Mpaka leo sijaijua thamani ya 'X'

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,133
Tuchukulie mfano unafanyika utafiti leo hii.... ni vitu vingapi tulivyojifunza shule (ya msingi, sekondari O - level na Advance Level) vinatusaidia katika maisha ya kila siku?

Najaribu tu kuwaza kwa sauti... mpaka leo sijawahi kutumia Four Figure, wala logarithm, wala Calculus, wala Quadratic na nimejaribu sana kupata thamani ya X katika maisha... sijaipata.Daah!!

Nimetambua kuwa elimu niliyopata iliniandaa kuajiriwa na serikali na sio kujiajiri.Yaani mfumo mzima wa elimu umetengenezwa kukidhi mahitaji ya serikali na sio kukidhi mahitaji yangu.SMH!!

Hapo ndipo nakubaliana na bwana mmoja aliesema,"Tanzania wenye elimu wapo, lakini kati yao wasomi ni wachache sana" Eee si ndio... asa kumbe nini; watu wana degree zao na haziwasaidii chochote katika maisha.

Hivi: 'Marking scheme' inasaidia kupanua uwezo wa mwanafunzi kufikiri au inabana?
Unakumbuka kibao cha shuleni kwenu... kiliandikwaje?... Elimu ni ufunguo wa maisha / Elimu ni utajiri /Elimu ni urithi wa kweli n.k

Swali ni je, mwalimu masikini anaweza kukupa wewe mbinu za kufanikiwa katika maisha? Au mpaka sasa umeshawahi kufundishwa na walimu matajiri wangapi?

Wasomi wanaishia kuajiriwa na wasiosoma.Wasomi wana elimu sana, wasiosoma wana fedha nyingi.Yaani wale waliokuwa wanapata A darasani huwa wanaishia kuajiriwa na wale waliokuwa vilaza!!! Aisee yaani..Ni nadra sana kumkuta tajiri alieajiriwa.

Baba yako alikwambia soma sana uje kuwa na maisha mazuri,... mimi nasemaje; soma sana nije nikuajiri unisaidie kutafuta thamani ya X.

Let X be valuable papers(Money):p Tumia "Pie" = 3.14!!!

Mimi.. ninashukuru.
 
Ukisoma PCB halafu ukaenda BCom in marketing hautaona maana ya dissection za vyura ulizofanya A level.

Hao ambao hawajasoma halafu wakawa Matajiri,wanahakikisha watoto wao wanasoma kweli kweli.
Watoto wengi wa matajiri wanasoma sana lakini elimu yao haiwasaidii... according to my experience thou
 
Wamesoma wengi ila wanayo elimu ya shule,ambayo inafundisha kuwajibika tu,Ila wengi hawana elimu ya msingi ambayo haipo shuleni IPO kitaaa
 
Haaa... saman ya X unaitumia kila cku.. hata ulichoandika hapo ni saman ya X.. X inakupa nafas ya kufikiria sana.. kama ulivyoweza kufikiria kuandika hvyo vitu ... hii ni sawa na kusema kidole cha kati cha mguu wako hakina faida... sasa ebu siku kikatike ndio utajua....
 
Unaipata mara nyingi tu sema shida yako ni kutoitambua. Ukijua purpose/ goal ya wewe kufundishwa hiyo equation na equations nyingine nyingi utaona zinavyokusaidia kwenye maisha.
Tunasoma masomo 9 boss!! Na mitaala yetu ilivyo.. ni ngumu sana kufaidika na kile unachosoma.
 
Haaa... saman ya X unaitumia kila cku.. hata ulichoandika hapo ni saman ya X.. X inakupa nafas ya kufikiria sana.. kama ulivyoweza kufikiria kuandika hvyo vitu ... hii ni sawa na kusema kidole cha kati cha mguu wako hakina faida... sasa ebu siku kikatike ndio utajua....
Thamani ya X ni mafanikio, ambayo nilitarajia kuyapata kutokana na kusoma kwa bidii.Kiuhalisia nimegundua thamani ya X haipatikani kwa kusoma sana.
 
Acha unafiki mzee, nani alikwambia mafanikio ni PESA?? Unaesema elimu haina msaada mbona hata wanao utawapeleka shule tena za gharama wapate elimu hiyo hiyo? Elimu haipo kwa ajili ya kukupa hela na hakna ilipoandikwa kwamba education is MONEY. Tafakari upya
 
Lengo la elimu hiyo ya awali ni kukufanya uwe na welewa wa jumla angalau wa kijuujuu wa mambo ya msingi hapa duniani, katika mazingira yako na hukooo katika malimwengu mengine. Ukitaka kuzama zaidi sasa ndiyo unaanza kujibana katika uwanja wako uliochagua katika shahada ya kwanza, unajibana zaidi katika Masters na unachagua kaeneo kadogo zaidi katika PhD.

