenyewe kwa shingo upande. Alice aliumia sana kumwacha kwa muda Mama yake wa kufikia lakini alijipa moyo kujituma zaidi huko endapo kwenye mashindano. Walipofika kwenye lile gari lilliokuwa likiwasubiri.
“..jamani ndugu na washiriki tuliotoka Mwanza, huyu hapa ni mshiriki mwenzetu na yeye ndiye atakayeliwakilisha kanda ya Chang’ombe katika mashindano haya yanayoenda kuanza.. anaitwa Alice Majaliwa..”
 
42.
Alice alionesha uso wa tabasamu huku akiwapa mkono watu karibia wote waliokuwa wameongozana na John katika safari ya kutokea Mwanza. Alipofikia kwa Jamila, Jamila hakutaka kabisa kumpa mkono alichokifanya, alibetua mdomo wake kisha akatoa jicho la dharau kumuangalia Alice. Alice hakuwa akijua chochote zaidi ya kumtolea tabasamu Jamila kisha akaketi kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea kambini. Mwendo wa nusu saa uliwatosha kabisa kufika katika hoteli ya Giraffe Green View ambayo ni maarufu sana katika kudhamini mashindano haya ya mrembo wa Tanzania. John akiongozwa na wale waandaaji wenzake walikuwa wa kwanza kushuka kisha wakafuatia washiriki wengine kama Alice na kina jamila. Makofi na vigelegele vilikuwa vimeanza kutawala kwa washiriki wengine ambao ndio walikuwa karibu kuwapokea. Alice alijihisi mwenye faraja sana kufikishwa hotelini hapo. Aliona sasa ile kazi aliofikiria muda mrefu sasa imefika pahala pake. Alitamani sana siku zikimbie tu mpaka ifike siku ya mwisho atangazwe kuwa mshindi. Kwa upande wa Jamila hakutaka kumuachia kabisa John kwani walipotawanyika Jamila alimfuata kwa kumkimbilia John kimya kimya huku akijifanya kuna kitu anamuwahishia John amekisahau..
“..Please mkuu, chukuwa hiki umekisahau kwenye gari ukiwa unashuka..”
Hakuna hata mmoja aliyegundua kitu anachotaka kukifanya Jamila zaidi ya kumuona mkononi kashika kitu kama anataka kumpa John. Alipofika karibu na John, Jamila alipooza sauti ya chini.
“..John, yote hii nafanya kwa ajili yako.. hii ni cheni ya kwangu lakini wale kule wote wanajua nimekuwaishia ulisahau kwenye gari wakati siyo yako ni ya kwangu..”
“..Sawa, enhee vipi mimi narudi kwanza kwangu nikampumzike, ila nitakuwa nakuja mara kwa mara hapa kambini na pia namba yako ya simu ninayo hivyo sina tatizo na wewe Jamila..”
“..hata kama unayo namba yangu John.. mie bado nakupenda na natamani hata tukalale tena mpenzi wangu..”.
“..Hapana Jamila, unajua tayari umeshaingia kambini hivyo mtakuwa chini ya mwalimu wenu na hakuna hata mmoja atakayeruhusiwa kutoka nje ya kambi hivyo kuwa mvumilivu mpaka siku ya mwisho kwani inachukuwa wiki mbili tu kambini, tutakuwa pamoja mpaka utachoka mwenyewe, cha muhimu nipe nafasi kwanza nikapange mikakati yote kuhusu wewe kuwa mshindi..”
“..Nikuulize kitu John..?”
“..lakini Jamila…? hivi si unaona kule mbaali kila mmoja anatuangalia hapa..? haya uliza haraka haraka unasemaje..?”
“..Nataka kujua kale kabinti tulichopanda nacho gari ni kanani kwako..?”
“..yule si mshiriki kama wewe..??, Sema yeye alikuwa amekuja kupandia gari pale alivyosikia tunakuja huku kambini..”
“..John..?? John..?? ndio mkumbatianae naye pale uwanja wa ndege..?”
“.. Jamila, embu hayo mambo mengine ni ya kuongea kwenye simu, hapa utafanya tumwahge mchele kwenye kuku wengi..”
John alikwepa swali na kisha akamuahca Jamila nakukimbilia mpaka ndani ya gari nakuondoka zake..
 
43.
“..mimi ndio Jamila, nitahakikisha haka kabinti hata kwenye mashindano hakafiki, nisipokauwa basi nakufa mimi..”
Alijisemea Jamila kimoyo moyo huku akiweka mikono nyuma nakurudi zake kujiunga na wenzake tayari kwa kujiandaa na mazoezi mbali mbali..
John alimwangalia Jamila mara mbili mbili huku akimuacha akirudi kujiunga na wenzake pale kambini.
“..Mmh.., hajanijua tu..!!, naendapo akinizalia nadhani atanijua vizuri.. wee acha adeke tu kwa muda huu..”
John aliongea peke yake kwa sauti ya chini chini huku akielekea kwenye gari tayari kwenda kazini kisha kurejea nyumbani kwake ambapo hakufika tangu aliposafiri kwenda Mwanza kwa ajili ya kuwatafuta warembo wawili ambao watawakilisha Jiji la Mwanza katika mashindano haya ya mrembo waTanzania. Muda wa masaa mawili yalijitosheleza kabisa kwa John kuweka sawa mambo yake ya kiofisi na kwa muda huu akawa mbele ya mlango wa nyumbani kwake.
“..Janet mke wangu..?? Janet fungua mlango..”
Janet aliufungua mlango ule wa sebuleni ambao alikuwa ameurudishia kutokana na kuwa bize kwa kumtengenezea mume wake chakula jikoni. Alimfungulia na kisha kumkumbatia sambamba na mabusu mazito mazito.
“..Karibu sana Mume wangu..!!, Karibu kwako sasa..?”
“..Asante sana..!!, Enhee niambie Mke wangu kwema lakini..?”
“..Ndio ni kwema tu wala hakuna tatizo lolote.. Twende chumbani kwanza ukabadili nguo uoge kisha ule ndio tuongee zaidi Mume wangu sawa..?”
“..Hapo ndipo ninapokupendea Mke wangu..!!”
John aliingia mpaka chumbani kwake kisha akabadili nguo nakuelekea bafuni huku akimwacha Janet akienda jikoni kuendelea na mapishi. Ndani ya dakika kumi John, alikuwa tayari kashamaliza kuoga na kuvaa kabisa nguo za kushindia nyumbani. Alienda mpaka sebuleni ambapo alikuta tayari Mke wake, Janet ameshaandaa chakula anamsubiri tu wale.
“..Enheee niambie Mke wangu..??, maisha umeyaonaje na Mwanangu Alice toka nimewaacha..??”
“..Mazuri tu Mume wangu.. nimeishi na Alice vizuri sana, nilikuwa naye pamoja toka kwenye yale mashindano mpaka akawa mshindi..?”
“..Hakukuwa na tatizo lolote lililotokea..??”
Janet alionesha kushtuka pale John alipouliza kuwa hakukuwa na tatizo lolote. Halmashauri ya kichwa cha Janet moja kwa moja ikampeleka huenda kuwa John anataarifa zote juu ya Alice kudondokewa na taa kule hotelini Kempinski.
“..Mhh.. Mhh hakukuwa na tatizo lolote jamani..”
“..Mbona umeguna Mke wangu..??, unauhakika na unachokinena..?”
“..Ndio jamani..”
Janet alijikaza nakujibu kiuoga kama yuko sahihi na anachokijibu.
“..Actually, Nimefurahi sana kusikia Janet ameshinda mashindano hayo. Na ujue sikujua kama zawadi ilikuwa ni nyumba..? Kwa hiyo keshakabidhiwa kila kitu..?”
“..Ndio Mume wangu..!!, mwanetu Alice alikabidhiwa nyumba ipo Kurasini na funguo zake zote ziko chumbani. Yaani ni jumba kubwa tu mbona..”
“..Kwa hiyo mmeshaanza labda kufanya chochote..?”
“..Hapana Mume wangu.., ni kwamba kwanza tumejitahidi kuitunza furaha yetu mpaka utakaporudi ndipo tuanze kufurahia kwa pamoja sambamba na kupanga tufanye kitu gani ile nyumba.”
“..Kwani Alice mwenyewe anasemaje kuhusiana na hiyo nyumba yake aliyokabidhiwa maana si mali yetu mali ya mshindi ambaye ni Alice..”
“..Unayosema ni kweli Mume wangu, lakini mtoto wetu Alice mwenyewe kasema hatahusika zaidi ya kutuachia sisi tuamue cha kufanya lakini alitoa wazo kama inawezekana tuipangishe na hela zitakazopatikana zitusaidie kuendesha maisha yetu kwa ujumla..”
“..Safi sana.. wazo zuri..”
 
44.
John alikuwa na furaha hata kabla hakuiona hiyo nyumba, alitamani asubuhi ifike haraka akaishuhudie hiyo nyumba ambayo alikabidhiwa Alice kama mshindi wa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Chang’ombe. Usiku wote huo John alikuwa katika furaha huku zile furaha akisherekea na Mke wake. Furaha ya John ilionekana kupitiliza hali iliyomfanya hata kukosa kabisa usingizi huku akitamani kukuchwe tu. Muda ulizidi kuyoyoma hatimaye asubuhi ikawadia na John akamuamsha Mke wake nakujiandaa kisha safari ya kuelekea huko Kurasini kwenye hiyo nyumba ikaanza. Walipofika ndipo John akaamini kama yale yaliosemwa na Mke wake ni kweli. Mawazo mengi yalimtawala kila akiingia kwenye chumba kimoja baada ya kingine, na alipofikia kwenye kile chumba cha kujitegemea alishangaa sana kwa jinsi kilivyorembwa na marumaru za kuvutia kuanzia chini mpaka bafuni. Kuna kipindi John mawazo mgando yakaanza kutawala kichwa chake nakutamani kama asubiri baada ya mashindano aje kumpangisha Jamila ili awe anampata kirahisi pindii atakapokuwa anamhitaji. Allibaki amezubaa sana pale chumbani mithili ya sanamu la kuchonga huku mawazo mengi yakimsonga.
“..John Mume wangu vipi tena mbona umezubaa hivyo..??”
“..Amm..!! mmh..!! hapana Mke wangu nafikiria mbali zaidi kwanza nafikiria kama kutakuwa na faida nyingi endapo tutapangisha..?”
John alibadilisha mada nakujifanya kama alichokuwa anawaza ni tofauti kidogo. Wakiwa bado wanashangaa mazingira ya ile nyumba punde John akapigiwa simu. Alibaki akiitolea macho ile simu kutokana na namba ngeni aliokuwa akiiona kupitia simu yake ikiita.

********

Joto kali ambalo bado liliendelea kulitikisa Jiji la Dar es salaam huku kila mmoja akitamani kulala na feni mpaka asubuhi. Kwa wale wenye pesa zao wao walikuwa wakiwasha viyoyozi mpaka asubuhi na wale walala hoi wao walikuwa katika kushikilia mashati yao hata pengine mashuka yao nakujipepea mfano wa zile feni za panga boi usiku kucha huku wakiiombea asubuhi ifike. Hali ilizidi kuwa tofauti sana kwa siku ya kwanza tu pale hoteli Girrafe Green View ambapo warembo wote watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia walikuwa wameweka kambi. Kila chumba kimoja cha hoteli kilihifadhiwa warembo wawili wawili. Ni mwalimu wao wa mazoezi mbali mbali ya hapo kambini ndio aliokuwa ameteua warembo wawili wawili wakae katika chumba kimoja. Miongoni mwa warembo hao ni Alice na Jamila ambapo walijikuta wamepangwa katika chumba kimoja. Tangu kupangwa usiku huo baada ya chakula cha pamoja Alice alionekana mnyonge sana kutokana na Jamila kumuonesha wazi kulinga sana. Matunzo ambayo alilelewa nayo Alice juu ya kuishi na watu ni kati ya vitu vilivyojijenga sana maishani mwake. Kimoyo moyo Alice aliapa hatakuja kumchukia mtu yeyote kwani ndio mbinu mojawapo ya ushindi.
“..Jamila rafiki vipi twende tukalale jamani..??, funguo yetu si umepewa wewe..??”
Jamila hakumjibu Alice zaidi ya kumuangalia kwa jicho la dharau kisha akamfanyia ishara ya kuongozana huku Jamila akiwa mbele na Alice nyuma tayari kwenda chumba cha kulala. Walipofikia chumba chao ambacho ni namba 24 bado Jamila alijawa na dharau huku akizirusha nywele zake kwa kutumia kichwa chake. Alice alijitahidi kujipendekeza sana japo kutamka maneno mawili matatu kwa Jamila lakini aliambulia masonyo na kebehi huku Jamila akizidisha maringo yake na kuufungua mlango mpaka ndani. Muda wa kulala ulipo wadia, Alice alibadilisha nguo zake nakuingia bafuni kujimwagia maji lakini kabla hajatoka alishangaa kupigana kikumbo na Jamila mlango wa kuingilia bafuni. Jamila alilisogelea sinki kisha akatapika sana. Haikuwa tapika ya kawaida kwani tumbo lilishaanza kumshika vilivyo huku akijihisi kitovu kinavutwa. Kichefu chefu cha ghafla kilichokuwa kikimtawala kilimfanya moja kwa moja kujihisi tayari mimba imeingia katika tumbo lake.
“..Oooh my God..??, Thanx..!! , Thanx..!!!”
Jamila alishukuru sana kupata mimba lakini Alice muda wote alikuwa amendelea kumtolea macho Jamila akitapika. Alice hakuwa anajua dalili zozote za mwanamke mwenye mimba maishani mwake. Alishangaa badala Jamila asikitike kwa kutapika yeye ndio kwanza anamshukuru mwenyezi Mungu.
 
45.
“..Pole sana Jamila..!! Pole jamani..!! sasa si ungekunywa da..??”
“..SSshhiiii..!!!!, Pumbavu mkubwa, tena uishie hapo hapo..!!..”
Jamila alimkatisha maongezi Alice kisha akamtukana nakuelekea kitandani kulala. Kila akiutafuta usingizi kwake ulikua shida alichukuwa simu yake na kumpigia John japo kumpa taarifa hizi lakini John hakupatikana kwenye simu, alikuwa ameizima. Jamila Alitamani sana asubuhi kukuchwe haraka japo John apate taarifa. Ile hali ya Joto katika jiji la Dar es salaam ukichanganyia na kuvurugika tumbo kwa Jamila kulimfanya ajisikie kizungu zungu nakumpelekea afungulie kiyoyozi japo kupata hewa. Alice muda wote alikuwa ameshapitiwa na usingizi baada ya kuona Jamila kawa mkali. Kile kiyoyozi kilichofunguliwa kwa fujo na Jamila sasa kikawa kimefika juu zaidi hali iliyomfanya Alice kujisikia vibaya. Baridi kali ambalo lilikuwa likipenyeza mbavuni mwake huku likihamsha mapafu yake nakumfanya kukohoa sana lilimfanya Alice aamke.
“..Samaahani Jamila unaweza kupunguza japo hicho kiyoyozi kidoogo, kwani kiafya sijisikii vizuri..”
“..Hujisikii vizuri..??, Eehhhee heeee..!!, MMhh wacha nicheke Jamila mie.. kwani..? Hujawahi kupuliziwa na kiyoyozi maishani mwako enheee..? sasa hapa sipunguzi kama unaenda kulala nje we nenda tu babu wee..”
Alice alijihisi mtu mkosaji sana duniani tena kwa baadhi ya watu. Aliaamini kuna vizingiti vikubwa na hii yote alichukulia kama mitihani ya maisha. Alice hakutaka kabisa ugomvi na Jamila, alichokifanya alichukuwa shuka lake la kulalia kisha akafungua mlango wa bafuni nakujifungia humo halafu akalala chini kwenye sakafu ya baridi. Haikupita hata lisaa, Alice akawa ameshapitiwa na usingizi. Kitu kilchokuja kumshtua ni maji maji yaliokuwa yametawala katika shuka lake la kujiifunikia. Alihisi kama shuka lote limelowa. Alivumilia kwa muda lakini uzalendo ukamshinda na kujikuta amelitoa shuka lote kisha macho yake yakakutana uso kwa uso na Jamila mbele yake.
“..Unasemaje Dada yangu..?”
“..Nani Dada yako..??, Pumbavu wewe na bado..!!”
Maskini Shuka lote aliokuwa amejifunika Alice kule bafuni likawa limelowa matapishi ya Jamila ya usiku wote. Mabaki ya chakula walichokula mara ya mwisho hotelini sasa yakawa yameshaenea katika lile shuka. Harufu kali ya bia aina ya Red’s ikawa imeshatawala katika lile shuka. Alice aliinuka na kisha kuliloweka kwenye sinki huku akitumia sabuni ile ya kuogea kulifua kwa usiku ule. Akiwa bado mule bafuni akilifua lile shuka mara Jamila naye akaingia mule bafuni tena.
“..Wee..?? wee..?? wee..?? unafanyaje usiku huu..? kwanini unamaliza hizo sabuni za hotelini..? kanunua Baba yako..? Enhee..???”
“..Hapana..!!”
“..Sasa kwanini unaifulia tena shuka wakati ni ya kuogea..? na mimi asubuhi nitaogea nini shetani wewe..? pumbavu wee..??”
Jamila alichukuwa mkono wa kushoto na kumpiga Alice. Alice aliliacha lile shuka nakujiziba usoni ili asiumizwe. Nguvu kubwa alizokuwa nazo Jamila zilimfanya Alice apigwe sana. Jamila alimuwekea Alice lile shuka chafu mdomoni kisha akaanza kumpiga sana huku Alice akishindwa kuhema wala kutoa sauti.
“..Ndio ukome kudandia waume za watu.. na leo nahakikisha nakuua kabisa ufe..??”
Jamila aliazidisha nguvu zake mpaka akashuhudia Alice amelegea mwili wote huku uso wake ukionesha dhahiri kumvimba. Kile kipigo kilimfanya Alice kupoteza fahamu huku povu jingi likimjaa mdomoni sambamba na damu nyingi kummwagika zikitokea puani. Ule moyo wa kijasiri alioumbiwa nao Jamila ulimfanya kushangilia ushindi ule na kisha akammalizia Alice kwa kumpiga mateke katika kifua chake huku akitoka kule bafuni nakuelekea kitandani mpaka kwenye begi lake kisha akachukua mkasi nakurudi nao tena bafuni. Jamila alianza zoezi zima la kumyoa nywele zote Alice mpaka akahakikisha amebakiwa na upara kisha akazichukuwa zile damu zilizokuwa zinatawanyika katika pua ya Alice na kumpakaza nazo kichwani. Alipomaliza hapo Jamila alienda moja kwa moja mpaka kwenye simu yake kisha akamwandkia John ujumbe mfupi..
“GAME IS OVER JOHN..”
 
46.


Furaha kubwa bado ilikuwa imetawala ndani ya moyo wa Jamila. Alijua sasa kile alichokitaka amekimaliza. Hofu ilianza kumnyemelea taratibu mwilini mwake kwani tayari akili yake ilimtatiza kitu cha kujibu endapo wakija chumbani kwao na kumkuta Alice amekufa. Chumba chote kilikuwa ni cha Jamila kwa kuranda randa usiku wote huku akiongea peke yake.
“..Yees..!!, Sio mimi niliyemuua.., Mwalimu na wenzangu wote ni kwamba mimi… Noo.., nooo..Hiyo siwezi embu ngoja.. Ni kwamba nililala naye usiku vizuri sasa sijui nashangaa nimeamka tu asubuhi tayari ana damu nyingi puani mwake huku kanyolewa upara.. Hapana hapa nitakosea watashtuka hii hapana.. Mwalimu ni kwamba nimeshtushwa kuamka tu nakutana na mwili wa Alice ukiwa tapatapa huku damu zimemuenea kila sehemu. Siamini sana mambo ya kishirikina lakini mwalimu inawezekana.. Yees ..! cha kujibu nimepata…”
Muda wote Jamila alikuwa ni mtu wa kujisemesha peke yake ni kwa jinsi gani atajibu maswali endapo kutakucha. Alijijengea taswira kwanza kwa washiriki wenzake watakavyoshtuka na hilo tukio na tena ni mara ya kwanza tu limetokea tatizo. Aliwaza sana mpaka mawazo yake yakampeleka kwa wahusika wenyewe wa hoteli. .
“..Mhh lakini ninaweza kuumbuka hapa kwa maana watu wa hoteli wanaweza kusema kuwa hakujawahi kutokea tatizo kama lile na nikaumbuka bure. Na je wakimpeleka kwenda kumpima hospitali alama za mikono..?”
Sasa mwili wa Jamila ukawa kama umepigwa ganzi kwa muda. Mwili wake ulikuwa tayari umeingia barafu tena lile la baridi. Alihisi hali ya hewa imebadilika kutokea joto mpaka baridi kali. Alichukuwa ule mkasi aliotumia kumnyoa Alice kisha akautupa kwa dirishani kupoteza ushahidi na kilichofuatia aliingia bafuni na kuchukuwa kipande cha sabuni alichokuwa akifulia shuka Alice na kisha kunawa mikono vizuri. Jamila aliamini kuwa kufanya hivyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kutojulikana kama ni yeye alihusika katika mauaji ya Alice. Alirudi mpaka kitandani kwake nakunyanyua simu yake kwa mara nyingine huku akijaribu kuipiga namba ya John lakini ikawa vile vile kama mwanzo kuwa haipatikani. Aliangalia tena ile meseji aliyoituma kama ilimfikia lakini bado ikawa inaonesha iko hewani, muda wowote endapo John akiwasha simu yake itamfikia. Kutokana na uchovu aliokuwa nao Jamila kwa vitendo alivyomfanyia Alice usiku kutwa alijikuta usingizi ukianza kumnyemelea taratibu huku macho yake yakionesha dhahiri kuzidiwa na usingizi.

*******
 
47.

Sauti za ndege wa porini wanaoishi mjini uku zikichochewa na mbwa wa mitaani ndizo zilikuwa zikiashiria kuwa imefika Saa kumi na mbili alfajiri. Kelele za milango za kufungwa na kufunguliwa nazo ziliwaamsha baadhi ya wapangaji wa hoteli. Jamila alikuwa mmojawapo kati ya watu waliokuwa wameamka asubuhi sana. Ule usingizi ulikokuwa umemptia usiku sasa ukawa wote ukawa umekatika huku macho akiyatoa sana kumuangalia mtu wa pembeni yake.
“..Aliice..?? Alice..??”
Mapigo ya moyo ya Jamila yalikuwa kasi zaidi huku yakichochea jasho kutiririka sambamba na mishipa pembezoni mwa shingo yake kumtoka. Alishangaa kumshuhudia Alice akiwa kajifunika shuka vizuri pembeni yake huku akionekana hana hata tone la damu. Jamila hakutaka kuamini mpaka akamfunua shuka lote nakumshuhudia Alice akiwa bado na nywele zake zile zile huku akikoroma kuonesha yupo kweye usingizi mzito sana..
“..Ohh..!!, This is not serious..?? (Hii si kweli kabisa..??)”
Jamila alijaribu kumuamsha Alice kwa kumtingisha labda huenda akashtuka. Kadri alivyomuamsha Alice ndivyo na Alice alikuwa akizidi kukoroma. Akili ya Jamila ikamuahama sasa akaacha zoezi zima la kumuamsha Alice na kukimbilia moja kwa moja mpaka bafuni kukagua vizuri kama ataziona zile damu zilizokuwa zikimwagika Alice usiku. Napo alipofika alikuta bafuni kweupe tena kusafi sana tu. Alichokifanya akarudi tena kwa mara ya pili mpaka pale kitandani. Alimgusa Alice mapigo yake ya moyo lakini yalikuwa yakidunda hivyo akaanza na kumuahamsha kwa mara nyingine tena.
“Alice my love..??, Pliizz amka tujiandae twende mazoezi.. Alice..?? Alice..??”
Kwa kuanza na jicho moja la kushoto na kisha la pii taratibu Alice akayafumbua macho yake yaliokuwa bado yamezungukwa na limbi la usingizi huku akimtolea macho yale Jamila.
“..Niambiae Dada yangu..”
“..Mhh Alice unalala wewe..?? yaani nimekuhamsha muda mrefu hata huamki mwenzangu..”
“..Nahisi nilikuwa nimechoka sana hata hivyo..?”
“..Ok.., Ingia bafuni basi kajiandae kwani muda si mrefu mwalimu atakuja kutuhamsha huku..”
Jamila hakutaka kabisa kuamini kama aliokuwa akiongea naye ni Alice. Mpaka pale Alice alipoamka nakuchukuwa taulo kisha akaingia bafuni tayari kwa kuoga. Mapigo ya moyo ya jamila sasa yakawa yamepungua kasi yake. Alibaki akitafakari sana ndoto mbaya ambayo ilimtokea usiku wote. Alijitahidi kurudisha kumbukumbu zake mpaka usiku mara ya mwisho walipoongozana na Jamila mpaka chumbani kisha akafungua mlango. Na Alice alikuwa wa kwanza kuingia bafuni kuoga kisha alipigana kikumbo na Alice akiwa anatoka kuoga na kile kikumbo ilikuwa ni haraka haraka za yeye kwenda kutapika kwani alijisikia kichefu chefu sana. Na baada ya kurudi kutapika alimkuta Alice ameshalala hivyo na yeye akalala na ndipo ndoto za ajabu zikaanza kumtawala usiku kucha.
“..Mmh..?? eti nimemuua Alice jamani..? hadi alitoka na damu nyingi puani mwake.. Allah niepushe na ndoto mbaya kama hizi..!!”
Jamila alibaki akiongea peke yake huku akiinuka na yeye kitandani nakujifunga taulo tayari kupishana na Alice akitoka kuoga na yeye aende kuoga. Na ndani ya nusu saa tayari Alice na Jamila walikuwa wameshamaliza kujiandaa. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kwa mara ya kwanza kuingia kambini hapo. Siri kubwa juu ya ndoto mbaya alioiota Jamila usiku ilibaki moyoni mwake. Kamwe aliapa kutomwambia Alice wala mtu yeyote kwani alijiwekea imani mara nyingi ndoto kama hizo endapo atamwambia mtu basi huenda ikatokea kweli. Sasa Jamila akawa ni mtu wa kuonesha upendo wa hali ya juu kwa Alice. Hata wakati wa kujipodoa ni Jamila pekee ndio alipendekeza Alice atumie vitu vyake. Kutokana na miili yao kuwa sawa, Jamila alitoa trakisuti yake na kumkabidhi Alice avae vivyo hiyo na Alice.
“..Alice..??, Pliizi nakuomba tuwe na urafiki wa karibu sana..!!, na pia sipendi urafiki wetu uishie hapa kwenye haya mashindano..”
“..Ni sawa tu Jamila, hata mie nitafurahi endapo tukaendelea kuwa karibu na nadhani hata Baba yangu atafurahi pia kusikia nina rafiki wa karibu katika haya mashindano..”
“..Kweli..??”
“..Yap.., Ndio Jamila..!!, kwa jinsi ninavyomjua Baba yangu alivyomchangamfu yaani atafurahi huyoo..??”
Jamila aliguswa sana na maneno ya Alice, alitamani sana siku moja aje amuone huyo Baba yake Alice. Alijihisi sasa mtu wa kumwambia siri zake zote za maisha ni Alice pekee.
“..Alice kuna story moja nataka nikwambiae inanihusu mimi..??”
“..Mmh..!!, umejuaje kama napenda sana story mie..??”
“..Unapenda..? Basi hiyo ni true story ambayo imenitokea na mpaka sasa hivi inaendelea lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu wa karibu najua utanipa ushauri mzuri sana.. Sasa sijui nikuhadithie kwa sasa hivi au jioni tena tukirudi kulala..??”
 
48.
“..Basi tufanye jiioni maana najua tu hapa utanikatisha utamu kama stoy za mwandishi Andrew Carlos yule wa Facebook..!!!”
“..Kumbe na wewe unamjua enhee..??”
“..Yaani wee acha tu.., mie story zake zinanifanya hata nakosa hamu ya kula chakula, kila muda nakodolea macho kwenye page ya uwanja wa simulizi tu nikijua ataendelea lakini anakuja kutoa baadaye, na akitoa tena ananiacha kwenye hamu ya kutaka kujua tena kinachoendelea, lakini story zake ni nzurii..”
Wakiwa bado katika kupiga story Alice na Jamila mara hodi ikagongwa katika mlango wao. Alice alikwenda kufungua, alikuwa ni mwalimu wao.
“..Haya.., haya muda umefika mpo tayari wote..”
“..Ndio mwalimu tupo tayari..!!”
“..Haya tuongozane kwenye basi nchni kabisa kisha tunaelekea Coco beach na tukitoka hapo tunarudi kujiandaa tayari kwa kwenda kituo cha watoto yatima Dodogodogo Centre kwa ajili ya kuwapelekea zawadi watoto yatima..”
Pilika pilika za kutwa zilianzia hapo. Alice na Jamila walliongozana pamoja mpaka chini kupanda basi. Upendo aliokuwa akionesha Jamila dhahiri utajua ni ndugu na Alice. Walikaa siti moja katika basi na mapaka wanafika Beach Jamila alikuwa pamoja na Alice katika michezo mbali mbali na hata wakati wanarudi bado walikuwa wamejitenga na wenzao huku wakipiga sana story na kucheka peke yao. Muda wakupeleka chochote kwa watoto yatima pia Alice na Jamila walikabidhiwa Ndoo ya mafuta ya kupikia ambapo waliibebelea wawili mpaka wakakabidhi. Upendo ulizidi, walikula chakula cha pamoja na wale yatima huku Jamila akifanya vituko kuwafurahisha watoto na pia Alice alikuwa pembeni yake akimuiga Jamila. mpaka jion inafika Jamila na Alice walikuwa hoi kwa siku nzima na sasa wakawa wameshamaliza kula chakula cha usiku cha pamoja na wameelekea chumbani tayari kwa ajili ya kulala.
“..Jamila..??”
“.Niambie..??”
“..Sasa ndio ule muda wetu muafaka ulioniambia, unakumbuka asubuhi uliniambiaje..??”
“..Mmh Alice husahau..?? Ok, kwakuwa tupo kitandani nitakusimulia lakini usilale bwana mpaka nitakapomaliza sawa..?”
“..Hee..?? kwenye story hata usingizi huwa sina mwenzako..!!”
“..Basi nikwambie Alice, kwanza kifupi Baba yangu na mie ni msukuma ila Mama ni mhehe wa Iringa. Mapenzi yangu kwao yalikuwa ni maziuri tu kwa kuwa nilikuwa mtoto pekee. Walinidekeza kwa kunipa kila nilichokuwa nikikihitaji. Lakini kwa bahati mbaya nilipofikia kidato cha tatu nikaamua kuachana na shule. Na hii yote ni kutokana na kumpenda sana Nick. Wee..?? haya mapenzi wewe yasikie tu Alice. Basi Nick akanifanya niache shule niishi naye kwenye geto lake na kwa kitendo hicho kilimkera sana Baba yangu. Alifanya kila analoweza kumzuia Nick lakini mapenzi yalizidi kwani niliamua kumwambia Baba hadharani endapo anataka kunipoteza Duniani basi aendelee kumtesa Nick wangu.. Kile kitendo kilimuuizi sana Baba yangu nakujikuta wamenitenga yeye na Mama.. Nilihangaika maisha na Nick huku nikimtegemea Nick kwa kila kitu.”
“..Kwan Nick alikuwa akifanya kazi..?”
 
Back
Top Bottom