Mpenzi wako amekusevu kwa jina gani katika simu yake?

1. Darling
2. Dear
3. Sweet heart
4. Jina lake
5. Jina lake la utotoni
6. Jina la mama yake
7 jina lake la ukoo
8. Kimeo
9. *****
10. Mkosi

majina yote ya kinafiki hakuna tofauti na dk"nchimbi"dk "kamala""
itateni majinayenu sio mnakaa weikimbili sweet mnabadilika kuitaana nyoka
 
Ukiona mtu kamsave mkewe au BF/GF jina la ajabu ujue anao wengi so anaogopa gonganisha magari.
Si unajua kuna mabinti ukimtwaa hasa kwa the so called mechi za kirafiki lazima apekue simu huwa wanakera hawa.........ni story tuu........ili apate jina halisi then aanze kuvuruga uhusiano wenu yeye atake chance.
Mi nimemsave jina lake la utotoni
 
Nimeshuhudia mtu kaseviwa kwa jina la Ng'ombe mna girlfriend wake. Jina lake ni bora haya mengine ni kuzinguana tu
 
Kuna shosti wangu mmoja from Kimalawi alikuwa anapenda kuniita Mwachusa since yupo near by mbeya basi anadhani kila mtanzania anatokea mbeya...so nina this another friends of mine mTz akalipenda sana hilo jina (mwachusa)...kumbe akaenda ku save kwenye simu yake jina langu as mwachusa...Kuna siku mama yake shosti wangu akaja kutoka africa...nikawa napiga simu hapokei kumbe alikuwa nayo her mama...so mama akawa hapokei since hamjui huyo mwachusa....siku moja akamwambia shosti wangu kuwa kuna mtu anaitwa mwachusa anakupigia sana simu na haachi msg...wacha binti acheke akasema huyu Binti maringo!....jamani siku zote hata sikujua kama jina langu limekuwa saved kwenye simu yake as Mwachusa jamani what a name is that kwa kweli....
 
Nikawa napekua cm ya gf wangu alikuwa kani save kama ATM nikamsubiri atoke maliwatoni nikamaliza haja yangu nilimtimua sikutaka maongezi nae tena.
 
Mtu jina lake linaandikwa kama lilivyo tena na la baba yake kabisa kumtofautisha na wengine wenye jinakama hilo. Hakuna vyeo kwenye simu yangu, kwani ni simu ya shirika? Maswali ya mbona mbona sitaki, hivyo vyeo feki tuitane mdomoni
 
Sijamsave kbs.no yake ipwa kwenye my memory ikiita nakukuruka nayo tu najua ni yy.lkn yy kanisave American Lady.
 
Kabla sijamuoa nilisave jina lake tu "Jane", sikumoja nikawa naitafuta namba yake kwa jina hilo sikuipata kumbe alikwisha zi hack kimya kimya simu zangu na kujisave "Dear Sweetiee!; kwnye simu ya pili pia akajisave "Honey" na ya tatu "Lovely Wife 2be".......Nilipouliza kwa nini amefanya vile akanijibu eti "nitamtofautishaje yeye na akina Jane wangu wengine wa Tandale Uzuri, kwa Mfuga mbwa huko au wa kwa Mtogole???.. Hakanionya kama nitabadilisha basi atajua simpendi kabisa na sina nia ya kumwona yeye.

Afanaleki, fisrt day tu ya ndoa tupo "honey moon" kakorokocha tena simu zote, ya kwanza kajisave "lovely wife", ya pili "my heart" hii ya tatua akaweka "my darl"....Nikaja nikacheka tu "sikumuuliza akaniambia usibadilishe hivyo nilivyo save" .


Four yrs ya maisha sasa, nakumbuka siku moja tumegombana akachukua simu zangu nikiwa nje akabadilisha " akajisave" (Jane, ya pili "Wife"na ya tatu "Mama Joto (jina la mtoto wetu)
Nilipoingia ndani akamaka "sitaki uniiite tena "dear, darling wala honey,niite jina walilonipa wazazi wangu (Jane) au ukishindwa "mama Joto" na kwenye simu zako zote nimebadili" manake sioni kama una mapenzi ya kweli na mimi, naona kama najipendekeza kwako tu...(hasira kali). Nikacheka tu moyoni.

Baada ya siku kadhaaa, mambo yametulia tunakwenda sawa, naangalia simu nakuta amerejesha vibwagizo vile vile alivyobalisha. Nikamuuliza vipi, akasema "Loooh, wenzangu, unaweza kuweka "darling wako mwingine humo kwenye simu ukipata tatizo au ajali apigiwe yeye na mimi mkeo kipenzi nije kuadhirika bure, niwe wa mwisho kuja kwenye tukio!".....Nikamuuliza kwani mimi umeni save kama nani akajibu "we tena, loh, "karibu kila siku nakubadilishaga "Leo my husband" jana niliweka " my dearest mume wangu" wiki iliyopita ilikuwa "Swetiee mupenzi" .......

Kudadadeki, simu za kiganjani hizi bana!takusave vyovyote utakavyo lakini "mzigo" unatoka kama kawaida kwa wale aliowasave "GS - MABIBO SALOON", MAMA GATI, SHAMILA WA MIKOCHENI, ABUU WA CHAKULA CHA MBWA, SUZY-MSICHANA WA KAZI, DOREN -CBE nk nk

Huyu wa kwako alikuwa kiboko hahaha
 
Back
Top Bottom