Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

Huyu aliwekwa..sasa sijui Pombe ana mbavu ngumu vipi kumzuia mamvi 'asirudi' tena mitaa ya TANROADS..
 
I don't understand this; kwani Kawambwa alishindwa na kitu gani au Magufuli kaja na nguvu gani nje ya zile ambazo Kawambwa alikuwa nazo; this just make Kawambwa aonekane vibaya. Haiwezekeni watu wamsubiri Magufuli. Msije kuniambia kuwa hata ATCL sasa imepata kiongozi?

Mwanakijij pale akukuwa na waziri ndugu yangu kulikuwa na waziri kivuli...Unajua Bomu Bomu kweli kweli
 
Sio swala la kupumbaza watu kusherehekea hilo!! maana wote wezi hao, wanajipanga nyie mnashangilia nini? Magufuli silolote si Chochote hajarudisha nyumba alizouza anatoa beki anaweka beki nyie mnashangilia kuweni makini Jamani maana hata huyo Mrema yawezekana katolewa kwasababu Mchaga

Mkuu Arafat, this is one of the stupidiest comments so far katika mada hii.
Kama hujui backgroud ya discontent juu ya utendaji wa Mrema na ufisadi wake ni bora kukaa kimya wenye akili waongee.
 
Magufuli na Mwakyembe walisema hawakwenda pale kuitengua torati bali kuitimiza.................Mkataba wa Mrema uliisha..........na sasa wakuu hao wametimiza torati kwa kumpa mkono wa asante na kwa heri kwa service yake...............and sorry we do not want your service anymore..........Ndugu Mfugale atakaimu nafasi.............
 
Kuna haja ya kwenda taratibu kidogo. Kuna wenzetu hapa wametia fikra nzito. Kushangilia tu kuondoka kwa Mrema ni kutaka kuona majawabu rahisi yanapatikana kwa matatizo makubwa sana. Hiyo inayoitwa "jeuri" ya Mrema haikuwepo hivihivi tu. Aidha, kwa baadhi yetu tuliowahi kufanya kazi katika wizara hiyo tunajua kwamba serikali (ikulu) na chama vimekuwa vikiitumia sana kwa ulaji mkubwa. Imekuwa conduit ya uvujaji wa mabilioni ya fedha za serikali miaka nenda miaka rudi. Pamoja na "juhudi" zake zote, mtu mmoja kama Magufuli hana miujiza ya kurekebisha mambo labda kama kuna mkakati kamili wa kuleta mapinduzi ya uhakika huko ujenzi. Vinginevyo itabakia kuwa mwendelezo wa "kuinuana mioyo" kwa msimu.
 
Hii serikali sidhani kama imeamua kumtosa huyu jamaa ila nadhani wanajisafisha kijanja ili watu waone na warudishe imani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ina maana siku zote raisi, waziri mkuu na wakuu wa sekta ya mabarabara walkua hawalioni hili????????????????? Barabara ya arusha namanga imejengwa kwa mwaka wa tatu sasa..................... Wizi mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hii danganya toto wakawafanyie wajukuu zao

hatudanganyiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mrema ang'olewa TANROADS


na Mwandishi wetu




HATIMAYE Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Ephraim Mrema, ameong'olewa rasmi katika nafasi hiyo na kukabidhi ofisi hiyo jana kwa Kaimu Mtendaji aliyeteuliwa, Injinia Patrick Mfugale.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri mpya wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alimtaka Mrema afanye kazi huku akiamini haondoki katika wadhifa huo na aweke matumaini ya kuishi kwa miaka 100.

Kwa kirefu Mrema amekuwa akiandamwa na tuhuma mbalimbali za kifisadi katika wakala huo, ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuvunja mikataba na makandarasi bila kufuata taratibu.

Hata hivyo, taarifa za kuaminika ambazo Tanzania Daima inazo kutoka TANROADS, zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya viongozi wakuu wa wizara hiyo kukutana na kujadili juu ya suala la Mrema na kufikia hatua ya kumuengua.

"Huu uamuzi umefikiwa leo na viongozi wetu wakuu, kwa kweli tumefurahishwa sana maana ukiangalia kwa kipindi chote alichokaa katika uongozi wake Wakala huu umepoteza sifa, huku akivunja mikataba kila mara ya makandarasi bila kufuata utaratibu," alisema mtoa taarifa wetu.

Alisema kuwa Mrema hajafurahishwa na uamuzi huo ambapo inadaiwa iwapo serikali itaamua kumchukulia hatua atakuwa tayari kuwataja vigogo wote waliokuwa wakiomba fedha ndani ya wakala huo.

Wakati huo huo, taarifa hizo zilifafanua kuwa kwa sasa ameandika barua akieleza kuwa amepata nafasi ya masomo nchini Uingereza kwa ajili ya shahada ya uzamivu ya ‘Civil Engineering'.

Uamuzi huo wa Mrema kuelekea nje ya nchi umeelezwa kuwa ni wa kutaka kukwepa ushahidi, kwa kile kilichoelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kuwa inaweza kumchunguza kwa tuhuma za kuisababishia hasara serikali.

Source: Tanzania Daima

Mtazamo:

Hapo kwenye nyekundu ndio tutakuja kugundua madudu mengi ya ajabu ya dizaini kama yale ya EPA
 
Muda wa mkataba wake ulishaisha,
Alitaka kuongezewa muda kinyemela na jk ndo maana wabunge last time wakapiga kelele sana nafasi itangazwe upya.
wabunge wakapiga kelele last time, last time ni lini? alitaka kuongezewa muda au alishaongezewa? Na kama muda wa mkataba wake ulishaisha mbona bado alikuwepo? Uliisha lini, jana?

"alitaka kuongezewa muda kinyemela na jk" mbona huyo huyo JK ndio amekubali ushauri wa magufuli kwamba ang'olewe, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti hapo juu?

Jakaya Kikwete alivyo, kwa wanaomfahamu kikazi, ni mtu ambae hawezi kumwondoa favorite wake mahala eti kwa vile some waziri Magufuli hampendi, Rais wetu hayuko hivyo, ni mtawala mmoja king'ang'anizi na mnazi (anachokipenda yeye ndo hicho atakachokifia) ile mbaya.

Tuseme Mrema kamaliza muda wake kimkataba, period
 
Well done mr. beer for padlocking fisadi mrema. Now please 'chungulia kule nyanda za juu kusini' and see what is going on at songwe airport project.
 
Soma Mwanachi upate taarifa kamili.Usicheze na Pombe
Kama ni kweli basi JF ni kiboko!! Maana watu wa Tanroads wenyewe hata habari bado hawajazipata. Kwa vile mleta hoja amesema ni tetesi then ibaki kuwa hivyo mpaka itakapodhibitishwa.
 
Ni uamuzi uliocheleweshwa. Kazi yenyewe alipewa kirafiki. Ameiharibu kabisa Tanroads kwa migogoro ya kujitakia na isiyokwisha mpaka ufanisi wa kazi ukawa umeenda chini kabisa. Huyu bwana lazima aliwekwa na wau wenye nguvu sana ila kama ilivyo kawaida....binadamu wote tunafanana kwa kuwa kila kitu kina muda chini ya jua.
 
Swala si ukabila et ni Mchagaa kama wengi wanavyotaka kusema hapana, lakini tukumbuke kuwa tangu anaondoka Dr Magufuli pale Ujenzi kuna matatizo sana sasa lets think deeper kwani pesa alizopewa Mramba na Kawambwa ni zaidi ya mara 3 au 4 ya zile alizopewa Magufuli alipokuwa Minister (ondoa inflation etc) lakini hawa 2 wamefanya kazi ndogo sana kuliko aliyofanya Pombe wakati huo. Unajua penye ukweli tuseme ukweli angekuwepo Pombe mapaka sasa barabara za lami zingekuwa zinaunga mikoa yote sasa. Wenzetu Kenya hapa jirani tu pamoja na tug of wars zao sasa wanaunga bara zao wilaya kwa wilaya!!
 
bora katoka jamaa alikuwa mla rushwa, baadhi ya jamaa wa tanroads wanasema waziri kawambwa na katibu mkuu eng. chambo walikuwa wanapelekewa 'cut' kubwa na mrema mpaka wakaziba masikio yako na kuvaa miwani ya mbao kwa chochote kinachomhusu mrema
 
Kama wadau wachache wanavyodokeza mara nyingi, watu wengi wana-comment au ku-conclude hizi issues bila kuwa na ufahamu au kufanya utafiti wowote.

