Mramba: Another Challenge!

Mramba: Another Challenge!

Mimi ninamfahamu huyu mama kwakuwa nilifanya nae kazi Iringa wakati huo akiwa meneja wa kanda LAPF miaka ya 2005-2008.
Huyu mama ni MKOROFI KULIKO MNAVYOMFIKIRIA. Anazo hizo qualifications za utawala lakini kwenye masuala ya Relations na wafanyakazi wenzake huyu mama ni SIFURI. Hana lugha nzuri, mbabe, anakutumikisha anavyotaka na ole wako umchallenge! Alimfukuza kazi dereva wake alikua anaitwa Mwakingwe kwa sababu za kipuuzi, Mwakingwe akakata rufaa akashinda akahamishiwa Arusha. Hafai.....

Kwenye hiyo nafasi ya Ubunge Pinda anam-back-up, nasikia wanamahusiano (sina hakika ni mahusiano ya nini kwakuwa huyu mama HANA mume) na walifahamiana huko huko Sumbawanga (kwa hulka yake ni vigumu kuwa na mume) ingawa ni mzuri sana(sura+body structure)
Ukiwa unaongea nae hivi kwa mara ya kwanza kama humfahamu, utajua huyu ni mtu wa maana, mzoee uone!!
Nafasi aliyonayo Mama Six yeye pia aliigombea 2005 akaangukia pua.

Anapenda siasa, anatumia muda mwingi kwenye siasa, LAPF Hawamtaki sio kwa sababu ya RUSHWA ila kufanya kazi na huyu mama kunahitaji UWENDAWAZIMU adhawaiz utafeli tu.
Huu ni UKWELI, Geza ulole usiudanganye umma wa great thinkers bana

- Strong na fair, mkuu ahsante sana tunasikiliza!

Respect.

FMEs!
 
Jimbo la Rombo linahitaji mwanasiasa mwenye vision,mwenye malengo marefu katika kuhakiksha jimbo linaimarika kiuchumi kutokana na faida ya kuwemo soko la pamoja East Africa.

Hili jimbo,tecnically liko ktk position nzuri zaidi kunufaika kwani liko mpakani na Kenya.Kunahitajika mwanasiasa mwenye ushawishi na mwenye utaalamu wa hali ya juu ktk ku-mobilise resources kwa ajili ya miradi mikubwa kama viwanda vya kusindika mazao,soko kubwa la bidhaa,uwekezaji katika sekta ya utalii hasa ukizingatia barabara ya lami inakamilika,uboreshaji wa mitaji kwa ajili ya vijana wajasiria mali bila kusahau matatizo kama maji,na elimu

Pia uwekezaji wa kilimo ktk ukanda wa chini ambao unahitaji zaidi kilimo cha umwagiliaji .Pia kubuni vitega uchumi vitakavyokuza uchumi wa halmashauri ya wilaya.

Rombo inahitaji kijana makini,mchapakazi,mwenye uwezo mkubwa wa ku-mobilise resources ndani na nje ya nchi pamoja na kuweka malengo ya muda mrefu.Huyu mama kama tabia zake ndizo hizo,zaidi ya kupata backup frm PM,bado hawezi kuwa mwakilishi mwenye manufaa ktk jimbo la Rombo.Nitakuja kuchangia zaidi katika hii thread!
 
Warombo hawana tabia wala kawaida ya kuchagua kiongozi mwanamke. Fuatilia historia na hata hali ya sasa utaona. Sina chuki na wanawake, ila nazungumzia tabia ya warombo kuhusu wanawake. Kule sifa ya uzuri wa mwanamke ni kuwa 'kubota', yale matrekta maarufu, yaani kufanya kazi zaidi ya punda. Hawatachagua mwanamke I can assure you.
 
- Kijana mdogo hii ni thread ya Mramba, kama kumuongelea Malecela anzisha kule, pole sana naona unahangaika sana kila kona humu vipi mkuu sema usaidiwe! ....... ni nyundo tu! remember unhh! upanga kwa upanga Bwa! ha! ha! huja-recover mpaka leo tu!

Es = Sauti Ya Umeme

Huwezi kunichagulia cha kuongelea, naongea chochote popote. Huwezi kuleta swaga za Mramba halafu utake swaga za Malecela ziachwe.

Hapa mbarrtata kila siku, hakuna matata so recovering is irrelevant, got it dogo?
 
