Mkuu kwa hiyo kina Hassanoo na wenzie kina Fazhaldin,kimwanga,Mlai, na Mwanga upepelezi wao haujakamilika?
Mbona unamtisha mleta mada?kichwa cha habari mbona hakiendi moja kwa moja na maada husika mtoa uzi tunaomba uzi uchanganue huyo mpemba kamponza vp DCI
Sema unamfahamu .....ukisema unamjua manake ulilala nae. .hujui kiswahili ww!
Mimi bado nipo na hoja ya MsemajiUkweli kuhusu Home shopping ambayo ni GSM
GSM inafanya kazi bega kwa bega na mkuu wa mkoa katika miradi kadhaa
Kuna ujenzi wa jengo la dini ambalo mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na kampuni ya GSM ambayo msemajiukweli amesema in 'uchafu' kwa jina la zamani, wanuendeleza.
Ikumbukwe hili ni Jengo la waumini na linatakiwa lisiwe na shaka juu yake.
Leo Mkuu wa Mkoa kaongoza kampeni kwa kutumia GSM.
Pili, kuna ujenzi wa wodi za hospitali ambapo GSM wanashirikiana na mkuu wa mkoa . Makamu wa Rais naye akajikuta anashirikiana na GSM na hatimaye serikali nzima
Kuna kila sababu za kuhoji mahusiano ya mkuu wa mkoa na GSM ! hawa GSM wana interst gani na serikali?
Tunajua awamu iliyopita HSC waliiweka'mikononi' kwa kila hali, je, hili ndilo linataka kutokea tena?
Mkuu wa Mkoa ana la kueleza umma na safari hii hatudhani anapaswa kuachwa kama lile aliloagiza wananchi watwangwe na Polisi yeye atajibu
Hili linaenda mbali na kugusu uadilifu wa serikali hii! Mkuu wa mkoa ameweka uadilifu wa serikali katika kupambana na maovu katika mashaka makubwa!
Tunapaswa tuelezwe uhusiano wa Serikali ya Magufuli na GSM kupitia mkuu wa mkoa
Siyo maneno yangu, msemajiukweli kasema Homeshopping ndio wamebadili jina na sasa wanaitwa GSM.Sasa HSC itakuwaje GSM?
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
. Noma sanaWenyewe wanajitetea, eti uandishi wa MWENDOKASI
unachokiandika huku nikwaajili ya watu na watu wenyewe ndosisi!! Andika vizuri heading ibebe kilichomo ndani sio unaandika kama magazeti ya makorokocho...kubali kukosolewa jamaaSasa ulitaka niweke maoni yako?
Kwani wewe umebadilika?
Hii ni thread yangu na nina haki ya kuandika chochote kama sivunji taratibu na sheria za Jamiiforums.
Kama unadhani hakuna lolote unaloweza kuchagia katika maoni yangu, ungesoma na kuondoka tu.
Jamiiforums has no room for dictatorial mentality.
Huwajui wabongo...akikuuliza usidhani hajakuelewa hapo ndiyo anakupoteza...anajua yoteMbongo ukishaweka kitu kwenye maandishi baasi umewaua. Juzi kuna chief accountant nimemtumia instructions zimeandikwa kila kitu in a simple way. Kasoma lkn bado kapiga simu anaulizia yaleyale yaliyoandikwa.
Kama humfahamu mtu anayejulikana kama ''mpemba'', ingia kwenye mtandao ya NGO zinazopambana na vita vya ujangili wa nyara za serikali au subiri kesi ya ''Malkia wa pembe za ndovu''.
Ukitaka kumfahamu ''mpemba'' pitia hii thread;
Katibu wa zamani wa Simba Hasonoo kortini kwa wizi wa pembe za ndovu
Watanzania wengi ni wagumu sana kubadilika!
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kila siku anawambia wabadilike kwa sababu zama zimebadilika lakini wameziba masikio na hawataki kubadilika.
Ndugu yangu Diwani Athumani alikuwa anadhani ni zama zileee ambazo unaweza kuweka uzio katika uchunguzi kwa sababu ya cheo chako au ukaribu wako na Ikulu na hakuna wa kuhoji kwa nini unaweka uzio .
Huu sio muda wa kukumbatia mitandao ya kijangili na kifisadi. Zama zimebadilika sana.
Kwa nini baadhi ya watu hawajifunzi kwa Home Shopping Center ambayo baada ya kunusa hatari iliyoko mbele wakaamua kujifilisi kisheria na kuibuka huku wamevaa ngozi nyingine kibiashara inayoitwa GSM Foundation.
Rais Magufuli kila mara anawaambia kama unafahamu ulikuwa unatenda dhambi za kisiasa na kiuchumi. Huu ni muda wa kutubu na kuachana na dhambi hizo.
Vita vya nyara za serikali imemuondoa Diwani Athumani.
Kuna wengine bado wako mbioni kusombwa na mafuriko.