Movie za Bongo Siziwezi

Movie za Bongo Siziwezi

tukiacha teknolojia hata wao tu hawapo serious...kuna vitu vingine vinahitaji akili tu na kujiongeza..kwa mfano kuna movie ya kibongo nikaona eti jini linaagiza redbull bar na wakati wa kuvuka barabara jini linaangalia kulia na kushoto...sasa hapo si hata mtoto mdogo ataona they are not serious!!!

Umenivunja mbavu na hio story ya jini linaloogopa magari.
 
Tukubali tukatae utandawazi pia unachangia sana tuone vyetu havifai. Na hii inatokana na ukweli kwamba tunajifananisha na wenzetu walio tutangulia hatua 1000 mbele yetu. Ulinganishaji huu haupo fair hata kidogo. Nakumbuka Enzi hizo kuna Maigizo ya mambo hayo jahazi ya kaole ya kina bishanga waridi sekioni kusema ukweli ilikuwa inavutia wengi sana kutokana na ukweli kwamba ni wachache sana miongoni mwa wana jamii walikiwa na Access ya kuangalia movie za nje. If am wrong katikati ya miaka ya 2000 hadi 2005 movie za ki Nigeria tulikuwa tuna zi appreciate sana kina Ramsey Noah Geneviev ila ni Wangapi leo wanazikubali hizi movie? Hata za kina bishanga leo hazina mvuto wakati enzi hizo zilikuwa ndo zenyewe. Nilikuwa nawaona wasanii hawafanyi vizuri lakini kusema ukweli tunapojilinganisha na wa nje ni sawa sawa na Timu ya taifa stars Vs Germany au Diamond Vs jay z huu ni uonevu wa hali ya juu. Imagine bongo movie 10 years ago ilikuwaje na imagine itakuwa vipi miaka 10 kutoka sasa.

Hivi wewe unaweza linganisha hizi muvi za sasa za akina Aunt Ezekiel na maigizo ya zamani ya akina mhogo mchungu,kibakuli, Seki au hata Jumba la Dhahabu na mengineyo au hata yanayoigizwa sasa hivi?,kikubwa ni kwamba hiz muvi zina kiwango cha chini mno na niabu,kuna mwanangu jsna alikuwa anaangalia na wenzie akawa ananiuliza "eti baba hawa kwenye hizi picha wanakaaga uchi tu" nilishangaa hata mtoto wa miaka minne anajua kuwa huwa wanavaa uchi? Na hapa sio kulinganisha kuwa eti tunapenda muvi za wazungu sio kweli,na watu wengi wanazipenda kwa sababu wanafanya vizuri na hizo tu kwani hata waigizaji wa Tamthiliya hapa Tanzania wanajitahidi sana na watu wa Comedy pia wako vizuri hao akina Ray muvi zao
nyingi hazina uhalisia wa kitanzania zinaigiza maisha ya kwenye Mahoteli makubwa makubwa na ya Ulaya zaidi,bora hata za Nigeria.

Mi nadhani ndugu yangu unazipenda sana hizo muvi za akina Ray,we endelea kutazama ndugu kila mtu na akipendacho lakini kwangu mimi nafuata kilicho bora!
 
Hivi watanzania nani kawaroga mpaka vya kwenu hata kama si vizuri mpaka mnavikataa? Hivi ni kweli kwamba hata vichwa vyenu tayari navyo vimebinafisishwa? Acheni ushamba wa kudharau kwenu na kutamani vya nje. Cha ajabu huko Ulaya au America hawashobokei za kwenu kama mnavyofanya nyinyi/ninyi. Mjilaumu wenyewe na mje na suluhu nini kifanyike kuboresha movie za ndani

We acha hizo yaani hata kama ni cha ovyo mtu apende tu kwa sababu ni cha Tanzania? mi mbona nayapenda maigizo/tamthiliya za bongo na Comedy? hizo muvi za akina Anti Ezekiel hazifai zaidi zaidi kimaadili!
 
Tukubali tukatae utandawazi pia unachangia sana tuone vyetu havifai. Na hii inatokana na ukweli kwamba tunajifananisha na wenzetu walio tutangulia hatua 1000 mbele yetu. Ulinganishaji huu haupo fair hata kidogo. Nakumbuka Enzi hizo kuna Maigizo ya mambo hayo jahazi ya kaole ya kina bishanga waridi sekioni kusema ukweli ilikuwa inavutia wengi sana kutokana na ukweli kwamba ni wachache sana miongoni mwa wana jamii walikiwa na Access ya kuangalia movie za nje. If am wrong katikati ya miaka ya 2000 hadi 2005 movie za ki Nigeria tulikuwa tuna zi appreciate sana kina Ramsey Noah Geneviev ila ni Wangapi leo wanazikubali hizi movie? Hata za kina bishanga leo hazina mvuto wakati enzi hizo zilikuwa ndo zenyewe. Nilikuwa nawaona wasanii hawafanyi vizuri lakini kusema ukweli tunapojilinganisha na wa nje ni sawa sawa na Timu ya taifa stars Vs Germany au Diamond Vs jay z huu ni uonevu wa hali ya juu. Imagine bongo movie 10 years ago ilikuwaje na imagine itakuwa vipi miaka 10 kutoka sasa.

