Mramba anasafishwa?

Huu ni ugonjwa mbaya sana unaotukabili wa Tanzania. It seems to me kwamba Mtanzania anakuheshimu tu pale unapomnyanyasa na kumfedhehesha. The more money you steal from us the more we respect you!! Unbelievable!!!!! Najua watu watasema ni njaa but this is BEYOND njaa kusema kweli...

- Mkulu Karandinga, hapa tupo ukurasa mmoja, saafi sana!
 
Nakubaliana na maneno yako; utashangaa kugundua kuwa sehemu kubwa ya hao "wapokeaji" ni watu waliokatiwa kitu kidogo.

...ama kweli umasikini ni kitu mbaya! Rushwa, takrima, 10%...
 
FMES,

..sina uhakika kama wananchi wa Chunya walitupia mawe msafara wa muungwana kwasababu ya masuala ya EPA, Radar,ndege ya raisi, etc etc.


..Mramba alishindwa kwenye uchaguzi kwasababu alionekana in-effective na wapiga kura wa Rombo. wananchi walitamka wazi kwamba hawata mpa kura kwasababu hiyo.

..hili suala ni more complex zaidi ya unavyoliwakilisha hapa. katika kipindi chake[Mramba] kama mbunge wa Rombo jimbo limeweza kupata mradi wa ujenzi wa barabara ya lami. hiyo ni kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru.

..kwa hiyo unapojaribu kuwa-analyze na kuwapa labels wananchi wa Rombo, zingatia ukweli wa mchango wa Rombo ktk maendeleo ya jimbo hilo.

..simtetei Mramba...pia sitetei ufisadi...lakini tukitegemea kwamba tutaindoa CCM madarakani kwa hoja ya ufisadi[richmond,epa,bot,..] peke yake tunaweza kujilaumu huko mbele ya safari.


..HILI SOMO MBONA LILISHATOKEA MONDULI LAKINI BADO TUNASHINDWA KUJIFUNZA?

NB:

..Mrema naye alijaribu kushinda uchaguzi kwa kutumia hoja ya ufisadi ya Chavda matokeo yake tunayajua.
 
Last edited:
Subirini jamani! Mramba amepata, atapata au ana uwezekano wa kupata mapokezi makubwa?

Na haya “mapokezi makubwa” yatakuwa, au yamekuwa ya aina gani? Kama ndugu zake na marafiki zake wametayarisha vyakula na vinywaji mnataka watu wasijitokeze kuvishiriki? Kwa msingi gani wakati Mramba hajatiwa hatiani?

Too many of you are immersed in a French legal framework whereby one is assumed guilty until proven innocent. In our own system, Mramba is innocent, at least for now!

Si kosa kisheria, kwa Waziri wa Fedha kusamehe mtu au kampuni kodi. Hata kama ushauri ulitolewa vingine na Waziri akaukataa, bado hakuna kosa kisheria. Mramba si anashtakiwa kwa kusamehe kodi? Wote tunajua atashinda. Na inawezekana wapiga kura wake wanajua hivyo.

Mzee ES amepongeza mara kwa mara watu waliopiga mawe magari ya viongozi. Hao watu ni wapuuzi na hatari sana! Hatutaki vurugu za kupigana kwa mawe.
 
- Ni baada ya mawe ya Chunya ndio misafara ya Kisutu ikaanza, sasa call me mpuuzi too na mtu wa hatari lakini I love it na I am down,

- Hili taifa tuna safari ndefu sana mpaka kufikia tunakokwenda maana kuna tunaofikiri mafisadi hawawezi kuwa makabila yetu wala dini zetu za kiKatoliki, ila ni lazima tu wawe makabila mengine na dini zingine!

- Mkuu Joka,

Huyu Mramba alishafukuzwa u-RC na wananchi wa Mbeya, ambao walimtaka Mkapa amuondoe haraka sana, kama Quaresi, mafisadi huwa hawana record nzuri hata siku moja, alituambia tutakula manyasi sasa ni zamu yake kula manyasi, ukienda NDC utakuta madudu yake ambayo ni aibu tupu!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
Watu tutasema tutachoka, lakini the facts zipo pale pale. Huyu samaki ameisha kauka na kumkunja haitawezekana.

Kubadilisha desturi (culture) ya Mtanzania itachukua zaidi ya maneno na debates hizi.

Mfano mzuri, hebu angalia zikitangazwa harambee za sherehe, Mtanzania yupo mbele kutoa mchango. Lakini Mtanzania hataki kupokea wito wakuangamiza haka kamdudu ajulikanako kama "Fisadi". Baadala yake.... tunaandaa mapokezi yakifalme....
 
FMES said:
- Ni baada ya mawe ya Chunya ndio misafara ya Kisutu ikaanza, sasa call me mpuuzi too na mtu wa hatari lakini I love it na I am down,

- Hili taifa tuna safari ndefu sana mpaka kufikia tunakokwenda maana kuna tunaofikiri mafisadi hawawezi kuwa makabila yetu wala dini zetu za kiKatoliki, ila ni lazima tu wawe makabila mengine na dini zingine!

- Mkuu Joka,

Huyu Mramba alishafukuzwa u-RC na wananchi wa Mbeya, ambao walimtaka Mkapa amuondoe haraka sana, kama Quaresi, mafisadi huwa hawana record nzuri hata siku moja, alituambia tutakula manyasi sasa ni zamu yake kula manyasi, ukienda NDC utakuta madudu yake ambayo ni aibu tupu!

FMES,

..kama muungwana na takukuru waliamua kwamba mafisadi waende mahakamani baada ya kupigwa mawe na wananchi wa chunya basi MUNGU awabariki wazalendo wa chunya.

..kuhusu manunguniko yako kuhusu DINI na MAKABILA kwa kweli sintopenda kuelekea huko. tukianza kuchambuana kwa dini na makabila yetu mapambano hayo hayatafika popote.

..sijafuatilia rekodi ya Mramba alipokuwa RC Mbeya, NDC, au hata SIDO ambako aliwahi kuwa GM. wana Mbeya wako JF na wanaweza kutoa ushuhuda kuhusu utendaji wake.

..ndugu yangu, nyinyi watu wa CCM siku zote huwa mnajigamba kwamba serikali ni ya kwenu.

..kwa msingi huo huo unaweza kudai kwamba serikali ya CCM imewapeleka mahakamani Mramba na Yona kwasababu inaamini wana hatia kwa makosa wanayotuhumiwa nayo.

..pia serikali ambayo Mramba na Yona wanatuhumiwa kuitia hasara ya mabilioni ni serikali ya CCM, kama mnavyopenda kutukumbusha siku zote.

..sasa kwanini chama chako cha CCM hakijawafuta uanachama Basil Mramba na Daniel Yona?

..hawa wangefukuzwa uanachama, na Mramba kuukosa Ubunge, basi haya mapokezi yasingefanyika.

NB:

..BADALA YA KUWAANDAMA WAROMBO KWA KUMPOKEA MBUNGE WAO, KWANINI HUKIHIMIZI CHAMA CHAKO CCM KIWAFUTE UANACHAMA WATUHUMIWA WA UFISADI?
 
1.
..ndugu yangu, nyinyi watu wa CCM siku zote huwa mnajigamba kwamba serikali ni ya kwenu...kwa msingi huo huo unaweza kudai kwamba serikali ya CCM imewapeleka mahakamani Mramba na Yona kwasababu inaamini wana hatia kwa makosa wanayotuhumiwa nayo.

- Kikatiba yetu chama kinachoshinda uchaguzi ndio kinachotakiwa kutawala, yaani tuna system ya the winner takes all, kwa hiyo sio makosa kwa CCM kudai kuwa inaongoza serikali kwa kutumia sera ilizoziuza kwa wananchi mpaka kuchaguliwa nao, haya ni masuala ya what katiba's says na sio kujigamba.

..sasa kwanini chama chako cha CCM hakijawafuta uanachama Basil Mramba na Daniel Yona?..hawa wangefukuzwa uanachama, na Mramba kuukosa Ubunge, basi haya mapokezi yasingefanyika...BADALA YA KUWAANDAMA WAROMBO KWA KUMPOKEA MBUNGE WAO, KWANINI HUKIHIMIZI CHAMA CHAKO CCM KIWAFUTE UANACHAMA WATUHUMIWA WA UFISADI?

- Roma haikujengwa kwa siku moja, hapo tulipofika nao sio padogo na believe me hatujafika mwisho ingawa ndio hivyo kwa mwendo wa kibongo na sio wa majuu!
 
FMES,

..hata mimi nakubaliana na wewe kwamba serikali ni ya CCM.

..sasa tueleze basi kwanini huwabebei bango CCM wawafute uanachama Mramba na Yona, badala ya kuendelea kuwashutumu walalahoi wa Rombo?
 

...kuwa mke wa mtu siku hizi sio tiketi ya kutokuwa na msela.......tena siku hizi wake za vigogo wakipata wasela wanakolea sana ....wanasema kila kitu...just kwa kuwa wanakuwa so deep na yule wanayempata kwani hawezi kuwa wazi kupata mwingine kama anavyotaka....

..mwanamke msela kama sofia ...anaweza asiwe na mume lakini pia anakuwa huru kuchukuliwa na mwanamume yeyote pale anapojisikia....sometimes one night stand man....sasa sidhani kama anaweza kuwa wazi namna hiyo...kwani hakuna enough intimancy...tena mara nyingi wanawake wengi maarufu siku hizi hupendelea wanaume wasela wasiokuwa na uelewa mkubwa...wa mambo zaidi ya "yale"...kwa kuofia akichukuliwa na mjanja anaweza kumuuza...so anakuwa falafala tu wala hutaamini...kama anazungusha mzigo wa ajabu...

pia kumbuka CONDY RICE naye ni single lady.....na katika list ya alio wa date yumo....waziri wa mambo ya nje wa canada,italia,and fomer uk foregn.....but pia wanajuwa wazi kuweka mstari kamili kati ya chumbani na kwenye gorvernment business.........

...ni mwanamke mjinga mwennye nafasi serikalini au kokote ambaye hatamshangaa mwanamume aliyemdate anaaza kumuuliza mambo ya kazini kwake...wakati kazi waliyoifuata walipo inajulikana.....mtu akiaaza kukuuliza mambo ya kazini sehemu kama hizo lazima atakuwa ametumwa anataka kukufanya "samson"

so .....lets put aside bedroom affairs au kuolewa na kutokuolewa au kuoa na kutoaooa kwenye kazi!!!!...unless otherwise!

Phi Mikael,
Usipotoshwe na news media; Condy yupo State Department, ki-constitution haruhusiwi kabisa kutembea na foreigner; hata diplomats wa US of America hawaruhusiwi kufanya hivyo vitendo wakiwa in a foreign land; otherwise wakishikwa wanapewa ndege inayofuata kurudi kwao!
 
- Ndio maana siwashutumu wananchi walalahoi wa Chunya, kama ninavyowashutmu wananchi wa Rombo, au?.


Lakini Mwaka 1995 watu wa Rombo si walijitosa kuchagua upinzani na hawakupata huduma zote.

Hivyo walichofanya ni kuturudishia kipenzi wa CCM. Sasa tunasema huyu ni fisadi. Alternative ni wao kuchagua upinzani.
 
Phi Mikael,
Usipotoshwe na news media; Condy yupo State Department, ki-constitution haruhusiwi kabisa kutembea na foreigner; hata diplomats wa US of America hawaruhusiwi kufanya hivyo vitendo wakiwa in a foreign land; otherwise wakishikwa wanapewa ndege inayofuata kurudi kwao!

Sasa wakazime wapi mashetani ???
 
Huu ni ugonjwa mbaya sana unaotukabili wa Tanzania. It seems to me kwamba Mtanzania anakuheshimu tu pale unapomnyanyasa na kumfedhehesha. The more money you steal from us the more we respect you!! Unbelievable!!!!! Najua watu watasema ni njaa but this is BEYOND njaa kusema kweli...


Hii kitu mbona tangu zamani tunayo. Yaani mtu akiteuliwa kwenye nafasi ya juu kama Meneja/Mkurugenzi wa Kiwanda, Waziri, n.k., basi sisi tutaitikia "eee walaaa, fulani kaula". Ikipita miezi sita, kama mtu huyo hajaanza ujenzi wa "hekalu" lake au kuendesha "shangingi" lake binafsi, tutaanza kumcheka: "aah, jinga hili". Ndiyo maana bado nashangaa kama kweli sisi wananchi tuko tayari kweli kuupiga vita ufisadi, ama tunacheza ngoma ya "wanasiasa" ambao ni "mafisadi in waiting".
 
Phi Mikael,
Usipotoshwe na news media; Condy yupo State Department, ki-constitution haruhusiwi kabisa kutembea na foreigner; hata diplomats wa US of America hawaruhusiwi kufanya hivyo vitendo wakiwa in a foreign land; otherwise wakishikwa wanapewa ndege inayofuata kurudi kwao!

