Nyie mnafanya mzaha na kuwasusuika wakubwa tu! Nyie mnavaa vya wapi? Acheni hizo! Najua wabongo wengi tuna tabia ya kugeuza kila kitu siasa (si hasa!) Tunachokitetea tunakinyanyapaa inapokuja katika yale tuyafanyayo binafsi. Sifa tu jamvini, lakini najua wengi wa hawa wasemaji ni washabiki wa 'vya nje'. Wangapi tukirudi bongo tunatafuta mavazi ya kitanzania kama yale watengenezayo Afrika Sana pale Sinza?
Hawa jamaa wameshonea hilo joho 'kwa mama' kwa sababu hawajui pengine pa kushone. Hawajui kuwa majoho ya spika, naibu wake na makarani wa bunge la Afrika Mashariki yalisanifiwa (hata kama hayakushonwa) na hao jamaa wa Afrika Sana!
Lakini msisahau pia kwamba kuna suala la maslahi ya kipesa (ufisadi!) kwa yule anayeagiza na anayeagizwa mizigo kama hiyo! Uliza bei yake sasa hilo joho! Mhm, kalagabaho!