Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

It's good jamaa kuondoshwa maana alikuwa na inferiority complex kiasi kwamba ikabidi awe autocratic leader kwa kutopenda challenges. Um really glad to hear this.
 
Suala la Mrema kama linavyoreportiwa ni suala kubwa sana na halipaswi kuchukuliwa kiushabiki wa kumshabikia Magufuli tuu kama inavyoonekana hapa. Nimesoma tuhuma za Mrema magazetini hazitofautiani sana na zile za mafisadi papa. Lakini ninavyofahamu mimi issue ya Mrema haitofautiani sana na ile ya Late Gavana wa Benki Kuu Tanzania. Kama magufuli anania ya kweli katika issue ya Mrema na si kuweka watu wake ili aweze kuendelea na mambo tunayoyafahamu basi alipaswa apate maelezo ya Mrema juu ya tuhuma hizo na ikibidi amshitaki na sio kumfukuza kazi tuu. Kinachoendelea TANROADS na Wizara ni struggle of power na sio ufisadi wa Mrema kwani ufisadi wote unatokea Wizarani na sio kwa Mrema yeye ni mtekelezaji tuuu. Natoa rai kwa wale waandishi wa habari za kiutafiti kulifanyia kazi na waujuze Umma wa Kitanzania unaopotoshwa kila kukicha na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.
 
Pombeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, safi bado na ile bara2 ya Nangurukulu Mandawa sio kabisaaaaaaaa, wale wachina walicheza tu pale.
 
Suala la Mrema kama linavyoreportiwa ni suala kubwa sana na halipaswi kuchukuliwa kiushabiki wa kumshabikia Magufuli tuu kama inavyoonekana hapa. Nimesoma tuhuma za Mrema magazetini hazitofautiani sana na zile za mafisadi papa. Lakini ninavyofahamu mimi issue ya Mrema haitofautiani sana na ile ya Late Gavana wa Benki Kuu Tanzania. Kama magufuli anania ya kweli katika issue ya Mrema na si kuweka watu wake ili aweze kuendelea na mambo tunayoyafahamu basi alipaswa apate maelezo ya Mrema juu ya tuhuma hizo na ikibidi amshitaki na sio kumfukuza kazi tuu. Kinachoendelea TANROADS na Wizara ni struggle of power na sio ufisadi wa Mrema kwani ufisadi wote unatokea Wizarani na sio kwa Mrema yeye ni mtekelezaji tuuu. Natoa rai kwa wale waandishi wa habari za kiutafiti kulifanyia kazi na waujuze Umma wa Kitanzania unaopotoshwa kila kukicha na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.

Mkataba wa Mrema kama mkurugenzi mtendaji wa TANROADS umekwisha majuzi kati hapa. Inakuwaje tena afukuzwe kazi?
 
Kama ni kweli basi mambo yamekubali. Safi sana. Magufuli fanya kazi.
 
wapo wwengine kama wawili hivi.....namuomba pombe awatoe
 
Wakuu

Kwawale mliokua mnafuatilia sakata la Mrema kupitia This nad na hata wale mlio ndani mtakubali kwamba his days were numbered... Its not because jamaa hajui kufanya kazi, hapana, ni kwasababu ya mfumo wake mwenyewe aliouweka wa kukubali lobbying na majungu

The guys is very intelligent na kuna mambo ya maana aliyofanya hasa wakati wa mwanzo wa ajira yake... Kwa sasa ameharibu sana na mbinu anazotumia si zenyewe kwani bado analazimishia kuwepo kazini kwa namna yoyote ile... A GOOD STEP FOR TOMORROW

Ila naomba wote tukubali kwamba matatizo ya tanroads hayataisha kwa huyu jamaa kuondoka kwani kwangu kama ndiyo yataongezeka, tanroads itakua kama tanesco, itakua sehemu ya fitna, majungu na siasa kwani serikali ya kikwete imebariki hayo

hata uajiri wa successor naanza kuuogopa

Na pia tuangalie sana mfumo wa sasa wa tanroads na kipato inacholeta kwa taifa... Je Mrema alisaidia seriakli kuongeza pato kwa mfumo wa zile kodi, kama ndio, je are they used rationally? kama no, je turudishe ule mfumo wa mkapa wa kodi ya barabara kujenga barabara na si kuweka kwenye kapu?
 
I don't understand this; kwani Kawambwa alishindwa na kitu gani au Magufuli kaja na nguvu gani nje ya zile ambazo Kawambwa alikuwa nazo; this just make Kawambwa aonekane vibaya. Haiwezekeni watu wamsubiri Magufuli. Msije kuniambia kuwa hata ATCL sasa imepata kiongozi?

