Movie za Bongo Siziwezi

Movie za Bongo Siziwezi

sio kudharau kuna muvi kama za kina majuto zina mvuto kweli ni full comedy hapa tupo kwenye bongo movie, hawa jamaa wanapromote uzinzi tu, kiingereza kibovu, picha mbaya mbona za marehem kanumba ziko vizuri. tunapenda sana vyetu ila kwa movie za kina wema bora nianggalie kipind cha watoto itv. mbona diamond nyimbo zake zinapendeka, ingekuwa hatupend vyetu angeendelea baki kigoma kwao
 
Kitu
Expendable
Blacksheep
No Retreat No Surrender
Iris
Krishna
Godfather
Airplane
Neria
Sarafina
Catch A Fire
The Graduate
Seven Samurai
Hotel In Rwanda
Sometimes In April
Themba
Good Dees
Rise And Fall Of Charles Tylor
Bongo Movie Huwezi Kukaa Unaangalia Na Mama Mkwe Wako.
 
Hivi watanzania nani kawaroga mpaka vya kwenu hata kama si vizuri mpaka mnavikataa? Hivi ni kweli kwamba hata vichwa vyenu tayari navyo vimebinafisishwa? Acheni ushamba wa kudharau kwenu na kutamani vya nje. Cha ajabu huko Ulaya au America hawashobokei za kwenu kama mnavyofanya nyinyi/ninyi. Mjilaumu wenyewe na mje na suluhu nini kifanyike kuboresha movie za ndani

We bumilo acha kutuzingua bhana, yani mi niangalie limuvi halina viwango kisa kupenda vya kwetu! Lisinema limajaa makelele ya mganga wa 'chenyeji' na matunguli yake, haiwezekani, hivi mfano wewe ukiwekewa hapo gari aina ya nyumbu na Toyota carina Ti utachagua ipi? hahaha (mfano tu).

Ukiwauliza wanakwambia bajeti, nikianza kuelezea udhaifu wa muvi zenu nitajaza seva ya watu bure, tuache tu. Ila las ukijua bongo hakuna muvi mkuu.
 
Ni kulialia, kufokeana, kuonyesha magari, tena kama wapo njiani utasubiri mpaka wafike.
Na kama ni mgonjwa wataonyesha mpk anavyotapika.
... siziwezi aisee !

Usiombe wakuoneshe mtu ana mawazo, basi atajikunyata hapo, atatikisa kichwa, atasonya, bila dakika tatu kwisha habanduki hapo, bila kusahau background music sauti juu kuliko maneno, halafu mziki mmoja mbaya tangu mwanzo mpaka.mwisho wa sinema, na kuiga sana unaijeria.
 
kuna moja jana nimekuta inatazamwa home sijui inaitwaje ile,,,,,,,,,,jamaa kasema NIPO NA WEWE BEGA KWA BEGA subtitle yake sasa I WILL BE WITH YOU SHOULDER TO SHOULDER,,,,,,,,!!!!

Na Mimi Mkuu Jana nilipigwa bumbuazi, kuna moja niliikuta kwenye mwaliko Wa Eid-el-fitr ikawa inasemwa LAZIMA ATAKUWA JINI kiingereza chake kikasema SHE MUST BE A GENIE! Kwa kweli nilikuwa sijui kama JINI kiingereza chake ni GENIE!
 
Na Mimi Mkuu Jana nilipigwa bumbuazi, kuna moja niliikuta kwenye mwaliko Wa Eid-el-fitr ikawa inasemwa LAZIMA ATAKUWA JINI kiingereza chake kikasema SHE MUST BE A GENIE! Kwa kweli nilikuwa sijui kama JINI kiingereza chake ni GENIE!

Na akiwa jini lazima awe anakodoa macho kama chura kabanwa na nyoka. Halafu lazima awe na kicheko kikali tena kwa sauti ya juu na meno na kucha kama za kitoweo cha kina kamwene.
 
Ahahahahahah idea zilezile.. Linabadilika jina tu

mata msichana tajiri kampenda maskini

mara msichana mwenye kaz nzuri kampenda muuza maji (bado natafuta)

mara mvulana tajiri kampenda msichana wa mtaani (chausiku)

mara msichana tajiri kampenda kijana msumbufu wa mtaani (too much)

idea ni ile ile ya zali la mentali ya profesa jay

kwa kweli movie za bongo zimekosa ladha tangu kifo cha marehemu kanumba
 
Yaani nipoteze muda nikae kabisa naangalia bongo movie !!!

labda majuto peke yake ila hawa wengine bora nilale
 
Mkuu unazungumzia KIGODORO KANTANGAZE? Ile muvi wamejitahidi sana na ina mafunzo na vichekesho yupo mama abdul na muhogo mchungu,tatizo watu wanaangalia za EATV halafu wanahukumu zile ni za zamani na hazina soko, mimi napenda sana movie za majuto.
movie ya kibongo zipo nzuri tujifunze kuheshimu vya kwetu.
mfano movie ya KIGODORO.
 
yani nimecheka hapa ofisini hadi watu wamenishangaa hii thread wenyewe wakiiona wataumia sana.
 
Halafu kingine kinachoboa

MsaniI kama JB kila movie anaigiza na SHAMSA FORD tu...... Baya zaidi maudhui yaleyale tehhhhhh
 
Ukisoma zile sub-title za English ndio utazimia kabisa. Yaani ni vioja na aibu kwa Taifa zima.
 
mwaka wa tatu sasa sijawahi kuziangalia na wala sina mpango wa kuziangalia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom