Mpambano mkali kituo cha Polisi Nzega stendi kati ya Abiria na Polisi

Mimi sasa hivi natafuta tu connection za wakubwa. Nmeshapata mmoja. Siku polisi wakinidaka watajua hawajui.
 
Lichukue kama case study, take it positive, kuna kitu cha kujifunza hapa. Tuvumiliane.

hakuna kitu hapa,wale jamaa wenye upuuzi shuleni ndio hawa hawa wwamekuwa wababa nowadays.

wamegoma kabisa kubadilika.
 
Walikiri kabisa walikuwa sahihi, na mimi niliona. Sema hatuwezi kutatua kila kitu kwa sheria, hekima ni mhimu. Unamchukua dereva, unawaacha abiria bila kuwataarifu, wana njaa, wamechoka na kibaya zaidi, hao ndio wanakulipa. inabidi ufikirie pande zote, utoe maamuzi sahihi.
Hapo unakuta kwenye bus kuna watoto. Askari hawana utu
 
View attachment 1967570
Wanabodi

Natumai mungu ni mwema kwa kila mmoja kwa kupata zawadi ya uhai.

Muhtasari wa habari.

Moja kwa moja kwenye mada. Mnamo tarehe 5/10/2021 nikiwa natoka Arusha kuelekea mwanza na basi la kiazi kitamu ulizuka msuguano mkali kituoni cha polisi Nzega stendi.

Polisi walimshusha dereva kwenye gari kimya kimya wakampandisha kwenye difender hadi kituo cha Polisi central. Abiria baada ya kutomuona dreva, tukaenda kituoni kuhoji, askari wa zamu anasema dereva kasnikwa, kapelekwa central, moto ukawaka, abiria tunamtaka dereva.

Habari kamili.

Safari kutoka arusha ilianza saa 11:57 alfajiri stendi ya mabasi ya kwenda mikoani. Gari baada ya kukaguliwa lilitoka. Baada ya masaa matatu, tulifika stendi ya babati mkoani manyara, trafiki polisi walikagua gari tena, wakakumbusha abiria kufunga mkanda, kama baada ya dakika 20 tangu kutoka stendi ya babati gari likaanza kutoa harufu kana kwamba matairi yanaungua kumbe ni clutch plate inaungua na imeisha. Gari likasimama likashindwa kwenda, abiria tusijue hili wala lile safari imesimama, konda akasema abiria tunaomba mvumilie, dreva ameenda kuchukua maziwa, kumbe ni fiksi, abiria wakamwambiia usitufanye watoto wadogo, gari ni mbovu, clutch plate iimeungua, gia haziingi, hakuna maziwa wala nini. Dereva akomba radhi akasema gari limeharibika.

Ilikua karibu saa 3:45 asubuhi, wakajaribu kutengeneza hadi saa tano kamili, gari likawashinda. Wakapiga simu, fundi akatokea Kateshi, akafika saa sita kasoro kama dakika 5 akiwa na clutch plate mpya. Utengenezaji ukaanza rasmi, baada ya masaa 3, karibia saa 9 na nusu mchana, gari likatengamaa.

Safari ikaanza, kwakweli tulikua tumechelewa sana, kwa wastani safari ya Arusha-Mwanza ni kwamba ukitoka saa 12 alfariji ukichelewa njiani basi saa 12 jioni unakua umefika mwanza.

Dreva alijitahidi kupiga gia, tuliingia mkoa wa Tabora, wilaya ya Nzega, Nzega stendi saa mbili kama na robo usiku. Wakati tunaelekea stendi tuliipita gari ya polisi, Toyota Hilux double cabin, kumbe ilikua ni gari yya RPC. RPC akapiga simu gari ishikwe stendi hapo Nzega kwasababu dereva yuko na mwendo mkali, kaipita gari yake wakati yeye RPC yuko kwenye themanini akutegemea apitwe na basi.