Hizi hapa chini ni baadhi tu ya changamoto zinazoikabili wilaya au jimbo la Rombo:

Kushuka kwa kipato cha wananchi wa wilaya ya Rombo. Pato la mwananchi wa Rombo linakadiriwa kuwa ni shs. 250,000/= kwa mwaka (DGDP Survey, 2007). Hii ni sawa na dola za Amerika 167 kwa mwaka. Dola 14 kwa mwezi au dola 0.5 kwa siku.
Zao kuu la biashara linazalishwa chini ya viwango vya kitaalam.Eneo lilimwalo kahawa lina uwezo wa kuzalisha tani 6,000 kwa mwaka. Ili kahawa hii ipate bei nzuri italazimu kuongeza ubora na wingi wake. Hii inapaswa kuanzia tangu kipindi cha matunzo shambani, namna ya umenyaji maganda, usafishaji hadi ukaushaji. Pamoja na yote haya yanahitajika madawa na mbolea zaidi na mashine za kumenya.
Msongamano wa watu ni mkubwa mno unaosababisha ufinyu wa ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo. Watu wanalazimika kuzalisha mazao kwenye eneo dogo.
Mahitaji ya shule za sekondari ni makubwa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanomaliza elimu ya msingi. Tatizo hili linakuzwa kutokana na uhaba wa maeneo ya kujenga shule na huduma nyingine za jamii.

Vijana:
Kuna vijana takriban 3,400 wasiokuwa na ajira za hakika

Per capital income inapokuwa 0.5 us dollars per day,inaashiria wananchi warombo wanaishi kk umaskini wa hali ya juu.Hatua kali,ngumu za muda mrefu na muda mfupi zinastahili kuchukuliwa ili uchumi wa jimbo na mwananchi wa kawaida upande
 
Mimi ninamfahamu huyu mama kwakuwa nilifanya nae kazi Iringa wakati huo akiwa meneja wa kanda LAPF miaka ya 2005-2008.
Huyu mama ni MKOROFI KULIKO MNAVYOMFIKIRIA. Anazo hizo qualifications za utawala lakini kwenye masuala ya Relations na wafanyakazi wenzake huyu mama ni SIFURI. Hana lugha nzuri, mbabe, anakutumikisha anavyotaka na ole wako umchallenge! Alimfukuza kazi dereva wake alikua anaitwa Mwakingwe kwa sababu za kipuuzi, Mwakingwe akakata rufaa akashinda akahamishiwa Arusha. Hafai.....

Kwenye hiyo nafasi ya Ubunge Pinda anam-back-up, nasikia wanamahusiano (sina hakika ni mahusiano ya nini kwakuwa huyu mama HANA mume) na walifahamiana huko huko Sumbawanga (kwa hulka yake ni vigumu kuwa na mume) ingawa ni mzuri sana(sura+body structure)
Ukiwa unaongea nae hivi kwa mara ya kwanza kama humfahamu, utajua huyu ni mtu wa maana, mzoee uone!!
Nafasi aliyonayo Mama Six yeye pia aliigombea 2005 akaangukia pua.

Anapenda siasa, anatumia muda mwingi kwenye siasa, LAPF Hawamtaki sio kwa sababu ya RUSHWA ila kufanya kazi na huyu mama kunahitaji UWENDAWAZIMU adhawaiz utafeli tu.
Huu ni UKWELI, Geza ulole usiudanganye umma wa great thinkers bana
Na utendaji wake je hapo Iringa? accounts zilikuwaje? makusanyo ya kodi yalikuwaje? Nidhamu ya kufanya kazi ilikuwaje? huko Sumbawanga mbona alifanya kazi hata kabla ya Pinda kuwa Mbunge? na makusanyo yalikuwa vipi? alisomesha mayatima wangapi? mishahara ililipwa ontime mara ngapi?

Lets be fair huyo dereva atakuwa alichemsha kama kawaida ya madereva wa mashirika maana navyojua hanywi ni molokole like sasa tusiongelee suala la kufukuzwa mtu m1 kazi na ku-link na ukorofi wa mtu! Ninavyomfahamu ni mchapa kazi na wavivu wala rushwa watamchukia! lets wait and see we need more details za huyu mama
 
kwa kutumia tu busara na michango ya wanaJF kwa ujuzi wa mambo yalivyo rombo, mzee Mramba angekaa pembani, kwa heshima yake, ifike hatua hawa watu wawekewe hata vikwazo na chama chao kushiriki uongozi, je ikiwa anachaguliwa tena na kesi akashindwa? ni hasara kwa serikali kufanya by-election kumreplace.....

hawa wote kina chenge, rostam, lowasa....and the like wapumzike siasa na uongozi wa kitaifa sasa.....
 
-bado Rombo inahitaji mbunge mwenye ushawishi wa kufanya resources mobilisation ndani na nje ya nchi.Wananchi wa Rombo wamekua wahanga wa wanasiasa uchwara,wabinafsi,ambao hawako karibu na wananchi kwa muda Mrefu

Kazi nyingi za jimbo la Rombo wanaachiwa madiwani,pia wabunge waliowahi kuliwakilisha hili jimbo wamekua karibu na wananchi occasionaly like either kipindi cha uchaguzi kikikaribia,waalikwe kwenye mahafali au kipindi cha maafa kwa nandra sana

-Pia pamoja na Mramba kujitahidi kuchangisha wananchi wenye asili ya Rombo waishio Dar,still kuna mikakati makini inahitajika katika fund raising kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo.Nitarudi tena,tuko pamoja
 
Mimi ninamfahamu huyu mama kwakuwa nilifanya nae kazi Iringa wakati huo akiwa meneja wa kanda LAPF miaka ya 2005-2008.
Huyu mama ni MKOROFI KULIKO MNAVYOMFIKIRIA. Anazo hizo qualifications za utawala lakini kwenye masuala ya Relations na wafanyakazi wenzake huyu mama ni SIFURI. Hana lugha nzuri, mbabe, anakutumikisha anavyotaka na ole wako umchallenge! Alimfukuza kazi dereva wake alikua anaitwa Mwakingwe kwa sababu za kipuuzi, Mwakingwe akakata rufaa akashinda akahamishiwa Arusha. Hafai.....

Kwenye hiyo nafasi ya Ubunge Pinda anam-back-up, nasikia wanamahusiano (sina hakika ni mahusiano ya nini kwakuwa huyu mama HANA mume) na walifahamiana huko huko Sumbawanga (kwa hulka yake ni vigumu kuwa na mume) ingawa ni mzuri sana(sura+body structure)
Ukiwa unaongea nae hivi kwa mara ya kwanza kama humfahamu, utajua huyu ni mtu wa maana, mzoee uone!!
Nafasi aliyonayo Mama Six yeye pia aliigombea 2005 akaangukia pua.

Anapenda siasa, anatumia muda mwingi kwenye siasa, LAPF Hawamtaki sio kwa sababu ya RUSHWA ila kufanya kazi na huyu mama kunahitaji UWENDAWAZIMU adhawaiz utafeli tu.
Huu ni UKWELI, Geza ulole usiudanganye umma wa great thinkers bana

Mie naota tupete Rais mwenye kufanya kazi kama huyu MAMA.

Ili mambo yaende, inabidi watu kadhaa wamwage damu. Wachina wanasema "Jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita". Tanzania likitoka jasho kidogo, watu wanalialia kama watoto.

Wee Mama, kama utasoma hapa, nakukaribisha UGOMBEE SIKONGE.
 
Ili uweze kuwaunganisha wananchi,viongozi walioko nyuma yako vizuri ktk kufanya kazi vyema na kuleta ufanisi basi huna budi kuwa na ukali wenye busara,kutokua na dharau na kiburi,hii itasaidia kujenga heshima ya kiongozi pasipo na nidhamu ya uoga na pia unawapa nguvu ya kufanya kazi nzito kwa hiayari yao

Unaweza ukawa umesomea utawala but still ukakosa ile nature ya utawala au uongozi...so huyu mama inaonekana ni mtawala na si kiongozi .jimbo la Rombo limeongozwa na watu wakorofi kama mkuu wa wilaya yule mmasasi ole molaimeti,lakini pamoja na jeuri,kiburi na kutumia nguvu katika uongozi jimbo la rombo lilizidi kuzorota

Sometimes ukali unahitajika ktk uongozi but si ukali utakaoathiri mfumo mzima wa utendeji
 
Ama kweli wabongo kichwa maji!..
nchi inaliwa mbele nyuma bado mnaweka matumaini ya kumtegema mtu fulani kuwa mbora zaidi ya mwingine..
Binafsi naamini kabisa kwamba hakuna mtu hata mmoja anayeingia bungeni kutafuta kubadilisha maisha ya mwananchi wake isipokuwa kupata nafasi ya kuvuta mishahara minono na ruzuku ambazo ni kivutio kikubwa kwao....wabunge waliopo na watakao kuja wote ni wezi watupu kwani huwezi kutumia mtaji wa zaidi ya millioni 300, fedha toka mfukoni mwako kujitangaza ati kwa ajili ya kuwatumikia wananchi..

Hivi sasa kila msikiaye anauza mali za urithi, mali za taifa hadi mchanga maadam wote wanajiandaa na uchaguzi... hii kweli inaingia akilini?. jamani hakuna mwema huko Dodoma wote chama moja - Madalali. Hawauzi kitu isipokuwa kwa kutegemea makato ya pato lao wenyewe..Ile 10% imefikia ilokuwa kwa viongozi wa juu sasa hivi imefika hadi serikali za mitaa, kwa hiyo hakuna biashara ya kanisa hapa. Kifupi hakuna afadhali, hawa wote wakipewa nafasi ya Mramba watayafanya madudu kama ya Mramba na pengine zaidi yake!
Nimesema hapa Bongo kila mtu ni strker, mpe nafasi atakufunga tu goli, hakuna cha sheria wala mjomba wake.. wanakula nchi kwa kwenda mbele kaa mchwa.
 
Mkuu wangu Mkandara,

Salute sana kamanda..uliyoongea hapo juu ni kweli ingawa sikubaliani na mawazo yako kwa sasa.

So,hapa unashauri nini mkuu?watu waache kupiga kura? au wasijitokeze kugombea?

Ofcourse kutegemea mtu mmoja kuleta maendeleo ni upunguani fulani lakini hoja ya msingi anahitajika mtu makini kwa ajili ya kuleta inspiration,motivation kwa watu anaowaongoza.mtu mwenye mawazo ya kufanya something remarkable kwa ajili ya maendeleo ya watu.Kiongozi mwenye kushirikiana na watu,mwenye uwezo wa kutumia fursa na au kutafuta fursa kwa ajili ya watu wake.Yeye awe anatilia maanani kwamba ameshapata ajira,basi kilichoko mbele yake ni ku-deliver.Hapa ndipo inapokuja tofauti kati ya kiongozi na kiongozi.Tatizo mazingira yaliyowekwa au yaliyozoeleka kwa muda mrefu ndiyo yanyotufanya tufikirie kwamba fulani atatuletea maendeleo,ni mawazo ya Ujima.Hata Mao kule china alileta maendeleo kwa kutumia uwezo wake wa motivationna inspiration ya maana kwa peasants,na si yeye binafsi.
 
Mkandara,

Ngoja akusikie George Ambwene Mwakalinga aka Mtanzania.

Kumbe na yeye anataka kwenda Bungeni kuvuta mshahara mnene? Nilifikiri Huawei anavuta mshahara mnene zaidi ila kama kweli Bunge linavuta zaidi ya hiyo, ngoja nijiandae mwaka 2015 nigombee jimbo la Sikonge.
 
He is a dead walking man

he is a sleep walker---------(a cop), lakini wengi wao mwaka huu ni sleep walkers, sijajua watu wa Monduli wanasemaje kuhusu hili, vipi hakuna kijana aliyejitokeza kumng'oa mzee wa grey hairs---au wanammwogopa
 
Na bado wengi watajitokeza,katika majimbo yatakayokua na upinzani mkali mwaka huu..basi jimbo la Rombo ni mojawapo,ni kipindi ambacho wananchi wa Rombo watapata fursa pana zaidi ya kuchagua.Nitarudi tena badaae
 
ubunge wa Rombo ni zaidi ya kuonyesha uwezo wa kupanda mlima kilimanjaro,ni zaidi ya kuwa mwandishi wa habari ni zaidi ya kuwa waziri wa fedha,miundombinu na ni zaidi ya kuwa m/ mwenyekiti wa TANROADS mkoa.Hapa najua nitaeleweka na wachache.Nitarudi bado
 
Ili uweze kuwaunganisha wananchi,viongozi walioko nyuma yako vizuri ktk kufanya kazi vyema na kuleta ufanisi basi huna budi kuwa na ukali wenye busara,kutokua na dharau na kiburi,hii itasaidia kujenga heshima ya kiongozi pasipo na nidhamu ya uoga na pia unawapa nguvu ya kufanya kazi nzito kwa hiayari yao

Unaweza ukawa umesomea utawala but still ukakosa ile nature ya utawala au uongozi...so huyu mama inaonekana ni mtawala na si kiongozi .jimbo la Rombo limeongozwa na watu wakorofi kama mkuu wa wilaya yule mmasasi ole molaimeti,lakini pamoja na jeuri,kiburi na kutumia nguvu katika uongozi jimbo la rombo lilizidi kuzorota

