Nini utafanya mke wako akimpa jina la ex wake mtoto wenu?

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Habari wa JF.

Hiki kisa ni cha kweli kilitokea huko Ulaya au USA nafikili.

Walikuwa mke na mume na mtoto wao wa kiume. Siku moja walitoa kwenda shopping yeye na mkewe.

Walipofika wakakutana na rafiki ya mke wake, mke wake akamwambia rafiki yake kuwa nina mtoto wa kiume, rafiki nae akamuuliza jina lake nani,
Mke akamtajia, rafiki akashituka na kumwambia mbona kama jina la ex boy friend wako wa high school.

Mume alishituka kidogo, na kumwangalia mkewe usoni. Jamaa alisema alijisikia kusalitiwa sana na mkewe wake. Baada ya kuongea nae sana na mke wake na yeye kufuatilia akaja kujua ex boy friend wake alikuwa black ila yeye na mkewe ni mzungu, kwahio mtoto ni wake ila shida ni jina.

Jamaa alisema jina la mtoto wao ni complicated kidogo. Ila ni jina la ex boy Friend wa mkewe. Alimuuliza mkewe kuwa kama ningerikuwa na mtoto wa kike nikampa jina la ex wangu wewe ungefanya nini? Mkewe alikuwa anamwangalia tu.

Kwa sasa wameachana.

Ungekuwa wewe ungechukua uhamuzi gani? Hasa kama umezaa na mkeo watoto 2 wa kwanza ni KE na wa pili ni ME.

Ukute mkeo mtoto wa kike kamuita jina la dada wa ex wake na mtoto wa kiume kaita jina la ex wake, kama mwanaume utafanya nini?

Najua cha kwanza ni kuhakikisha kama watoto ni wako.

La pili utafanya nini?
 
Dada zetu huku utashtuka tu sababu majina yenyewe changamoto. Mtu ana x anaitwa izzo wa kitaa kazi yao ilikuwa kuvuta shisha pamoja hata jina la mzazi wake halijui.
 
Back
Top Bottom