Moto mlima Kilimanjaro waingia siku ya 7 huku juhudi za kuuzima zikiendelea

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mamlaka nchini Tanzania kwa kushirikiana na wananchi wanapambana kuzima moto uliozuka katika eneo la Indonet-Rongai lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).

Mpaka sasa chanzo cha moto huo ulioanza Jumapili iliyopita bado haujafahamika ambapo tayari umeteketeza ukanda wa juu mita 3,900 kutoka usawa wa bahari, kaskazini mashariki mwa hifadhi hiyo iliyopo wilaya ya Rombo.

Hata hivyo mamlaka zimeeleza kuwa moto huo umedhibitiwa kwa asilimia 90, huku eneo lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 17 sawa na asilimia 0.9 ya eneo lote la hifadhi, likidaiwa kuteketea kwa moto.

Akizungumza kutoka wilayani Rombo, Kaskazini mwa Tanzania, Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa uhifadhi, Angela Nyaki amesema eneo ambalo limeungua lina mimea jamii ya Erika na majani ambayo ikishika moto huwaka kwa kasi.

Amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana lakini akabainisha kuwa huenda shughuli za kibinadamu zikawa chanzo.

Hili si mara ya kwanza moto kutokea kwenye maeneo ya Mlima Kilimanjaro. Mnamo 2022, moto uliwaka kwa zaidi ya mwezi mmoja na kuharibu maelfu ya hekta za msitu inayozunguka mlima huo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Wanataka kuuza mlima, wameanza kuwatengenezea zengwe akina mangi. Siku sio nyingi wataambiwa waondolewe, wahamishiwe Lushoto!

 
Pesa ya kuuzima utasikia b 1 imetoka , njia za upigaji ni nyingi asee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom