Mpenzi wako amekusevu kwa jina gani katika simu yake?

Mpenzi wako amekusevu kwa jina gani katika simu yake?

1. Darling
2. Dear
3. Sweet heart
4. Jina lake
5. Jina lake la utotoni
6. Jina la mama yake
7 jina lake la ukoo
8. Kimeo
9. *****
10. Mkosi

Mimi nimemsave kama "My Missed Always" na kwenye simu nyingine nimemsave kama "My Only One Forever"
 
unanikumbusha cku moja mdogo wa frnd wangu alitoka kwa bfrnd wake akaja hapo kwa sis waee akilia sana, sis wake akamuuliza kulikoni? akasema alikuwa anapekuwa cm ya fulani kuangalia kam save kwa jina gani mana akiangalia jina lake halioni ikabidi ajical cm yake inaita na bfrnd kam save kama "bwana shamba"...yaani mwenze2 analia cc tulikaukia kucheka.....nimesave " husband" na yeye ka save "wife"

Kuna mtu aliomba simu ya rafikiye mpigie demu wake akakuta rafiki kam-save yule demu kama KIFANYIO
 
mimi na uzee wangu wote huu bado nimemsevu bibi yenu...my life time partner
 
The most beatiful woman,baby,darlin,wife and soulmate. Amen.

Kabla sijamuoa nilisave jina lake tu "Jane", sikumoja nikawa naitafuta namba yake kwa jina hilo sikuipata kumbe alikwisha zi hack kimya kimya simu zangu na kujisave "Dear Sweetiee!; kwnye simu ya pili pia akajisave "Honey" na ya tatu "Lovely Wife 2be".......Nilipouliza kwa nini amefanya vile akanijibu eti "nitamtofautishaje yeye na akina Jane wangu wengine wa Tandale Uzuri, kwa Mfuga mbwa huko au wa kwa Mtogole???.. Hakanionya kama nitabadilisha basi atajua simpendi kabisa na sina nia ya kumwona yeye.

Afanaleki, fisrt day tu ya ndoa tupo "honey moon" kakorokocha tena simu zote, ya kwanza kajisave "lovely wife", ya pili "my heart" hii ya tatua akaweka "my darl"....Nikaja nikacheka tu "sikumuuliza akaniambia usibadilishe hivyo nilivyo save" .


Four yrs ya maisha sasa, nakumbuka siku moja tumegombana akachukua simu zangu nikiwa nje akabadilisha " akajisave" (Jane, ya pili "Wife"na ya tatu "Mama Joto (jina la mtoto wetu)

Nilipoingia ndani akamaka "sitaki uniiite tena "dear, darling wala honey,niite jina walilonipa wazazi wangu (Jane) au ukishindwa "mama Joto" na kwenye simu zako zote nimebadili" manake sioni kama una mapenzi ya kweli na mimi, naona kama najipendekeza kwako tu...(hasira kali). Nikacheka tu moyoni.

Baada ya siku kadhaaa, mambo yametulia tunakwenda sawa, naangalia simu nakuta amerejesha vibwagizo vile vile alivyobalisha.

Nikamuuliza vipi, akasema "Loooh, wenzangu, unaweza kuweka "darling wako mwingine humo kwenye simu ukipata tatizo au ajali apigiwe yeye na mimi mkeo kipenzi nije kuadhirika bure, niwe wa mwisho kuja kwenye tukio!".

Nikamuuliza kwani mimi umeni save kama nani akajibu "we tena, loh, "karibu kila siku nakubadilishaga "Leo my husband" jana niliweka " my dearest mume wangu" wiki iliyopita ilikuwa "Swetiee mupenzi"

Kudadadeki, simu za kiganjani hizi bana!takusave vyovyote utakavyo lakini "mzigo" unatoka kama kawaida kwa wale aliowasave "GS - MABIBO SALOON", MAMA GATI, SHAMILA WA MIKOCHENI, ABUU WA CHAKULA CHA MBWA, SUZY-MSICHANA WA KAZI, DOREN -CBE nk nk
 
Interesting thread, Nimemsave Princess, yeye kanisave mobali na ngai.
 
Back
Top Bottom