PostGE2025 MoU ya TEC na Serikali irudi Bungeni

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hahaha wakatoliki hoi hakuna janja janja tena. Nyie si mnasema watu wa haki? Haki hiyo irudishwe bungeni wabunge waipitishe au waikatae, hakuna kificho tena.

Hongera kwako mleta mada
Katoliki watapoteza nini? Maana hizo ni ajira watapoteza watanzania ambao serekali itabidi kuwapa ajira kwingine. Yaani kuna vitu hamuwezi na hamtakaa muweze. Katoliki wameshika pabaya.
 
wewe jamaa ni changamoto sana.

Mimi nikionaga I'd yako Huwa naona kama ni mgonjwa,na sasa naamini wewe ni mgonjwa(ashakum si matusi).

Waislamu wote nchi nzima ndiyo waje kutibiwa Hindu mandal na Aghakhan?
Ndugu,

Nikupe mfano wa jinsi Kanisa lilivyo na nguvu hii nchi na hakuna wa kulifanya chochote...

Kusini kwenye uislamu/waislamu wengi Kuna hospitali giants za kikristo-Roman Catholic kubwa nyingi kuliko za serikali.

1.Saint Benedictine Ndanda ambayo ni kama nchi inayojitegemea/nchi ndani ya nchi) Make Google your friend,Hapa Kuna taasisi nyingi kama Vatican.

2. Saint Walburga Nyangao (Lindi)ambayo ni kubwa kuliko Temeke ila imeharibiwa na upuuzi wa serikali kufanya hybrid na kanisa(ambayo ndiyo concern yako mleta mada). Sasa hivi huduma zao upande wa serikali siyo nzuri sana.

3. Sister Birgita Lindi.

4. Mkomaindo Masasi.

Na hospitali nyingine mdogo mdogo kadhaa. Hiyo ni kusini kwenye uislamu sana.

Hizo hospitali siyo tu zinatibu hadi wasiokuwa wakristo,bali pia zinatibu hadi watu kutoka nje ya nchi kama msumbiji na nchi zingine jirani kama Comoro.

Mnapoandika hizi mada zinazohusu kanisa muwe mnatafakari kwanza.
 
Hata ukienda kwenye hospital za serikali mambo ni Yale Yale, kama huna fedha hupati matibabu, bahati mbaya ukifa utalipia gharama za kuhifadhi mwili.
 
mpaka leo hii hospitali nyingi za wilaya ambazo ni za serikali hazina lolote na rufaa zao wanapeleka hospitali za DDH za catholic
Huyo kilaza hajui lolote kuhusu MoU kimsingi serikali ndio inafaidika zaidi na MoU kuliko kanisa.

Na hizo hospital zimekuwepo zikitoa huduma kwa miaka mingi tu kabla ya MoU

Nyasi ndio zitaumia mafahari wawili wakipigana
 
Hata ukienda kwenye hospital za serikali mambo ni Yale Yale, kama huna fedha hupati matibabu, bahati mbaya ukifa utalipia gharama za kuhifadhi mwili.
Lakini pesa ile tunao lipia hospitali za serikali zinarudi serikalini kuhudumia wananchi, sasa za bugando zinaenda kanisani wakati huo serikali ndo inalipia mishahara ya wa tumishi wa hospitali.
 
Kwani ukiwa huna pesa si unapata huduma bure Muhimbili? Basi nenda huko achana na Bugando, Kcmc etc. Au anzisha hospitali zako uwe unatoa huduma bure. Jenga shule zako, ajiri waalimu, halafu utoe elimu bure.
 
Huu ujinga acheni mtaipelekea nchi kurudi nyuma kwenye dark ages, Catholic watoa social services zenye viwango bora kama afya, elimu na baadhi ya miundo mbinu ambayo serikali miaka zaidi ya 60 imeshindwa ku offer!

Acheni siasa kwenye mambo ya msingi🚮🚮
 
Kwani ukiwa huna pesa si unapata huduma bure Muhimbili? Basi nenda huko achana na Bugando, Kcmc etc. Au anzisha hospitali zako uwe unatoa huduma bure. Jenga shule zako, ajiri waalimu, halafu utoe elimu bure.
 
Zanzibar wanatibiwa ktk hospital gani?
 
Hapa ndio huwa mnafanya waisilamu wote kuonekana wajinga. Hata kama kuna MoU, hiyo ndio imezuia waisilamu kuwa na shule na hospitali zao? Waisilamu hebu himizaneni hata muoteshe miti kuzunguka misikiti maana kwa haraka haraka hata ukiangalia mazingira ya makanisa na misikiti ni tofauti. Au hata kuotesha miti kuzunguka nyumba za ibada ni MoU nayo?
 
Umetoa MAELEZO mazuri, ila kwanini hujasema PESA zinatoka wapi??

Sasa pesa za WAJERUMANI mnataka kuwapangia namna ya KUZITOA??

Kitu pekee serikali inatoa ni msamaha wa kodi, VAT pamoja na kupeleka watumishi wake kwenye baadhi ya Hospitali za kanisa, ili:
  • Hizo hospitali za dini zifuate sera ya afya ya taifa kama Matibabu bure kwa Wazee, watoto na wajawazito
  • Matibabu bila ubaguzi

Na hilo ni JAMBO dogo, tu ambalo kwasasa MNAWEZA KULIFUTA hata muda huu.

Nashangaa mnabonga sana kwa mambo madogo.

Kama vipi serikali itoke hadharani iseme huwa inawapa kiasi gani???
 
Hiyo MoU ikajadiliwe upya maana imekuwa ni kichaka cha Masheikh kuwashambulia maaskofu badala ya kuishambulia serikali ambayo ndiyo yenye powers.

Tena Maaskofu wakijitoa katika MoU ili kukata pua kuunga wajihi itaepusha shari nyingi.
Pesa wanatoa GERMAN.

Serikali inasaidia watumishi na msamaha wa kodi kwa baadhi ya hospitali, kwa mashariti wafuate sera ya afya ya nchi kam matibabu bila ubaguzi na bure wazee, watoto, na nyingine.

Na inatoa pia msamaha wa kodi.

Ni vitu vidogo sana ambavyo serikali ndio itapoteza.

Ndio maana huwa hawasemi wazi.

Waziri wa Afya ni MOHAMED MCHENGERWA, mwambieni ATOE HADHARANI aseme.

Mna MAMLAKA YOTE mnaogopa NINI??
 
Lakini pesa ile tunao lipia hospitali za serikali zinarudi serikalini kuhudumia wananchi, sasa za bugando zinaenda kanisani wakati huo serikali ndo inalipia mishahara ya wa tumishi wa hospitali.
unajua ni asilimia ngapi ya watumishi wa bugando wanaolipwa na serikali, kwa taarifa yako hawafiki hata asilimia 30 wengi wanalipwa na hospitali,
pia je hao wanaolipwa na serikali wanawatibu wakatoliki peke yao?

kubali serikali lenu halina hela za kujenga hospitali kubwa mpaka waliomba ushirikiano na Catholic

leo hii takribani 70% ya wilaya za tanzania hazina hospitali za wilaya wanatumia za catholic, Dr magufuli ndio alijitahidi kujenga jenga hospitali za wilaya nazo mpka sasa zingine hazijakamilika zingine ziko polini zinatoa huduna za OPD pekeake,

catholic ni maji usipoyaoga utayanywa,
 
hawa mburura wataelewa basi
 
Ndugu yangu we! Unahangaika na watu ambao kiongozi wao duniani anabariki mashoga na kuunga mkono ndoa za jinsia Moja. Hao TEC hata uongozi wa familia hawana, Leo hii watufundishe kuhusu kuendesha nchi??
 
MAMBO YOTE YA DINI YA ONDOSHWE SERIKALINI KUANZIA MAVAZI ...UJENZI WA MAKANISA AU MISIKITI ...MAVAZI YA DINI KWENYE SHULE ZA SERIKALI ...VIAPO VYA WABUNGE NA VIONGOZI , WAAPE KWA KATIBA NA SHERIA NA HAKI SIYO DINI ZAO .....MASOMO YA DINI YASIWEPO KWENYE SHULE ZA SERIKALI WALA ZA BINAFSI ...SHULE ZA DINI ZIWE NI ZA DINI ...HIVYO WANAFUNZI WAKITOKA SHULE , NDIYO WAKITAKA KWENDA KWENYE SHULE ZA DINI SAWA ...WAISLAMU WANA MADRASA WAKRISTO WANA SUNDAY SCHOOL..hivyo dini zifundishwe huko ...KUHUSU MKATABA WA SERIKALI NA KANISA , HUO NI KAMA BAKWATA VYOTE VIFUTWE ...KWA MAANA HATA BAKWATA INAKULA MAMILIONI YA PESA ZA SERIKALI KAMA ILIVYO KWA MAKANISA ...HIVYO UNAPO ZUNGUMZIA MIKATABA UKUMBUKE NA BAKWATA PIA Malaria 2...BILA KUSAHAU TENDA NA MIKATABA INAYO TOLEWA KIDINI MFANO DP WORLD. adriz Al-mukheef FaizaFoxy Covax Jagina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…