Uwepo wa Kawambwa kipindi kile hata ukiniuliza mimi kafanya nini kwenye hiyo Wizara obviously nitakujibu kuwa hakuna jambo la maana alilolifanya sio kwamba alikuwa incompetent la hasha yawezekana kuna baadhi ya mambo alikuwa anawaachia watu wajifanyie wao wenyewe bila yeye kufuatilia, sasa baada ya kuingia Magufuli hapo ndio inakuja kuonekana kipindi ambacho alikuwepo Kawambwa hakuna chochote cha msingi alichofanya
 
Acid

Ni kweli kabisa wana jamvi wanatakiwa kujadili mambo kwa kina na mapana, badala ya kuishia kushabikia Mrema kuondoka. Tusije ishia kufanana na hadithi ya kijiji kimoja chenye hospitali ya misheni. Naambiwa kwamba wakati nchi inakaribia kupata uhuru, watu wa kijiji kile waliambiwa kwamba baada ya uhuru, zile nyumba zote za wamisionari zitakaliwa na wazawa! Hawakuwa na mawazo ya kupata wataalam wazawa wa kurithi taaluma ile ya udaktari, bali Chifu, Balozi, kuingia kwenye nyumba hizo, BASI!

Inawezekana kabisa, matatizo ya TANROADS ni zaidi ya Mrema. Je, miradi yote imekuwa ikipata fedha kwa wakati? Uingiliaji wa Wizara?Serikali kwenye shughuli za TANROADS ni wa kiasi gani? Nini kifanyike ili taasisi hiyo ifanye kazi kwa kujitegemea na kama timu moja?......
 
Sio swala la kupumbaza watu kusherehekea hilo!! maana wote wezi hao, wanajipanga nyie mnashangilia nini? Magufuli silolote si Chochote hajarudisha nyumba alizouza anatoa beki anaweka beki nyie mnashangilia kuweni makini Jamani maana hata huyo Mrema yawezekana katolewa kwasababu Mchaga
 
swala si kutimua tu watu bali tunataka kujua nini hasa tatizo mpaka mtu anatimuliwa maana isije kuwa kuna ka ujanja ka upande wa pili wa shilingi, ninakuondoa kwa kashfa za kwenye magazeti naweka wangu wa kunilinda

Tunataka kusikia watu wamepelekwa mahakamani kujibu ufisadi waliofanya sio tu kutimuliwa hapa kesho unasikia yupo wizara nyingie tena kubwa ya serikali
 
Sijui kama wanajamvi kuna kitu tunajifunza hapa sijasikia hoja ya uonevu au kaondolewa kwasababu ya dini yake ?.Ngoja mtendaji mkuu wa NSSF aguswe utasikia hana kosa anaonewa kwasababu ni .......ebo wakati mwingine tunatakiwa kukua kidogo mtu akikosa asitetewe kwa vigezo vya dini au kabila lake.

Kwakuwa Ephraem Mrema sio wa dini ile, haliwezi kuwa suala la udini. Lakini akiguswa tu wa dini ile hata kama kuna solid evidence, utasikia makelele meeengi, anabaguliwa kwa sababu ya dini yake!
 
Habari njema Mrema kaondolewa lakini siungi mkono siasa za ubabe,kama hakutaka kuonana na Mrema ni kwamba hakumpa nafasi ya kujitetea.Magufuli ni kati ya mawaziri wachache nina waunga mkono lakini inabidi apunguze papara la sivyo ita mbackfire kabla ya 2015.
 
HILI BADO HALIJAHITIMISHWA.....mara ngapi ametimuliwa na ANAJIREJESHA?
 
Sio swala la kupumbaza watu kusherehekea hilo!! maana wote wezi hao, wanajipanga nyie mnashangilia nini? Magufuli silolote si Chochote hajarudisha nyumba alizouza anatoa beki anaweka beki nyie mnashangilia kuweni makini Jamani maana hata huyo Mrema yawezekana katolewa kwasababu Mchaga

Mkuu hapo kwenye RED paangalie sana. Aidha wewe si mfuatiliaji wa mambo kwasababu Mrema ilisemekana alipewe barua ya kukabidhi ofisi miezi mitatu iliyopita kabla ya hata uchaguzi kufanyika. Naogopa hizi hisia za UCHAGA umeziona vipi. Katika yooote yaliyosemwa hata bungeni kuhusu utata wa mkataba wake na tuhuma kibao lakini umeona inawezekana kaonewa kwa uchaga wake! Hii ni hatari.
 
Back
Top Bottom