CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,361
- 6,441
Hakuna ubishi kwamba chadema ndio chama kikuu cha upinzani angalau kwa sasa nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na cuf ambao nao waliirithi kutoka kwa NCCR-MAGEUZI ile ya Mrema na Marando ambae kwa sasa yuko chadema huku Mrema yeye akiwa na chama "chake" siku hizi.
Lakini katika hali ya kusikitisha taarifa kutoka chanzo cha kuaminika(mshauri mkuu wa chadema)zinaeleza kwamba ndani ya chedema kuna mpasuka mkubwa kuhusu nani anapswa kuandaliwa kugombea urai kati ya mwenyekiti mbowe na katibu dr slaa.Ama hakika hii si habari njema sana kwa wapenda demokrasia na mabadiliko kiujumla.
Ushauri wangu ili kunusuru hali hii ya mpasuko isizidi kusambaa,Mbowe na slaa wake pembeni,hii itawavunja nguvu wapambe wao,watakuwa hawana tena kinachowatofautisha na pia itwapa muda mzuri mwenyekiti na katibu wake kushiriki mchakato huru wa kuitafutia chadema mgombea akaekidhi matarajio ya chama hicho ambayo siamini kama ni just kuwwa chama kikuu cha upinzani tu.
Mi naanza kuonyesha njia,majina haya sita kati yao anaweza kuipeperusha vyema bendera ya chadema kwenye urais.
1:Kitila Mkumbo(dr)
2:Zitto Kabwe
3:Halima Mdee
4:Abdallah Safari(prof)
5:Godbless Lema
6:Tundu Lisu
Nawasilisha.
Huu sio mpasuko hata kidogo! Ni mawazo tofauti ya wadau wa CDM. Mwishowe atapatiakna mmoja. Ukiona hakuna anayetoa wazo tofauti, hapo kuna walakiniand most probably kuna elements za kukosa demokrasia. Watu lazima watofautiane katika mawazo, ila at the end wanafikia uamuzi wa wengi.
Na hiyo list yako, sidhani kama kunamtu ana ushawishi mkubwa kama Slaa alivyo. Kitila ni nani, watanzania wangapi wanamfahamu jamani!!! na wengine humo katika list yako