Hahaa, tunatajirika tukiendesha magari mtumba toka Japan, nguo toka China, tukiumwa tunaenda India kutibiwa...!Lengo la elimu hiyo ya awali ni kukufanya uwe na welewa wa jumla angalau wa kijuujuu wa mambo ya msingi hapa duniani, katika mazingira yako na hukooo katika malimwengu mengine. Ukitaka kuzama zaidi sasa ndiyo unaanza kujibana katika uwanja wako uliochagua katika shahada ya kwanza, unajibana zaidi katika Masters na unachagua kaeneo kadogo zaidi katika PhD.
Hisabati na hii x unayoilalamikia lengo lake ni kuimarisha uwezo wako wa kufikiri kidhahnia (abstract reasoning). Uwezo huu peke yake ndiyo unamtofautisha binadamu na wanyama wengine wote na ni uwezo wa muhimu sana kwa binadamu. Ndiyo maana karibu dunia nzima wanafunzi ni lazima angalau wafundishwe kidogo kuhusu udhahnia huu kupitia somo la Hisabati ambalo kulingana na akina Albert Einstein ndiyo "lugha ya Mungu!"
Kuhusu utajiri, elimu haina lengo la kumfanya aipataye atajirike. Lengo lake hasa ni kumwonyesha aipataye kuhusu mambo ya msingi katika dunia hii na kumfanya kuyatawala mazingira yake. Ni Afrika tu ambako elimu inaonwa haina faida na eti lengo lake ni kuufikia utajiri. Ukienda Ulaya na Marekani utagundua mapema sana kwamba kumbe profesa anaweza asimiliki hata gari na hategemewi kuwa tajiri. Profesa huyu huyu utamkuta anashinda lab mpaka siku moja anagundua kitu kinachosukuma mbele maarifa na ujuzi wetu hapa duniani. Sisi tumekazana kutajirika, wenzetu wamekazania maarifa na kuhakikisha kuwa kizazi kipya kinaandaliwa sawasawa. Tungeiacha elimu angalau ikafanya lengo lake badala ya kuivika hili joho chafu la ubinafsi na utajiri, pengine ingeweza kutusaidia katika ukombozi wetu. Tunazalisha wasomi wazuri sana lakini wote lengo lao ni kutajirika ndiyo maana haoo wanakimbilia kwenye siasa ili wakafisadike huko na kutajirika. Waafrika tuna matatizo. Hata tunavyofikiri ni matatizo tupu. Inasikitisha!!!
Na kama lengo kuu la elimu ni kutajirika, hakuna hata sababu ya kwenda shule!
Sí angeanza nayeye kwanza kujiajiri tukamuona wa maana.
Asante Himawari. Mdau anataka kila msomi atajirike na kama hajatajirika basi siyo msomi na elimu yake haijamsaidia. Kwa fikra kama hizi tutaendesha magari mtumba ya Japan, nguo toka China na kila siku matajiri wetu (...wasomi) watakuwa wanafia India na kuletwa katika masanduku milele. Wangekuwa wanautumia utajiri wao kwa faida ya jamii kama wanavyofanya akina Bill Gates, Warren Buffet, Zuckerberg na mabilionea wengine wa dunia angalau ningesema wasomi wetu wamefanikiwa. Mafanikio haya ya kujirundikia mali mwisho unafia India unaacha mabilioni yako yakiwa yamezagaa kwenye mabenki yakigawanwa na watoto wako wa kubambikiwa yana faida gani kwa jamii hii masikini? Hili ndilo lengo kuu la elimu? Ubinafsi wa kutisha na hiki ndicho kitambulisho cha mtu mweusi popote alipo hapa duniani. Halafu akina Trump wakitutukana kuwa weusi tuna matatizo hata katika mfumo wetu wa kufikiri tunaanza kulalamika na kuwaita wabaguzi. I say we deserve it!Hahaa, tunatajirika tukiendesha magari mtumba toka Japan, nguo toka China, tukiumwa tunaenda India kutibiwa...!
Ushahidi unagoma,... wasomi bado ni waajiriwa, mostly wa serikali.Entrepreneurs ndo matajiri, ambao mostly wako deep kwenye "knowledge" ambazo zinawasaidia ktk kazi zao moja kwa moja.Hawana mambo mengi kichwani.Niliwah kuwa na mawazo kama yako ndugu na niliipuuza sana Hesabu, ila nilivyoingia chuo nikakutana na TAX na QM lazima usome, na faida zake unaziona nje nje. Ikiwa ulitaka kuikimbia na ukafanikiwa bas ishi na upumbavu wako, usiambukize wanao tu kwani dunia tuliyonayo leo hii matajiri ni wasomi. Kaa hapo ukariri
Ofcourse nmesema sijaipata, which means naendelea kuitafuta.Siku nikiipata uwe na uhakika nitawasaidia wengi ambao pia bado wanaitafuta.Kwani thamani ya "x" ulikuwa ukiipata hivihivi kwa kuiangalia au ulifanya maneuvre kuitafuta. Bro acha kuota, tafuta njia ya kuipata thamani ya x. Cross multiply , gawa, zidisha, jumlisha, toa... utapata thamani ya "x".
Endelea kuingalia tu x ama utafeli mtihani.
Nimependa line 2 za mwisho umeweka na msingi wa Fid Q.Huna pesa huthaminiwi, hata usipokuwepo vikao vya familia vinaendelea... sasa pata pesa uone, hawafanyi kikao mpaka "mukubwa" ufike.
Look around you, kama huna kitu ukipata rafiki umefanikiwa kichizi.
No Trump is selfish himself.Asante Himawari. Mdau anataka kila msomi atajirike na kama hajatajirika basi siyo msomi na elimu yake haijamsaidia. Kwa fikra kama hizi tutaendesha magari mtumba ya Japan, nguo toka China na kila siku matajiri wetu (...wasomi) watakuwa wanafia India na kuletwa katika masanduku milele. Wangekuwa wanautumia utajiri wao kwa faida ya jamii kama wanavyofanya akina Bill Gates, Warren Buffet, Zuckerberg na mabilionea wengine wa dunia angalau ningesema wasomi wetu wamefanikiwa. Mafanikio haya ya kujirundikia mali mwisho unafia India unaacha mabilioni yako yakiwa yamezagaa kwenye mabenki yakigawanwa na watoto wako wa kubambikiwa yana faida gani kwa jamii hii masikini? Hili ndilo lengo kuu la elimu? Ubinafsi wa kutisha na hiki ndicho kitambulisho cha mtu mweusi popote alipo hapa duniani. Halafu akina Trump wakitutukana kuwa weusi tuna matatizo hata katika mfumo wetu wa kufikiri tunaanza kulalamika na kuwaita wabaguzi. I say we deserve it!
True, math's inaongeza thinking capacity. Wasi wasi wangu ni kuwa we're overloading.Mathematics inasaidia kwenye kuongeza thinking capacity... hauwezi kuona tofauti until u know nothing.
Hatimaye nimepata kichwa tunachofikiri sawa.Siongezi wala kupunguza chochote mkuu.Daa nimeipenda mada, kiuhalisia mtoa mada kachokoza watu kujitambua. Kiuhalisia hesabu zote zinamaana katika maisha. Zinakupa uwezo wa kukabiliana na changamoto, mfano wa logarithim unapewa kitabu four-figure kutoa majibu, utumiaji wa kitabu hicho na kufikia jibu inakupa uwezo wa kukabiliana na jambo na kufikia hitimisho kusudiwa.
Kuhusu thamani ya "X" haina jibu moja ila kila mtu anatafuta thamani ya "X" yake, hapa pia haijalishi umesoma au hujasoma ila jinsi unavyoyakabili mazingira yako ndio utaweza fanikisha thamani ya X yako.
Kuhusu kutajirika au la ni namna wewe binafsi unavyojituma na kujitoa mhanga "risk" kwa kile unachofanya, kwa aliyesoma huenda kwa tahadhari sana kwa project aliyoplan japo wakati mwingine huweka woga sana kwa huyu msomi na kukata tamaa, tofauti na asiyesoma huenda tuu mbele kwa mbele akikosa poa akifanikiwa pia kwake poa sana.
Pesa haiepukiki kufikia mafanikio whether ya kitaaluma au ya kijamii, nabaya zaidi mfumo wa elimu yetu hautoi mtu kujitafutia maarifa zaidi ya kuwa wa kutafutiwa maarifa, pili serikali zetu haziwapi nafasi ya kutosha wataalam wetu kuonesha ujizi walionao. Mifano ni mtaalam wa tiba ya Meno au Upasuaji unakuta kapewa wizara ya ulinzi au habari. So kiujumla wewe binafsi una X yako itafute .