Hisabati na hii x unayoilalamikia lengo lake ni kuimarisha uwezo wako wa kufikiri kidhahnia (abstract reasoning). Uwezo huu peke yake ndiyo unamtofautisha binadamu na wanyama wengine wote na ni uwezo wa muhimu sana kwa binadamu. Ndiyo maana karibu dunia nzima wanafunzi ni lazima angalau wafundishwe kidogo kuhusu udhahnia huu kupitia somo la Hisabati ambalo kulingana na akina Albert Einstein ndiyo "lugha ya Mungu!"

Kuhusu utajiri, elimu haina lengo la kumfanya aipataye atajirike. Lengo lake hasa ni kumwonyesha aipataye kuhusu mambo ya msingi katika dunia hii na kumfanya kuyatawala mazingira yake. Ni Afrika tu ambako elimu inaonwa haina faida na eti lengo lake ni kuufikia utajiri. Ukienda Ulaya na Marekani utagundua mapema sana kwamba kumbe profesa anaweza asimiliki hata gari na hategemewi kuwa tajiri. Profesa huyu huyu utamkuta anashinda lab mpaka siku moja anagundua kitu kinachosukuma mbele maarifa na ujuzi wetu hapa duniani. Sisi tumekazana kutajirika, wenzetu wamekazania maarifa na kuhakikisha kuwa kizazi kipya kinaandaliwa sawasawa. Tungeiacha elimu angalau ikafanya lengo lake badala ya kuivika hili joho chafu la ubinafsi na utajiri, pengine ingeweza kutusaidia katika ukombozi wetu. Tunazalisha wasomi wazuri sana lakini wote lengo lao ni kutajirika ndiyo maana haoo wanakimbilia kwenye siasa ili wakafisadike huko na kutajirika. Waafrika tuna matatizo. Hata tunavyofikiri ni matatizo tupu. Inasikitisha!!!

Na kama lengo kuu la elimu ni kutajirika, hakuna hata sababu ya kwenda shule!
 
Tuchukulie mfano unafanyika utafiti leo hii.... ni vitu vingapi tulivyojifunza shule (ya msingi, sekondari O - level na Advance Level) vinatusaidia katika maisha ya kila siku?

Najaribu tu kuwaza kwa sauti... mpaka leo sijawahi kutumia Four Figure, wala logarithm, wala Calculus, wala Quadratic na nimejaribu sana kupata thamani ya X katika maisha... sijaipata.Daah!!

Nimetambua kuwa elimu niliyopata iliniandaa kuajiriwa na serikali na sio kujiajiri.Yaani mfumo mzima wa elimu umetengenezwa kukidhi mahitaji ya serikali na sio kukidhi mahitaji yangu.SMH!!

Hapo ndipo nakubaliana na bwana mmoja aliesema,"Tanzania wenye elimu wapo, lakini kati yao wasomi ni wachache sana" Eee si ndio... asa kumbe nini; watu wana degree zao na haziwasaidii chochote katika maisha.

Hivi: 'Marking scheme' inasaidia kupanua uwezo wa mwanafunzi kufikiri au inabana?
Unakumbuka kibao cha shuleni kwenu... kiliandikwaje?... Elimu ni ufunguo wa maisha / Elimu ni utajiri /Elimu ni urithi wa kweli n.k

Swali ni je, mwalimu masikini anaweza kukupa wewe mbinu za kufanikiwa katika maisha? Au mpaka sasa umeshawahi kufundishwa na walimu matajiri wangapi?

Wasomi wanaishia kuajiriwa na wasiosoma.Wasomi wana elimu sana, wasiosoma wana fedha nyingi.Yaani wale waliokuwa wanapata A darasani huwa wanaishia kuajiriwa na wale waliokuwa vilaza!!! Aisee yaani..Ni nadra sana kumkuta tajiri alieajiriwa.

Baba yako alikwambia soma sana uje kuwa na maisha mazuri,... mimi nasemaje; soma sana nije nikuajiri unisaidie kutafuta thamani ya X.

Let X be valuable papers(Money):p Tumia "Pie" = 3.14!!!

Mimi.. ninashukuru.
Utoto huu .
Hakuna hesabu hata moja isokuwa na matumizi .au faida
 
Mkuu inaelekea umejitafsiri elimu kama njia ya kupata pesa tu, jiulize pesa ni nini? pesa vipande vya sarafu au karatasi vinavyotumika kama njia ya kubadilishana huduma na bidhaa tu, pesa sio maendeleo, maendeleo ni kuboreka kwa hizo huduma na bidhaa tunazobadilishiana kwa kutumia fedha, so elimu inatakiwa imfanye mtu kuboresha huduma na bidhaa hizo, na fedha ni matokeo tu
Topic yako ingejikita kwenye kwa nini wasomi wa Tanzania na Afrika kiujumla tumeshindwa kutumia elimu yetu kuboresha huduma na bidhaa tunazozalisha badala yake tunaagiza kutoka nje miaka nenda rudi, sio kusema kwa nini tumesoma halafu hatupati hela... utaonekana kama elimu haijakusaidia

elimu hasa Sayansi nadhani lengo lake primarily sio kumfanya mtu atajirike, bali kumuwezesha mwanadamu kuishi comfortable zaidi kwa kuya master mazingira yake na kutajirika ni matokeo yake ya pili kwa watakao tumia elimu hiyo kutoa service ambazo watu watazilipia
 
Acha unafiki mzee, nani alikwambia mafanikio ni PESA?? Unaesema elimu haina msaada mbona hata wanao utawapeleka shule tena za gharama wapate elimu hiyo hiyo? Elimu haipo kwa ajili ya kukupa hela na hakna ilipoandikwa kwamba education is MONEY. Tafakari upya
Hujasema unasoma ili iweje kwa hiyo? Usiogope kuukubali ukweli kuwa... tunaposema mtu ana mafanikio kwa vyovyote vile hata ukwepe vipi lazima pesa ihusike.
 
Lengo la elimu hiyo ya awali ni kukufanya uwe na welewa wa jumla angalau wa kijuujuu wa mambo ya msingi hapa duniani, katika mazingira yako na hukooo katika malimwengu mengine. Ukitaka kuzama zaidi sasa ndiyo unaanza kujibana katika uwanja wako uliochagua katika shahada ya kwanza, unajibana zaidi katika Masters na unachagua kaeneo kadogo zaidi katika PhD.

Hisabati na hii x unayoilalamikia lengo lake ni kuimarisha uwezo wako wa kufikiri kidhahnia (abstract reasoning). Uwezo huu peke yake ndiyo unamtofautisha binadamu na wanyama wengine wote na ni uwezo wa muhimu sana kwa binadamu. Ndiyo maana karibu dunia nzima wanafunzi ni lazima angalau wafundishwe kidogo kuhusu udhahnia huu kupitia somo la Hisabati ambalo kulingana na akina Albert Einstein ndiyo "lugha ya Mungu!"

Kuhusu utajiri, elimu haina lengo la kumfanya aipataye atajirike. Lengo lake hasa ni kumwonyesha aipataye kuhusu mambo ya msingi katika dunia hii na kumfanya kuyatawala mazingira yake. Ni Afrika tu ambako elimu inaonwa haina faida na eti lengo lake ni kuufikia utajiri. Ukienda Ulaya na Marekani utagundua mapema sana kwamba kumbe profesa anaweza asimiliki hata gari na hategemewi kuwa tajiri. Profesa huyu huyu utamkuta anashinda lab mpaka siku moja anagundua kitu kinachosukuma mbele maarifa na ujuzi wetu hapa duniani. Sisi tumekazana kutajirika, wenzetu wamekazania maarifa na kuhakikisha kuwa kizazi kipya kinaandaliwa sawasawa. Tungeiacha elimu angalau ikafanya lengo lake badala ya kuivika hili joho chafu la ubinafsi na utajiri, pengine ingeweza kutusaidia katika ukombozi wetu. Tunazalisha wasomi wazuri sana lakini wote lengo lao ni kutajirika ndiyo maana haoo wanakimbilia kwenye siasa ili wakafisadike huko na kutajirika. Waafrika tuna matatizo. Hata tunavyofikiri ni matatizo tupu. Inasikitisha!!!

Na kama lengo kuu la elimu ni kutajirika, hakuna hata sababu ya kwenda shule!
Kwanini nisome kitu ambacho sitakuja kukitumia maishani?

Mimi nadhani elimu inapaswa kunisaidia kuishi... haina maana nikiwa nina masters halafu siwezi hata ku-afford kujenga nyumba ya kuishi!!!

Niambie tafsiri yako ya mafanikio ni ipi.
 
Back
Top Bottom