Mrema TLP na picha ya aibu

Mrema TLP na picha ya aibu

waendelee tu kupiga picha maana hawa ndio wale wakikurupuka kupiga kura wanasema tu ndioooooooooo hata kama hoja ni ya kipuuzi. hawako makini kusikiliza majembe kina Lisu wanavyowatetea walalahoi. hawa wanasubiri tu posho, hawaoni kama mijadala ina maana yoyote kwao ndio maana wanasinzia ( tena wanalala bana hadi udenda unawatoka??? kule kwetu wanaita lutau!!).
 
Duh, Mzee wa Mapipa ya Lami, Mbona Mbabuko bado japo alipiga kikombe?
 
Siku zote nilijua wachaga ni watu wajanja na makini sana lakini kwa hili la kumchagua Mrema wamapiga chini
 
Pamoja na hayo. Ni picha mbaya ambayo itamuandama mjwahuzi (mpiga picha) hadi atajisikia vibaya. Zaidi ya huyo dada aliyetapika. Mujwahuzi ni mwanahabari asiye na maadili ya kazi wala mipaka ya kiutendaji na maamuzi. Hata huyo mhariri wa gazeti naye ana kasoro. Mbona huu ni udhalilishaji? Kuna suala la umri, maradhi, majukumu, pamoja na kukabiliana na tusiyoyajua kesho. Sasa huyu mwandishi hayaoni haya. Familia yake inajisikiaje? Nasema tena, huu ni udhalilishaji na matumizi mabaya ya maamuzi

Wenyewe CCM wanasema huyo mwandishi anatafuta umaarufu yawezekana anataka kugombea 2015
 
Picha inaonyesha hivyo vinavyotoka kwa kuona je vile vingine ambavyo mpaka usikie!!!?kama kuna mwandishi aliweka mic karibu yake atusaidie kuturushia hizo sauti.Uyu ndie mtetezi wa CCM aliyebakia nawala sio mwakilishi wa vunjo.Juzi alikuwa anadai posho anasema ajalipwa atahacha kutetea,nayeye ndio anajua vitu vingi.
 
Angekuwa ni mbunge wa upinzani kala hapo, ungeshangaa gazeti la uhuru ambavyo lingetoka na shoking headline! Kwa mtindo huu tusahau kupata maendeleo!
 
NAunga mkono hoja wapigwe picha ili mimi kama mwananchi niliyempigia kura yangu nijue anafanya nini anapokuwa bungeni. Kama ni kulala akalale nyumbani lakini sio pale nilipomtuma kuniwakilisha. OLE WAKO MBUNGE WANGU MNYIKA UTOLEWE gazetini umesinzia?? sijui utatuambia nini wananchi wako ukizingiatia gazeti hili linazalishwa jimboni kwako.

wee Laura wewe, alale Mnyika??? thubutu yake! akili inachemka ile, damu bado ya moto, angalia vizuri, wote wanaosinzia ni wazee tene wale wa kijani.....teh! na hiyo ni reflection ya bongo zao na reflection ya umaskini wanaotujengea.....navishukuru sana vyombo vya habari kwa kufunua uvundo huu. ni kweli inauma lakini no jinsi, ni lazima mfalme aambiwe yupo uchi kuliko kumdanganya kavaa suti maridhawa wakti ukweli yu uchi na nyeti zote kazianika....udumu uhuru wa kujieleza!!!
 
Naona unaanza kuchanganyikiwa,ccm imewakaa kichwan mpaka wa tlp nae ccm,poor

weweMichele, unataka kumdanganya nani hapa???!!!!nani kakuambia mrema si ccm c???????!!!!! unafkiri sis wajinga kushindwa kuelewa tlp ni chambo tu la kutudanganyia??????? ha........tu........da.......nga.......nyi...........kkkkkkiiiiiiiiii!!!!!!
 
Akikurupuka tu, anaanza kuongea hovyo akijuwa bado yeye ni ccm anaponda upinzani. hii ndiyo aina ya watu wanaotuwakilisha huko mjengoni hao.

Mamndenyi shimbong shyavoo??? unajua hizi dizaini huwa hazifikirii kwa kichwa, wana viungo vyao vingene vya kufikiri, ntakutajia sku nyingine....
 
Mkuu hapo umenena... viongozi wetu sasa inawabidi waanze kuangalia lishe zao

Mkuu tatizo hawa wenzetu tafsiri ya afya nzuri kwao ni Obesity kuuuubwa a.k.a kitambi. tumbo likijaa choo hadi likapanda juu basi kwao eti ni afya nzuri. utaskia wanapongezena "aah muheshimiwa umeachia(umenenepa) siku hiziiii, unakula nini mwenzetu???? wasijue wanajimaliza wenyewe, mbafu sana hawa!!! kazi kufakamia manyama choma tuuuu wakitumia pesa za posho wanazotuibia, no balanced diet...
 
Picha ya huyu mbunge katika gazeti la mwananchi leo imemtapisha dada mmoja ofisini kwetu.

Kweli kutunza mate/udenda kazi, yataka uwe macho!!!!!
Kwa utaratibu huu huyu anaweza jaza ndoo ya Udenda!!!
 
Siyo vizuri kupiga picha kama hiyo, nakumbuka Pinda alikuwa sehemu fulani sitataja akala usingizi mzungu mmoja akapiga picha ikatoka chicha aliishia kudelete angemtoa angeona kilichomnyima kuku kwenda haja ndogo.

Kwa hii ya mrema siyo vizuri hata mimi mimi sijaipenda.

CD
Kwanini hujaipenda kwamba hakulala au nini? Mi nadhani kwa kazi ya muhimu na makini aliyotakiwa kuwa anafanya pale, yeye na wabunge wengine hakuna anayetakiwa kulala, fikiria maamuzi muhimu yanayopitishwa katika chombo hicho, kwa kura za Ndiyooo tulizozoea, huoni kuwa ni wabunge wa aina hii ndio wanaharibu. Kwa mimi hii ingekuwa ni sababu tosha ya kunyimwa posho na kufungiwa japa two weeks, kwa Uzembe. Ni kosa kabisa hili !!!
Tungeshauri itungwe sheria ya kukatwa posho ya siku hiyo, akirudia siku nyingine ana simamishwa kuhudhuria japo two weeks, akizidi mara ya tatu anafukuzwa kabisa, bora kuchagua mbunge mwingine kuliko mzembe wa namna hii.
Tena tuongeze wapiga picha wengi kuwaumbua ma Bogus kama hawa!!!
 
Picha ya huyu mbunge katika gazeti la mwananchi leo imemtapisha dada mmoja ofisini kwetu.

270073_10150245147449589_841309588_7058007_6092276_n.jpg
She must be pregnant!
 
Jamani Mzee alikula akashiba vizuri sasa kinachofuata na kula mboji mwanzo mwisho.Inavyoonekana kikombe cha babu hakijasaidia.
 
Lakini angalauanapoamka huwa anaweza kutetea kwa bidii pensheni yake ya unaibu waziri mkuu
 
Mrema , kielelezo cha Bunge la watu wasio makini
270073_10150245147449589_841309588_7058007_6092276_n.jpg


Alianza John Komba,akafuata Wasira sasa Mrema..............Komba alijibu,Wasira alijibu..haya sema na wewe mrema.............
 
Kama utapata gazeti la Mwananchi tarehe 30/06/2011 ukurasa wa mbele kabisa basi utakutana na picha ya muheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema mbunge wa jimbo la Vunjo akiwa amelala na udenda ukiwa unamtoka kwenye kikao cha bajeti bungeni. Kweli kwa mtazamo wangu mimi binafsi siungi hoja ya wapiga picha kutoa picha kama hii hata kama ni uhuru wa viombo vya habari huku ni kumzalilisha mtu, gazeti la Mwananchi tena wanasema gazeti la watu makini huku sasa ni kuvuka mipaka naomba wanaJF wenzangu mimi sio mwanachama wa TLP naona ifikie wakati pale bungeni wapiga picha wawe wanapewa mipaka ya kupiga picha. Nawasilisha lakini siungi hoja picha kama hizi au tulifananishe gazeti na magazeti ya udaku?
Wabunge pale wapo kazini kufanya Kazi waliyotumwa na Wananchi na wanalipwa Mamilioni kutokana na Kodi zetu kuingia tu Mjengoni Posho elfu sabini nashindwa kuelewa Akili yako unaposema kwamba wanazalilishwa kwani walitumwa kwenda kulala humo!!Wabunge kama kina Zitto wanaopiga kazi usiku na Mchana wanasema Posho hizo ni dhuluma huyu Mpiga Bönji anawadhihaki kwamba Posho mlizikuta na Mtaziacha afu we unatetea huu Utumbo.
 
Back
Top Bottom