Mradi wa umeme utakaojengwa mto Malagarasi mkoa wa Kigoma

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Juzi niliona uwekaji sahihi kuhusu Mradi wa umeme utakaojengwa Mto Malagarasi mkoani Kigoma. Nilijiuliza, kama tutakuwa na Mradi mkubwa Julius Nyerere Hydro Electric Power ambayo itatosheleza nchi nzima na kuuza ziada, Je ni kwa nini tunapoteza fedha tena kujenga mradi wa umeme kule Malagarasi?.
 
Habari za bwawa la nyerere kutosheleza nchi nzima zimekaa kisiasa. AKatika hali ya kuwekeza viwanda vizito huko mbele hio ziada unayo isema itatosha? Leo watanzania wote tukisema tutumie majiko ya umeme hiyo ziada itatoka wapi?

Acha vyanzo viwe vingi na mimi naungana na serikali katika hilo.

Na nitaungana na serikali tukianza kurutubisha uranium kwa ajili ya nishati. Sijui kwanini hatujaangazia huko?
 
Tunapaswa kuwa na vyanzo vingi vya Nishati ingawa kwa bahati mbaya vingi ni vya kuzalisha umeme wa maji. ( Changamoto ya vyanzo vya umeme wa maji ni mabadiliko ya tabianchi yanayopelekea ukame)

Serikali izalishe umeme mwingi kadri inavyowezekana, katika hili iangalie vyanzo vingine ili kuiweka nchi tayari kwa uwekezaji wa Viwanda vikubwa na miradi mingine.
 
Unatakiwa Kifikiria Kesho sio Leo
Wenzetu wapo kwenye 10000Mw
Sie bado tunapigania Kuifikia 5000
Bado Tunasafari Japo Viongozi tulio Nao Ndio Mtihani Mkuu mungu Ametupa Watanzania
 
Unatakiwa Kifikiria Kesho sio Leo
Wenzetu wapo kwenye 10000Mw
Sie bado tunapigania Kuifikia 5000
Bado Tunasafari Japo Viongozi tulio Nao Ndio Mtihani Mkuu mungu Ametupa Watanzania
Aisee kiukweli bado tupo chini sana
 
Juzi niliona uwekaji sahihi kuhusu Mradi wa umeme utakaojengwa Mto Malagarasi mkoani Kigoma. Nilijiuliza, kama tutakuwa na Mradi mkubwa Julius Nyerere Hydro Electric Power ambayo itatosheleza nchi nzima na kuuza ziada, Je ni kwa nini tunapoteza fedha tena kujenga mradi wa umeme kule Malagarasi?.
Nakupa mfano mmoja ili uelewe ninachosema. Uwanja wa Uhuru una uwezo wa kujaza watu 20,000. Serikali iliposema inajengs uwanja wa Mkapa wa watu 60,000 nilijiuliza watu watatoka wapi. Cha ajabu umejengwa, watu wanajaa.
Hilo bwawa la JNHEPP likianza kazi kwa kutoa mw 2300 wanazosema. Tusishangaa zikapungua. Nina hofu hawataki kusema mahitaji halisi ya umeme nchi hii kuhofia watu kuwa na hofu. Migodi mingi Geita inatumia majenereta, inapenda kutumia umeme.
Umeme unahitajika sana.
 
Back
Top Bottom