...huu utaratibu hata hapa kwetu upo..kuna nafasi ukifika huruhusiwi ku mess..ovyo na wanawake wa kigeni..lakini nadhani haufuatiliwi...kwani mawaziri wetu na watu wa vyombo vyetu hasa wakiona wanawake wa ki tutsi wanakosaga akili kabisa,,,..i have seen this several times..enzi za mwalimu hakuwa na utani na hili,mtu angeweza kukosa nafasi kwa ajili ya tabia za aina hii...

nadhani tungekuwa serious na hili ..hata yule aliyekuwa waziri wetu wa mambo ya nchi za nje ....alipotumwa new york wakati fulani..asingeishia kwenye chumba cha hoteli cha waziri wa nchi jirani mwanamke wa mambo ya nje na kufanya naye ngono hadi wakakosa vikao...rais wa jirani hakufanya ajizi kwani barua ya kumfukuza kazi waziri wake ilimfuata huko huko new york.........aliyekuwa waziri wetu hakupewa hata onyo ...sembuse kuulizwa!

maadili hakuna na wala sijui ile tume ya maadili ambao ndio wako responsible na haya wako wapi.........
 
Utaendeshaje vita dhidi ya ufisadi kama wananchi sisi wenyewe tunasema pole kwa kushikwa kwa ufisadi lakini hongera sana, siku nyingine uhakikishe hushikwi!!!!!!!!!

“Kwa kuzingatia ibara hizo za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mahakama inakubaliana na ombi la Mramba kwa sababu bado hajakutwa na hatia, pia ana haki ya kutembea ili mradi asivunje sheria za nchi, na kwa sababu hiyo kuanzia sasa mshitakiwa anaruhusiwa kutoka nje ya mkoa huu.
 
Developments hizi zinakatisha tamaa sana.Kwa mtizamo wangu mimi, katika mazingira haya,vita dhidi ya ufisadi hatuwezi kushinda.Inakuwaje wananchi wasione kwamba vita dhidi ya ufisadi ni yao na kwamba na wao wanapashwa kushiriki angalau hata kwa kumsusia mtu kama huyu?Lakini hata hivyo kwa watani zangu hawa tunategemea nini, kama sio kushabikia wizi?


Mramba aandaliwa mapokezi mazito
• Mahakama yamruhusu kutembelea jimbo

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Rombo, anayekabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha, Basil Mramba, kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku 29 kwenda kuwasalimia wananchi jimboni mwake.

Kutokana na ruhusa hiyo, Mramba sasa anatarajia kwenda jimboni kwake kesho ambako inaelezwa kwamba ameandaliwa mapokezi makubwa kutoka kwa wapiga kura wake kwa lengo la kumpa pole kwa matatizo yaliyomfika.

Diwani wa Kata ya Kelamfua Makola, Kata ya Mkuu Rombo, Festo Kilewe, aliiambia Tanzania Daima kuwa Mramba aliyekuwa rumande kwa kesi hiyo na baadaye kuachiwa kwa dhamana, ameandaliwa mapokezi makubwa na atafanya ziara katika kata za jimbo lake kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Mipango hiyo imethibitishwa pia na msaidizi wa mbunge huyo, Roman Kilega, ambaye alisema Mramba atakuwa na ziara ya siku nne, ambapo ataanzia Kata ya Tarakea na Useri kuhamasisha ujenzi wa madarasa ya shule pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tarakea hadi Mkuu Rombo na kutoka Mkuu Rombo hadi Marangu.

“Kwa vile mahakama imetoa ruhusu hiyo leo (jana), tunatarajia atawasili hapa kati ya Ijumaa na Jumamosi na wapiga kura wake wamejiandaa kumpokea kwa kishindo ili kumpa pole,” alisema Kilega.

Uamuzi wa kumruhusu Mramba kwenda jimboni mwake, ulitolewa jana na mahakama hiyo kutokana na ombi la Mramba lenye kumbukumbu namba 10RCA/A1/64/2009, lililowasilishwa Ijumaa iliyopita na wakili wake, Hubert Nyange na Peter Swai, kutaka aruhusiwe kwenda jimboni kuwasalimia wapiga kura wake.

