Dkt. Biteko: Matumizi ya umeme Dar na Pwani ni zaidi ya nusu ya matumizi ya umeme Tanzania nzima

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Chalinze kujionea kinachoendelea kwenye mchakato huo.
photo_2023-10-12_11-38-44.jpg

photo_2023-10-12_11-38-46.jpg
Baada ya kutembelea mradi Dkt. Biteko ameweka wazi kuwa mradi huo umefikia Asilimi 84 na unatarajiwa kukamilika kusikia mwishoni mwa Novemba kisha kuanza majaribio Desemba 2023.

Amesema Watanzania wanachohitaji ni umeme kwa sasa lakini ni vizuri pia kuwaambia kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kumaliza changamoto ya nishati hiyo.

Amesema “Ujenzi wa mradi wa kituo umefikia Asilimia 84, imani yetu ni kuwa hadi kufikia mwishoni mwa Novemba kuelekea Desemba Mwaka huu (2023) kitakuwa kimekamilika na kukabidhiwa kwa ajili ya kuanza kupokea umeme kutoka kwenye Mradi wa Julius Nyerere.

“Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa inayotumia umeme mwingi kutokana na wingi wa viwanda ukiwa unatumia Megawati 132 ikiongozwa na Dar es Salaam inayotumia Megawati 500, hivyo mikoa miwili tu inachukua zaidi ya nusu ya umeme wote wa Nchi. Hivyo, lazima uwekezaji mkubwa ufanyike.
photo_2023-10-12_11-38-46 (2).jpg
“Ukuaji wa miji unaongezeka, idadi ya watu inaongezeka, watu wanajenga viwanda, mahitaji ya umeme sio anasa tena kwa sasa bali ni lazima kutokana na shughuli za kiuchumi.”

Aidha, ameongeza kuwa pamoja na juhudi za kuleta umeme Megawati zaidi ya 2,000 kutoka kwenye Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere, Serikali inaendelea kuboresha vyanzo vingine kwa kuwa matumizi yataongezeka ndani ya miaka ijayo kama gesi, umeme wa jua na upepo.

Amesema “Tunachoomba ni subira hapa katikati, nawapongeza TANESCO (Shirikia la Umeme Tanzania) kwa kusimamia, itakapofika Novemba 30 kazi zote za msingi zitakuwa zimekamilika na tutaanza majaribio mwezi mmoja ili ikifika Desemba 30 kazi zote ziwe zimekamilika.

“Kupitia hiki kipindi cha muda mfupi cha kutafuta utatuzi wa changamoto, tunaendelea na taratibu za ndani za maboresho ya mitambo yetu iliyokuwa imekamilika na kuongeza uzalishaji wa gesi kupata umeme wa kuingiza kwenye gridi ya Taifa.

“Changamoto ya miundombinu ya umeme unatakiwa kuwa na muda kuiandaa kupata umeme, kwa taarifa niliyopewa kwa Mwaka tunaongeza Megawati 150, hivyo ndani ya miaka 10 ijayo mahitaji inawezekana yakawa makubwa zaidi.

“Hivi karibuni tulikuwa na upungufu wa Megawati 400 kwa siku lakini tumeshuka na tunacheza kwenye Megawati 200 hadi 300, wikiendi iliyopita tulishuka hadi Megawati 160, tunachukua hatua kwa miundombinu tuliyonayo kupunguza mahitaji.”

Akizungumza na Wafanyakazi waliopo katika Mradi huo, Dkt. Biteko amewapongeza kwa kuacha njia ya kulalamika na kuingia kazini kufanya kazi kisha akawapa zawadi ya Tsh. Milioni moja.

"Kwa niaba ya Rais nawapongeza Wafanyakazi wote, nilichokuwa nasoma nikiwa ofisini nimeona kwa uhalisia, fanyeni kazi watu wapate umeme.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika ziara hiyo amesema “Hatua ya kuja kuona maendeleo ya ujenzi ni maamuzi mazuri, kwani kukaa ofisini unaweza kupewa mrejesho kwa lugha nzuri na kuamini kila kitu kipo sawa, lakini kufika mwenyewe maana yake kuna jambo kubwa unaloweza kulileta.”

Amesisitiza kuwa Mradi huo unaenda kufaidisha Tanzania nzima na sio Pwani au Chalinze pekee.

Pia soma:

Nadhani na Kilimanjaro, Arusha na Manyara baada ziara tarehe 14 tutarudi kule kule
Ndugu Arusha Nilikuwepo Mwezi wa 8
Hapana Sio Kama Huku Urambo-Kaliua nilipo wauliza Wanakuambia Kiboko ni Masika Ikitokea Wingu kidogo Wanakata kwasiku Wanaweza Kata na kurudisha hata mara 10
 
Megawati 132+500 ni 632MW. Na hii ni zaidi ya nusu ya umeme tunaozalisha nchini. Maana yake uzalishaji wa umeme hafiki au unakaribia 1200MW!! Tuweni serious.
 
Ni sawa si ndio Mikoa ya viwanda Mzee
 
Ndugu Arusha Nilikuwepo Mwezi wa 8
Hapana Sio Kama Huku Urambo-Kaliua nilipo wauliza Wanakuambia Kiboko ni Masika Ikitokea Wingu kidogo Wanakata kwasiku Wanaweza Kata na kurudisha hata mara 10
Baba mwezi wa 9 ilikuwa ni balaa, tangu last week ndiyo naona pametulia kdg baada ya kusikia maza atakuwa maeneo haya, kuna kipindi alikuja Arusha kama sikosei mwezi wa 3 alikaa kama siku 3 hivi, kabla ya ujio wake wiki 1 umeme ulitulia haswa, siku anasindikizwa KIA akiwa maeneo ya USA umeme kwao
 
Felchesmi Mramba aliwahi kusema PSPF Twin Tower, Uhuru Height na Viva Tower kwa pamoja yanatumia umeme mwingi kuliko ule unaotumiwa na baadhi ya mikoa nchini kama Ruvuma, Manyara, Singida, Kigoma na Rukwa. PSPF peke yake linahitaji megawati tano na Uhuru Height megawati 2.5, Viva Tower megawati 2.5 na Benjamin Mkapa Tower megawati mbili.

Alitaja matumizi ya umeme katika mikoa hiyo na megawati zake kwenye mabano kuwa ni Manyara (10) Mtwara (8), Singida (7), Lindi (5.5), Kigoma (6), Ruvuma (4.7) na Rukwa (6.8).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom