Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro.
Mramba ambaye amepata kuwa Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, alichaguliwa kushika wadhifa huo jana wakati wa kikao cha bodi hiyo kilichofanyika mjini hapa.
Mbunge huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya ufisadi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya sh bilioni 11.7 wakati akiwa Waziri wa Fedha, atashika nafasi hiyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye kwa utaratibu mpya wa serikali, ni mkuu wa mkoa huo, Monica Mbega.