Wewe unadai elimu haisadii ila umetolea mfano kutafuta thamani ya X ambayo ni topic moja ya hesabu basic maths ya Algebra!!!!??
Mbona hukuizungumzia elimu yoote unazungumzia topic moja ya hesabu!!
Ila Algebra mbona ina application nyingi tu mkuu labda nikupe mfano simple tu, umekopa hela benki ukafanyie biashara inayokadiriwa kukupa mapato flani kwa mwaka ni lazima ujue riba itakuwa kiasi gani, rate ya marejesho kiasi gani na uncertainty ya business yako , haya yote ni algebra itakusaidia,
pia production za simple kama kukadiria labda mahindi kiasi fulani zitazalisha mifuko mingapi ya unga, kwa kutumia unit ngapi za umeme na kwa muda gani, na faida gani, algebra pia,
kujua nitalima heka ngapi za shamba ili trekta nililokodisha lisinipe hasara utatumia algerbra pia,
kujua mtaji wangu wa kufugia kuku niutumie kiasi gani kwenye kununua vifaranga na kiasi gani kwenye kujenga banda na kuzilisha ili usijikute umeanza na kuku wengi kuliko mtaji pia utatumia algebra,
Kujua mtaji wangu wa milioni 50 nikikopesha watu kwa miaka 5 nitavuna ngapi kwa muda huo pia ni hesabu
Hii ni mifano simple nimekupa kwa mtu ambaye labda hajaajiriwa na hajui atafaidikaje na elimu yake ( tena topic ya Algebra tu) kama akijiajiri
Ila hesabu ina application nyingi ambazo ni complex na zinarahisisha mambo mengi sana kwenye hii dunia
elimu hasa Sayansi nadhani lengo lake primarily sio kumfanya mtu atajirike, bali kumuwezesha mwanadamu kuishi comfortable zaidi kwa kuya master mazingira yake na kutajirika ni matokeo yake ya pili kwa watakao tumia elimu hiyo kutoa service ambazo watu watazilipia