Akitoa uamuzi huo jana, Mwankenja alisema, amezingatia ibara ya 13(6)(B), inayotamka kwamba mtu asichukuliwe kuwa ana hatia hadi mahakama itakapomkuta na hatia na ibara ya 17 ya katiba ya nchi, inayosema kila mtu ana haki ya kutembea.

“Kwa kuzingatia ibara hizo za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mahakama inakubaliana na ombi la Mramba kwa sababu bado hajakutwa na hatia, pia ana haki ya kutembea ili mradi asivunje sheria za nchi, na kwa sababu hiyo kuanzia sasa mshitakiwa anaruhusiwa kutoka nje ya mkoa huu.

“Pia niliipitia kwa kina sheria ya Bunge la Tanzania kabla ya kutoa uamuzi huu, kuona mbunge anayeshitakiwa mahakamani kwa kesi za jinai, anatakiwa atendeweje, nimebaini sheria hiyo haisemi chochote katika hilo, hivyo nimetoa uamuzi wangu kwa kutumia ibara hizo nilizozitaja ambazo zipo kwenye katiba ya nchi,” alisema Mwankenja.

Ijumaa iliyopita Mramba kupitia mawakili wake aliwasilisha ombi mahakamani hapo akitaka aruhusiwe kutoka nje ya Dar es Salaam kuanzia Januari 3 hadi Februari mosi mwaka huu.

Ruhusa hiyo itamwezesha pia mbunge huyo kuhudhuria mkutano wa Bunge unaotarajia kuanza Januari 27, lakini pia huenda akalazimika kuomba muda mwingine kwani kwa ruhusa ya sasa, ana uwezo wa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku sita kabla ya muda aliopewa wa Februari mosi kumalizika.

Mramba ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya jinai namba 1200 ya mwaka jana, ambapo anashitakiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Awamu ya Nne pamoja na Yona na Mgonja, wanakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

Ilidaiwa kuwa kwa makusudi au kwa kushindwa kuchukua tahadhari kwa mujibu wa taratibu za kazi, akiwa Katibu Mkuu Hazina na wakiwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu waliruhusu kutolewa kibali cha serikali kilichoisaidia Kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) Government Bussiness Corporation kutolipa kodi, tofauti na mapendekezo ya Mamlaka ya Mapato (TRA), uamuzi ambao uliisababishia serikali hasara ya sh 11,752,350,148.00.

Wakati huo huo, Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya, amesema Januari 16 mwaka huu, atatoa uamuzi wa kukubali au kutokubali mtuhumiwa wa 21 wa wizi wa Fedha katika Akauti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jonathan Munisi, aunganishwe kwenye kesi inayomkabili ya mfanyabiashara Japhet Lema.

Lyamuya aliyasema hayo jana baada ya kusikiliza hoja za upande wa wakili wa serikali Fredrick Manyanda na wakili wa utetezi Evarist Mbuya ambapo upande wa utetezi uliomba mteja wao, aunganishwe kwenye kesi inayomkabili Lema kwa sababu mashitaka yake, yanafanana na yanayomkabili mteja wao.
 
Huu ni ugonjwa mbaya sana unaotukabili wa Tanzania. It seems to me kwamba Mtanzania anakuheshimu tu pale unapomnyanyasa na kumfedhehesha. The more money you steal from us the more we respect you!! Unbelievable!!!!! Najua watu watasema ni njaa but this is BEYOND njaa kusema kweli...

...Aisee hii ni njaa tu!! na nnaelekea kufikiri njaa ya AKILI(common sense) ni hatari kuliko ya MATUMBO!!
**thats my humble opinion.
 
[QUOTE=Hauxtable;356032]...Aisee hii ni njaa tu!! na nnaelekea kufikiri njaa ya AKILI(common sense) ni hatari kuliko ya MATUMBO!!
**thats my humble opinion.[/QUOTE]


It baffles my mind to see these individuals who have been accused of crimes, some of which are tantamount to treason in other countries, receive heroes welcome from their constituents. What are the underlying motives for all this?What does all this mean and what does it say about us as a people? I agree with you kwamba wananchi tuna mental hunger pangs kali sana!!! Anyway lets continue the struggle because they say even a broken clock is right at least once a day....
 
Sitashangaa nikisikia wananchi wa Rombo wametupiwa mabomu ya machozi kwa kumzomea na kumfanyia fujo Mramba ama kamata kamata imeanza baadaya ya wananchi kumtupia mawe Mramba.

Ama ninaota tu ?
 
Back
Top Bottom