‘’Mpemba’’ amponza DCI, Diwani Athumani

‘’Mpemba’’ amponza DCI, Diwani Athumani

Ahaaaa hapa unatuambia jambo jingine pengine bila kufahamu, au umesahau au unachoma utambi

Hawa GSM si ndio wanaoshirikiana na Mkuu mmoja wa mkoa kujenga Hospitali na si ndio wanaosaidia kujenga jengo la dini moja chini ya mkuu huyo?
Au nitakuwa nimechanganya mambo!!!
MsemajiUkweli inaonekana hana taarifa kwamba vinara wa ufisadi nchi hii ni HSC. Katika awamu iliyopita waliitia TRA hasara ya karibia TZS trilioni Tisa. Lakini pamoja na hayo, akiwa na jina lake la awali la @mwanadiwani,alikuwa mstari wa mbele kutetea viongozi waliokuwa wanakula na HSC. Leo hii anawatetea katika muktadha wa corporate law, inawezekana ni kwa sababu amewajengea ukumbi wao mpya wa mikutano Dodoma, ukumbi uliotumika kumpitisha mgombea wao mwaka jana. HSC anaendelea kuweka viongozi mfukoni, ana fadhili wateule wa Rais muadilifu, anawanunulia magari, anawapa posho za kujikimu, tukishangaa haya kutokea chini ya awamu hii yenye kuchukia ufisadi, MsemajiUkweli anajibu kwamba hayo hayaihusu serikali, ni suala la corporate law. Pengine anaweza kutuelimisha zaidi kuhusu Corporate Law kwa mapana zaidi.

MsemajiUkweli, katika muktadha wa corporate law, Kwanini Kitilya yupo ndani wakati liability yake is limited by shares in a company where hes a director? Corporate law inasemaje hapa. Waziri aliyepitisha dili ni marehemu; CEO wa kampuni ya akina Kitilya ambae ndiye aliyehusika moja kwa moja ni marehemu; CEO wa benki iliyotoa hizi Fedha alikamatwa, akabambikiwa kesi ya uraia na kukimbizwa nje ya nchi kwa amri asirudi tena. Baada ya hapo, kesi ndio ikafunguliwa. Mambo ya ajabu kabisa haya.

Lugumi nae, mnazuia mijadala ya bunge isionekane kisha huko ndani mlipojifungia mnampa mhalifu huyu siku tisini amalize kazi aendelee ili Kula maisha. Wahalifu wa escrow wanakingiwa kifua na awamu hii inayochukia ufisadi, wengine wanapewa na vyeo. MsemajiUkweli, nini kinaendelea kama sio ulaghai?
 
Mbongo ukishaweka kitu kwenye maandishi baasi umewaua. Juzi kuna chief accountant nimemtumia instructions zimeandikwa kila kitu in a simple way. Kasoma lkn bado kapiga simu anaulizia yaleyale yaliyoandikwa.
 
Nilichojifunza hapa. Kabla ya uchaguzi wa 2015, kikundi kilichokua kinajitapa kupinga maovu sasa hivi ndio kina tetea maovu tena kwa nguvu sana.
 
mtoa mada ni mpuuzi square..as if walichofanya home shopping centre ni kitu ethical
 
Mkuu wa Mkoa awakane kwa kosa gani? Unataka awakane kwa hoja za kisiasa ambazo hazina nguzo kisheria?

Nimekupa mfano wa Clinton na Trump kuhusu kodi na kama huwezi kuelewa basi sina cha kuongeza.

Kwa nini akae kimya wakati nchi yetu inaishi katika msingi wa presumption of innocence unaosema, innocent until proven guilty.
Hao wanaotumbuliwa nani anaprove guilty?
 
Oooh My God
Yaan wewe ndio wale wa Division 5
Kwa Hiyo DDP (Director of Public Prosecutions ) Utasema ni Mktugenzi wa washatakiwaji na Umma
Anataka kujifanya mjuaji matokeo yake kageuka kituko. Hawa ndio kwenye usafiri wa umma wanapiga sana kelele wakichangia kila mada, kumbe hawajui lolote.
 
Mleta mada Huenda amekuta habari inaishilizia kwenye vijiwe vya kahawa, na Yeye akachukua alichoambulia akaleta. Pia NDIYO ELIMU ambayo CCM imetuchagulia watanzania
Hamna haja ya kushambulia mleta maada, mleta maada ni msomi anayejua madhara ya kutaja majina ya watu na hasa katiza zama hizi za makosa ya kwenye mitandao, kafumba lakini kafumbua sasa fumbo mfumbie mjinga wajanja tumeshang'amua Mpemba ni nani kupitia hiyo link aliyoiweka. Asasa kama meno huna ujue mfupa umeshakushinda.
 
Mbona kamutaja kuwa ni Hassanoo, katibu wa zamani wa Simba. Na kuwa alifikishwa mahakama ya Kisutu mwaka 2012 kwa kesi ya kuuza meno ya tembo Hongkong ya thamani ya zaidi ya billion 1 ya Tshs. Kesi hiyo hadi sasa upelelezi haujaisha na Mpemba anaendelea na biashara yake ya meno.

Muwe mnasoma vizuri thread za watalaamu. Huwa hawasemi direct.
Tatizo wengine wanataka watafuniwe kila kitu.
 
Mkuu kwa hiyo kina Hassanoo na wenzie kina Fazhaldin,kimwanga,Mlai, na Mwanga upepelezi wao haujakamilika?
 
MsemajiUkweli hapa hukusema ukweli.

Kichwa na utumbo wa habari ni vitu tofauti kabisa.

Hassanoo na upemba wapi na wapi, tuulize wa Kariakoo tunaemjuwa toka walipohamia na baba'ke akiwa mdogo kutokea Mafia pale mtaa wa mvita kwa Binti Athumani.
Tupe picha yake basi.
 
MsemajiUkweli hapa hukusema ukweli.

Kichwa na utumbo wa habari ni vitu tofauti kabisa.

Hassanoo na upemba wapi na wapi, tuulize wa Kariakoo tunaemjuwa toka walipohamia na baba'ke akiwa mdogo kutokea Mafia pale mtaa wa mvita kwa Binti Athumani.
Sema unamfahamu .....ukisema unamjua manake ulilala nae. .hujui kiswahili ww!
 
Mimi siju kazi za DCI ila kwa system ya Tanzania, cheo chake kinatosha kukwamisha utendaji wa Watendaji wa Wanyamapori. Mi nampongeza JPM kama kweli huyu jamaa anahusika. Bado tu kwenye kubana wafanyakazi, dah baba, tutakufa njaa.
 
Tamko la kurugenzi ya ikulu linasema Rais ametengua uteuzi wa Athman Diwani na kwamba atapangiwa kazi nyingine. Kwanini apangiwe kazi nyingine na siyo kuchukuliwa hatua kali kama kuachishwa kazi kabisa au kushtakiwa kama kweli tuhuma dhidi yake ni za kweli.
 
Back
Top Bottom