Sometimes ukali unahitajika ktk uongozi but si ukali utakaoathiri mfumo mzima wa utendeji
Mkuu Ben,
Huyu Mama mbona unataka kumdhoofisha? japo kama simfahamu lakini nikisoma maelezo ya watu wanakiri kuwa akliweza ku-deliver sehemu mbali mbali alizofanya kazi na nikizingatia tabia za kazi serikalini na maofisi ya serikali, ili msimamizi aweze ku-reverse ofisi ya wilaya ianze kutoa maendeleo yanayotakiwa na huyo msimamizi awe ni mwanamke kwenye hiyo mikoa inayotajwa, nadhani anastahili sifa.
Zaidi hapa tumeshakiri mara nyingi kuwa kwa kweli nchi nyetu inahitaji viongozi madikteta kama kina Paul Kagame walio na mwelekeo na nia njema na Taifa lao. Kama huyu Mama ameweza kufanya hayo yaliyoelezwa hapo juu na katika vituo tofauti basi anastahili kupewa nafasi na ni ya miaka hiyo ya uchaguzi, mitano itakuwa imeshaeleweka. Sasa tunataka kiongozi anayekwenda kuomba watu wafanye kazi zao? huyo tunaye na kazi haziendi, anakwenda kutembelea bandarini mazungumzo na habari si uliyasikia! kumebadilika sana pale leo hii? Hebu tupe jina la kiongozi bora zaidi pale leo hii basi. Hizo sifa hapo ni za kiongozi mwenye kuthubutu kubadilisha vitu viende sawa!
 
Na utendaji wake je hapo Iringa? accounts zilikuwaje? makusanyo ya kodi yalikuwaje? Nidhamu ya kufanya kazi ilikuwaje? huko Sumbawanga mbona alifanya kazi hata kabla ya Pinda kuwa Mbunge? na makusanyo yalikuwa vipi? alisomesha mayatima wangapi? mishahara ililipwa ontime mara ngapi?

Lets be fair huyo dereva atakuwa alichemsha kama kawaida ya madereva wa mashirika maana navyojua hanywi ni molokole like sasa tusiongelee suala la kufukuzwa mtu m1 kazi na ku-link na ukorofi wa mtu! Ninavyomfahamu ni mchapa kazi na wavivu wala rushwa watamchukia! lets wait and see we need more details za huyu mama
Katika muda wote niliokaa pale LAPF Iringa, SIKUWAHI kuona akikaa ofisini kwa siku 5 za wiki za kazi Consecutively.Kila siku ni Trips kuzungukia "MAKUSANYO" ya michango. Ukweli ni kuwa alikuwa anakula imprest na per diem tu lakini kazi hakuwa akifanya. Staff wake woooote walikuwa wanamwogopa kuliko wanavyomwogopa shetani. Alikuwepo dada mmoja (sijui kama yupo hadi sasa) anaitwa Amina yeye ndo alikuwa anamchana live. Wengine wote walikuwa wanamwogopa.

Huyu mama aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara moja pale LAPF HQ, wakamdemote kumleta kanda ya Kusini (Iringa) kwakuwa HAKUWA na mahusiano mazuri na staff wake. Akafight aka honga lakini akachemsha. Baadae WM huyu alipoutata u-PM baada ya EL akarudishwa tena HQ ambapo na po hakukaa, nasikia Mkurugenzi mkuu wa LAPF alikataa kufanmya nae kazi. Kwakuwa LAPF na ofisi anayofanyia kazi zipo chini ya WM, kilichofanywa ni kuhamishwa tu. Kuchapa kazi sio tatizo maana hata Muungwana nae ni Mchapa kazi lakini katika uongozi, vitu vitatu vinatazamwa, 1. Resources (watu=equipments), 2. Rerations (dhidi yako na watu=equipments) then Results.
Relations+Relations=Results.
Ukiitazama hiyo hesabu utagundua ni kwa nini huyu mama HAFAI
 
jimbo la rombo ni la joseph selasini to loose, jamaa anajulikana sana na wananchi wa rombo. huyu mama ajulikani kabisa rombo na ukizingatia yeye ni mwanamke na tabia za watombo kuhusu mwanamke ni sababu tosha hawezi kupata.
baba yake joseph selasini ana uwezo mkubwa sana wa kumobilize voters wa rombo na ukizingatia yeye ametoka mkuu ambayo ndiyo central na ina watu wengi sana rombo.
 
Back
Top Bottom