Saddest movies I've ever seen. What’s yours?

Saddest movies I've ever seen. What’s yours?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
7,604
Reaction score
15,535
Kama fan mkubwa sana wa movies, sometimes inabidi kuangalia genre nyingine out of my favorite genres
Napenda action na horror ila sometimes naangalia genre nyingine na ninaenjoy just fine

Kuna movie niliangalia tu just for fun nikajikuta zinaniacha na huzuni. Ndio hapa naona wamarekani wako serious sana na profession zao. Yani movie inaanza tu kawaida, wanakuacha uelewe story, uwajue characters halafu ghafla unaanza kucatch feeling, na unajua kabisa it's just a movie ila bado ikitokea emotional scenes unafeel pain na uchungu.
Wengine wanalia kabisa, japo hii haiwezi kutokea kwangu hadi naingia kaburini
Ila I admit wamarekani wanajua sana kutengeneza emotional movies

Katika movie zote nilizoangalia, hizi ndio my 5 saddest movies ever

5. Straw (2025)
Screenshot_20260419-173059.png

Straw (2025) ni thriller-drama movie ya Netflix iliyoandikwa na kuwa directed na Tyler Perry, inahusu maisha ya Janiyah, single mother mwenye maisha magumu anayekutana na matatizo, ambapo maisha yake yanakuja kuwa magumu katika siku moja ya majanga. Movie hii inabeba themes za maisha, umasikini, na kutokuzingatiwa na mifumo ya kijamii.
Moja ya movie zilizovunja hisia za watu wengi sana mwaka jana. Very sad movie


4. The Long Walk (2025)
onesheet.jpg

The Long Walk ni movie ambayo asili yake ni riwaya ya mwaka 1979 iliyoandikwa na Stephen King. Inahusu shindano la kikatili la kila mwaka linalofanyika katika nchi ya Marekani ya kidikteta na ya kidhanifu.
Katika shindano hilo, wavulana wenye umri wa kwenda shule wapatao 50 hadi 100 lazima watembee kwa kasi ya angalau maili 3 kwa saa bila kusimama milele, wote wanatembea bila mwisho mpaka wote wachoke abaki mmoja tu ambaye ni mshindi. Hapa ukichoka njiani unauliwa na wanajeshi ambao wao wapo kwenye magari wanawafuatilia siku zote mnazotembea bila kusimama usiku na mchana
Mwishoni mwa movie vifo vya baadhi ya vijana, na vijana wengine wanavyoumia kuona marafiki zao wakifa inahuzunisha sana. Especially kifo cha mwisho kabisa wa movie, It will break your heart


3. All the Bright Places (2020)
9786020363363_all_the_bright_places_cov_movie.jpg

Hii ni drama inayowahusu vijana wawili Theodore Finch na Violet Markey, wanaokutana wakati wote wawili wakiwa wanafikiria kujiua kutokana na msongo wa mawazo na kukosa furaha maishani mwao, walipokutana wakawa marafiki
Wakawa pamoja katika project ya kuzunguka maeneo mbalimbali ya jimbo la Indiana kwa ajili ya school project, kila group linapaswa kuwa na watu wawili kwa hiyo wakachaguana na kufanya project pamoja wakiwa wawili.
Walisaidiana kukabiliana na majonzi, msongo wa mawazo, na matatizo ya afya ya kisaikolojia, na wakaanza kuwa na furaha. Hatimaye, wanagundua kuwa hata nyakati ndogo kabisa maishani zina maana kubwa.
Mwisho wa hii filamu ni so heartbreaking, ukiangalia machozi yanaweza kukulenga, seriously wala sitanii 😅

2. Five feet Apart (2019)
b80c9e52ccf0fafd421a51da8412abbac5ba82b54d0b1a14cadbd2881b4f3f1e.jpg

Hii ni Romantic drama inayohusu vijana wawili wenye ugonjwa wa cystic fibrosis (CF) ambao wanapendana wakiwa hospitalini, lakini wanalazimika kukaa mbali na kutokaribiana kabisa ili kuepuka kuambukizana maradhi mengine, lakini wanapendana na wote wamelazwa hospitali moja na huu ugonjwa wao wakikaribiana hatari ya ugonjwa inaongezeka, wanabaki kutamani kuwa huru kukaribiana, waweze kushikana na kufurahia nyakati zao za shida wakiwa wanapambania maisha yao hospitalini
Filamu hii inaangazia mapambano yao ya kutaka kuwa karibu, huku ikionesha umuhimu wa human touch

1. The Son (2022)
MV5BYjVmMWRhZTItNDdlZi00YWEwLWJhZTAtZDlmMjRkNWM0ZGY2XkEyXkFqcGc@._V1_.jpg


Out of all these, hii ndio my favorite 🔥
Hii ni heavy drama inayomhusu baba mmoja (Peter) anayejaribu kumsaidia mwanawe mwenye umri wa miaka 17 (Nicholas), ambaye anapambana na msongo mzito wa mawazo (severe clinical depression) yaliyotakana wazazi wake kupeana talaka.
Filamu hii inachunguza jinsi matatizo ya afya ya akili yanavyoleta shinikizo ndani ya familia, hisia za hatia wanazopata wazazi, na kushindwa kwa watu wazima kutambua ukubwa wa maumivu anayopitia kijana mdogo wanapoamua kuachana
Hii movie hata nikirudia kuangalia huwa inaniacha na huzuni tena na tena. Very emotional movie
 
The long walk inafanya Nini hapo?
Nenda kaangalie train to Busan 1 utulie kabisa bila kupepesa macho uone kama hutalengwa na machozi.

Kuna mtu nilikuwa naangalia nae nikashangaa machozi yanamdondoka
 
The long walk inafanya Nini hapo?
Nenda kaangalie train to Busan 1 utulie kabisa bila kupepesa macho uone kama hutalengwa na machozi.

Kuna mtu nilikuwa naangalia nae nikashangaa machozi yanamdondoka
Train to Busan nayo nimesahau kuitaja
Ile ni sad sana kule mwishoni, na saddest part ni father kubadilika kuwa zombie mbele ya binti yake
 
Hiyo no. 5 nilisikia Mtu humu JF ety aliichek mpaka akalia, nikasema Ngoja nikaichek 😂 nkaishia kucheka tuu.

Movie ya kawaida mno
 
Hiyo no. 5 nilisikia Mtu humu JF ety aliichek mpaka akalia, nikasema Ngoja nikaichek 😂 nkaishia kucheka tuu.

Movie ya kawaida mno
😂😂 Ni kama mimi kwenye horror movie za kuuana vibaya, kutoana makoromeo, kuuana kwa chainsaw, Watu wanasema zinatisha ila hazijawahi kunitisha hata kidogo
Ndio hii feeling unayoongelea
Ila mimi kwa sad movies huwa zinamanage kunifanya sad, ila siwezi kulia. Sijafikia hiyo level 😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom