1.
- Mkuu wangu ninawaona sana wanafunzi wa Vyuo vikuu sasa wanavyolazimishwa kuchangia elimu, ndipo ninaiheshimu sana CCM kama chama cha siasa kwa sera za kuweza kunisomesha shule hizo hizo bure bila kulipa hata senti tano, ikiwa ni pamoja na kunisafirisha bure kwa kutumia warrants.
2.
- Enlightenment sio lazima ionyeshwe kwa kuwa mpinzani wa chama kilichokusomesha bure, inaweza pia kua ni pamoja na kukiosoa kwa manufaa yake kna taifa kama ninavyofanya hapa JF, na wewe ukikikosoa kutokea Upinzani, tunalisaidia taifa letu kwa hoja mbadala, badala ya kulilia wote hapa tuimbe wimbo mmoja.
3.
- Wakoloni walimsomesha Mwalimu kwa makusudi mazima ya siku moja kumpa uhuru na uongozi, ndio maana Mandela hakuuliwa mapema na makaburu ni kwa sababu walijua kua siku moja wanaweza kumpa uhuru na uongozi, na besides hizi ni ishu mbili tofauti kudai uhuru wka wakoloni na kushindwa kwetu kuutumia uhuru tulionao tayari, sio makosa ya CCM kama chama cha siasa, ila ni uzembe wetu wananchi.
4.
- Anyways, CCM bado haijapigwa buti kama hizo nchi kwa hiyo again hii hoja sipaswi hata kuijibu maana ni batili from mwanzo wake, licha ya mwisho.
5.
- CCM haikunisomesha bure peke yangu, kushindwa kwake kuwasomesha bure wananchi leo naamini ni tatizo la uchumi zaidi kuliko muundo wa serikali yake ya sasa, kubadilika kwa sera za uchumi za dunia kumewafanya hata Soviet na China wabadilike, so was sisi Tanzania na CCM, lakini ni fact kwamba mpaka leo wananchi wa Tanzania wana imani na CCM ndio maana wameweza kuipa nafasi ya kutawala for the last 47 years,
Ninasema hivi CCM kama chama tawala cha siasa kina matatizo mengi sana, na ni kutokana na kelele zetu hapa JF na vyama vya upinzani, ndio maana sasa inajaribu kujirekebisha ingawa sio wka mwendo ambao wengi hapa JF tunautaka, lakini mimi binafsi bado nina imani kubwa na chama changu kwamba viongozi wachache wabovu watasafishwa na kurudi inapotakiwa kuwa, lakini ni muhimu sana wananchi wenye uelewa tuka-maintain mawazo mbadala badala ya kujaribu kulazimishana kuwa na uniformity mind hiyo ni hatari sana kwa taifa letu, maana ndio hasa mawazo mabovu yaliyotufikisha taifa letu hapa tulipo sasa,
Otherwise, heshima mbele kwa angalau kuwa na hoja nzito.