Bana kumbe dere alipoingia stendi, wakashuka kama kuchimba dawa, trafiki polisi wa zamu/sajenti, akamshika, akamuweka chini ya ulinzi, patrol defenda ikafika, ikamchukua mpaka central ya Tabora usiku huo. Abiria tulitangaziwa, chimbeni dawa jamani, chukueni chakula, tukitoka hapa hatusimami popote. ilipopita nusu saa safari haianzi, ndipo abiria mmoja akasema, wakati ameenda haja, ameona dereva kapakiwa kwenye difenda, abiria tukachachamaa.

TUKAENDA WOTE KITUO CHA POLISI HAPO STENDI

Sajenti, dereva yuko wapi? Ameshikwa kwa amri ya RPC na kapelekwa central. Abirira wakamuuliza, tunaendeleaje na safari? Akajibu, dereva mwingine yupo, awapeleke. Abiria wakahoji, dereva mwingine yuko wapi? Na, kwanini umchukkue dereva bila kututaarifu? Inakuaje unafanya kazi katika hali ya ajabu namna hii? Aaaya , tupe dereva uyo wa pili atupeleke. Afande kimya. Abiria, sisi tumetoka Chuga na dereva mmoja na huyo pekee ndiye tunaye.

Kama hoja ni overspeed, mbona gari nyingi zina-overspeed? Abiria wanamhoji sajenti, sajenti kimya. Abiria na connection zetu tuakapiga simu usalama wa taifa, kwa IGP na media kadhaa na kwa RTO mkoa wa Tabora. RTO akaja, alipofika, akakutana na wananchi wenye hasira na waliochoka na safari, baada ya kubanwa kwelikweli, ikabidi awe mpole. Akaomba apige simu awasilaine na wakubwa wake, mwishowe aksema, dereva anakuja. Abiria wakafurahi.

Yapata saa sita na dakika tano usiku, dereva akaletwa na difenda, dereva akitabasamu baada ya airia kumtoa ndani huko ambako alikua ameishawekwa. Safari ikaendelea. Wazee wa PGO ziro Abiria 3

MAFUNZO MAKUU KATIKA SAFARI HIZI ZA MIKOANI NNILIYOJIFUNZA

1. Polisi/wazee wa PGO bado wao hawafanyi kazi kwa weledi, wanachukua sana rushwa, magari flani yanazuiwa na magari flani hayazuiwi.

2. Polisi ndio chanzo cha ajali. Arusha wameruhusu gari itoke stendi wakati ina dereva mmoja peke yake, kitu hiki ni kinyume na sheria, inakuaje Tabora ndio wagundue?

3. Wamiliki wa mabasi, baadhi yenu, hakikisheni mnafanyia service vyombo vyenu. Haiwezekani kama hili la liazi kitamu clutch plate iungue namna ile bila kufahamika, tumetoka tabora saa 6 usiku, kufika shinyanga, gari likapiga pancha, tukapoteza muda tena.

4. Raia, simamia sheria, polisi ni waoga sana mkishindana nao kwa hoja na mkiwa na umoja, lolote lile linawezekana.

MWISHO KABISA

Mungu ni mwema, safari ilimalizika saa 9:45 alfajiri tarehe 6/10/2021 kila abiria akiwa salama salmini.

View attachment 1967536
.

View attachment 1967534
Gaidi Mkuu kuna kazi yako huku
 
Hongera kwa Camera nzuri
 
Huyo fundi from Katesh namfahamu sana, mwanangu sana huyu. Anaitwa Gift Lyimo, dogo yupo vizuri sana. But thanks kwa ushirikiano mzuri, nimeelewa kwanini waziri wao alisemaga police waliosoma vizuri au waliofauru mitihani, hawatakiwi huko, reasoning capacity yao ndio hi yaani. Sasa unamkamata dereva halafu umpeleke Tabora mjini, (kwa faida ya wasio fahamu, from Nzega to Tabora ni +160 km ) imagine, sasa najiuliza, hivi RPC alikua anafikiria abiria wangefikaje Mwanza? Yaani unawaadhibu hadi watu wasiokua na HATIA kwasababu tu wewe umepitwa na basi?
 
Back
Top Bottom