Upo sahihi kabisa,nakumbuka ile tamthilia ya Jumba la dhahabu ilipendwa sana,na ilikuwa ikionekana ni tamthilia ya kiwango cha juu hapa bongo na waigizaji wake tuliwaona wa kiwango cha juu.Lakini kama sikosei mwaka jana waliirudia ila dah! Nilishangaa hivi tulikuwa tukiipendea nini,maana niliiona ovyo tu ukiliinganisha na movie zetu hivi sasa.
 
Kama mimi vile yaani zangu ni NOLLYWOOD kwa sababu zinamafunzo ndani yake. Simjui mwigizaji yeyote wa Bongo movie kwa jina

Dah! Mie hizo za wanaigeria siku hizi ndiyo sisiwezi kabisa yani bora bongo movie,maana story zao wanaigeria ndiyo zilezile toka miaka ile, hasa hasa utaona wanafanya uchawi mwishoni kanisani.
 
Dah! Mie hizo za wanaigeria siku hizi ndiyo sisiwezi kabisa yani bora bongo movie,maana story zao wanaigeria ndiyo zilezile toka miaka ile, hasa hasa utaona wanafanya uchawi mwishoni kanisani.

Siku hizi wamebadilika sana ziko za action na upelelezi sana.
 
Bongo muvi ni hovyo kabisa tangu afe The Great Kanumba.
Unakuta muvi ina part 1 na 2 ila sasa angalia hyo part tu mbna utakoma na roho yako mfano ni hii muvi inaitwa Bado nipo hai ilioneshwa EATV siku ya jumamosi aisee mule ndani ni hovyo hawajui hata jinsi ya kumaliza muvi. Waigizaji hawajielewi full makelele tu kamera inatikisika hovyohovyo mara sauti ipande na kushuka yaani halafu wanasema wanaibiwa kazi zao mi kwa kazi ipi hadi niibe ujinga huo.
Bora kanumba angekuwa hai ningekuwa naangalia filamu zake maana alikuwa anajua nn anafanya.

Kwani movie za Kanumba ndiyo zilikuwa nzuri?
 
Kitu
Expendable
Blacksheep
No Retreat No Surrender
Iris
Krishna
Godfather
Airplane
Neria
Sarafina
Catch A Fire
The Graduate
Seven Samurai
Hotel In Rwanda
Sometimes In April
Themba
Good Dees
Rise And Fall Of Charles Tylor
Bongo Movie Huwezi Kukaa Unaangalia Na Mama Mkwe Wako.

Movie zengine za zamani hapo ukiziangalia sasa hivi ni Sheeeda!
 
mimi natofautiana na wewe! waigizaji wa sasa hawana ubunifu na sidhani hata kama wana muda wa kujielimisha zaidi kuhusu uigizaji! kila mmoja utamsikia akijisifia kuwa uigizaji uko damuni mwake tangu utoto kitu ambacho siyo kweli! akina bishanga walianza vizuri na hata leo ukiziangalia picha zao bado zina make sense! walitakiwa kujiendeleza kutokea pale ikibidi waende shule za sanaa (drama schools) ikibidi hata nchi za nje kama south africa ambako wako vizuri sana kwa kuigiza!

tatizo la wabong wanawaza kupiga pesa na siyo kuwekeza ili wapige pesa nyingi mbeleni! utawasikia wanalalamika kuwa watanzania hawapendi vitu vya kwa wanasahu hiyo ni kazi na biashara! mtu anataka kitu/bidhaa inayoendana na thamani ya pesa yake!

Hivi sasa unaweza kuziangalia zile tamthilia za itv za zamani ambazo hao akina Ray walipoanzia?
 
Baadhi ni nzuri na zina uhalisia kabisaa' mfano ni KIGODOLO imeongozwa na Zamrad
 
Niko poa Kadoda, umesharudi bongo?

Tatizo sidhani kama hawa watayarishaji wa hizi tunazoita muvi wana muda wa kutembelea majukwaa kama haya ili kupata feedback ya kazi zao but its about time we changed jamani. Tusilazimishane tu kupenda visivyopendeka. Hiyo ishu ya sumu ya panya imeniacha hoi mkuu hahaha, umeua. Tutafutane kaka.

Tatizo zinawalipa ndiyo maana hawajisumbui kuboresha.
 
Juzi niliamua kuangalia "filamu" inayojulikana kama Funga Kazi iliyotolewa mwaka 2009. Humo ndani ni vioja vitupu. Sehemu iliyoniacha hoi ni pale mhusika mkuu, akiwa jela, alipokuwa akikumbuka jinsi alivyolazimishwa na majambazi kuwaua wazazi wake alipokuwa mtoto mdogo mwenye umri wa kama miaka mitano. Kilichonishangaza ni kwamba sebuleni kwa wazazi wake kulikuwa na TV flat screen. TV za aina hii zimekuja miaka ya karibuni. Haiwezekani mtu uonyeshe tukio la miaka 20 au 25 iliyopita halafu waonekane watu wanaangalia flat screen. Ni sawa na kuigiza tukio la miaka ya 1970 lakini humo ndani watu wanaendesha Toyota Mark X au Nissan Murano.
 
Kwa producer's hawa hawa, editer's hawa hawa, director's hawa hawa na actor's hawa hawa, hakutatokea mabadiliko kwenye bongo film, tunahitaji mawazo mapya toka kwa watu wapya kuleta mabadiliko, tatizo walio ndani wamejijengea uzio ili waendelee kuwepo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom