Mrembo aliyepotea

Mrembo aliyepotea

20.
“..Hapana dokta na kiumbe changu..”
“..Ni kwamba mimba inaonesha ilikuwa ndogo sana hivyo imesharibika na hii harufu kali unayoendelea kuisikia ambayo hii damu iliobadilika rangi na kuwa ya kijani na manjano imetokana na hii mimba iliyoharibika, Na huenda mimba ikawa imechangia kifo cha huyu japo sijapima vipimo vingine vilivyompelekea kifo chake. Cha muhimu ni kumshukuru Mungu kwa kazi yake aliyoitenda..”
“..Noo, Noo, Nooo Dokta siwezi kuvumilia..!!, Dokta nashindwa kujizuia..!!, ni nani ataliziba pengo hili.., nani atanizalia Doktaaaa….”
Daktari akabaki na mshangao, Mshango wa kile anachoendelea kukishuhudia kwa John, Alijitahidi sana kumbembeleza lakini ndio kwanza alikuwa akizizidisha hasira za John ambazo sasa zilikuwa zinamshinda nguvu na kusababisha mdomo wake kuanza kuropoka ovyo na kwa sauti ya ukali. John na yule daktari Wakiwa bado wodi ya wagonjwa mahututi mara Nesi akatokea huku akionesha anahema sana na amekuja kwa taarifa.
“..Dokta..??, Dokta…??, Dokta..?? Yyyuuu uule mgonjwa uliyetuambiaa tut u tuumpeleke kule wooddini.., tumemuwekea ile oksijeni ili apate hewa lakini oksijeni yote imejaa damu na sasa yupo anafurukuta kama anataka ku..”
“..Unasemaje..??, Alice anakufaa..?”
John alishikwa na butwaa nakuropoka.., hakuamini maneno ya yiule Nesi, wakaondoka wote na Yule Dokta mpaka kwenye wodi alipokuwa amelazwa Alice napo walipofika walishuhudia kitanda chote kikifurika bahari ya damu huku Alice akijikunja kunja mithili ya mtu anayetaka kukata roho..

******************************

ITAENDELEA
 
Lost soldier imeishia wapii sasa
IPO MKUU, ENDELEA KUFUATILIA KATIKA UZI HUU

 
20.
“..Hapana dokta na kiumbe changu..”
“..Ni kwamba mimba inaonesha ilikuwa ndogo sana hivyo imesharibika na hii harufu kali unayoendelea kuisikia ambayo hii damu iliobadilika rangi na kuwa ya kijani na manjano imetokana na hii mimba iliyoharibika, Na huenda mimba ikawa imechangia kifo cha huyu japo sijapima vipimo vingine vilivyompelekea kifo chake. Cha muhimu ni kumshukuru Mungu kwa kazi yake aliyoitenda..”
“..Noo, Noo, Nooo Dokta siwezi kuvumilia..!!, Dokta nashindwa kujizuia..!!, ni nani ataliziba pengo hili.., nani atanizalia Doktaaaa….”
Daktari akabaki na mshangao, Mshango wa kile anachoendelea kukishuhudia kwa John, Alijitahidi sana kumbembeleza lakini ndio kwanza alikuwa akizizidisha hasira za John ambazo sasa zilikuwa zinamshinda nguvu na kusababisha mdomo wake kuanza kuropoka ovyo na kwa sauti ya ukali. John na yule daktari Wakiwa bado wodi ya wagonjwa mahututi mara Nesi akatokea huku akionesha anahema sana na amekuja kwa taarifa.
“..Dokta..??, Dokta…??, Dokta..?? Yyyuuu uule mgonjwa uliyetuambiaa tut u tuumpeleke kule wooddini.., tumemuwekea ile oksijeni ili apate hewa lakini oksijeni yote imejaa damu na sasa yupo anafurukuta kama anataka ku..”
“..Unasemaje..??, Alice anakufaa..?”
John alishikwa na butwaa nakuropoka.., hakuamini maneno ya yiule Nesi, wakaondoka wote na Yule Dokta mpaka kwenye wodi alipokuwa amelazwa Alice napo walipofika walishuhudia kitanda chote kikifurika bahari ya damu huku Alice akijikunja kunja mithili ya mtu anayetaka kukata roho..

******************************

inaendelea
Mkuu usitupe arosto wengine hatuziwezi
 
21.

“..Lete mashuka mengine..??, Na muondoe mashuka haya hapa..??”
“..Sawa Dokta tumekuelewa..!!”
Haraka haraka kukafanyika kwanza kitendo cha kubadilisha mashuka ambayo yalikuwa yametapakaa damu na kuweka mashuka mengine.
“..Haya nawaombeni wote mtoke nje mniache kama baada ya nusu saa niweze kumtibu huyu mgonjwa..”
Dokta aliamrisha kisha baadhi ya manesi wa zamu wakiongozwa na John wakatoka nje na kumuacha Dokta akiendelea na zoezi la kumtibia Alice. Akili ya John muda wote bado ilikuwa imeganda kwa marehemu mpenzi wake Angel na haswa alikuwa akifikiria kiumbe kilichopotea tumboni mwa Angel. Alijitahidi kuvuta kumbukumbu vizuri kuanzia kipindi kile ambacho alimkuta Angel akijiuza Posta usiku wa manane na kisha akamshawishi kumuomba amzalie na wakakubaliana hadi Angel mwenyewe ndio aliotoa taarifa kwa John kuwa ameshika ujauzito. Ile furaha na ahadi ambazo John alikuwa amemuhaidi Angel sasa akawa anaona kama ni ndoto ambayo amelala usiku nakuamka asubuhi hamna kitu. Alitamani sana tukio lote aliloshuhudia usiku ule ligeuke nakuwa ndoto.
“..Shiiiiit…!!!!, Why me God…!!, Kwanini mimi tu Mungu wangu, Nimekosa nini kwako..?? najua umenipatia Mwanamke nikamuoa hakuwa na uwezo wa kuzaa.., Nikatafuta njia nyingine nikafanikiwa kumpa Mwanamke mwingine ujauzito na sasa amefariki, umemchukuwa..??, Why me…??, kwanini Mungu..?? AAahhh…!!!”
John alijikuta akipiga mateke fuko la uchafu ambalo lilikuwa pembeni yake huku akijishika shati lake kwa nguvu kama anataka kulichana. Sura yake sasa ikawa imezoea mateso kwa muda. Ule uso wa huzuni ukamzidia mara mbili kwani ulikuwa umetuna haswa huku macho yake yakionekana kuwa mekundu sana. Alikuwa kama nusu chizi nusu mzima kwani hata lile shati lake alilikunja mikononi nakuwa kama mtu anayetaka kuingilia ugomvi ama kutaka kupigana kabisa. Hatua za kuelekea kule wodini zikaanza.
“..Hapana haiwezekani Angel wangu afe hivi hivi..??, Nani atakuwa amemuua..??, ni nani nasemaa.??.”
“..Wewe Kaka vipi..??, unaenda wapi huko si Dokta kasema asiingie mtu..??.”
“..Niacheni..!!, nielekezeni mochwari mlipompeleka mchumba wangu Angel nikamuage..??, Nipelekeni nimesema..??, Nipelekeee..??”
John alikuwa mkali kidogo kwa awale manesi wa zamu. Alihitaji kumuona tena Angel wake. Bado hakuamini kabisa kama Angel wake amepoteza uhai. Kwa woga waliokuwa nao wale manesi na walitaka kutii ile amri ya Daktari wao kuwa asiingie mtu mule wodini, walijikuta waakimuelekeza John mochwari ilipo napo John akaongoza mpaka mlangoni nakukutana na mlinzi wa zamu ambaye alikuwa ni Mzee wa makamo.
“..Namtaka mke wangu aliyeletwa humu usiku huu..??”
“..Unasemaje kijana..??”
“..Kama ulivyosikia namtaka mke wangu..??, Ameletwa huku..!!”
John alikuwa mbishi hakutaka kabisa kujibizana na yule mlinzi wa ile monchwari, kwa kuwa yule mlinzi alikuwa mzee japo si sana lakini John alifanikiwa kumsukuma nakuingia mpaka ndani ya monchwari. Alipofika ndani hakuweza kuutambua mara moja kutokana na yale mazingira aliokuwa ameyakuta. Kuna maiti ambazo zilikuwa zimelaliana huku zikionesha zimevimba sana. John alijitahidi kuangalia kama atamuona kwa wale waliolaliana lakini hakuambulia kitu.
 
22.
Sasa zoezi likawepo kwenye kufungua yale majokofu yaliokua nayo yamehifadhiwa miili ya watu waliokufa moja baada ya jingine. Ile hali ya ujasiri ikaanza kumpotea John akajikuta akilegea kila akifungua jokofu na kushuhudia maiti za watu wengine. Kuna waliokuwa wamepata ajali sura zao zikiwa hazitamaniki, Wengine wamepondeka sura. Hatimaye akafanikiwa kukutana na jokofu lililokuwa limehifadhiwa maiti ya Angel. John alitoa sana machozi, alitumia mikono yake kushika kichwa cha Angel huku akikilila.
“..Angel..??, Kwanini hukuniambia kama unakufa..? nani sasa atanizalia Angel.. nasema nani..? mdogo wako umemuacha peke yake na sasa nayeye anataka kukufuata huko ulipo.., Pliiz japo fungua macho Angel uniage nitaridhika.., fungua Angel..??, Angeeeelllll….????”
Nguvu zikaanza kumlegea John nakujikuta taaratibu miguu ikikosa nguvu huku mikono ikimtetemeka zaidi mithili ya mtu aliyepigwa shoti ama aliyemwagiwa maji ya barafu, hivyo akadondoka peke yake mpaka chini nakupoteza fahamu

*****

Namba za simu, Pasipoti ya kusafiria ambazo ziikuwepo katika mifuko ya suruali ya John vikiambatana sambamba na funguao za gari lake ndizo zilikuwa zikimjulisha John Mapunda. Kazi yake ya kusimamia warembo wa miss Tanzania ndio ilimpa jina sana. Sura yake haikuwa ngeni kwa baadhi ya wafuatiliaji wa mashindano ya ulimbwende. Taarifa juu ya John kuwa hoi na kulazwa hospitali ya Amana usiku wa manane sasa ikawa imeshamfikia mkewe Janet. Janet alipokea simu kwa mtu asiyemfamhamu lakini alijitambulisha kwa jina moja tu kuwa ni Daktari katika hospitali ya Amana, ndipo na simu nyingine kutoka kwa baadhi ya marafiki zake na john zikaendelea kumiminika kumpa taarifa juu ya mumewe. Akili ya Janet moja kwa moja ilihamia kwenye ajali, Alijua ni wazi John atakuwa amepata ajali ya gari kwa sababu tabia ya mumewe kuendesha gari huku amelewa ni tabia yake ya kila siku. Haraka haraka Janet akaingia jikoni nakutengeneza uji wa ulezi aliokuwa akiupenda sana mumewe kisha akapika ndizi zikawa laini sana akavipaki, halafu akampitia rafiki yake wakaribu, Mary na safari ya kuelekea hospitali ya Amana kwa kutumia teksi iliyowatoa magomeni ikaanza.
“..Kwani jana hakukupigia simu alipotoka kazini..??”
“..Hapana..!!, yaani nashangaa tu leo kupigiwa simu, Namimi nilishamkatazaga haya mambo yake ya kuendesha gari huku amelewa ona sasa yaliomtokea..!!”
“Janet usisimeme hivyo jamani..!!, yaani badala umsikitikie na kwenda kumpa pole wewe kabla hatujafika umeanza kumsemea vibaya..!! usifanye hivyo mpendwa..!”
“..Hapana Mary..!!, John amezidi..!!, kwanza kutwa ni wasichana utafikiri hana mke..??, na hiyo mipombe yake ndio kabisaa..!!”
Janet alikuwa bado anahasira.
 
23.
Njia nzima kuanzia kwenye teksi waliokodi yeye na mwenzanke Mary, alikuwa akimsemea vibaya John.
“..Yaani Mary, mie nimechoka.., nimechoka.., ni bora angekufa tu nikajua sina mume kuliko anavyonifanyia.. wewe rafiki yangu na ni kama ndugu tena wa muda mrefu unajua sana matatizo ambayo ninayo ya kutokuzaa.., sasa John ndio amechukulia ni jambo la kumkosesha raha ya maisha wakati watu wengine wanaishi vizuri kwenye ndoa zao.
“..Ndio Janet..!!, Lakini John..?? , MMmhh..!!!”
“..Na jana nilipewa ushaurii juu ya ya tatizo letu nikaambiwa kuwa inawezekana sana tukapata mtoto wa kupandikiza. Sasa ndio nilikuwa nataka nije tushauriane ona alichokifanya kapata ajali huko na Malaya zake..”
Njia nzima ilikuwa ni ya Janet kuongea huku Mary akiwa kimya kwa kumuitikia. Haikuwachukua muda wakawa wamefika hospitali ya Amana, alimkabidhi yule dereva teksi pesa yake kisha akachukuwa simu nakuanza kupiga zile namba alizopigiwa na Dokta.
“..Samahani Dokta..!!, Nimeshafika hapa Amana na nilikuwa namuulizia Mume wangu ambaye umeniambia yupo hapa hospitali kalazwa..”
“..Anhaa.., nyosha na njia ya kuingilia hapo getini moja kwa moja kama unaelekea mochwari angalia wodi ya pembeni yako unayotizamana na hiyo mochwari halafu ungie hapo.., Ingia mpaka kwenye kitanda namba 26 ndio utamkuta hapo..”
Ramani yote aliyopewa na Daktari sasa ikawa imeshahamia ndani ya halmashauri ya kichwa cha Janet. Janet alikuwa rahisi sana kunasa kitu. Sasa akawa njia moja na rafiki yake Mary huku wanaangaza huku na kule wakisoma namba za pembeni mpaka wakafikia namba waliotajiwa yaani namba 26. Watu waliokuja kumtembelea walikuwa ni wengi japo si sana. Janet alimkuta mumewe katika hali ambayo haikuwa nzuri kwani mwili wake kuanzia sehemu za usoni ulikuwa umemvimba sana japokuwa hakuwa na majeraha yeyote. Alichokifanya Janet ni kushusha kapu ambalo alikuwa amebebea vyakula na kisha akachukuwa mkono wake wa kulia na kumshika John maeneo ya usoni kuanzia mashavuni mwake. Uzalendo ukaanza kumpotea kabisa Janet, Akasahau yale yote aliokuwa akimlaani mumewe njiani na sasa akawa kama kuna kitu kimepungua katika mwili wake. Janet alijihisi kuchanganyikiwa ghafla, machozi ya hasira sasa yakaanza kupenya ndani ya uso wake huku akijihisi kama amepigwa ganzi.
“..Mume wangu nini kimekusibu..??, Kwanini lakini ..?? Na kwanini hukunipigia simu wewe wakati unatoka kazini..??? Kwanini..??? Ona sasa ulivyokuwa..??”
 
24.
Maneno ya taratibu naya majonzi yakaanza kumtoka Janet huku akimsema mumewe John aliyekuwa bado katika usingizi, alilalamika sana kiasi cha kila mmoja aliyekuja pale kumshangaa. Muda wote huo John alikuwa bado hajahamka.
“..Amka basi Mume wangu unijibu maswali yangu..? Amka John wangu..??, Nakupenda sana Mume wangu..!!, Amkaa japo ule.., Amka John.., Mimi ni wako milele kama tulivyoahidi kanisani wakati tunafunga ndoa.., Amka nikulishe Mume wangu..??”
Taratibu John akaanza kufungua jicho lake moja na baadaye likafuatia jngine na sasa akawa anaangaza huku na kule nakushangaa watu waliokuja kumuona..
“..Mke wangu yuko wapi..? Angel wangu yupo wapi nimesema..??”
John alishtuka nakuanza kumtaja Angel hali iliowafanya kila mmoja wa marafiki zake kumshangaa hadi mkewe wakajua atakuwa amechanganyikiwa na kukosea kwa kumtaja Angel badala ya mkewe Janet. Akili ya Janet sasa ikawa ni kuhakikisha mumewe anajua kuwa yupo pale nakuwa amrekebishe mumewe asimtaje Angel amtaje Janet.
“..Mume wangu..??, nimekuja ni mimi Mkeo Janet.., amka ule..??”
“..Hapana najua wewe ni Janet lakini namtaka Angel wangu sasa hivi..”
“..Angel ndio nani..??, kwanza Angel hayupo hapa yupo kwao hukoo..!!”
Janet alijikaza bila ya kujua angel anayezungumziwa na John hivyo akaona kama amemdanganya atatulia tu.
“..Jamani sitaki mivyakula yenu namtaka Angel nimesema..??, Kwanza Alice nayeye amepona..?? yupo wapi..??”.
Hasira kali zilizoambatana na wivu ndani yake zikaanza kujijenga kichwani mwa Janet, Ule uvumilivu aliokuwa ameuonesha toka mwanzo ukawa sasa umeisha. Aliona dunia chungu kwa muda, Hakuamini kama Mumewe John yupo siriazi kwa kutaja hao wanawake asiyewajua hata kwa sura. Alifikiria mengi sana mpaka akajiona hana thamani hata kwa mwanaume yeyote, aliamini kila rafiki yake aliyekuja kumtembelea atakuwa anajua matatizo yake ya kutokuzaa hivyo hata hao anaowataja John watakuwa wanamjua ila wanamficha tu. Sasa akaamua kujishusha kama mwanamke aliyefundishwa na wazazi nakuanza kumbembeleza John ale kwa mara nyingine.
“..Mume wangu John..!!, kula basi halafu ndio uongee hayo mambo mengine..!!”
“..Hivi hamnisikii heee.., wewe nimesema sikutaki tena maishani mwangu, na ni mmoja tu aliokuwa amebeba mimba yangu na nilimpenda sana, Angel..!! Yes! Angel..!! nipelekeni nikamuone..”
John hasira zilimpanda zaidi akachukuwa bakuli ambalo tayari Janet alikuwa amemimina zile ndizi na kumwaga chini, Kisha akajitoa ile dripu aliokuwa amefungwa nakuinuka.
“..Haya namtaka Angel wangu sasa hivi..??, Na pia nataka nimuone Alice..??”
 
25.
*********
Ule uvumilivu ambao ulikuwa ukioneshwa na marafiki zake na John na hata wafanyakazi wenzake sasa ukawa umefika ukingoni. Walijitahidi sana kumvumilia nakumuona kama mgonjwa, sasa ikawabidi waingilie kati ugomvi ule aliokuwa ameuanzisha John mule wodini.
“..Hivi John rafiki yetu..?? Uko sahihi kweli kwa unachokinena mbele ya mkeo.. hivi unajua thamani yake wewe..? Si mkeo wa ndoa huyu..”
“..Hata kama mke wa ndoa jamani lakini siwezi nikaponeshwa hiki kidonda ambacho kimenitokea cha kuondokewa na Angel..??”
“..Angel..? Angel ndio nani..??, Maana sisi kama wafanyakazi wenzako tunamtambua Janet kama mkeo na hata kwenye nyaraka zote za kwako za ofisini zinamtambua mkeo kama mrithi wa vitu vyako japokuwa bado huna mtoto..”
Akili ya john sasa ikawa kama imeaza kuelewa kitu gani anachosemeshwa, Japo alinyanyuka alijikuta mwenyewe akirudi tena mpaka chini kukaa kitandani huku akichukuwa mkono wake na kumshika mkewe Janet. Alimuangalia mkewe kwa jicho la aibu na kukaa kimya kwa muda kisha.
“..Nakupenda sana Mke wangu..!!”
“..Nakupenda pia Mume wangu..!!”
Mwili wa Janet ulijihisi kusisimka, Alimwangalia rafiki yake Mary waliokuja naye kwa tabasamu. Aliifananisha siku hii kama ile siku yake ya ndoa walipokuwa wakifungishwa kanisani na mchungaji. Kitendo cha kuchukuwa chombo kingine na kumuwekea tena uji mumewe alifananisha na tukio la kuchukuwa pete na kumvalisha John. Moyo wa Janet haukuwa tayari kuvunjika haswa kwa mtu ambaye hata hamfahamu. Jina la Angel sasa likawa limemfutika John ghafla. Alijihisi kuwa na ganzi ya muda, kila akinyosha shingo yake kuwaona wageni waliomtembelea ndipo na akili yake ikawa inafanya kazi vizuri.
“..Haya kunywa basi Mume wangu,,”
“..Sawa nipe taratibu tu..”
John alikubali kupokea vijiko vya uji kutoka kwa mkewe Janet nakunywa. Hakuwa mbishi tena kama alivyokuwa hapo awali. Kila mmoja aliyekuja hapo kumtembelea alikuwa na sura ya tabasamu kuona John akiwa katika hali ya furaha na amani kwa mkewe. Alipomaliza kunywa uji tu, Bosi wake aliyekuwepo pembeni akamkabidhi bahasha ya kaki iliyokuwa na kiasi kidogo cha pesa ndani yake kisha akamuaga. Muda wote Mary jirani yake na Janet alikuwa pembeni akimsubiria Janet waondoke lakini haikuwezekana kuongozana naye tena.
 
26.
“..Janet..??, wacha na mimi niwahi nyumbani kupika si unajua sijaandaa chochote na watoto niliwaacha wameenda shule..”
“..Haya mimi acha niwe karibu na mgonjwa wangu, tutaonana huko huko nyumbani shosti..”
“..Haya baadaye, shemeji..??”
“..Naam..!!”
“..Ugua pole shemeji wangu nitakuja kukuona jioni au kesho asubuhi sana..!!”
“..Ok ahsante kwa kuja..!!”
Watu karibu wote walikuwa wameshaondoka, na sasa John alibaki kitandani na mkewe pembeni huku akimfariji. John alijihisi ni dhambi nyingi sana anazo kwa kumtendea mke wake katika kipindi cha nyuma. Wazo la kumng’ang’ania Angel na kumtaja ovyo akaliyeyusha ghafla. Ni kama aliendewa kwa mganga kwa muda maana alivyomsahau ghafla hata hakutaka kuamini. Alijipa moyo na kuhaidi kuendelea kuwa na mkewe milele.
“..Sasa Alice atahudumiwa na nani..?? Nndio inabidi niachane na Angel kwanza ameshafariki lakini nitakuwa na dhambi endapo nitamtelekeza na Alice.. Hapana hapa haiwezekani..??”
John alijikuta akiusemea moyo huku akimfikiria sana Alice. Alikuwa katika dimbwi kubwa la mawazo, Alishinda kabisa jinsi ya kumuanza mkewe juu ya Alice kwani ni lazima angemtaja Angel ambaye walizua ugomvi muda mfupi uliopita. Alijitahidi kujikaza na kuvumilia mpaka muda ambao Daktari alikuwa akiwapitia na kuwajulia hali ndipo John akanyanyua kinywa chake na kuuliza.
“..Samahani Dokta..??”
“..Bila samahani mgonjwa uliza..??”
“..Jana nilikuwa naamuulizia yule mgonjwa wa kike niliyekuja naye usiku wa jana..”
“..Annhaa..??, ndio wewe kumbe..?”
“..Ndio mimi Dokta..!!”
“..Yule binti kajitahidi kutuelekeza lakini tumeshindwa kukufahamu vizuri kama ni wewe ndio uliokuwa na yule. Kwa maana mlipokelewa na manesi wa zamu wengine ambao kwa sasa hawajafika mpaka usiku ndio zamu yao ikabidi tusubiri wakija hiyo usiku ndipo waweze kukutambua.. Aisee umefanya jambo la busara sana.. sasa..”
“..Ndio Dokta..”
“..Kwa sababu yule binti hakuwa na tatizo sana zaidi ya kuishiwa pumzi hivyo mpaka kufikia alfajiri hali yake ilikuwa safi na alikuwa akipumua vizuri tu na kwa sasa tumemuacha apumzike tu huku akisubuiri ndugu zake waje kumchukuwa..”
“..Ndugu zake ndio sisi Dokta..?””
John alijibu kwa haraka haraka hali iliyomfanya Janet kutokuelewa kitu na kuona kama John ameanza tena kuchanganyikiwa kama hapo awali alivyokuwa akifanya. Kitendo cha kusema ni ndugu yao wakati hata kwa sura Janet hamfahamu huyo binti anayezungumziwa ilikuwa ni fumbo kubwa sana kwa Janet.
 
27.
“..Ngoja nikamchukuwe nakumleta sasa hivi..!!, wala msiwe na shaka..”
Yale maneno ya Dokta yalimfanya Janet amuangalie mumewe John kwa jicho la ukali na hasira ya hali ya juu, Japokuwa walibaki wawili tu pale kitandani lakini tayara Wivu ulikuwa umekizunguka kichwa na mwili wake kwa ujumla, Janet alikuwa na wivu sana katika suala zima la mapenzi. Alijua ni wazi watakuwa ni visichana vyake ambavyo John hutembea navyo pindi amelewa hivyo mara ya mwisho watakuwa walikuwa wote wakinywa na mpaka wakapata ajali. Hakutaka kuropoka wala kufanya ugomvi lakini duku duku ambalo lilimkaa moyoni alikuwa akitaka kulitoa..
“..John Mume wangu..??”
“..Eenhee niambie mpenzi..”
“..Samahani lakini Mume wangu kma nitakuwa nimekukosea..”
“..Bila samahani niambie tu Mke wangu..”
“..Eti..??, huyo Binti aliyeenda kuletwa na Daktari ni nani kwako..??”
Janet alionesha kujiamini kwa kumuuliza John huku akimtolea macho kwa msisitizo akitaka ajibiwe juu ya huyo Binti. Kwa kujiamanini John alimuelezea vyote kuhusiana na mchezo mzima aliokuwa akiufanya juu ya Angel mpaka alipokuja kujuana na Alice ambaye ndiye mdogo wake na marehemu Angel. Janet alisikitika sana kwa mimba ambayo alikufa nayo Angel. Aliona mumewe anamakosa sana lakini akaapa kutoka moyoni mwake kuwa amemsamehe na kuahidiana kamwe haitakuja kutokea tena kitendo kama hicho cha aibu. Sasa Janet ana John wakarudi kama zamani kama Mke na Mume waliokamilika na kwa muda huu walikuwa pamoja huku John ameegemea katika kitanda cha wagonjwa wakimsubiria Alice ambaye alienda kuchukuliwa na Daktari. Muda wa dakika takribani kumi zilimtosha Dokta kwenda na kurudi na Alice, hakuwa amevaa mavazi yake ya jana yake usiku sababu yalilowa sana na damu hivyo alikuwa amevalishwa mavazi spesho ya hospitali na sasa alkuwa ameshikwa mkono na Dokta huku wakikaribia eneo ambalo alikuwepo John na mkewe.
“..Alice.. hujambo..? ”
“..Sijambo kaka shikamoo..!! , Shikamoo Dada..”
“..Marhaba!!, Vipi unajisikiaje..”
“..Hapana sina tatizo tena kaka.., najisikia vizuri tu..”
Alice alijibu kwa uoga huku akimtolea macho Mke wake John bila ya kumfahamu kama ni mke wa John au la!. John Alimpokea vizuri Alice na kisha Dokta yule akaondoka hivyo wakabaki watatu. Kikao kifupi ambacho John alikitengeneza cha yeye Mkewe na Alice kilikuwa jibu tosha kwa Janet kumfahamu Alice. Alimsikitikia sana na kuahidi watakuwa pamoja katika kumsaidia Alice. Japo Alice alikuwa bado katika majonzi ya kuondokewa dada yake lakini Alice alijiona tena mwenye bahati ya mtende baada ya Janet na John kuafikiana kumsaidia Alice kwa hali na mali mpaka mwisho wa maisha yake.

******
 
28.

Muda wa mwezi ukawa umekatika kwa Alice kumsahau Dada yake Angel. Kwakuwa Angel hakuwa na ndugu yeyote hapa Dar na wala hakukuwa na mtu aliyepafahamu nyumbani kwao Kigoma hivyo ikabidi azikwe chini ya Manispaa na zoezi hilo lilifanyika kwa haraka nakuhuduriwa na Alice, Janet na John tu. Alice alijitahidi kusahau lakini ilikuwa ni vigumu kidogo. Mali zote ambazo Angel alikuwa nazo zikawa chini ya Alice. Ni John pekee ndio alitoa wazo la kuziondoa mali zote nakuzihamishia kwake na pia kuishi na Alice kwakuwa alikuwa ndio kwanza ana miaka kumi na nane na hakuweza kujitegemea mpaka angekuwa na mtu au anafanyakazi. Wazo hilo lilipokelewa na Alice bila kizuizi chochote na sasa akawa chini ya familia ya John na mkewe Janet. Furaha yake ya maisha ikarudi pale pale kwa kuwa janet hakuwa na uwezo wa kuzaa hivyo alimchukulia Alice kama mtoto wake wa kumzaaa. Elimu yake ya darasa la saba aliyosomesha na Baba yake miaka ya nyuma haikukidhi kabisa kuelewana na mtu yeyote msomi. Hivyo John alikuwa bega kwa bega katika kumsaidia Alice na kitu alichokifanya ni kumpeleka kozi ya kiingereza kisha akampeleka kujifunza kompyuta. Sasa Alice akawa siyo Alice yule wa zamani. Uzuri wake ukaongezeka maradufu. Aliijiheshimu sana mbele ya John na Janet kwakuwa aliwachukulia kama wazazi wake wa kumzaa. Kazi aliyokuwa akiifanya John ya kusimamia walimbwende wa Tanzania sasa ikawa imehamia kwa Alice. John alitaka Alice ashiriki mashindano hayo.
“..Alice mwanagu..??, nahitaji ushiriki katika Miss Tanzania mwaka huu..??”
“..Kweli Dady..??”.
“..Ndio kwani nakuona kwa sasa unafaa na unaweza kushinda na ukafika mbali sana tu..”
“ ..I love you Dady wangu..!!”
“..Hivi ukiwa kama mrembo anayeiwakilisha Tanzania mwanangu vitu gani utavifanya..??”
“..Kwanza kabisa kama shughuli ambazo huwa zinateuliwa za kusaidia jamii, nitahakikisha nimeisaidia jamii yangu kwa asilimia kubwa tu na malengo yangu haswa ni kusaidia wanawake wasiojiweza hapa namaanisha vikongwe. Ujue nini Baba..? Serikali yetu inawasahau sana hawa watu sasa mimi nitakuwa bega kwa bega kuhakikisha wanapata huduma zinazostahili..”
John alibaki akitikisa kichwa akishangaa kwa maneno ambayo Alice akiongea, hakuamini kama Alice huyu anayemjua ndio anaongea ama ameambiwa na mtu mwingine. Ilimbidi amtege tena.
“..Eenhee mwanangu na kitu gani kingine utakifanya ukiwa kama mrembo anayewakilisha hapa Tanzania..??’
 
29.
“..Natamani sana kuwasaidia vijana wenzangu ambao wamepoteza mwelekeo wa kimaisha, hapa naamaanisha kwa wakiume na wakike. Kuna Dada ambao wameshakata tamaa ya kuishi na hata wengine wameishia kujiuza miili yao na wengine kuhamia kwenye madawa ya kulevya. Ujue Baba sisi wanawake ndio tunaonewa na kunyanyaswa sana haswa tunapoingia katika suala zima la ndoa, Wanawake tumekuwa hatuthaminiwi nakupewa haki zetu za msingi hivyo basi nikiwa kama mrembo atakayeiwakilisha Tanzania nitahakikisha nakuwa sambamba na taasisi ambazo zinajishughulisha na masuala haya ya kusaidia wanawake ili kuweza kutokomeza tatizo zima la kunyanyaswa. Na kuhusu wanaume napo vijana wenzangu wengi sana wamepotea haswa kwa kufuata mikumbo wanajikuta mwisho wa siku wana ingia katika biashara za kuuza madawa na hata wengine kuyatumia na mwishowe kuwa mateja na hata kupoteza nguvu ya taifa..”
John sasa akawa ameshusha pumzi zake kwa maneno ya ushawishi ambayo alikuwa akiyatoa Alice. Hakutaka kuamini hata kidogo kama aliyekuwa akizungumza naye ni Alice kweli ama mwingine lakini ikabidi aamini ukweli aliokuwa akiushuhudia mbele ya macho yake.
“..Sasa mwanangu si unajua mashindano haya huwa yanaanzia ngazi za mikoa lakini kwa hapa Dar yamegawanyka kwa wilaya hivyo kuna mkuu mwenzangu anasimamia kanda ya chang’ombe na wewe ndipo utakapoenda kugombea huko, haina wasiwasi kuhusu ushindi kila kitu tutaweka sawa cha msingi onesha kujiamini tu mwanangu..”

..sawa Baba nakuhaidi sintokuangusha, Wewe mwenyewe utajionea, naweza Dady niamini kwa hilo, naweza na tena napenda sana..”
John alionesha tabasamu kwa kukubaliana na Alice. Kuanzia sura umbo na hata muondoko ulimthibitishia kuwa Alice anafaa kujiunga na mashindano hayo. Siku nzima ikawa ni furaha sana kwa Alice, alijihisi ndoto zake za miaka ya nyuma juu ya maisha yake sasa zinaenda kufanikiwa. Alijihakikishia Tanzania nzima na dunia kwa ujumla iweze kumtambua mchango wake na kumjua yeye ni nani katika jamii. Hata Janet mke wa John alihafiki kitendo cha Alice kujiingiza rasmi katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania. Baraka zote alizopewa Alice zilizidi kumuweka katika hali tofauti. Alifanya kazi zote kwa bidii, hakutaka kamwe amuuzi Janet wala John katika maisha yake kwani ndio walikuwa walezi wake kwa sasa.
 
30.
*****

Hoteli ya Rozalimo iliyopo Bagamoyo mjini ndio sehemu ambayo kuliwekwa kambi warembo waliokuwa wanachuana kanda ya Chang’ombe. Takribani washiriki ishirini na mbili walikuwa wakijichua haswa kwa mazoezi mbali mbali na hata muda mwingine walikuwa wakitoka kambini na kutembelea taasisi mbali mbali zinazosaidia jamii. Pia walipata fursa ya kuona baadhi ya makampuni ya kutengeneza vinywaji kama vile kampuni ya Bakhresa. Kila mmoja alionekana kuwa karibu na mwalimu ambaye alikuwa akiwafundisha mbinu mbalimbali jinsi ya kuwa mshindi. Maswali na majibu mbali mbali ambayo yalikuwa yakitolewa na baadhi ya washiriki kwenda kwa mwalimu wao yalikuwa yakijibiwa kiufasaha. Warembo wote walikuwa ni wazuri na wenye sifa za kukubalika kuliwakilisha Taifa hili la Tanzania. Miongoni mwa warembo hao alikuwepo Alice Majaliwa akifuatilia kila pointi aliokuwa akiitoa mwalimu wao huyo. Alice alikuwa mdadisi sana na mwenye kutaka kujua mengi na hali hiyo ilimfanya hata baadhi ya warembo wenzake kumchukia na kumuona kwamba anaringa sana.
“..Sasa mwalimu kwa mfano ukitaka kutoa misaada unafanyaje sasa mpaka unakutana na vyombo vya habari ili wajue kuwa unawakilisha kitu..??”
“..Safi sana Alice..!! Ni kwamba ukiwa kama mrembo unaowakilisha nchi, Ni dhahiri kwamba vyombo vya habari vinakuwa karibu yako. Hapa namaanisha kuwa utakuwa na ofisi yako ambayo itakuwa inaratibu shughuli zako zote ikiwa ni pamoja na safari zako na hata misaada utakayokuwa unapeleka..”
“..Na je mwalimu..? kuhusiana na skendo ambazo huwa zinatolewa na magazeti ya udaku, hiyo unakabiliana nalo vipi kama mtu anakuwa mrembo wa kuliwakilisha Taifa..??”
“..Ukiwa kama mrembo unayewakilisha Taifa lako kwanza kabisa unatakiwa usiwe mtu wa kuruka ruka na wanaume na hata kuolewa mpaka kipindi chako kiishe, pili ni lazima upewe ulinzi. Hapa namaanisha kuwa utakuwa na mawakili wako au wakili wako ambaye atakuwa bega kwa bega na wewe katika kuhakikisha hayo mambo hayatokei na hata wakati mwingine sisi kama waratibu wa mashindanno hayo huwa tunahusika kuingilia kati tunapoona mrembo amechafuliwa jina..”
 
31.
Alice alionekana kuridhika kwa maswali, na sasa akawa anatamani sana siku yenyewe ifike ili awadhihirishie watanzania kwamba anaweza kufanya yale yanayotakiwa hata kuikwakilisha nchi. Alice alikuwa hajui kuogelea lakini alijua huko huko kambini. Viatu virefu wala nguo fupi hakujua kuvivaa lakini kutokana na mashindano yalivyo na huko kambini ilibidi kujua kuvaa hivyo ili aendane na mazingira. Michezo mbali mabali ya ufukweni ilimfanya ajione mtu tofauti sana hapa duniani. Akili yake yote ilikuwa siku ya kutangazwa mshindi wa Miss Chang’ombe na Tanzania kwa ujumla. Mazoezi yake binafsi ambayo alikuwa akijifanyia baada ya kufundishwa na mwalimu yaliufanya mwili wake kuwa mwepesi na hata kuwa na pumzi ya kutosha. Alijitahidi sana kuwa anaongea mbele ya wenzake ii kumuondolea woga siku ikifika kama atahojiwa mbele ya umati. Mawasiliano na wazazi wake wakufikia yaani John na Janet yalikuwa karibu na mara zote John alikuwa akimpa moyo na kumuhaidi mengi mbeleni na kumuhakikishia kwa asilimia zote kuwa ni lazima atashinda ila kinachotakiwa kwake ni ushiriki na wenzake ili isije kuonekana kuwa wamepanga matokeo.Wiki mbili zilitosha kabisa kwa warembo wanaowakilisha Chang’mbe kuweka kambi katika hotel ya Rozalimo huko Bagamoyo.

Basi ambalo liliwachukuwa mara ya kwanza sasa likawa limekuja kuwachukuwa moja kwa moja na kuwapeleka katika ukumbe wa TCC chang’ombe ambapo mashindano hayo yalifanyika. Kila mmoja alikuwa na hofu ya kushinda, kwa upande wa Alice naye alikuwa na hofu lakini kwa mavazi ambayo yalibuniwa na Abduel Urassa alijiona hamna mtu wa kuweza kumfikia. Muziki mkubwa uliokuwa unatokea ndani ya ukumbi ulitetemesha sana mioyo ya warembo wakijihisi sasa wanaelekea kifungoni ama kushinda ama kubaki uraiani. Ni wawakilishi wawili tu ambao watatakiwa kutoka katika kanda hii ya Chang’ombe kwenda kuwakilisha mashindano makubwa tena ya Miss Tanzania. Waliposhuka tu pale ukumbini warembo wote walienda nyuma ya jukwaa kuu na baada ya hapo wakavalishwa tisheti za wadhamini wa mashindano na kuelekea jukwaani kujitambulisha. Walipofika jukwaani kwanza warembo wote walicheza kwaito na kisha wakarudi nyuma ya jukwaa tayari kujiandaa mmoja mmoja kuanza kuonesha mavazi yake. Alice alijihisi woga umeanza kumpata, Mwili wake ulikuwa kama umemwagiwa maji ya baridi ghafla huku midomo yake ikimtetemeka, Alijihisi kama amerogwa ghafla kwani kichwa kilianza kumzidia, haraka haraka alimwomba mwalimu wake aelekee chooni mara moja kujisaidia.
 
Back
Top Bottom