Movie za Bongo Siziwezi

Ni kulialia, kufokeana, kuonyesha magari, tena kama wapo njiani utasubiri mpaka wafike.
Na kama ni mgonjwa wataonyesha mpk anavyotapika.
... siziwezi aisee !
Halafu wanapenda kuchomeka chomeka maneno ya kiingereza.
Utaskia mmoja anasema "I am not OK, dear"
Mwenzake anaitikia "woah!"
Mwingine atapiga "what" "you, you"
 
UMALAYA TUUU.... na HAWAANGALII USANII BALI NI UCHANGUDOA tuu kama Aunt SIJUI NANI???? hapo ukimtoa Kanumba,Majuto na Monalisa Wengine ni Mapu????????
 
Ahahaha mkuu umenichekesha sana. Kuna moja niliiangalia inaitwa Hostel, humo ndani kila mtu ana gari, tena ni wanafunzi wa chuo kikuu. Yaani huu ushamba wa wasanii wetu kuonyeshana magari sijui utaisha lini, na ukizingatia kwa maisha ya sasa magari yamekuwa ni kitu cha kawaida sana. Mi nadhani kama wakibalidilika na kuacha ushamba wa kuonyeshana smartphones na magari na wakawa wanaonyesha uhalisia wa watanzania na maisha yetu basi movie zao zinaweza kuwa nzuri tu. Najua humu jamvini wamo so watakuwa wameupata huu ujumbe, manake wasanii wengi siku hizi wanatumia internet.
 
Sometimes anaoneshwa mwanaume anamtongoza mwanamke hadi anakubali........ Yani maneni yote bila tukio kubadilika

au anaoneshwa mtu anatoka nyumbani na gari hadi anafika ofisin barabara nzima

au mtu anapata ajali anaoneshwa njia nzima mpk anafika hospitali

daah ukiona hivyo ujue stori ni fupi na ubunifu hamna
 
Wakiwa wanakula sasa.Utaonyeshwa tonge la kwanza hadi la mwisho.
 
1. filamu haiishi bila mwanaume kumtoa "lanchi" binti fulani,
2. asilimia kubwa ya filamu zote wahusika wana maisha ya kitajiri (majumba makubwa, uani yamejazana magari) wakati jamii kubwa haina maisha kama hayo
3. kiingereza cha kubabaisha wakati hakuna ulazima wa kukitumia
5. ray ndio anaharibu kabisaa hizi filamu. makelele yasiyo na tija
6. asilimia kubwa ya waigizaji wa kike ni warembo kana kwamba nchi hii wanawake wote ni warembo
 

Ningekua na uwezo wa kumzuia Ray asiigize ningefanya hivo maana hajui kitu kabisaaaaa anaboa vibaya
 

mimi natofautiana na wewe! waigizaji wa sasa hawana ubunifu na sidhani hata kama wana muda wa kujielimisha zaidi kuhusu uigizaji! kila mmoja utamsikia akijisifia kuwa uigizaji uko damuni mwake tangu utoto kitu ambacho siyo kweli! akina bishanga walianza vizuri na hata leo ukiziangalia picha zao bado zina make sense! walitakiwa kujiendeleza kutokea pale ikibidi waende shule za sanaa (drama schools) ikibidi hata nchi za nje kama south africa ambako wako vizuri sana kwa kuigiza!

tatizo la wabong wanawaza kupiga pesa na siyo kuwekeza ili wapige pesa nyingi mbeleni! utawasikia wanalalamika kuwa watanzania hawapendi vitu vya kwa wanasahu hiyo ni kazi na biashara! mtu anataka kitu/bidhaa inayoendana na thamani ya pesa yake!
 

Mkuu siku zote tunachotaka ni satisfaction kwa pesa unayotoa kununua cd ya movi, bila kujali ni ya nje au ndani. Ndiyo uzuri wa soko huria, mwenye bidhaa nzuri ana win soko. Pia movi zaidi ya kutoa burudani inatoa somo, sasa kuna movi za kibongo ile iko robo ushajua itaishaje!
 
Msikonde wakuu!!!
Kuna filamu ya kibongo inakuja na ni ya ukweli kinoma.
Baadhi ya picha za filamu hii zimepigwa S.Africa.
Mimi binafsi nimo ndani ya FILAMU hiyo na pia mimi ndiye mtunzi wa story nzima.
Itatoka mwakani maana bado haijakamilika.
Ni filamu ambayo itakua na majonzi mengi sana!!
 

bongo movie S.Africa hapo inahusikaje sasa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…