Katika hili suala la Chief Executive wa TANROADS ilitabiriwa kabla kuwa pindi mzawa atakapokalia nafasi hiyo ndipo vita itakapoanza. Hii inatokana na kwamba sisi wengi pamoja na viongozi huwa tunaangalia maslahi aidha binafsi au ya groups zetu kuliko interests na benefits kwa general public.

Wakati wa CE wa kwanza ambaye alikuwa Mnorway (kutokana ya kwamba NORAD na World Bank wamekuwa wakigharimia hizi structural changes na kuanzisha executive agencies kama TANROADS), alipigwa vita especially na Waziri wa Ujenzi wakati huo Magufuli. Mara tulisikia chokochoko za kulipwa mishahara mikubwa, matumizi ya magari na petty issues nyingine. Kwa mtazamo wangu tatizo pale lilikuwa ni kupungua kwa influence ya wizara katika eundeshaji kutokana kwamba TANROADS wana budget kubwa (kwa mfano miaka ya hivi karibuni ni zaidi ya 1 trillion Tshs).

Lengo la wafadhili na international financing institutions ambao wanachangia sehemu kubwa ya budget, ni kwa TANROADS kuwa autonomous, yaani iwe taasisi inayojiendesha bila bila kuingiliwa sana na serikali na wanasiasa ambayo ni muhimu kwa ufanisi. CEO wa huyo mzungu alikuwa hapendi kuingiliwa katika utendaji wake hivyo mkataba wake ulipoisha hukutaka kundelea kufanya kazi na waswahili. Akaingia CEO wa pili aliyetoka Ghana ambaye alipasha kiti moto bila kufanya chochote serious kwa kipindi cha mkataba wake wa miaka 3. Alkuwa alikuwa mjanja anayejua namna ya kukaa na waswahili na kula kiulaini. Nasikia aliambiwa afanye mabadiliko serious pale TANROADS lakini alikataa akisema yafanywe baada ya yeye kuondoka.

Mchakato wa kumpata CEO wa tatu nasikia ulikuwa ni mgumu kwasababu ya group interests. Mrema siyo engineer lakini amesomea building economics na construction management. TANROADS ni procurement agency hivyo inahitaji watu wenye uzoefu katika project management. Huyu bwana amesoma na kufanya kazi katika construction industry huko UK kwa zaidi ya miaka 15 akarudi nyumbani na kuendelea kufanya kwenye construction industry muda wote. Hivyo waliokuwa wakimbeza kuwa hana elimu walikuwa wanajua ni vijembe tu. Alikuwa ni outsider kabisa katika ile system ya wizara ya ujenzi na alipelekwa pale kwa ajili ya kufanya mabadiliko ambayo Dr. Ado Abedi alichelea kuyafanya. Alikuwa very bold alipoingia pale na kuwaondoa vigogo waliotakiwa kuondolewa bila kungoja. Kilichofuata baadae baada ya miaka 3 ambayo amekaa pale na vita iliyokuwa inaendelea ni historia sasa.

Huyu bwana amejaribu kuendesha TANROADS kama taasisi ambayo inajitegemea zaidi lakini resistance imekuwa kubwa na imemshinda.Watu especially media ambao hawelewi habari za mikataba wamejaribu kuonyesha CE amefanya kosa kuvunja mikataba ya wakandarasi ambao wameshindwa ku-peform lakini nadhani alitakiwa kusifiwa kama CE mzalendo ambae amethubutu kuadabisha makampuni ya kigeni na mengine yakiwa ya kimafia kabisa yasiyojali ustawi wa taifa letu. Nasikia baadhi ya kesi (arbitration) serikali imeshindwa kutokana na collaborations zinazotokana na personal interests.

Nadhani watu wangeangalia haya mabadiliko pale TANROADS kwa tahadhari kubwa kutokana na unyeti na majukumu ya taasisi hii. Mnajua, barabara ni politics na pia fedha zinazoenda pale ni nyingi hivyo lazima politicians wapende kuwa na influence na control.
 
Back
Top Bottom