| ||
|
sasa kama shirikisho haliwatambui, waliingiaje mjengoni?
Mpinzani wa JK apeta TUCTA
Wabunge wa CCM watimuliwa
na Grace Macha
ALIYEKUWA Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Nicholaus Mgaya, amechaguliwa kwa kura nyingi kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, huku akiahidi kufanya maamuzi magumu katika kudai haki za wafanyakazi, ikiwemo kuendesha migomo.
Mgaya ambaye taarifa za awali zinaonyesha kuwa zilitumika nguvu kubwa kujaribu kumzuia asiibuke mshindi ndiye kiongozi pekee aliyeshambuliwa vikali na Rais Jakaya Kikwete baada ya chama hicho kutishia kuhamasisha wafanyakazi wasimpigie kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Akizungumza na walioitwa wazee wa jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Kikwete aliyeambatana na wakuu wote wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini, alimshambulia vikali Mgaya kiasi cha kufikia kutoa kauli ya kutozitaka kura za wafanyakazi.
Katika uchaguzi huo wa aina yake, Mgaya alipata kura 324 akiwaacha mbali wagombea wenzake James Mnyeti aliyepata 24 na Honoratha Chitanda aliyeambulia kura 28.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo, Mgaya alisema kazi yao kubwa ni kujadiliana na serikali kutatua madai ya msingi ya wafanyakazi, lakini kama njia hiyo itashindikana, atahamasisha na kusimamia migongo nchi nzima hadi kieleweke.
Alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu kutafuta ufumbuzi wa kero za wafanyakazi, hususan kupunguza kiwango kikubwa cha kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi ambayo pia ni midogo kwani haiendani na hali halisi ya maisha.
Alisema kuwa watashughulikia tatizo la mafao madogo yanayotolewa na mifuko ya jamii kwa wafanyakazi wanaostaafu hali inayowafanya waishi maisha ya mateso baada ya kumaliza utumishi.
Aidha katibu huyo alisema watapigania mabadiliko ya Katiba ili iweze kuwanufaisha zaidi wafanyakazi.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha wajumbe kutoka vyama 13 vya wafanyakazi hapa nchini, Omary Juma alifanikiwa kutetea nafasi yake ya urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi huo uliokuwa na kila aina ya ushindani ambao ulilazimika kwisha usiku wa manane.
Nafasi ya makamu wa rais wa shirikisho hilo ilichukuliwa na Nortburga Masikini aliyepata kura 180 akimwangusha Dk. Diwani Mrutu aliyepata kura 126.
Nafasi ya naibu katibu mkuu ilichukuliwa na Ezron Kaaya aliyepata kura 212 akiwaacha kwa mbali Salma Chande aliyepata kura 84 na Mchafu Chakomu kura 39 na James Kalanje alifanikiwa kutetea nafasi yake ya uweka hazina kwa kupata kura 243.
Waliochaguliwa kuwa wadhamini wa Tucta na kura zao kwenye mabano ni Charles Mngodo (76 ) , Rehema Mlongelakweli (84), Cecilia Mpamila( 84) na Clement Mswanyama (71).
Nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya wanawake imekwenda kwa Asia Kapori na katibu wake ni Zainabu Matavale.
Wabunge wa CCM watimuliwa
Katika hatua nyingine wabunge wawili wa viti maalum (CCM), Zainab Kawawa na Angellah Kairuki, wamezuiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa shirikisho hilo kwa vile hawatambuliwi.
Mgaya alisema TUCTA haiwatambui wabunge hao wa viti maalum walioingia bungeni kwa mgongo wa uwakilishi wa shirikisho hilo kwani hawakutoka ndani ya shirikisho hilo.
<hbr />sasa kama shirikisho haliwatambui, waliingiaje mjengoni?
Jibu ni taratibu huwa zinapindishwa kukidhi matakwa ya watu...(we regulate our procedures to suit personalities)sasa kama shirikisho haliwatambui, waliingiaje mjengoni?
sasa kama shirikisho haliwatambui, waliingiaje mjengoni?
Huleeee Mgaya wewe ni AK47 kwenye uchaguzi wa 2015 ila chunga uhai wako maana wanaweza kukukolimba!
Alafu huwa nachoka wabunge wawakilishi wa wafanyakazi hawatambuliwi na TUCTA apo CCM ndo mwaniachaga hoi kwa kuforce Kinga