Mradi wa ujenzi wa mji serikali (Mtumba - Dodoma): Ushauri wangu kwa CS Hussein Katanga na VP Dkt. Phillip Mpango

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
182
250
Habarini wakuu,

Leo napenda nami pia kupongeza uteuzi wa Mh. MPANGO na Mh. KATANGA kwa nafasi ambazo wameaminiwa na Mheshimiwa Rais na taifa kutumikia.

Nijielekeze ktk mchango wangu wa mawazo juu ya mradi muhimu wa ujenzi wa mji wa serikali, nikichagizwa na furaha ya kuhakikishiwa na Rais wetu na waziri mkuu kuwa hakuna jambo litakaloharibika, pia teuzi za VP na CS inatoa dira kuwa tumedhamiria kweli.

Najua ipo miradi mingi inayoendelea lakini nijikite ktk mradi wa mji wa serikali ambapo wizara zote zina majengo hapo.

Kutokana na kasi ya ujenzi kwa awamu iliyopita kutokuwa kubwa vyakutosha, kutokana na gharama za malipo ya pango ambayo wizara nyingi zimekuwa zikilipa kwa taasisi ambamo zmepanga na pia kutokana na gharama za usafiri hasa mafuta kutokana na baadhi ya wizara kuwa na majengo zaidi ya mawili ambayo yapo maeneo tofauti jijini dodoma hivyo kupelekea kuhitajika kuzunguka sana kwa magari katika kutekeleza majukumu.

Napenda kushauri serikali katika ujenzi wa majengo makubwa na yakudumu ya wizara katika mji wa serikali Mtumba, ili kuongeza kasi ya kukamilisha, itumie utaratibu wa kujenga kwa kutumia taasisi za ujenzi za serikali au binafsi kama NHC, ambazo zinaweza kutumia fedha zao binafsi kujenga kwa haraka kwa kuzingatia ramani zilizopangiliwa na serikali yenyewe, hii ni kuhakikisha kuwa majengo yanakamilika kwa wakati.

Kwa upande wa malipo wakati wa ujenzi serikali italipa kwa kutumia fedha zinazotengwa kupitia bajeti ya ujenzi wa majengo ya wizara, lakini pia mara baada ya ujenzi kukamilika na wizara kuhamia, fedha iliyokuwa ikitumika kulipa kodi ya pango ndiyo itumike pia kuendelea kulipa gharama za ujenzi kwa kampuni au taasisi iliyojenga majengo husika. Hata kama gharama itaongezeka kidogo kutokana na kulipa kwa awamu na kwa muda mrefu kidogo, si mbaya maadam wizara husika zitaendelea na kazi katika majengo yake yaliyokamilika kwa wakati.

Nawasilisha
Asante sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom